Jikoni na Mwifwa, upishi wa mboga(samaki)

Jikoni na Mwifwa, upishi wa mboga(samaki)

Mkuu ugali mkubwa sana huo kwa single hauwezi kuumaliza!
Au hupendelea kurudia mlo ama kunywea chai kiporo?
Vinginevyo ni matumizi mabaya ya rasilimali.
Menu ya watu 2 mkuu, na ilifunikwa kama kawaida bila kusaza hata punje ya tonge
 
Haya mdogo wetu kapika tena pishi shatashata. [emoji3][emoji3]

Uje umfunze kupika na mchuzi wa nazi sasa. Japo nawaza tu hiyo nazi ataikuna vipi? [emoji3]
Najua kukuna kabisa tena kwa umaridadi wa hali ya juu. Ila sasa sina kibao cha mbuzi[emoji3]
 
Hilo zoezi la kuwaweka samaki kwenye maji yaliyochemshwa umeniacha kwenye mataa Mkuu. Sijawahi kuona wala kusikia na nimebahatika kuwaangalia wapishi wazuri sana akiwemo Mama yangu. Yeye na wengine samaki wa kukaangwa huwekwa kwenye sufuria iliyoko jikoni hivyo hivyo bila kuwaweka majini na ladha ya mchuzi wake na samaki acha kabisa Mkuu.

3. Nimechemsha maji na kuloweka samaki waliokaangwa ili walainike.

4. Nimekaanga vitunguu, karoti na hoho kwa pamoja kwa mafuta hadi vikaiva kabla ya kuweka nyanya nilizokatakata.

5. Nimeweka nyanya nilizomenya na kukatakata(sina kifaa cha kusagia) kwenye sufuria yenye vitunguu, karoti na hoho vilivyoiva ili nipate mchanganyiko wa supu nyanya zitakapoiva.View attachment 1177890
 
Back
Top Bottom