Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Halafu ukizingatia wanaume kama INSIDER tuko wawili tu Duniani.Hivi wanawake wenzangu huyu insider mwenye roho nzur hivi naacbaje kimpa penzi??
Au ni Mimi tu ? najisikia hivi
Kwamba angetoa mimba ya Prisca?Kosa kubwa analilofanya Insider mpaka sasa, ni kuwaacha wanawake wafanye maamuzi kwenye masuala ya muhimu. As a man, you're always supposed to lead!
Just imagine, Prisca anatambua kua alifanya maamuzi ya kipumbavu kubeba mimba, ila Insider aliona ni sawa tu. Japo hatujafika, ila tayari naliona hilo timbwili la kifamilia linalokuja mbele!
Kwa Iryn tatizo linafahamika. Mwanamke akitaka umkaze then ukazingua, basi attitudes za kipuuzi ndizo zitakua malipo kwako. So far, mimi naona fanani umefeli kwenye mahusiano yako yote kuanzia kwa mkeo, Prisca mpaka kwa Iryn. Ngoja tuone kama kuna comeback!
Insider is Smart ...but ana Lack Boundaries tu sometimes!Kosa kubwa analilofanya Insider mpaka sasa, ni kuwaacha wanawake wafanye maamuzi kwenye masuala ya muhimu. As a man, you're always supposed to lead!
Just imagine, Prisca anatambua kua alifanya maamuzi ya kipumbavu kubeba mimba, ila Insider aliona ni sawa tu. Japo hatujafika, ila tayari naliona hilo timbwili la kifamilia linalokuja mbele!
Kwa Iryn tatizo linafahamika. Mwanamke akitaka umkaze then ukazingua, basi attitudes za kipuuzi ndizo zitakua malipo kwako. So far, mimi naona fanani umefeli kwenye mahusiano yako yote kuanzia kwa mkeo, Prisca mpaka kwa Iryn. Ngoja tuone kama kuna comeback!
Unamtunuku tuuu kwani shingapi bhana😂😂😂😂😂😂😂😂Hivi wanawake wenzangu huyu insider mwenye roho nzur hivi naacbaje kimpa penzi??
Au ni Mimi tu ? najisikia hivi
We mpe tu ulichopewa bure kwann umnyime mwenzio😅😅Hivi wanawake wenzangu huyu insider mwenye roho nzur hivi naacbaje kimpa penzi??
Au ni Mimi tu ? najisikia hivi
“Nakupigia simu hupokei.”
“Nilikuwa nimetingwa kidogo, nakutumia ripoti soon na mzigo nakwenda peleka now.”
“Kesho tuonane kwaajili ya suala la mkataba wako wa kazi.” Na alitoa sauti ya mtitizo sana tena yenye u-serious, na akakata simu.
He's "too nice".Insider is Smart ...but ana Lack Boundaries tu sometimes!
Kama angeweza kuset boundaries mapema, hata wasingefika huko kwenye mimba!Kwamba angetoa mimba ya Prisca?
Mzee, umefanya jambo zuri kumpa Jane gari...hapo utaishi kwa amani.EPISODE: 53
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”
Ilikuwa ni mwezi tayari umetimia tangu kifo cha Mzee Pama kitokee. Kwa upande wangu ndani ya huu mwezi nilikuwa nimepitia msoto sana kwani nilikuw namuota sana usiku na mara nyingi nilikuwa namuota yuko na mwanae. Nilikuwa naweweseka sana usiku honestly nilipata tabu sana kuzoea kifo chake kwa kipindi hiki, mpaka nilikuwa nawaza huenda Mzee hajafa.
Kwa upande mwingine kutokana na sakata la Muajemi niliwaza kumfanyia jambo la kimafia maana aliniharibia kwa Iryn afu akawa hajibu text. Nilikuwa najua sina maisha marefu sana kwa Iryn kwanza kitendo cha kuchukua gari kwa Mama Janeth kilinipa ukakasi sana.
Nilipanga kumpiga pesa Muajemi ili kulipiza machungu yangu na nilijisemea nitaandaa mpango mzuri wa kumuingia na kufanikisha hili suala. Nilicheki whatsapp nikaona text niliyo mtumia mara ya mwisho ilikuwa iko delivered lakini ilikuwa kama haijasomwa. Nikapata wazo la kumcheki Telegram maana ndo mtandao anaopenda sana kuutumia pia ameweka namba yake ya Iran.
Nilifungua Telegram na nika-scroll mpaka chat history zetu nikamuandikia ujumbe “Bro how are you? I have good news, please call me ASAP.”
Baada ya kumtumia ujumbe mimi niliendelea na mambo yangu muda huu, maana nilijua akiona ile text lazima atanirudia tu.
