Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa mkuu kama una mzigo mkubwa inakuwaje kwenye habari ya usafirishaji? Hawa amazon ni kwa soko la US peke yake au ni worldwide?mkuu inategemea na mahali ulipo,ila DHL ipo almost mikoa yote,hivyo kama upo wiliyani unaweza order tu,ukifika DHL watakupigia simu kuwa mzigo wako umewasili na watataka ukauchukue. nadhani kama umeuagiza nje ya nchi haitokuwa ngumu kuchukua usafiri kufuata mzigo wako mkuu.DHL wanaweza kukuletea mpaka mlangoni kwako ila wilayani ni mbali na huwa hawatoko nje ya mji.FEDEX wapo sehenu chach na USPS ni posta hivyo naamini wilayani masanduku yapo na utapokea mizigo yako palepale posta mkuu.
Bank gani mkuu...
Nimejaribu kucalcutor mzigo wa 3 Kg kwa hawa jamaha wa Stackry.com naona DHL ndio imekua the cheapest one,sasa nimeshindwa elewa kwa nini hvyo!je na masuala ya ushuru ukituma kwa DHL inakuaje wakuu?maana nasikia uwa inakua included humo!na je kuna mtu yeyote mwenye idea na EMS services toka USA to Tanzania?
2:Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.
Mkuu kwanza asante sana kwa elimu murua.
Nimefuatilia uzi kwa kiasi kikubwa.
Bado nahitaji kunijazia kidogo;-
1.Ninapokamilisha manunuzi kule amazon kuna kitu gani ambacho kitaniunganisha na hawa forwading company(comgateway)?
2.Au wao amazon wana option za mimi kuchagua kampuni ninayotaka kusafirisha mzigo wangu?
3.Na kama hii ya juu ndio je hilo kampuni itafahamu vipi kama mimi nimenunua mzigo kule amazon unataka kusafirishwa?
Bank gani mkuu...
Kinachokuunganisha Amazon na comgateway ni shipping adress/Billing Adress
Comgateway wanakupa adress ya US ambayo utaijaza kwenye Amazon account
Mzigo utasafirishwa kuja Hiyo Adress ya comgateway na baada ya hapo comgateway watasafirisha kwa adress yako ulo wapa wakati wa usajili
2:
Mkuu kwanza asante sana kwa elimu murua.
Nimefuatilia uzi kwa kiasi kikubwa.
Bado nahitaji kunijazia kidogo;-
1.Ninapokamilisha manunuzi kule amazon kuna kitu gani ambacho kitaniunganisha na hawa forwading company(comgateway)?
2.Au wao amazon wana option za mimi kuchagua kampuni ninayotaka kusafirisha mzigo wangu?
3.Na kama hii ya juu ndio je hilo kampuni itafahamu vipi kama mimi nimenunua mzigo kule amazon unataka kusafirishwa?
sawasawa mkuu,, kitakacho kutambulisha wewe ni account yako ya fowarding company uliyojiunga.. unapojiunga na fowarding company yeyote inakupa shipping adress ya marekan au ilopo hiyo fowarding company,sasa inachotakiwa wewe ni kuchukua hiyo address na kuiingiza kwenye account yako ya amazon,ebay nk. hapo amazon,ebay au soko ulilojiunga litatuma huo mzigo kwenda kwenye hiyo shipping address ambayo ni fowarding company yako.wao wakipokea mzigo imediately wanakutumia e-mail kukujulisha unamzigo na kama utataka kutumiwa..kisha utaenda kwenye website ya fowarding company na ku log-in kwenye account yako, utakuta notification ya mzigo utachagua namna unavyotaka ukufikie Tanzania-hapo ndo utachagua DHL FEDEX au courier yeyote amae ni cheap au fast au utakavyoona wewe choice ni yako... natumai nimekujibu mkuu kalendi.
bwana njunwa yuko sahihi kabisa...(sikuangalia vizuri hapo juu)
Ushuru wenyewe ni asilimia ngapi?Ushuru kwa DHL hapa Dar ni innevitable kwa items zote zilizo eligible kutozwa ushuru
Ushuru wenyewe ni asilimia ngapi?
Import duty
na VAT
Sina hakika ipi ni 20% na ipi ni 18%
Hivo mzigo kama ni 100$ na uko valid kupigwa ushuru basi watachukua (100$ × 0.18) + (100×0.20)
Na huo ndo ushuru wako ila ikumbukwe educational materials hazipaswi kugongwa ushuru