Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Daah story ni tamu sana kuna vitu vingi sana nimejifunza your the best bro sema umekata Tamaa haraka sana
Uwezi AMINI watu wengi wanafatilia huu Uzi ujui ni wangapi wanajifunza kutokana na hicho ulichoandika

Usisitishe kile ulichokianza kama Kuna kitu umekusudia watu wajifunze endelea Tu
Maneno Huwa yapo Tu yasikufanye uache kutusimulia kile ambacho ulitaka hasa tujifunze kama haters ni 2 Kwa 200 wanafatilia uoni kama hutendei haki wale wenye Nia ya dhati ya kutaka kujua nn kimejili
Usikate Tamaa kiboya be strong move on bro
 
Ndugu zangu wana JF kwa heshima ya watu wote humu ndani naomba kuisotisha hii story iishie hapa sitoimaliza maana inaonekana ni chai. Na mimi siwezi kupoteza muda kuandika kitu ambacho watu wanasema ni uongo.

Nina mambo na majukumu mengi ya kufanya na hakuna anayenilipa kwenye hii story, napoteza muda wangu kuwapa watu story kilichonitokea na mpaka nikaamua kuandika lakini inaonekana ni 0,

Nafikiri kila mtu aendelee na mambo yake kwa stage iliyofikia kumaliza story itakua ngumu, nafikiri tuishie hapa. Kama mtu ameshasema story ni chai kuna haja gani ya kuendelea kuandika?.

Kwa wale tuliokuwa pamoja ahsanteni kwa muda tulionza pamoja ila mimi binafsi nimeshindwa kuendelea kuandika, maana watu wanakatisha sana tamaa.

Story haijaisha hapo niko na matukio ya March, lakini mtu kashaaanza kutukana, haters wamekua wengi, lakini hii ni JF kila mtu anahaki ya kuongea. Ustaarabu mngesubiri story iishe hapo ndo muanze kujudge, maana hivi vyote nilivyoandika na ushahidi navyo kwa picha, Contracts nilizoingia nawateja zangu zote ninazo mpaka Iryn.

Story haijaisha mtu watu wameanza kukosoa anyway ndo wabongo walivyo, sinaga muda na JF ila haya matukio yalinitokea ni kweli na nilikua ndo nimeanza kuingia kwenye kiini cha story na nilikua nimepanga kuandika Epsodes 30 tu.

Wabongo tunakosa kitu kinaitwa patient hapa ndo tunafeli sana, story haijaisha hata mjue lengo la kichwa cha story lakini watu wameanza kushout. Siwezi endelea kuandika kwa style hii inakatisha tamaa, ndomana story nyingi za JF zinaishia njiani.

Wale ambao tunawasiliana PM na tumebadlishana namba tutaendelea kuwasiliana tuko pamoja, ila niseme biashara ya Uber ilinipa mafanikio sana na mpaka sasa naendelea kunufaika.

ALL THE BEST
Dah kwahiyo umeamua kuwasikiliza mbweha walio wachache kuliko sisi wadau wako, mkuu umetuangusha[emoji21]
 
Huko episode za nyuma msimuliaji mwenyewe alisimulia kuwa iryn alimwambia mara moja moja imetokea katombwa na wateja ila mpaka awe kampenda, sasa huko sio kujiuza. Sisi watetezi wa walaji tuna details na tunasoma between lines kuhakikisha walaji hamdanganywi na mtoa simulizi.
[emoji23] nyie sio watu wazur mmetuharibia Uzi wetu aisee
 
Angesema hadithi sawa lakini ye katuaminisha mwanzo ni true story ndo alipokosea, hajui kuna watu humu jf hatuna bongo nyepesi yaani hatuangalii Netflix wala hatujashikwa na series za kikorea, hivyo ukisema kitu ni true story tunafuatilia tupate la kujifunza ila ukisema ni hadithi tu pia tutafuatilia labda tutapata la kutuburudisha kama hamna tutaondoka kimyakimya.
Sio unasema true story afu unawafunga kamba watu, lazima tuloshtuka tukupopoe kwa sababu umetupotezea muda tumefuatilia true story isiyo burudisha, elimisha wala kusisimua zaidi ya kujimwambafy na kujipigia promo kwa jf's b*tchz, angetoa tangulizo this is for the ladies, maniqqa tungepita kushoto.
Bandiko lolote litalonipotezea muda kulisoma afu mwisho wa siku nigundue anatufunga kamba lazima nimpe za uso kabla ya kuacha kulisoma.
Ukiangalia watu mnaojifanya kujua literature criticism ni wale mme join 2014-2020 , means they are matured people who in one way or another Wana ka frustration ya maisha after what magufuli did to them financially...Sasa Wana hasira na yeyote anaye onekana kuwa au kuzungumzia maisha Bora... Shida si sisi wenyewe kwa wenyewe ...ni CCM ndio imetufikisha hapa tulipo...tupeleke/ tuelekezeni frustration zetu huko.
 