Wakati nikiendelea kufikiri pale mbinu ya kumpiga hela Muajemi nilipata ujumbe kwenye whatsapp yangu na alikuwa ni dada Gorata (Mbotswana). Baada ya kufungua ujumbe alionitumia alikuwa anataka nimfate Airport na anatarajia ku-land Tanzania saa 11 jioni akitokea Kenya.
Saa 15:30 alasiri niliondoka kwenda JNIA na baada ya kuwasili pale terminal 3 nilipark gari vizuri nikaenda kukaa kwenye kiukuta upande wa arrivals. Nilifika mapema sana maana 16:30 ilinikutia nikiwa pale Airport, na muda huu simu yangu ilianza kuita, naam ni Muajemi alikuwa anapiga.
Nilipokea simu yake kwa haraka sana ni kama nilivyotegemea lazima atapiga tu maana akisikia habari njema anajua ni Iryn, ni jinsi gani alivyokuwa fala kwa Iryn.
MIMI: “Bro! habari yako za ukimya.”
MUAJEMI: “Kaka salama sana, samahani sana nilipata emergence nikaondoka bila kukuaga.”
MIMI: “Toka uongee na Iryn ndo ukapata emergence hata text ukawa hujibu, hata hivyo umepiga sababu nimekwambia na habari njema.”
MUAJEMI: “Hapana bro nimebanwa sana nilikuwa naplan nikirudi nikucheki.”
MIMI: “Anyway tuachane na haya na habari njema kwaajili ya Iryn but naomba kwanza unambie nini kiliendelea ile siku? Maana Iryn alinichukia sana ni vile ananiamini ndomana bado niko naye.”
Kwa ufupi Muajemi alicheza rafu mbaya sana alikuwa anamtongoza Iryn kupitia mgongo wangu. Yaani yeye aliamini kupitia mimi angempata, alimwambia Iryn mimi ndo nili organize kwenda Zanzibar ile siku na mimi ndo ananitegemea kwenye kufanikisha hili suala. Japo alikuwa kuna vitu anahide kusema na mimi sikutaka endelea kumuuliza maswali maana nilikuwa naplan zangu.
MIMI: “Sasa ilikuwaje kaka ukasema hivyo?”
MUAJEMI: “Bro sorry niliingia kwenye trap yake maana alinambia niseme ukweli kuhusu kinachoendelea kati yangu na wewe. Pia bro ile siku niliyokupa pesa kule Zanzibar anasema alikuwepo room na alinibana sana nikafanya kumwambia ukweli. Baada ya kusikia alikuwa room yako niliumia kaka kuona mrembo kuwa analala kwako.”
MIMI: “Aisee bro ulifeli sana Iryn alikuwa anacheza na emotion zako tu yaani umezingua sana, uliingiaje kwa trap kijinga hivyo asee.”
MUAJEMI: “Kaka katika maisha yangu sijawai kutana na mwanamke mwenye challenge kama Iryn ana maswali very technical, nilipoteza mpaka confidence.”
MIMI: “Kaka shida uliingia kwa trap lakini nilikuambia mapema sana, so mlifikia wapi sasa kwenye mazungumzo yenu?.”
MUAJEMI: “Alisema hatuwezi kuwa kwenye mahusiano zaidi ya urafiki tu sababu nina familia. Kaka nafikiri nilikosea kumwambia ukweli suala la familia angekuwa amenikubalia.”
MIMI: “Hahahaha hamna bro! Ulikuwa unampata ila uliharibu pale uliponihusisha na mimi.”
MUAJEMI: “Kaka nimemwambia namjengea nyumba, namnunulia gari anayotaka pamoja na kumfungulia biashara kubwa anayotaka, akubali hata kunizalia tu lakini aligoma. Bro! sijawahi kukutana na mwanamke mgumu kama huyu nimekula warembo wengi ila huyu hatari. Baadae kabisa nikaomba mzigo ndo akanambia atanifikiria, atanipa jibu.”
MIMI: “Ok tuachane na haya, ulikosea padogo sana. Sasa mimi naplan ya wewe kumpata Iryn maana ananisikiliza sana, ila unatakiwa kufanya mambo mawili tu. Jambo la kwanza usimtafute kwasasa wala kumsumbua, la pili nina mpango nimeundaa ila nitahitaji kiasi cha pesa kidogo tu. Kwa huu mpango niliouandaa nakuhakikishia mrembo atakuwa kwenye himaya yako, uzuri mpaka sasa kashajua lengo lako kwa upande wangu haitakuwa shida.”
MUAJEMI: “Bro! always sina shida ila nambie ni mpango gani huo? Maana nishakata tamaa pale tayari.”
