SEASON 2
CHAPTER 33:
โA TRUE STORY BY INSIDER MANโ
PREVIOUS:
Ghafla nikaona Jimmy kanyamaza na alikuwa akiangalia kitu nyuma yangu. Nilipogeuka, namuona Iryn amesimama, tumbo limekua kubwa, anangโaa sana na amekuwa mzuri maradufu. Sikuamini nachokiona muda huu ni kweli au naota? Nilisimama, tukaanza kuangaliana.
CONTINUE:
Sikutarajia, nilihisi kama niko ndotoni. Kumwona Iryn akiwa na tumbo kubwa namna hii kulinifanya nisite kwa muda. Bila kujishauri, nilisogeza miguu yangu karibu naye, nikamkumbatia kwa nguvu. Alinijibu kwa kunikumbatia pia, mikono yangu miwili ikapumzika kwenye mashavu yake, wakati yeye alizungusha mikono yake kiunoni mwangu. Kilikuwa kitendo kilichogusa hisia za kila mmoja aliyekuwepo pale. Ilikuwa kama kuangalia movie za kikorea;
MIMI: โBaby, nimekumiss sana. Siwezi kueleza furaha niliyo nayo kukuona ukiwa na mimba. Siamini, lakini ukweli ni kwamba nakwenda kuwa baba.โ
IRYN: โDo you remember what I told you before? I said that I would protect this child no matter what, and Iโm here now."
Na muda huu nilianza kulishika tumbo lake, halafu nilikuwa kwenye furaha ya ajabu sana;
MIMI: "Do you know I had lost hope of having a child?"
IRYN: "Donโt be, you're going to have a daughter."
MIMI: โWow, itโs a girl?"
IRYN: "Yes, darling. You know she can hear you, and she misses you so much."
Nilifurahi sana, na wakati wote huu tukiwa tumesimama, Jimmy alikuwa amekaa kimya akituangalia. Kisha tuliketi na kuanza maongezi.
Nilikuwa na maswali mengi sana ya kumuuliza ambayo nikihitaji majibu kutoka kwake na namna alivyoweza kunipata huku Dodoma. Jimmy aliondoka na akatuachia uwanja wa mazungumzo kati yangu na Iryn.
MIMI: โNilikukosea sana mumy naona msamaha kwa hili.โ
IRYN: โNi kweli ulinikosea na uliniacha kwenye kipindi kigumu sana ambacho nilihitaji sana ukaribu wako.โ
MIMI: โNaomba niambie ni nini kilichoendelea before?โ
Iryn alikaa vizuri na akaanza kunisimulia jinsi mambo yalivyokuwa;
Kipindi nilipokuja Dar es Salaam kuonana na wewe, lengo langu lilikuwa tukae tujadili mipango ya kumaliza hili jambo, bila kuleta mafarakano kwenye familia yangu. Nilikuwa na mpango mzuri sana ambao ungeweza kusaidia. Nadhani unakumbuka kilichotokea siku ile pale hoteliniโtulimaliza kwa kugombana na wewe kunipiga.
Ulinipiga pasipo kuwa na kosa lolote lile, ukaniita na malaya juu, ukweli niliumia sana, sikuwahi tegemea ipo siku utakuja kunitamkia maneno kama yale. Mbaya zaidi ulishindwa hata kuniomba msamaha tuyamalize, lakini ukawa hujali kabisa kuhusu mimi.
Baby, ulishindwa kutambua mimi ni mjamzito sometimes tabia zetu zinabadilika? Tangu tumeishi wote kuna siku ulishawahi kunishtukia nakucheat?. Niliridhia kuwa mwanamke wako wa pembeni tena kutoka moyoni, tambua wewe ni mwanaume ambaye nakupenda sana ndomana nimekupa huyo mtoto kama zawadi kwa yote unayonifanyia.
Nafikiri hutambui thamani uliyonayo kwangu, ndomana unanishushia heshima kwa kutembea na kina Asmah. Upendo nilionao kwako ni wadhati, nimekupa kampuni na mali zangu zote uziangalie sababu ninakuamini sana.
