Jeshi la wananchi laonywa lisivunje katiba ya nchi kwa kufanya majukumu yasiyo yake kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi

Jeshi la wananchi laonywa lisivunje katiba ya nchi kwa kufanya majukumu yasiyo yake kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi

Sana tu, katukana viongozi kimyaa, kamtukana Rais kimyaa, Kawatukana police kimyaa sasa anataka kutest maji, Nadhani atawataja walioko nyuma yake very soon. Ana act kama vile ndio kahamia Tanzania juzi wakati jitu lina miaka 60 huko. Nchi zote duniani watakosoana lakini siku zote wanalipa jeshi lao heshima hata kama kuna mapungufu. USA walisema hakuna mwanajeshi wao atashtakiwa kwa kuvunja haki za binadamu japo wao ni machampion wa mambo hayo. Israel alikataa wanajeshi wake kushtakiwa.. na wengine wengi. Hawa sio wajinga. Sasa huyu kafika sehemu anataka kuhatarisha amani ya nchi. shida hapa ukiwakashifu jeshi au police na wakakulia kimya unafungua mlango na kufunga itakuwa too late. Mshughulikieni huyu haraka.
Education is keyyyy of lifee,~Luck dube
 
Majeshi yenye akili yanapindua serikali mbovu na kufanya research zenye tija.

Jeshi letu tatizo wamejaa viraza wao wanadhani wakivaa mabaka yao wamemaliza kazi. Namuunga mkono Mwambukusi, hao wahuni waache mara moja mpango wao wa kijinga.
Nchi ikipinduliwa nyie mmmashoga mtajinyea ovyo,huna akili wewe
 
Mwabukusi anajua kaabisa wanaoenda kutwa na hizo nguo za jeshi Mdude, Mwabukusi na Slaa. Kesi ya uhaini itafuata baada ya hapo.
 
Alichokiandoka ndicho sahihi.kuingilia kazi ambazo si majukumu yao ni uvunjifu wa sheria na katiba ya nchi na tukiacha hayo yaendelee siku moja nguvu ya umma yao itajichukulia sheria mkononi.
 
Jeshi kuwekeza kwenye Research za HIV, COVID, Nuclear, Balistic Missiles, Ndege Jeshi, Submarines, wao wana hangaika na mitumba za Marehemu Wa Kizungu. Kiwanda chao cha Nyumbu kimeshindwa hata kuzalisha Bajaji za Abiria.
Exactly [emoji817]..
Mkuu issue ni ELIMU usifanye utani..hahahaha
 
Watanzania uzuzu wetu umeanzia kuonekana hapa hapa kwenye huu uzi. Yaani kabisa kuna watu wanamdhihaki na kumwona Mwambukusi kama amekosea. Watu kama hao unatarajia kuna siku watakomboka na kuwa huru kifikra???
Exactly [emoji817]
 
WAKILI MWABUKUSI ANATAKA MKUU WA MAJESHI AZUIE UVUNJIFU WA KATIBA.

"Nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria na katiba. Kazi ya kukamata wa halifu ni ya Jeshi la Polisi. Jeshi la wananchi halina mamlaka kisheria na kikatiba kuingia kufanya msako mitaani kwa kisingizio cha kutafuta sare zao. Jukumu lao ni kulinda mipaka ya nchi. Cha ajabu hawajatuambia walizipeleka lini huko mitaani au zilichukuliwa na nani au waliibiwa lini? This is more than a comic [Huu ni usanii]!

Mwanajeshi hana mamlaka ya kupekua mtu katika makazi yake au maungo ya raia. Hii ni kazi ya Polisi wetu. Isipokuwa pale kunapokuwa na hali ya hatari au tishio dhahiri la mapinduzi.

Sheria inaruhusu kukataa ukamataji haramu na iwapo jeshi litaingia kwa namna hii ni haki ya wananchi kukataa ukamataji au upekuzi haramu usiofuata sheria ikiwemo kumshtaki Mwanasheria mkuu na Mkuu wa Majeshi ili kulinda sheria na Katiba ya Nchi na kudai fidia ya usumbufu.

Kama jeshi limeibiwa sare zake likaripoti Polisi. Polisi wafanye uchunguzi na wakibaini kosa Polisi ndiyo wenye utaalamu wa kupeleleza uhalifu wa wizi. Jeshi au wanajeshi hawako juu ya sheria [hivyo] wapunguze mihemko.

Kumekuwa na ujasiri wa uvunjaji katiba na sheria na kuwatisha wananchi katika taifa letu katika uongozi huu wa sasa na kwa hili hatutakubali na tutalitolea tamko rasmi kupinga vurugu hizi katika utumishi wa umma.

