Jina la sasa la Twitter" X" lina utata sana

Jina la sasa la Twitter" X" lina utata sana

Toka billionaire Musk auchukue mtandao wa Twitter kuna mabadiliko kadha wa kadha amefanya.

Moja ya mabadiliko hayo ni kutoka kuitwa Twitter mpaka kuitwa "X".

Hili jina limekuwa na ukakasi mwingi sana hasa katika kulitumia kutambulisha mtandao unaotumia hata kufungua app yake katika kundi la watu lililo kuzunguka.

Hili jina "X" limejenga picha sio nzuri katika sehemu kubwa duniani ndani ya jamii hasa upande wa maadili.

Kuutamka mtandao "X" mbele ya watu lazima usindikize na Twitter ili usieleweke vibaya, naoa watangazaji wengi wa vipindi vya runinga na redioni lina wapa ukakasi mkubwa kulitamka.

Mfano: Mwanzo videos zilizopo Twitter zilikuwa zinaelezwa kama "Twitter videos" sasa hivi inabidi useme "X videos" tafrani tupu.

Sijui mtaalamu musk aliwaza nini juu ya hili jina maana limekaa kimagumashi balaah.
X lina ubaya gani
 
Naona ameamua kuita mtandao X ili uendane na kampuni yake ya Space X inayohusika utafita nje ya dunia (kwenye sayari)
 
Sio Twitter tu,

Hata mtandao wa "Tigo" nao kwa sasa ni vigumu kumwambia mtu kwamba unatumia Tigo kama mtandao wako wa mawasiliano.

Mtu ana kuuliza, mkuu unatumia mtandao gani?

Kwenye kumjibu lazima usindikize neno "mtandao" kwanza, Maana ukijibu tu haraka haraka kwamba "Natumia Tigo"

Kuna ukakasi hapo, jamii isha tafsiri vibaya neno Tigo, Kwamba ni yaleyale maeneo ya Buza.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Ukiwa na pesa lazima uwe Kama mwehu fflani kama unabisha kamcheki kwevo
 
Just imagine unafungua hii kitu mbele ya umati wa watu

View attachment 2769676
kuna siku kuna dogo mtot wa mshua wangu alikua antafta magemu kweny simu yngu si akOna hiyo application ya X dah dogo naona alieaza mbaLi sana mwshowe akaniuliza nkamwambia hyo twitter imebadilishwa jina imagine dogo aliemaliza la saba juzi tu halafu
 
ni utata, zile picha mbaya za ngono tunazita picha za X, sasa ukisema picha x ni utata mtupu, ama za ngono au za mtandao wa X. Angalia sentensi hii, "natazama picha za x kwenye mtandao wa x, ni utata mtupu
Hii haijakaa poa kabisa
 
Kumbuka elon ana Space X kabla hata kununua twitter, anapenda hata product zake kuwa hivyo.
Kuhusu space X sio tatizo kabisa shida ni mtandao wa kijamii kupewa hilo jina la X moja kwa moja mawazo yanayo kuja kichwani ni ya kipuuzi tu.
 
Back
Top Bottom