MIMI: “Bro! wanawake hawahitaji vitu vikubwa hasa kwa Iryn ambaye hana shida na pesa. Mpango wangu ni simple tu nitakwenda naye Serengeti National Park na tukaa huko hata siku 5 tu zinatosha. Kwa mazingira haya kwanza itakuwa surprise kwake hata nikiongea naye suala lako atakubali tu. Iryn kwa sasa yuko single labda nikwambie hivyo ndo utaelewa, pia unatakiwa utambue mwanamke anaye jitambua huwezi mtongoza papohapo na akakubalia hautakiwi kukata tamaa. Huu mpango unauonaje?”
MUAJEMI: “Bro! your fuckin genious. How much do you want for this plan.”
MIMI: “Kaka hapo kila kitu million 10 inatosha vizuri kabisa.”
MUAJEMI: “Nita transfer hii amount kwenye account yako ya bank soon.”
MIMI: “Ok bro! No problem.”
Baada ya kumaliza maongezi niliishia kumtukana tu muda huu maana niliona Muajemi ni boga-bogast kabisa.
Baada ya lisaa Gorata aliweza kuwasili pale Airport na baada ya kuniona tuliishia kukumbatiana tu muda huu.
“Ooh! my sister I have missed you.”
“Thank you so much for coming.”
Tulielekea parking niliko-park gari na tuliondoka kuelekea Golden Tulip hotel ya Masaki. Njiani tulikuwa tunapiga sana story na pia Gorata alisema hatakaa kabisa Dar kwani Jumatatu ataondoka kwenda Mozambique. Baada ya kuwasili pale Hotelin tulikwenda moja kwa moja mpaka chumba chake alichokuwa amebook.
Jambo lingine alisema kwa kesho jumapili angehitaji saloon ili atengeneze nywele zake. Nilimwambia kwa kesho sitoweza kuwepo lakini jumatatu nitakuwepo kumpeleka Airport na kuhusu saloon nilimwambia nitampa namba za dada (Sumaiya) ili amsaidie.
Ilikuwa saa 12 jioni tayari muda huu na mimi nilimuaga, wakati naondoka alitaka kunilipa lakini nilimkatalia nikamwambia ataunganisha na jumatatu.
******
Jumapili nilipanga kwenda kumkabidhi Jane gari yake na hii siku sikwenda kanisani. Nilianza kwenda pale Juliana kuosha gari ile asubuhi na baada ya gari kuoshwa niliondoka kwenda Namanga pale Mbuyuni.
Lengo la kwenda Namanga nikaonane na wale wauza maua ili waipambe gari kwaajili ya kuipeleka kama zawadi. Baada ya kuwasili pale na kuonana na wahusika niliwakabidhi gari waishughulikie. Gari ilipambwa vizuri sana pande zote mpaka kwenye rim za gari na kutokana na ile rangi yake iling’aa sana na ilipendeza.
Nilimpigia simu Jane na nikampa taarifa za kwenda pale kwake na nikamwambia aniwekee na lunch. Nilitoka pale Namanga na safari yangu ilikuwa ni kwenda Mbweni, ni mwendo wa dakika 45 nilitumia mpaka nawasili pale kwake na baada ya kupiga honi alitoka dada kunifungulia geti.
Niliingiza gari mpaka karibu na usawa wa mlango wa nyuma kibarazani na nikashuka na niliacha gari on pamoja na double hazard. Niliingia ndani na nilimkuta Jane akiwa seblen na mama yake na dada mmoja alikuwa mgeni kwangu.
MIMI: “Shem njoo nina surprise yako.”
JANE: “Surprise gani hiyo shem mbona siioni.”
MIMI: “Wewe njoo iko nje hapo.”
Jane aliinuka na mimi nikamfumba macho kwa nyuma tukasogea mpaka usawa wa gari na nikamwambia “open your eyes”.
“This is your gift shem from Mr.Pama.”
“Insider mbona sikuelewi that is my gift?.”
Muda huu Jane alikuwa kama kapagawa maana alikuwa kama haamini ile gari ni yake, muda huu pia yule dada mgeni pamoja na mama yake walitoka pale nje.
“Ndio Mzee Pama alikununulia hii gari muda mrefu sana hata kabla hujaanza udereva ila alitaka uanze kwanza kujua kuendesha ndo akupe.”
“Jamani! alijuaje naipenda Dualis?”
Muda huu Jane alianza kulia lakini yalikuwa ni yale machozi ya furaha na mimi nikamsogelea nikamkumbatia nikatoa kitambaa nikamfuta machozi.
Jane aliingia kwenye gari akaanza kuishangaa gari mle ndani na hakuishia hapo akazunguka pande zote za gari na muda huu mama yake alikuwa anatabasamu tu.