Baada ya kumaliza mitihani nilikupigia simu kukupa taarifa twende Ethiopia, lakini majibu uliyonipa yalinikatisha sana tamaa. Niliwaza sana, hivi huyu Insider ana akili kweli? nawezaje kuwaambia wazazi kwamba hii mimba ni ya mume wa mtu?, kwanza ni kitu ambacho hakiwezekani.
Hata kama usingeweza kwenda Ethiopia, bhasi nilitegemea unipe hata majibu ya kunitia moyo nione kweli tuko pamoja. Hii mimba sikubeba kwa reason zangu, nilibeba kwaajili yako ndomana unaona mpaka sasa ninayo na wewe ndiyo baba wa huyu mtoto.
Mambo yalianza kuwa magumu baada ya mama Janeth kupewa taarifa kuhusu ujauzito wangu na wewe ndo mhusika. Mama Janeth alimwambia mama mkubwa kwamba Insider kanipa mimba halafu anamke na mtoto. Familia baada ya kusikia haya maneno walikasirika sana na walinipigia simu kuniuliza kuhusu hili.
Nilibaki najiuliza ni nani kasema haya maneno? Ndiyo kufahamu mama Janeth katoa hii siri na hapa ndo kupatwa na hasira na nikampigia simu.
IRYN: โMama nakuheshimu sana, lakini naona unavuka mipaka, masuala ya mahusiano yangu wewe yanakuhusu nini?โ
MAโ JANETH: โWhat do you mean?โ
IRYN: โUlipaswa unipigie simu kuniuliza kuhusu huu ujauzito na sio kutoa maneno ya kuchonganisha kwa familia yangu, hapa umenikosea sana.โ
MAโ JANETH: โIryn ulifikiria nini kubeba mimba ya Insider na unajua fika ni mume wa mtu?โ
IRYN: โIlikuwaje na wewe ukazaa na baba yangu na unajua fika mama alikuwa ni rafiki yako?โ
MAโ JANETH: โIryn unaongea nini? Unakosa adabu sindio?โ
IRYN: โUlimzunguka mama na ukazaa na baba yangu unafikiri sijui kwamba Smith ni mdogo wangu? Kuna siku ulisikia nimetoa hizi taarifa? Sababu nakuheshimu kama mama yangu mdogo, lakini wewe unavuka mipaka.โ
MAโ JANETH: โCalm down nani kakupa hizi taarifa?โ
IRYN: โMimi ni mtu mzima, movement zako zote nazifahamu, unakuja South Africa na unakutana na baba kwa siri mnafanya yenu, au bado unanibishia?โ
Mama Janeth alikuwa mpole;
MAโ JANETH: โIryn naomba tuonane tuzungumze kuhusu hili, please.โ
IRYN: โSahivi ndo unataka tuzungumze? Kwanini hukutana kuzungumza na mimi baada ya kupata taarifa na ukaanza kuongea mambo ambayo mimi ndo nilipaswa kuongea?
MAโ JANETH: โIryn, I said calm down.โ
IRYN: โUmenitengezea mazingira magumu sana nyumbani. Pamoja na elimu na wadhifa ulionao, umeshindwa kufikiri hili? Ikiwa mimba hii ikipata matatizo, unadhani Insider atanichukuliaje? Najua unamchukia, lakini tambua kwamba ndiye mwanaume aliyeweza kuwa nami kwenye kipindi kigumu, na hata wewe unatambua hilo.โ
MAโ JANETH: โMaamuzi ya kuzaa na mme wa mtu hapa ndo umekosea kama binti yetu, tunajali future yako.โ
IRYN: โSasa ndio mnajali kuhusu mustakabali wangu? Mlikuwa wapi kabla? Naomba nisikilize kwa makini, sitaki kukuona tena ukiwa unafuatilia maisha yangu. Insider nampenda sana na hii mimba niliamua kuibeba kwa ajili yake, na nitazaa. Baadaye, nitamzalia watoto wengine. Tafadhali, kaa mbali na maisha yangu, huwezi kuamua mustakabali wangu.โ
MAโ JANETH: โIryn..,โ nikakata simu.
Mama Janeth alinipa maudhi sana, na hapa ndipo ugomvi wetu ulipoanzia na nilimpa taarifa Lucy kuhusu hili. Suala la kuanza kukuchukia lilikuwa wazi kwangu, nilikuwa naelewa kwa undani jinsi hali ilivyo.
