Jiji la Dar limenishinda kuishi. Wengine mnawezaje au mnajikaza?

Ukianza kuona kero za kelele na purukushani zinakupa stress ujue umeanza kuzeeka ni muda muafaka kuhamia nje ya mji au mkoani kwenye wilaya tulivu au shambani kabisa. Huu ni uzoefu wangu.
 
ukiwa kwenye sgr au gari lolote lenye Ac, ukifika dar ukashuka tu, unaanza kuona jinsi hali ya hewa ilivyokuwa chafu ya huo mji wenu.
 
ukiwa kwenye sgr au gari lolote lenye Ac, ukifika dar ukashuka tu, unaanza kuona jinsi hali ya hewa ilivyokuwa chafu ya huo mji wenu.
Dar hakufai mkuu, jana nlikuja mida ya mchana na Private kwa lengo la kutafuta hotel ya kufikia nipange ratiba zangu za viwanja hali ya hewa na makelele vikanishinda ikabidi tu nivuke maji
 
Ikiwa jiji Dogo kama Dar linakupa shida je utaweza survive New York n.k
New York kuna hekaheka gani mkuu zinazoizidi Dar? Hekaheka anazozungumzia jamaa ni zile ambazo zipo kwenye big cities za kwenye informal economies kama Tz: e.g. foleni, kugombania seat kwenye daladala, wamachinga kila mahali, biashara ya ngono, joto, etc. Haya yote ni karibu hayapo kabisaa NY. Kitu pekee NY inaizidi Dar in terms of hekaheka labda ni biashara ya madawa ya kulevya na gun violence.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…