Jane aliizima gari na akashuka pale,
“Shem mpaka umeipamba kwaajili yangu, leo nafuraha sana, twende tukale kwanza maana nilikuwa nakusubiri wewe tu ili tule pamoja.”
Wakati tunapata lunch nilikuwa namwelezea Jane jinsi tulivyoandaa mpango na Mzee wa yeye kwenda mafunzo na mpaka gari inanunuliwa.
“Shem una Roho nzuri sana, naamini Mungu atakubariki kwenye maisha yako. Suala la gari nilikuwa sijui kabisa kama Pama alinunua.”
“Usijali shem nilikuwa nabuy time ili uwe Dereva mzuri ndo nikupe gari yako maana Mzee alisisitiza sana hili.”
“Hata hivyo nashukuru sana shem kwa yote, itabidi tukitoka hapa tuingie wote barabarani na hio gari.”
Baada ya kupata lunch nilitoka kukaa pale nje kibarazani nikimsubiri Jane atoke tuondoke. Muda huu nikasema acha nimjulie hali mama kijacho wangu Prisca, ili nipate taarifa zozote kuhusu huko kwao. Nilimpigia simu kama mara mbili hivi hakupokea nikaamua kuachana naye, na muda huu Jane alikuwa katoka tayari.
“Shem tuondoke niko tayari.”
Wakati nataka kufungua mlango wa gari simu yangu ilianza kuita kucheki alikuwa ni Prisca na mimi nikapokea simu yake muda huu,
“Nambie swirry ulikuwa wapi? Hupokei simu.”
“Baby Nilikuwa bafuni, hata hivyo kuna jambo nilitaka kukuambia badae, sababu umenipigia acha nikwambie tu now.”
“Jambo gani tena unataka kuniambia?”
“Babe! Baba amejua nina mimba maana mama amemwambia yaani amefoka sana na amesema anataka kuongea na wewe na anataka akufaham”
Nilishusha pumzi zito sana muda huu, ofcourse nilijua ni lazima hili suala litafikia huku na nilijua Mzee lazima amind na pia suala la ndoa litafuata. Maana haiwezekani umjaze mimba mtoto wa watu afu wakuchekee sio kwa utamaduni wa Africa na hakuna mzazi ambaye atakubali huu ujinga.
TO BE CONTINUED
TOMORROW
Suala la Prisca kama vile hakatambi lakini kanaweza kuleta tafrani sana! Huyu Iryn huyu, we ngojaHaka ka prisca kanatumia hisia enhee eti yupo tayari kukuzalia tena mxiiu
Halafu huyu Irene huyu atarudi kwako na machozi tupo hapa tunamzoom
Kigi Makasi njoo uone huku
Hizi episodes chache za mwisho na hata hii inaonesha kabisa Iryn alikuwa rafiki mnafiki...
Pamoja na kwamba amekusaidia sana, hata wewe pia umesaidia tena si kwa habari ya kazi tu bali hata kisaikolojia...
Ningelikuwa ni wewe katika stage hii aliyofikia, ningemchana live na kubwaga manyanga "kuresign"...
Hahaha...achana naye, Sema labda mpige Marry, au ukimshindwa Marry nipe mimi mkuu[emoji23][emoji23][emoji23]Mzee unataka Mzee aanze kunitokea usiku?
Nadhani cha moto alikionaga, halafu eti bado aliendelea kumchuna muajemi kwa hoja ya kumuunganishia iryn, ningekuwa muajemi hzo 10m kama alimpaga kweli angezitapika kupitia tundu lolote.Aiseeh!! Yaani hakuna Jambo Baya Kama mwanamke akianxa kukuchukia.
Ni hatari Sana, hasa mwanamke ambaye alikuwa anakupenda.
Anaweza kukuharibia ndani ya Dakika Tu. Mbaya zaidi ni kama uyo mwanamke atakuwa ni mtu unayemtegemea Kwenye hustle zako.
Ndo mana huwa sipendi mahusiano ya mapenzi mahali pa kazi.
Mbona story inazidi kunoga.......mwanamke akiwa anakuchukia +ana maokoto kukuendesha ni jambo dogo SanaEPISODE 54
CONTINUE
Baada ya kumaliza mazungumzo na Prisca niliingia kwa gari na tukaondoka na Jane ili nimuone kama ataweza kuiendesha Dualis. Nilimuelekeza vitu vidogo sana na nikamwachia gari aendeshe na tulikwenda mpaka Bahari Beach Hotel tukageuza.
Jane aliendesha gari vizuri kabisa na sikuwa nawasiwasi wa kumuachia gari. Kwa upande wake Jane aliomba nimuachie Ist aendelee itumia mpaka azoee mazingira ndo nitampa Dualis. Nilimkubalia ombi lake na mimi niliondoka na ile Dualis, hata alivyokomaa barabarani tulikuwa tuna badilishana magari akiimisi ist yangu nampelekea au anaifata ananiachia Dualis yake.
