Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

Nikitaka kununua vitu Amazon. Com nikiwa Tanzania nafanyaje wajuzi tusaidiane. Kuna mawakala wao Tanzania?
 
Mkuu mimi sikupingi ila nahisi una uelewa mdogo wa mambo au la sivyo hujui kuuliza.
Humu jf kuna watu wanajua mambo mengi kwelikweli , sasa chakufanya tafuta namna nzuri ya kuuliza swali lako.

naamini unaeza ukawa na point ya mana ila kwa jinsi ulivyouliza huezi pata jibu sahihi hapa
Nsamehe kama nimekukwaza
 
Wala ucjar ndugu sina box namba ila nilisikia kuwa unaweza weka namba ya Simu na mkoa unatoka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi naweza kufanya manunuzi online kwa kuandika sehemu nilipo bila kuwa na box namba na mzigo ukafika

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio inawezekana.

Ongea na seller atume mzigo wako kwa njia ya DHL ambapo huwa inahitajika Phsical Address ya mahala ulipo na namba ya simu tu.

Iwapo utahitaji mzigo uje kwa njia ya posta waweza tumia huduma yangu fuata hii thread: www.v.ht/buy4me

KARIBU
 
Mm nishawahi nunua kitu Alibaba online na nikawa nimekipata, cha msingi ama hatua ya kufuata ni

1. Uwe na anwani kamili mfano sanduku la barua, namba ya eneo mtaa kwa baadhi ya maeneo hapa dar na Arusha wanazo zimebandikwa, mawasiliano yawe kwa njia ya email

2. Uwe na TIN no.

3. Ni kuomba invoice ikiwa imejumuisha na gharama ya usafirishaji mf. DHL, FEDEX nk

4. Unaenda TFDA wao ndo watafanya mawasiliano ya hiyo kampuni kama ipo ama laah na mwisho wa siku watakupatia kibali cha kuagiza ndo unaweza lipia.

Na huwa inapendeza ukicheza na soko la dollar siku ikishuka unatuma. I
Ni hayo ingawa pia huwa kuna usumbufu upande wa clearance huchukua muda mrefu.

NB. Ni vyema kwenda TRA kwenda kujua kodi ya mzigo ambao utaagiza tofauti na hapo utaishia kuutazama tu kwa macho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wanunuz wa aliexpress na alibaba muagizapo mzigo inachukua siku ngapi mzigo kufika?

Jee ukilipia shipping cost itachukua siku ngp
Free shipping je
Naomba kama umewahi kununua bidhaa naomba kujua uzoefu wako kwamba ilichukua siku ngapi?
 
Mkuu vipi salama uko! Mbna unarudia umo kwa umo kama unapiga msuaki.

Maswali yako yote jibu lake ni moja tu maana maswali yote yanauliza muda gani mpaka mzigo kufika
Inategemea na caurier gani umetumia
Free shiiping mara nyingi hua ni "china post odinary small package plus" hii huchukua 30-60 day

China post registerd air mall 15 - 30 day
Aliexpress standard shipping 14 - 25 dys
Singapor post 20 - 40 day

Nyengine ni epress shipping kama dhl 1-5 dys, fedex economy 5-10 dys
 
Back
Top Bottom