Mkuu wa Majeshi awajibike haraka kuzuia ukora huu wanaotaka au kupanga kuufanya!

Najisikia aibu sana kuishi na kushuhudia viroja hivi. Mungu bariki Watanganyika! Mungu ibariki Tanzania! Mungu waadhibu na kuwakemea madhalimu wote.

Boniface Kajunjumele Mwabukusi!
Kiingereza cha nini aongee kiswahili tu kwani akiweka kiingereza ndo ataonekana nani yeye, ulimbukeni tu huo
 
Huyo mpuuzi jeshi halifanyi ujinga ukiona hivyo ujue kuna tishio kubwa sana la usalama, na toka matukio ya kibiti Police haiaminiki tena kwenye mambo nyeti, undercover police wasaliti walikuwa wengi sana
Wew ndio bumunda uliona wapi pawe na tishio halafu uwastue waharifu badala ya kwenda kuwakama kimya kimya.
Ninyi mazuzu ndio mtaji wa ccm mkiambia chochote mnakubali tuu. Kesho ukiambiwa jeshi wanataka kukagua makalio yako utawapelekea tuu kwa kuwa jeshi linakagua waharifu.
 
Nchi inapo ingia vitani maana yake wanaobaki kutegemewa ni jeshi huku vyombo vingine vikiwa vimeufyata
Nitajie hiyo sheria mkuu. Kazi ya jeshi la wananchi ni kulinda usalama wa mipaka ya nchi. Kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao. Hii ni kwa mujibu wa sheria mama (katiba) na sheria nyinginezo na si vinginevyo. Inapotokea vita majeshi mengine yote yataungana na jwtz kulinda mipaka ya nchi yani kupigana vita majeshi hayo mengine yakiwa chini ya jwtz. Lakini jukumu la ulinzi wa raia na mali zao bado linasalia chini ya jeshi la polisi. Kumbuka mtaalam aliyesomea usalama wa raia ni polisi.
 
Na maanisha wale wanao lalamika jeshi kutoa tamko kuwataka walio na magwanda kurejesha. Mbona ni jambo la kawaida tu. Unagwanda rejesha.
Mara ngapi watu wamerejesha siraha walizo nazo isivyo kihalali bila kuchukuliwa hatua?
Jeshi wamesema usiporejesha watakuja wao wenyewe kuchukua kwani wanajua. Sioni shida jeshi kutoa tangazo. Kinachotakiwa watu waatii.
Hoja nzito na inayoelekea kuvunja haki za raia iliyo ktk tamko la jwtz ni pale wanaposema kuwa wataendesha msako wa nyumba kwa nyumba.

Huu ni uvunjifu wa sheria, katiba na haki za binadamu hasa fargha za watu vinginevyo walipaswa kutangaza hali ya hatari ndipo wafanye mengineyo.
 
Nitajie hiyo sheria mkuu. Kazi ya jeshi la wananchi ni kulinda usalama wa mipaka ya nchi. Kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao. Hii ni kwa mujibu wa sheria mama (katiba) na sheria nyinginezo na si vinginevyo. Inapotokea vita majeshi mengine yote yataungana na jwtz kulinda mipaka ya nchi yani kupigana vita majeshi hayo mengine yakiwa chini ya jwtz. Lakini jukumu la ulinzi wa raia na mali zao bado linasalia chini ya jeshi la polisi. Kumbuka mtaalam aliyesomea usalama wa raia ni polisi.
Umeshinda mwanajeshi.
 
Watanzania tuache kuchekea ujinga. Jwshi linapaswa kufanya mambo serious na sio kuanza kusumbua raia. Jeshi linapaswa kuwa sehemu ya raia kukimbilia pale ambapo vyombo vingine vyote vimeshindwa
Sheria zetu zinasema je?
Kama tumejiwekea sheria kufuata mnapata taabu ya nini
 
Wew ndio bumunda uliona wapi pawe na tishio halafu uwastue waharifu badala ya kwenda kuwakama kimya kimya.
Ninyi mazuzu ndio mtaji wa ccm mkiambia chochote mnakubali tuu. Kesho ukiambiwa jeshi wanataka kukagua makalio yako utawapelekea tuu kwa kuwa jeshi linakagua waharifu.
Wewe kibwengo tu subiria upatikane na hizo nguo ndio utaongea vizuri
 
Mnaleta utani kwenye ulinzi wa Taifa, acheni upumbavu tutawafuata majumbani uniform za jeshi ni haramu kutumiwa na raia
Sheria zetu zinawaruhusu kama nyiye mnavunja sheria je tumejiwekea utaratibu wa nini basi
 
Back
Top Bottom