Muda tuliotumia ni kama lisaa mpaka tunarudi Mbweni kwake na baada ya kuachana naye pale nilimpigia simu Prisca na nikamwambia ajiandae tuonane ili tuongee hili suala. Suala la kwenda kwao kwa upande wangu niliona haliwezekani kabisa.
Saa 11 jioni nilikuwa nimeshawasili pale kwao na yeye alitoka tukaondoka kwenda Upepo garden.
Baada ya kuwasili pale tulitafuta angle nzuri tukakaa na mazungumzo yakaendelea.
PRISCA: “Babe nina hamu na wine kidogo.”
MIMI: “Tena usithubutu tutagombana sasa hivi, agiza kinywaji chochote kisichokuwa na kilevi.”
PRISCA: “Sawa babe.”
MIMI: “Bora umerudi kwa mama akupe elimu ya ujauzito. Niambie kinachoendelea kwanza huko nyumbani.”
Ilibidi muda huu nianze kumuuliza Prisca ni nini kinaendelea baada ya kurudi kwao akiwa mjamzito.
PRISCA: “Babe home hawana shida kabisa hata mama hajaonesha sign yoyote, ila ndo kama nilivyokwambia kuhusu baba ndo amekuwa mkali sana. Wazazi wanataka waongee na wewe kuhusu hili suala, Baba akirudi alisema nikupe taarifa muonane, babe wewe usiwe na wasiwasi wewe njoo tu.”
MIMI: “Huko kwenu siwezi kuja Prisca, wazazi wanataka kuniuliza kuhusu masuala ya ndoa wala sio kitu kingine. Unakumbuka nilishakwambia before? Haiwezekani nikujaze mimba afu wazazi waridhie uishi kama single mother.”
PRISCA: “Mimi ndo niliye ridhia hii mimba wewe njoo hata wadanganye ili mambo mengine yaendelee.”
MIMI: “Unajua sipendi kuongea uongo wala kutoa ahadi ambazo najua sitoweza kuzitimiza, kuwadanganya wazazi sio busara nitakuwa natafuta laana tu. Njia sahihi me naona wewe ukae kwanza chini na wazazi wako waambie ukweli kuhusu hio mimba.”
PRISCA: “Babe, sidhani kama hii ni good idea utafanya nichukiwe pale home kwa maamuzi yangu ya kipumbavu. Insider hata kama nimefanya maamuzi ya kijinga lakini isiwe sababu ya mimi kugombana na familia yangu. I know you are very smart ndomana hata mama alivyojua mimba ni yako hajaonesha sign yoyote ile, niseme mama yangu amekupenda. Ombi langu angalia namna gani ya kuongea na wazazi wangu, lengo tuwe na chemistry nzuri honey.”
MIMI: “Ni kweli but hili sio suala jepesi kama unavyolichukulia. Ningekuwa sina mke lingekuwa lishaisha muda mrefu sana, mzee wako anataka kusikia nina mipango gani na wewe bhasi. Kwanza Mzee wako anarudi lini?”
PRISCA: “I think next week, babe usiwe na wasiwasi na mimi sawa eeh!, na pia sifikirii kama nitakuja kuwa na mwanaume mwingine zaidi yako hata ukitaka mtoto mwingine nitakuwa tayari kukuzalia.”
MIMI: “Nipe muda nitafute njia nzuri ya kuongea na wazazi kuhusu hili jambo. Kwasasa home unaweza waambia nimesafiri niko mkoani.”
PRISCA: “Sawa honey, pia nampango wa kufungua biashara ya cosmetics ili nipunguze utegemezi pale home na kwako pia.”
MIMI: “Suala la biashara hata mimi nakuunga mkono, umewaza jambo zuri naf…..”
PRISCA: “Babe sorry da Mary anapiga embu nimsikilize anasema nini.”
Prisca alipokea simu ya Mary na nilikuwa nikisikia wanacho zungumza ilikuwa ni masuala ya kutoka out na baada ya kumaliza kuongea na simu tuliendelea na mazungumzo yetu,
MIMI: “Mary anasemaje?”
PRISCA: “Anataka twende Kidimbwi anasema anahamu ya kutoka leo, babe twende nikapunguze stress za mitihani.”
MIMI:”Mwambie Mary atangulie, sisi tutamkuta.”
PRISCA: “Ngoja nimtumie text hapa.”
MIMI: “Na vipi kuhusu hio plan yako ya biashara, una experince na hii biashara? Na mtaji ni kiasi gani?”
