Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

Um
Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania. Baadhi ya thread zilianzishwa na zimeelezea mengi sana kuhusiana na manunuzi haya ya mtandaoni, ila tulipata ufumbuzi mdogo.

Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi. hii ni kwa kutumia FOWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni;

1: Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri marekani au uingereza UK) au US Shipping Address

2: Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia (eidha amazon,ebay au lolote lile lisilo ship Tanzania)

3: Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL,FEDEX,UPS,USPS NK baada ya kujua kazi ya fowarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo (kwa wageni wasiofahamu/hawajapitia previous threads:

1: CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana almost bank zote hapa Tanzania (kasoro NMB sina uhakika), ni kadi yeyote ya visa au mastercard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni(online purchases) na mara nyingi huchukua maximum 24hours kuactivate.

2: KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa paypal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.

3: KUJIUNGA NA FOWARDING COMPANY
Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi fowarding company na kujiunga (sighnup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma... nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi

4: KUTAMBUA SOKO BORA LENYE HUDUMA NZURI(ONLINE MARKET)
Hapa tunazungumzia website za masoko kama ebay,amazon, bestbuy, apple.com, dell.com, toshiba.com nk.. masoko haya ndipo utakapo nunua bidhaa yako.

PROCESS NZIMA KUANZIA UNANUNUA MPAKA MZIGO UNAKUFIKIA IKOJE?

Hii iko hivi....

1: Ingia katika soko lako ulilolichagua au unalopendelea, hapa nasuggest kutumia sana amazon(ndilo ninaloliamini) amazon ukiingia utakuta bidhaa nyingi ila kuwa makini kuchukua zile bidhaa zilizo na alama ya prime chini...alama hiyo inamaanisha kuwa huo mzigo unauzwa, utapakiwa, na kutumwa na amazon wenyewe, so no utapeli hapo, yani u get what u wanted.

2: Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.

FOWARDING COMPANIES ZENYEWE:

1: MYUS.COM link- MyUS.com - #1 International Shipping, Mail and Package Forwarding Service - MyUS.com. Hii ni company niliyoitumia na nina expirience nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wana charge pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika upesi sana bila ya zengwe lolote.

Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga na huduma zao

Uzuri wao: watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,

2: COMGATEWAY
Link: Shop US Stores and Ship Internationally | comGateway - Hawa pia ni fowarding company nzuri sana (thanks tu Mwl.RCT), nimepitia site yao na huona wana policy nzuri sana, cha kwanza ni sales tax-free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi marekani, hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courie DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi.pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus..

3: BORDERLINX
Link: Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx - Hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ... Wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia..Hawa pia hawana registration fee na wanakupa option tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.

4: SHIPITO
Link: USA Address & Mail Forwarding Shipito.com | English - Hii pia ni kampuni kongwe ya fowarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao

5: STACKRY
Link: Stackry - US shopping, global shipping - Hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mabo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao. waungwana ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mabo kabla ya kuchukua uamuzi.

STACKRY na BORDERLINX walikuwa recommended sana na wanasifiwa mno angalia hii link -http://tech-vise.com/10-parcel-forwarding-services-for-international-shoppers/ pitia hizo websites na ujionee mwenyewe chagua moja na utazame kama wanakufaa.

HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI WAKUU , Please evaluate kindly.

Nilikuwa nataka kuonyesha steps ila naona thread haitoshi maana nimeagiza mzigo na nimechukua hatua zote ili mpate kuona ila I think there are limits..