INSIDER HAPO UTAKUWA UNAKOSEA SANA.
Hata the best movies in the world hazikosi critics, unfortunately JF hawana option ya kuenyesha viewership ila I am sure kuna watu wengi wanafuatilia your story kuliko sisi critics. You can stop a story just because few of us tuna question the realistic of the story, from the story unavyoadisia and how you handle issues you are BETTER THAN THIS. Kuacha just because of critics, you have a very good talent of telling a very interesting story whether it’s true of fiction and JF is one of the better place to show readers what you have. Huwezi fanya kitu bila kupata critics. Pia imagine thread ingekuwa inaenda bila mabishano ya critics isingefika mbali hivi and very active, soon unaweza beat record ya RIKIBOY. Please for the sake of the other critics naomba nikuombe uendelee kutupa burudani.
Sure, thread ikikosa critisim haiwezi toboa ht, kwnz insider anatakiwa ajivunie maana wafuatiliaji wamekua Ni active na wengi,
 
Kwanza binafsi nikupongeze kwa moyo mkunjufu kabisa, pamoja na hayo umejitahidi sana hata kufikia hapa ulipo amua kuishia (niliona hili mapema sana na nikaanza kuhisi kama hii simulizi haitokua na mwisho mzuri kutokana na ujuaji wa wengi hapa jf).
Nakupongeza sana na ingekua mimi ndio wewe kwa maneno ya wapuuzi humu ningesha acha kuandika muda mrefu sana.
Lakini pamoja na kuburudika, nimejifunza mambo mengi kupitia simulizi hii ingawa nilitamani iendelee but sina namna nyingine ya kubadilisha maamuzi yako.
Jf ilikua nzuri sana miaka ya nyuma kidogo kabla vijana wengi maJobless hawajaanza kumiliki simu, ambazo wamekua wakizitumia vibaya kutokana na stress za ukosefu wa ajira, basi wanahamishia makasiriko na chuki zao kwa watu wengine ambao wamefanikiwa.
Vijana wa skuizi wamekua na maneno mengi, uvumilivu hawana na ujuaji mwingi usio maana ambao hupelekea makasiriko na wivu wa kijinga kwa watu wengine.
Ukitaka kujua jf imebadilika, chunguza utakuja kugundua memba wengi wameacha kuandika nyuzi na hakuna tena nondo za maana kama zamani wakati watu waliheshimiana sana hapa ndani.
Wengi tumebakia kua wasomaji tu, tumeacha tena kuweka mawazo ya maana na fikra pevu zaidi ya kua wasomaji na wachangiaji tu.
Nakuona kabisa moyo wako ulivyo vunjika, na kutokana na maneno ya wengi mabaya na matusi juu yako bila kusita naamini unaenda kutoweka ama kubadili ID ama kuanzisha ID nyingine, then unabadilika na kua mpenzi mtazamaji hapa jf.
Jf ilikua nzuri sana miaka ya nyuma kidogo kabla vijana wengi maJobless hawajaanza kumiliki simu, ambazo wamekua wakizitumia vibaya kutokana na stress za ukosefu wa ajira [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wewe fala kasome.vizuri jamaa amelipa dollar 6500 sawa na million 17.

Aliyetaka kumbaka iryn.

Hivi million 17 mnaijua nyie.

Halfu insider akampa mlinzi elfu 50 chai chai
Kuna siku nilikuwa kijiji kimoja usukumani kwetu. Simu niliyokuwa nayo ilikuwa ni infinix hot 10 play. Kuna jamaa akaniuliza ni bei gani. Nikamwambia nimenunua laki tatu na hamsini. Akashangaa sana akanijibu hao si mbuzi karibu 10. Sasa yeye alikuwa na tecno ya button, nikamuuliza yako sh ngapi? Akaniambia ef 40. Nikamwambia nawe ni sawa na kuku 10. Akacheka sana, ila tukaelewana.

ukielewa utofauti wa mazingira na uthamani wa fedha wala haikushangazi.

Wewe ukiingia bar hapo ukatumia 50 wala si ajabu, ila nenda kijijini hela hiyo tumia kwe pombe pale 'senta', kijiji chote kitapata taarifa zako.
 
Sijawahi ku comment huku hata siku moja ila nimegundua huku kuna watu wana mambo ya ajabu saaba any way

Maisha yako usinifananishe na maisha ya mtu mwingine ukiona kwako haiwezekani kwa mwingine inawezekana.

Bwana insider kaamua kusitisha story hata kama ndo mimi ningefanya hivo.