PRISCA: “Experience nitapata kwa mamdogo Ney, yeye ndo anafanya hii biashara, atanisaidia kwenye kupata mzigo na baadhi ya vitu. Kuhusu mtaji wewe usiwe na wasiwasi labda utanisaidia kidogo sana kama nitakwama.”
MIMI: “Kumbe umejipanga eeh!, na ulianza lini huu mpango?”
PRISCA: “Muda toka nijue nina ujauzito ilibidi nikae chini nifikiri kuhusu maisha.”
MIMI: “Good naona sahivi utoto umeisha kidogo umekuwa matured sasa.”
PRISCA: “Babe sipendi uchokozi wako ujue.”
Tuliongea mambo mengi sana muda huu hasa mipango ya kimaisha. Prisca alikuwa anakwenda kuwa mama mtoto wangu, hivyo ilibidi tupange mipango ya pamoja kwaajili ya mtoto na yeye.
Saa 2 tuliondoka maeneo haya na tulikwenda mpaka Kidimbwi kumeet na Mary maana alikuwa kafika muda sana akitusubiri.
Baada ya kuwasili pale tulikuta ameandaa sehemu tayari hivyo tulikaa na tukaagiza vinywaji.
MARY: “Prisca leo haturudi home tutakwenda kulala kwako nimeshaongea na mama tayari.”
PRISCA: “Funguo ziko home sasa.”
MARY: “Nimebeba.“
Na muda huu tuliishia kupigana jicho na Prisca.
Kwa upande mwingine Prisca aliniomba sana tukalale wote hii siku kule kwake na pia suala la kwenda na Mary bila mimi lingeleta maswali sana, maana Mary alikuwa hujui kama mimi sikai pale.
MIMI: “Mary nitakuacha ulale na Prisca afu mimi nitarudi home sawa?”
MARY: “Mimi nitalala seblen tu hata msiwe na wasiwasi.”
Baada ya kuona Mary amekaza ilibidi nikubali kwenda kulala na Prisca. Ukweli toka Prisca ahamie kwake nilikuwa nimelala mara 1 tu kipindi kile nimetoka msiba wa Pama. Nilijisikia hukumu moyoni na niliona anahaki ya kuwa pamoja na mimi kama Baba mtoto, ilibidi nimkubalie tutakwenda kulala wote.
Na muda huu ilibidi nimtumie text mama J nimwambie nimekwama bandarini kuna mzigo nafuatilia wa ofisi hivyo naweza chelewa kurudi na yeye alinijibu “Sawa takecare.”
Tulikaa pale mpaka saa 6 usiku ndo tukaondoka maana Prisca alikuwa hanywi so alikuwa amelala kwenye mapaja yangu muda wote na alionekana kuchoka sana.
Baada ya kufika kwa Prisca sisi tulikwenda kulala chumbani lakini Mary alilala pale seblen.
Muda huu ilibidi tutengeneze njia ya kupita mtoto na ilichukua kama lisaa hivi kukamilika. Baada ya hapo Prisca alilala lakini mimi sikuwa na usingizi kabisa, nilikuwa nawaza kule home kwa wife, machale yalikuwa yakinicheza sana.
Roho yangu ilikuwa na wasiwasi sana kwakweli hata sijui nilikuwa naogopa nini, kucheki muda ilikuwa saa 8 na madakika. Muda huu ilibidi nikaoge kwanza then nifanye harakati za kuwakimbia pale, maana niliwaza kutokulala home sio jambo nzuri, niliona ni bora kuchelewa kuliko kurudi asubuhi kwanza ni dharau kwa mama J.
Muda huu Prisca alikuwa amelala tayari yuko hoi, pale seblen Mary naye alikuwa naye kalala. Nilifungua mlango taratibu pamoja na kuufunga afu ufunguo nikautupia kwa dirishani na nikaondoka.
Baada ya kuwasili home niliingia ndani mara nyingi huwa natembea na funguo zangu. Wife baada ya kusikia nimefika aliamka pale kitandani na alikwenda kwanza washroom.
WIFE: “Baba J ulikuwa wapi? Usiku huu.”
MIMI: “Nilikuwa bandarini kama nilivyo kuambia muda ule.”
WIFE: “Mbona unakuwa muongo hivi? Nimewasiliana na Iryn amekataa hajakutuma huko bandarini.”
Nikajisemea leo kimenuka kumbe wife alipiga simu kwa Iryn hii ni hatari sasa. Muda ule namtumia text hata sikutegemea kama angemuuliza Iryn kuhusu hili jambo, ilibidi nijiongeze kama mwanaume.
