Mwanza haikupaswa kuwa Tanzania ilipaswa iwe sehemu ya Spain Madrid,nakumbuka Kenyatta road,kirumba , pasiansi,buzuruga nyegezi kwenda Malimbe SAUT, Sweya kwenda mpaka Chuo Cha uvuvi TAFIR unanyosha kuja BUTIMBA hadi Mkuyuni soko la Juma pili. HAKIKA MWANZA PATAMU. Mji umepambwa kwa mandhari nzuri ya Miamba ya ajabu ilibebana na kuzuiana Kama Kuna mtu aliyabebanisha, hapo usisahau upepo mwanana kutoka Ziwa let kuuuubwa yaani Ziwa Victoria lenye samaki watamu Kama Sangara na Sato. Kibiashara pamechangamka ukienda soko la jioni pale Rwegasore karibu na Tanganyika Parker's chini ya maeneo ya Sahara unakutana na samaki wa kila aina wakiwa bado wanapumua wanarukaruka wakiwa wametoka mita 100 lilipo Ziwa. HAKIKA nitarudi Mwanza.
MAENEO YA KUJIDAI KWA WAKATI HUO.
1. Golden Crest Hotel
2.Mwanza Hotel.
3.Jembe ni Jembe
4. Charcoal Ribs
5 Kilimanjaro hotel na nyingine nyingine.