Mkuu mnaposema nature ya mwanaume ni kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja mkae mkijua, ni sawa na kusema na mwanamke naye awe na mwanaume zaidi ya mmoja maana wanaume wanafanya ngono na hao hao wanawake hawafanyi na viumbe vingine, kwa sababu ratio ya population duniani kwa jinsia zote ni almost iko sawa ila wanaume wamezidi kidogo
So mnapotunga hivyo vitheory vyenu kuwa mwanaume ana tamaa hatosheki na mwanamke mmoja na kusingizia nature, mkumbuke kwamba hiyo hiyo nature imewasaliti kwenye upande wa population maana kama nature ingekuwa upande wenu, population ya wanawake ingetakiwa kuiacha mbali sana ya wanaume ili hiyo theory yenu iwe logical and applicable
Yani kama kila mwanaume atataka kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja basi automatically mnakuwa mnalazimisha na mwanamke naye awe na mwanaume zaidi ya mmoja, kitu ambacho huwa hamtaki kusikia wala kukubaliana nacho ilihali ndio uhalisia wenyewe huo yani kwa kifupi idadi ya watu wote duniani na hata nchi moja moja inawakataa na inapingana na hiyo theory yenu, hiyo asili inaweza kuwa imempatia mwanaume tamaa kubwa ila imesahau kumpatia na idadi kubwa ya wanawake wa kumtosha so jitafakarini