Help Mwl.RCT
Umefumbua macho watu wengi sana.
Lakini nina hitaji msaada kujua maana kuna bidhaa unakutaa zinaandika haziwezi tumwa Tz, je baada ya kulipia bidhaa destination naweka ya yule dalali au naweka yangu. Hapo sijakupata vizuri
 
1. usalama wa fedha apo hakuna tatizo sana.
.
2. Ukiona huna uhakika na bihaa picha, basi check imenunuliwa mala ngapi(orders) pia shuka mpaka sehem iliyo andikwa feedbacks uta tazama apo comments za walio nunua hio bidhaaa na wengine huweka picha ya bidhaa hio,
.
3. Inategemeana na shippment methode uliyo itumia ku safilisha mzigo wako, kwa izi njia za bei rahisi mimi nai amini sana ALIEXPRES STANDARD SHIPPING METHOD hii hua niki iona tuu kwenye bidhaa, basi na amini mzigo ntaupata ndan ya wiki 3 adi 4, apo nipo MBEYA.
.
4. Ondoa shaka, niliwai nunua SMARTWATCHES kadhaa kwa laki 3, zilipo fika uku zikawa azishiki mtandao, naisi nikwa sabu ya kuto kua registered tcra, basi nili Open refund, nikapewa pesa yangu yote na saa nika ambiwa nibaki nazo. Ila refund zina chukua mda sana kufika bongo, ili bidi nisubilie miezi mitatu ndo pesa ikawa tayar..
🙂🙂🙂🙂🙂
 
Kama una VISA card au MasterCard iliyiverified kwa ajili ya online purchases,nenda play store download Ali Express fanya mambo kuwa rahisi

Sent using Jamii Forums mobile app

Habari. Mimi nahitaji kujua kama nimeagiza mzigo alibaba na umefika bandarini je taratibu za clearance nafanyaje na mimi nipo mkoani? Je inawezekana wasafirishaji wanakaifanya kama ndio gharama zikoje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi nipo mkoani? Je inawezekana wasafirishaji wanakaifanya kama ndio gharama zikoje?
Mzigo utakaotumwa huwa na documents zake (BL)

Hizi documents hufika mapema kabla ya mzigo.

Unachotakiwa kufanyani kumtafuta agent na kumkabidhi hizo documents (BL)

Na atafuata taratibu zote za kuutoa mzigo pindi ukifika, na atakujulisha ghalama zote unazotakiwa kutoa kabla ya mzigo kupa release.
 
Mzigo utakaotumwa huwa na documents zake (BL)

Hizi documents hufika mapema kabla ya mzigo.

Unachotakiwa kufanyani kumtafuta agent na kumkabidhi hizo documents (BL)

Na atafuata taratibu zote za kuutoa mzigo pindi ukifika, na atakujulisha ghalama zote unazotakiwa kutoa kabla ya mzigo kupa release.
Asante sana Mwl.Rct kwa majibu yako. Na documents zitakuja kwa posta au wanatuma kwa email

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na documents zitakuja kwa posta au wanatuma kwa email
BL huwa wanatuma kwa DHL au EMS, hivyo pindi unakamilisha manunuzi, hakikisha unagusia swala la BL ili ujue watatuma kwa njia gani.

Huwasili nchini ndani ya siku 14 tangu mzigo utumwe.

Wakati mzigo husika unachukua wiki kuanzia Tatano hadi saba.
 
BL huwa wanatuma kwa DHL au EMS, hivyo pindi unakamilisha manunuzi, hakikisha unagusia swala la BL ili ujue watatuma kwa njia gani.

Huwasili nchini ndani ya siku 14 tangu mzigo utumwe.

Wakati mzigo husika unachukua wiki kuanzia Tatano hadi saba.
Asante ndugu,ubarikiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii mada inatakiwa iwe Stickymaana bado nadhani kuna uhitaji mkubwa kwa huduma hii.
 
Ntapataje wakuu hii mashine ya kushonea mazulia (hand tufted gun) kutoka china?? Na bei itagarimu kama kiasi gani ukichanganya na kodi na kila kitu.

Nb. Ya bei rahisi zaidi

New Rug tufting gun electric, 110v, Cut pile. Loop pile also available. | eBay
Hand-tufting-gun-9-18-mm-.jpg_640x640(1).jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom