Jiji la Mwanza vs Jiji la Arusha: Lipi ni zaidi kwenye hili?

Jiji la Mwanza vs Jiji la Arusha: Lipi ni zaidi kwenye hili?

Naanzisha mjadala kwenye barabara bomba kati ya Mwanza vs Arusha.

IMG_4821.JPG

Arusha City

IMG_4824.JPG

Mwanza City.
Barabara mpya ya Airport.
 
tukitoka hapa naomb tuhamie kwa mamvi na maparangoto
 
Arushaaaaa, there's no place i would rather be. Cool weather, national parks, cool people you name it.
Mwz na Arusha kuifananisha ni makosa maana kuna tofauti kubwa mno kwa mfano Arusha ni mji wa kitalii unaitwa geneva ya Africa mpaka hapo utalinganishaje na mza? Mza kwa takwim za hivi karibuni toka nbs ni kati ya mikoa maskini, mza ina hotel za maana chache mnoo, arusha zipo nyingi, ahhhh jamani mza na arusha haifanani hata!!!!
 
Ni sawa kuuliza swali chai Na kahawa kipi kitamu. Kila jiji Lina taste zake Na Kila jiji Lina natural resources zake Na geographical features tofauti
 
Arusha ni mkoa wa tatu kwa utajiri baada ya dar na kilimanjaro.
Arusha ina mbuga za wanyama zenye kuitambulisha tanzania(rerengeti,ngorongoro na iko karibu na manyara)
Hali ya hewa ya arusha ni ya ubaridi na jua mara chache inayosababisha kutokuwepo na mvumbi kabisa.
Arusha ndo jiji linaloongoza kuwa na usafi tanzania.
Ndo jiji linaloongoza kuwa na shule ya serikali zinazofanya vizur kwa form six(Ilboru ,kisimiri).
Ni jiji la pili lenye hoteli za kifahari baada ya dar
Ni jiji linaloongoza kuwa na vitu ghali tanzania.
Arusha kuna kiwanja kidogo kimoja cha ndege na ipo karibu sana na uwanja wa kimataifa wa KIA.
Arusha ndo kiungo cha mauzo madini ya tanzanite one(yanayotoka mereran karibu sana na arusha japo ipo manyara)
Arusha ina vyuo japo si vingi.(ARU,TUMAIN,MANDELA{arusha technical kwa ufundi})

kwa haya sijaona sababu ya kufananisha mwanza kisa ina watu weng na arusha kamwe mtalii hawez kuja kutembelea mwanza akaacha arusha
 
Ongeeeni tu lakin mwisho wa yote ni new york [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Arusha inasatelite city mbili
Mwanza Hamna Ata moja....

Arusha hotels za zenye wadhifa kibao
Mwanza hakuna

Mall mwanza yao kubwa kuliko ya Arusha

Mapato ya Jiji mwanza wako juu ya Arusha

Kwa wastani Arusha ni Moja ya mikoa tajiri Mwanza ni Moja ya mikoa masikini. ..

Arusha inaizidi Mwanza kwa ujumla
 
Back
Top Bottom