MIMI: “Ipo hivi Jumanne kuna mzigo nilikwenda kuuchukua bandarini lakini nilichukua nusu tu sababu ya usafiri ambapo mwingine niliplan ningeuchukua jumatano lakini sikwenda kuufuata na hili Iryn hajui. Jana alinipa taarifa Jumatatu atafanya ukaguzi ndo nikaona nikaimalizie mzigo uliobaki maana angekuta hesabu haiko sawa asinge nielewa na angeniona mzembe.”
WIFE: “Una uhakika na unachoongea?”
MIMI: “Ndio mimi sikujua kama ungewasiliana na Iryn maana hajui hili na akijua atamind sana.”
WIFE: “Okay, Unanuka pombe hata hivyo.”
MIMI “Nilipitia sehemu kupunguza mawazo maana leo nimetapeliwa Million 3 swahiba, usinione hapa ninamawazo sana.” Nilibadilisha mada kijanja.
WIFE: “Ilikuwaje mpaka unatapeliwa pesa zote hizo?”
MIMI: “Acha tu kesho nitakuambia mke wangu tulale.”
Niliwaza pale kitandani Iryn ameshindwa kunifichia siri kaamua kunikataa kwa mama J lakini sikutaka kumlaumu sababu sijui mama J alimuingiaje. Muda huu niliwaza niandae mpango kabambe ambao nitakuwa ninakwenda kulala kwa Prisca bila shida yoyote.
********
Jumatatu asubuhi niliwasiliana na Gorata ili anipe ratiba zake na akanambia ataondoka na ndege ya saa 7 mchana. Baada ya kupata breakfast niliondoka kwenda Mikocheni na muda huu nilionana na Lucy na tukaanza story,
“Insider mbona sikuoni pamoja na Iryn mpo sawa kweli?”
“Yeah tuko sawa vipi kuna tatizo?”
“Mmhh hapana nimeuliza tu, ni muda sijawaona pamoja na Iryn naye kama hayuko sawa kama kuna kinachoendelea niambie.”
“Hapana Lucy mimi namuona Iryn yuko sawa mbona.”
Niliondoka pale Mikocheni baada ya kuona Lucy ameanza umbeya na nilimpigia simu Gorata akanambia nimpitie saloon. Baada ya kuwasili pale saloon niliingia ndani na nilimkuta yuko na Sumaiya akifanyiwa make-up.
“Insider natakiwa kucheck-in saa 5 nitawai kweli na sasa ni saa 3.”
“Mmh utawai tu kwani bado sana?”
“Sio sana ndani ya dakika 15 nitakuwa nimemaliza.”
Na muda huu Sumaiya alikuwa akiniangalia sana ni kama alikuwa anashangaa kuona nikiongea na Gorata. Sumaiya alikuwa kama anataka kuniuliza kitu lakini anasita sita, na mimi nilimsoma muda nika-amua kutoka nje.
Baada ya dakika 20 Gorata alikuwa amemaliza na tukaondoka kuelekea hotelini kuchukua mabag yake na tukaanza safari ya kwenda JNIA. Njiani Gorata alinipa mpango wa biashara zake ambazo anaplan ya kuja kuwekeza nchini na alisema kama mpango wake utafanikiwa bhasi tutafanya kazi pamoja. Kwa upande wangu sikuwa na pingamizi maana alikuwa na mpango mzuri sana, nilimwambia akiwa tayari anijulishe.
Baada ya kuwasili pale JNIA terminal 3 nilimpa kampani mpaka ndani ndo tukaagana pale.
“Insider next time tutakwenda kutalii wote Serengeti sawa?”
“Sawa dada yangu wewe niambie mapema ili niandae mazingira.” Na tuliishia kukumbatiana tukaagana.
Mimi baada ya kuachana na Gorata niliamua kwenda Changanyikeni kwa Prisca maana niliondoka katika mazingira sio mazuri. Sasa wakati niko pale mataa ya External Iryn alinipigia simu na mimi baada ya kuona ni yeye nilijua lazima litakuwa suala la wife.
“Hello bossy habari yako.”
“Insider mbona unafanya mambo kama sio matured? Hivi unaanzaje kuniingiza kwenye mambo yako?. Naomba tuwe na mipaka tafadhali sana, sitaki kugombana na mama J kisa ujinga wako.“
Iryn alikuwa kawaka sana afu alionekana kukasirika sana.
“Ok samahani lakini sio kama unavyofikiri mama J alikurupuka tu, sasa na wewe ulishindwa kunitetea?”
“Insider ulitaka nimjibu nini? Nimdanganye ili nilete matatizo? Umejaribu kuwaza kama ningekubali afu kumbe mpo wote angenionaje?, tafadhali sana tambua sijapenda ulichokifanya kitaniletea matatizo na mke wako kwa upumbavu wako.” Na akakata simu.
