Jiji la Kampala linaweza kufananishwa na mji gani wa Tanzania kwa uzuri na maendeleo?

Jiji la Kampala linaweza kufananishwa na mji gani wa Tanzania kwa uzuri na maendeleo?

Hujatembea wewe, Nimesoma Kampala 2004 to 2007 na huwa naenda mara kwa mara hata sasa...Kampala ni jiji la kawaida mno, kwa Tz laweza kufananishwa na Mwanza au Arusha
Sidhani! Naona kama Kampala ni kubwa kuzidi Mwanza na Arusha.
 
Kwa siku chache ambazo nimekuwepo hapa Kampala, nimeweza kujionea, japo ni kwa sehemu ndogo tu, jinsi lilivyo.

Ni jiji kwenye hadhi ya kuitwa jiji. Lina mandhari nzuri na pia hali ya hewa nzuri.

Pamoja na kwamba ni jiji, lakini ukililinganisha na jiji la Dar Es Salaam ni kulionea, na ukisema ulilinganishe na jiji la Tanga au Mbeya ni sawa na kulitukuna.

Ikiwa halijalifikia jiji la Dar Es Salaam, na pia limeyaacha mbali majiji ya Mbeya na Tanga, ni mji upi Tanzania unaweza kulinganishwa nao?
Mdau hebu kaa zaidi kidogo kuna mengi hujayaona hapo. ili ukirudisha mrejesho utuongezee watalii toka Tanzania.
1. Kampala hakuna bidhaa au huduma utaambiwa haipo. Hakuna neno haiwezekan hadi wapasiane kazi mji mzima bila kuathiri bei ya awali. Dar kuna uchoyo au uzembe flan katika kila jambo.
Hata wapiga dili bongo wakienda Kampala wanageuka wateja kwa sabab lile jiji wanawekeza sana kwenye utapeli.
2. Kampala ndo jiji pekee bado wanapika vyakula vya asili [non organic] kuanzia ngazi ya mama lishe hadi hotel kubwa. Yaan mlo kamili. [Mf mlo wa kimaskin mamalishe... ndizi+mhogo+gimbi+pumpkin+ papai/nanasi+kisamvu+ nsanyuse+ dagaa mbumbo + mchicha] Dar unakaribishwa mchemsho ni nyama kwenye maji! limao na chumvi ndo bonus!
3. Kampala ndo wanawake weng weusi ila wanang"aa ngozi kama koboko! Ukiwa mweupe kwa asili km dada zangu wa nyanda za kati na kaskazini utawindwa kama para na wanahonga vizuri sana!
Ila weupe wa mkorogo kama dada zangu wahaya na wanyakyusa ni kama chuma chakavu huna maana.
4. Kwa wanaume wanaopenda kudekezwa kama wafalme usimpende mwanamke wa kiganda mana hutarudi Tz hata kupiga kura! Ni wanajari na kujinyenyekeza mpaka unahisi ni tamthilia!
Matukio ya kwenye wimbo wa mboso msinitafute cha mtoto.
5. Waganda ni washawishi mno kila sekta, hasi au chanya. Wana subra.
Anaweza kukuamini kibiashara au kimahusiano hadi akakuachia mamilion bila dhamana akakujenga lakini ole wako siku ukimpa zako!
6. Kampala ndo jiji utaweza kulipia kiingilio kuangalia wanaokwichi kwenye ulingo, live kama wanamasumbwi [kimansure]... full light! Muhim mhudhuriaji usipande ulingoni kujihudumia.
7. Kampala wanapenda utani na mizaha iwe kwa mgeni au kati yao.
Hata miziki yao, shootings zao lazima utiemo vichekesho/vituko ndo utaeleweka.
Sio Nai kila mtu yuko serious utadhan mna mgogoro. Poor hospitality!
8. *Welcome to Kampala [muchibuga], The city of Squiters! ...hapa sitoi ufafanuz zaid ya .......hapa ndo general rule inageuka exception na kinyume chake!
...Yote tisa, kumi ni Tz is the best place to live on earth, until you become a politician!!!!!
 
Unanikumbusha mbali maeneo kama Bweyogelele, Mengo, Nakitete, Entebbe..e.tc..

Kampala Jiji tamu sana hilo..

Nilikua nafikia hotel moja inaitwa Sunrise Hotel
images (2).jpeg
 
Barabara ya Mutukula kwenda Kampala utagundua kwa nini viongozi wanapendelea MAV8! Japo ni lami lakini kwa hivyo "vishimo" utatamani bodaboda
Kalisizo,, Kyotera, Masaka to Kampala.

asieeh ile barabara ya Masaka to Kampala imenyooka sana.
 
TZ jiji ni moja tuu
Ukitumia Vigezo vya kimataifa vya Uanishaji Miji kuwa Jiji, Tanzania Hakuna hata mji mmoja uliokidhi vigezo vya kuweza kuwa Jiji. Hakuna kabisa.

Mathalani, ukichukua kigezo kimoja tu cha Kupangilika kwa Mji katika Muktadha wa Mipango-miji(Town Planning, Urban and Infrastructures Development), tayari miji yote iliyopo Tanzania inakuwa disqualified kuweza kuwa Majiji.

Ukichukua percentage ya Ardhi iliyopimwa(surveyed land) na ambayo ipo katika Mpangilio mzuri wa kimipango-miji, utagundua kwamba Hakuna hata mji mmoja nchini Tanzania ambao angalau 50% ya Ardhi ya mji wake wote imepimwa na ipo katika Mpangilio. Miji mingi Sana ipo unplanned, squatters, Kama wamejitahidi Sana basi haizidi 30% ya Ardhi yake ndio imepimwa, ipo katika mioango-miji, na ipo katika mpangilio mzuri.

All in all, and bad enough, takribani 60% ya Nyumba na Majengo yote kabisa yaliyopo kwenye vijiji na miji mingi Sana nchini Tanzania hazifikiki kwa barabara za uhakika, zaidi ya kufikika kwa njia tu za watembea kwa miguu, zipo vichochoroni ambako hata pikipiki haiwezi kufika.
 
Back
Top Bottom