Mama yangu mkubwa na familia kwa ujumla walichukia sana. Mama alinipigia simu na kunambia maneno makali sana, waliniona mimi ni malaya na sijitambui, kukubali kubeba mimba ya mume wa mtu.
Waliitisha kikao nyumbani wakati mimi nikiwa shuleni, nikiendelea na mitihani yangu. Unaweza kujiuliza kwanini walikuwa wanafanya haya yote. Sababu ni wosia alioundika mama kabla ya kifo chake. Pia, mila na desturi zetu ni kali sana, hasa kwa sisi wanawake.
Nilihitajika kwenda Ethiopia kuonana na familia baada ya kumaliza mitihani. Lakini kaka Jimmy alinitonya kwamba nisithubutu kwenda Ethiopia maana mtoto anaweza asiwe salama. Aliniambia maamuzi waliyo yachukua kwenye kikao ni kuwa natakiwa kutoa hii mimba, japo kulikuwa na mkanganyiko juu ya hili. Kaka Jimmy alinambia nifunge line nisipatikane kwa simu ili wakinitafuta wasinipate, huku yeye akiendelea kufuatilia kwa ukaribu kinachoendelea.
Kutokana na mambo uliyokuwa unayafanya, nilijikuta naanza kuwa na mawazo mabaya juu yako. Imagine nimeamua kupokea lawama kutoka nyumbani pamoja na kutishiwa, lakini niliamua niwe side yako.
Nilitafakari sana nikaona yanini kugombana na familia kisa mtoto? Halafu mwanaume mwenyewe haeleweki?. Sikuona umuhimu tena wa kuwa na mtoto na nikapanga niende Ufaransa kufanya abortion, ili niendelee kuwa na mahusinao mazuri na familia.
Nilimpigia simu Lucy kumtaarifu kuhusu hili pamoja na Jimmy na mipango yangu nikafanyie Ufaransa. Kaka Jimmy alinisihi sana nisifanye abortion, na kesho yake, jumamosi, alikuja South Africa kuzungumza na mimi kuhusu hili.
JIMMY: โSister sioni haja ya wewe kufanya abortion, kisa familia. Kumbuka huyo mtoto hana hatia na hatujui atakuja kuwa nani hapo baadae.โ
IRYN: โIโm really tired of this bullshit, ni heri nikafanya hivi. Unafikiri nikipata matatizo nitakimbilia wapi na Ethiopia ndiyo home?โ
JIMMY: โBaba mdogo umemshirikisha juu ya hili?.โ
IRYN: โBaba hawezi sema lolote juu ya hili, yeye anadai mimi ni mtu mzima tayari hawezi kunipangia cha kufanya, lakini kiuhalisia sidhani kama anafurahi kusikia mimi nina mimba ya mume wa mtu. Bora hata Insider angekuwa anaonesha kumtaka mtoto ndo kwanza hana habari juu ya hili, nigombane na familia, kisa insider.?โ
JIMMY: โWewe ulibeba hiyo mimba kwa interest zako kama unaona Insider hana habari, achana naye wewe zaa huyo mtoto. Badilisha namba za simu wasikupate kwa kipindi hiki mpaka utakapo jifungua, mimba ni kubwa tayari, umevumilia kipindi chote uje utoe leo?โ
IRYN: โNitazaa huyu mtoto, lakini itabidi nipostpone chuo ili kuepusha usumbufu.โ
JIMMY: โPostpone kwa muda mpaka pale mambo yatakapokuwa yako sawa, mimi nitaendelea kuliweka sawa hili suala kati yako na familia.โ
Kaka Jimmy ndo alifanya nighairi abortion na nilipanga kuzaa mtoto na kumlea mwenyewe kama tulivyokubaliana na kaka Jimmy. Niliandika barua ya kupostpone masomo sababu ya uzazi yangu na nikaatach online.
Jumapili tuliondoka kwenda Dubai kupumzisha akili. Nilikaa Dubai kwa wiki moja na nikaondoka kwenda Ufaransa, kaka Jimmy alirudi Ethiopia kuendelea na majukumu yake.
