Jikoni na Mwifwa, upishi wa mboga(samaki)

Mkuu ugali mkubwa sana huo kwa single hauwezi kuumaliza!
Au hupendelea kurudia mlo ama kunywea chai kiporo?
Vinginevyo ni matumizi mabaya ya rasilimali.
Menu ya watu 2 mkuu, na ilifunikwa kama kawaida bila kusaza hata punje ya tonge
 
Haya mdogo wetu kapika tena pishi shatashata. [emoji3][emoji3]

Uje umfunze kupika na mchuzi wa nazi sasa. Japo nawaza tu hiyo nazi ataikuna vipi? [emoji3]
Najua kukuna kabisa tena kwa umaridadi wa hali ya juu. Ila sasa sina kibao cha mbuzi[emoji3]
 
Hilo zoezi la kuwaweka samaki kwenye maji yaliyochemshwa umeniacha kwenye mataa Mkuu. Sijawahi kuona wala kusikia na nimebahatika kuwaangalia wapishi wazuri sana akiwemo Mama yangu. Yeye na wengine samaki wa kukaangwa huwekwa kwenye sufuria iliyoko jikoni hivyo hivyo bila kuwaweka majini na ladha ya mchuzi wake na samaki acha kabisa Mkuu.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…