Niliwaza pale na kwa upande mwingine niliona Iryn kama yuko sawa lakini niliishia kumlaumu mama J kwa wivu wake wa kijinga. Kitendo cha urafiki wao kilianza kunipa maswali niliona kama nilikosea sana kuwaweka karibu.
Baada ya kufika pale home kwa Prisca niliwakuta wako seblen wanaangalia movie na mimi niliwasalimia pale, lakini wote walikuwa wakinitizama sana usoni.
MIMI: “Mtu na dada yake mnapendana sana kama mapacha.”
PRISCA: “Babe umeondoka muda gani leo asubuhi ?”
MARY: “Hata mimi nasubir jibu hapa sijasikia kabisa mtu akifungua mlango.”
MIMI: “Mnalala kama maiti haiwezekan nafungua geti Mary husikii, kidogo Prisca naweza mtetea maana alikuwa chumbani.”
PRISCA: “Da Mary ndo kawaida yake analala sana pia mvivu wa kuamka.”
MIMI: “Mmeshajiandaa lakini? maana nataka niwapeleke kwenu au mmeghairi?”
MARY: “Tunawahi nini? tutakwenda hata badae.”
PRISCA: “Mary kapike chakula bhasi.”
MARY: “Kwanini tusitoke kula lunch? Insider kaja na usafiri.”
MIMI: “Mary unapenda sana vyakula vya kudownload.”
PRISCA: “Ndo alivyo mvivu mvivu sana.”
MARY: “Sio mvivu mimi ndo mpishi wa pale home Sema kula vyakula vya home kila siku inakera, sometimes inabidi unachange ladha.”
MIMI: “Mary sio mvivu hata msibani nilimwona anachacharika, Mary kapike bhasi leo nionje mapishi yako huenda nikawaoa wote.”
MARY: “Insider twende jikoni unicompany.”
Wakati niko na Mary jikoni tukisaidiana kupika simu yangu ilianza kuita na ile kuangalia alikuwa ni Iryn akipiga tena na mimi nikapokea simu yake.
“Hello Bossy.”
“Insider hujanitumia ripoti za jumamosi na jumapili mpaka sasa kuna shida gani?”
“Ooh sorry nilisahau asee but ziko tayari.”
“Unaanzaje kusahau vitu muhimu kama hivi? Pia hujapeleka mzigo kule Posta napigiwa simu hapa.”
Iryn alionekana kukasirika kwa hili na mimi niliishia kunyamaza tu maana nilikosa cha kujibu na akakata simu. Kwa upande wangu niliona kweli nilizingua kutotuma ripoti na suala la kupeleka mzigo posta niliwaza kuupeleka baada ya kula lunch.
Baada ya kula lunch ya pamoja niliona bora nitoke niende Masaki nikachukue mzigo then nipeleke Posta. Posta kuna Saloon huwa tunashirikiana nao ni ya mama mmoja mhindi rafiki wa Mama Janeth ni kama partners hata sisi tukikwama huwa tunakwenda kuchukua mzigo kwao.
Wakati natoka Mary aliomba tuondoke wote ili nikamuache Mlimani City akatume hela na baada ya kuwasili maeneo yale niliamua kuingia ndani ili kumpa kampani.
Tuliachana pale na mimi nilikwenda Parking nilikopark gari ili niondoke lakini nilikumbuka sijalipia parking hivyo ikabidi nitoke nikalipie.
Baada ya kurudi nilikuta missed call ya Iryn alipiga tena simu maana niliiacha simu ndani ya gari,
“Huyu b*tch anataka nini tena muda huu?”
Na mimi niliamua kuipotezea ile simu yake, lakini wakati nageuza gari ili niondoke alipiga tena simu, ikabidi niipokee nimsikilize anataka nini muda huu.
“Yes Bossy.”
“Nakupigia simu hupokei.”
“Nilikuwa nimetingwa kidogo, nakutumia ripoti soon na mzigo nakwenda peleka now.”
“Kesho tuonane kwaajili ya suala la mkataba wako wa kazi.” Na alitoa sauti ya mtitizo sana tena yenye u-serious, na akakata simu.
Na mimi muda huu nilijua kibarua kishaota nyasi tayari. Kwanza Iryn kwenda kuchukua gari kwa mama Janeth ilinipa maswali kwamba hahitaji tena usafiri wangu. Pili, toka nifanye maendeleo yote ya kampuni kama kuweka zile Canvas na mapambo mengine pamoja na zile T-shirts hakuwai hata kunipongeza, ni mama Janeth pekee aliyenipigia simu na kunipongeza kwa lile jambo.
Muda huu niliwaza nimtafute mama wa2 anipe assist ya kazi maana alisema muda wowote nikiwa tayari nimjulishe.
TO BE CONTINUED.
20:00