Asante sana bwana insider nimejifunza vingi.
 
Bwana mdogo na ukali wote wa maneno kumbe fundi uashi, embu jaribu kuwa mstaarabu kwenye nyuzi za watu. Pia kumiliki pasi ya kusafiria sio ujanja, unaweza kuwa nayo na usiitumie ipasavyo kama inavyotakiwa.
Mfano mm Nina leseni ya gari Ila mpk Leo hii sijaendesha gari coz I'm not interested [emoji23]
 
Nimejaribu kupitia post za nyuma za INSIDER MAN nimegundua jamaa yuko real sana, kwanini nasema yuko real?

1. Kuna uzi aliandika kuhusu kukata tamaa ya kuapply kazi

2. Kuna uzi alindika akiomba kazi

3. Aliomba msaada maana akikutana na dem wake anakojoa haraka, aliomba ushauri humu JF.

Jamaa anaonekana real na so confident, Smart na Genius, personal life yake anaiweka sana JF bila kujali.

Kwenye hii story nilitaka kujua.

1. Iryn ni nani? Maana anaonekana sio mtu wa kawaida.

2. Muajemi mwisho wake

3. Mary na Prisca

4. Mama J

5. Maisha yake ya sasa, anafanya nini.

Wahuni wameharibu thread.
3. Aliomba msaada maana akikutana na dem wake anakojoa haraka, aliomba ushauri humu JF. [emoji23]
 
Mdugu zangu nitamalizia hii story sababu ya heshima ya JF. Kuna watu wengi wamenitumia ujumbe na watu ambao nawaheshimu wameomba nimalizie story.

Nimegundua story inafuatiliwa na watu wengi sana mpaka sasa tuna views almost 400k ni watu wengi sana.

Nitawapa mwendelezo na huu mwezi 8 story yetu itakuwa imeisha yote.

Kitu kingine sitajibu swali lolote kwa mtu atakayeuliza, ila nitajibu maswali yote baada ya kumaliza kuandika story.

Naomba heshima iwepo kwenye uzi kusiwepo na watu kutukanana sio jambo jema sisi sote ni Watanzania japo kuna foreigners pia wanapitia huu uzi. Kwa mtu ambaye atakiuka na kuleta taharuki nitamreport kwa mods waangalie namna ya kudeal naye.

Kama unaona huwezi kwenda na hii story unaweza uka ignore huu uzi, ukaacha watu ambao wako tayari kusoma.

Nilikua naomba mfanye maamuzi nyinyi wenyewe;

1. Niandike Epsode zote then nizipost?

2. Ndani ya week niwe napost episode 3?

Option ipi kwenu itafaa?

BY INSIDER MAN
 
Mimi naanza vipi kujuana na wapuuzi kama wewe? Huwa sifanyi biashara na wehu!

Acha wivu mtoto wa kiume. Yani ukisikia mtu anashobokewa na wanawake wewe roho inakuuma? Kwani wewe haudindi? Au ulitaka umshobokee wewe?

Soma story, kama haikuvutii pita kule. Acha wanaoipenda wafuatilie.

I have my reliable sources of information. Ukiendelea kusumbua naweka na picha zako. Nimetumiwa hapa naziangalia, sura mbovu kama gari la jeshi!

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
hahahaha watu wameshavurugwa...
 
Mdugu zangu nitamalizia hii story sababu ya heshima ya JF. Kuna watu wengi wamenitumia ujumbe na watu ambao nawaheshimu wameomba nimalizie story.

Nimegundua story inafuatiliwa na watu wengi sana mpaka sasa tuna views almost 400k ni watu wengi sana.

Nitawapa mwendelezo na huu mwezi 8 story yetu itakuwa imeisha yote.

Kitu kingine sitajibu swali lolote kwa mtu atakayeuliza, ila nitajibu maswali yote baada ya kumaliza kuandika story.

Naomba heshima iwepo kwenye uzi kusiwepo na watu kutukanana sio jambo jema sisi sote ni Watanzania japo kuna foreigners pia wanapitia huu uzi. Kwa mtu ambaye atakiuka na kuleta taharuki nitamreport kwa mods waangalie namna ya kudeal naye.

Kama unaona huwezi kwenda na hii story unaweza uka ignore huu uzi, ukaacha watu ambao wako tayari kusoma.

Nilikua naomba mfanye maamuzi nyinyi wenyewe;

1. Niandike Epsode zote then nizipost?

2. Ndani ya week niwe napost episode 3?

Option ipi kwenu itafaa?

BY INSIDER MAN
Mkuu kwanza nashukuru umézingati maombi ya sisi wasomaji wako kuturudishia burudani hii nzuri.

Pili, option ya kwanza ni nzuri zaidi.
 
Back
Top Bottom