Mwezi uliopita nilipiga simu chuoni kuongea na academic supervisor wangu kuhusu masuala ya academic na akanitaarifu kwamba ulikuja kuniulizia;
MADAM: โKuna watu walikuja kukuulizia hapa chuo anaitwa Insider, alikuwa pamoja na dada yake. Walikuwa na wasiwasi huenda umepatwa na matatizo kwanini hupatikani kwa simu?โ
IRYN: โWalikuja lini madam.โ
MADAM: โWalikuja february mwishoni, ulifanya nao mawasiliano?โ
IRYN: โHapana mpaka sasa hatuna mawasiliano.โ
MADAM: โMtafute aliacha namba yake ya simu, kutoka Tanzania mpaka South Africa, wanaonesha wanakujali na kukupenda.โ
IRYN: โThank you madam.โ
Nilijiuliza pale, Insider alikuja South Africa akiwa na dada yake kwaajili ya kunitafuta na tulipishana kidogo tu. Kwa upande mwingine madam alirudisha memory yangu kuhusu wewe na nilijikuta naanza kukumisi tena.
Madam alinitumia namba yako na baada ya kukupigia haikuwa ikipatikana na nilikupigia sana bila mafanikio yoyote. Sikuwa na namba ya mtu yoyote pale ofisini maana nilibadili simu, pia sikutaka kuwa karibu na watu wanaokuzunguka. Nilifuta akaunti zangu zote mpaka social media ambako nilijua lazima utakuwa unanitafuta kwa bidii.
Kadri siku zinavyokwenda nilizidi kukumiss na nilitamani mtoto awe karibu yako, hata akisikia sauti yako. Kwa hiyo, nikapanga nirudi Dar es Salaam nikutafute.
Nilianza kupitia taarifa za kampuni na nikaziona ripoti zote, hadi barua yako ya kwenda likizo niliisoma. Niliipata ripoti kuhusu kukopa pesa kwa agent kwa sababu ya ukosefu wa pesa, na Hilda alielezea kwamba wewe ndo ulihusika.
Nilibaini umeacha kazi na kutopatikana kwako kulizidi kunichanganya, na nikajikuta nazidi kukumiss sana. Nilimshirikisha kaka Jimmy kuhusu hili, naye alikubali na kusema kwamba mimi nipange tarehe ya kurudi Dar es Salaam.
Nimerudi Dar es Salaam wiki iliyopita jumamosi, nikiwa na kaka Jimmy. Mara baada ya kufika, kitu cha kwanza nilikwenda moja kwa moja nyumbani kwako, lakini nikakutana na taarifa mbaya, umehama.
Nilienda Mikocheni kuonana na Lucy, naye akanambia hana mawasiliano na wewe toka march. Lucy alisema anakutafuta sana bila mafanikio na mbaya zaidi pale home umehama, hivyo anahisi huenda umehama na familia.
Nilienda kuonana na Sumaiya pamoja na Asmah, na hata wao walikuwa na wasiwasi kuhusu wewe kwa sababu hupatikani. Hadi hapo, nilijua sina ujanja tena maana hatukuwa na chaguo, pia nilipaniki sana. Niliongea na kaka Jimmy kuhusu hili, naye alisema tutulize akili kwanza, lazima tutakupata.
Jana asubuhi nilienda ofisini Masaki kwa mara ya kwanza, na nilipokelewa vizuri sana. Nilikaa na Hilda anielekeze jinsi kampuni iliweza kusurvive wakati mimi na mama hatupatikani. Hilda aliniambia hatua zote mlizozichukua hadi kampuni kuendelea kusimama mpaka sasa.
IRYN: โKwa hili mnastahili pongezi, nitaangalia namna ya kuwashika mkono.โ
HILDA: โKwani ulikuwa wapi? Tumekutafuta sana, hasa Insider kakutafuta sana kwa simu.โ
IRYN: โNilienda kupumzisha akili, lakini nimerudi na Insider hayupo, hadi amehama na sijui namtafuta wapi. Nimekuja Dar kwa ajili yake, na nimekumbuka sana. Niko kwenye kipindi ambacho namuhitaji sana kabla ya kujifungua.โ
Hilda alishusha pumzi zito na alionekana kama anajua kitu;
HILDA: โBossy naweza kukusaidia hili, suala la mimba limenigusa sana ukizingatia yeye ndiyo baba.โ
IRYN: โWhat do you mean?โ
HILDA: โInsider alinipa namba yake mpya ambayo anaitumia sasa na yuko Dodoma anafanya mambo yake. Amekuwa akinisaidia sana pale napokwama ofisini, ndiyo maana alinipa namba yake ili niwe nampigia simu. Japo alinipa masharti nisiiotoe kwa mtu mwingine na iwe siri sana, hata Lucy hajui hili.โ
IRYN: โPlease give me his number.โ
Nilimwambia Hilda akupigie simu ili nijihakikishie kama ni kweli na unapatikana. Hilda alipiga simu, na ukapokea, mkafanya maongezi ambapo uliulizia maendeleo ya kampuni na ukamuahidi kumtafuta ukirudi Dar mwishoni mwa mwezi huu.โ
Tulishauriana na Jimmy kuhusu hili, naye akashauri ni busara tukajaa Dodoma, kisha tukupigie simu.
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu, nilihisi uchungu sana kufahamu yale yote aliyopitia Iryn. Nilijuta kwa jinsi nilivyokuwa nimezembea katika kushughulikia hali hii. Lakini, nilipomuona tena, akiwa mjamzito, furaha isiyoelezeka ilinizidi.
Tulienda chumbani na tukaendelea na mazungumzo, tukijadili hasa mipango ya maisha kwa ujumla, maana Iryn alikuwa anatarajia kuwa mama. Alionyesha shauku ya kujua ninachofanya huku Dodoma, nami nilimueleza kwa undani, na akanipongeza kwa juhudi zangu. Muda huu wote wakati tunaongea nilikuwa nalichezea tumbo lake, naye alikuwa akifurahi na kuhisi raha kwa pamoja.
Sikuwa na uwezo wa kuondoka tena, hivyo ilibidi nilale hotelini na Iryn. Usiku, wakati wa dinner, Jimmy alituambia kuwa kesho ataondoka kurudi Ethiopia kuendelea na majukumu yake, akijua kuwa nipo, na hivyo Iryn yuko mikononi salama.
Baada ya dinner, Iryn alirudi chumbani kupumzika, wakati sisi tulielekea kwenye baa ya hoteli hiyo na kuendelea kupiga stori. Nilimshukuru sana kwa msaada wake, ambao umepelekea Iryn kuwa mjamzito na kufika hatua hii salama.
JIMMY: "Bro! Sisi ni wanaume, na kupendwa na mwanamke kama hivi ni bahati ya pekee. My sister anakupenda sana, na mimi siwezi kuingilia mahusiano yenu. Cha muhimu ni kwamba ana furaha, mambo mengine ni majaliwa."
MIMI: โBro, hilo usiwe na shaka, nitahakikisha anaendelea kuwa na furaha. Na kuhusu home, unaona mambo yatakaa sawa?"
JIMMY: โHili ondoa wasiwasi, maana mpaka sasa home hawajui Iryn aliko. Akijifungua, atakuja Ethiopia, na ni muhimu uwepo pia, maana kila kitu kwa sasa kipo wazi. Familia inajua kuwa Iryn ndiye aliamua kubeba mimba, hivyo wewe uje tu na usiwe na wasiwasi juu ya hili."
MIMI: โThis time lazima nije sitokuangusha.โ
JIMMY: โLife is too short bro! These women are here for us, if you have a chance, f*ck them.โ
MIMI: โHahahaa cheers bro.โ
Baada ya dakika 20, alikuja mrembo pale bar, alikuwa ni pisi kali kweli kweli, na Jimmy alinitambulisha akasema kwamba katokea Dar es Salaam. Nilishangaa sana kuona Jimmy akimlipia dada tiketi ya ndege kwa ajili ya kumla tu. Niliamua kuondoka na kuwaaga ili niwape nafasi ya kuongea, kisha nikarudi chumbani kwa Iryn maana alikuwa ameshaanza kunipigia simu.
Asubuhi Jimmy aliondoka kurudi Dar es salaam kwaajili ya safari yake ya kwenda Ethiopia na nilimpa kampani mpaka airport. Baada ya kuagana na Iryn, tulimwambia abaki apumzike, kisha tukaondoka akiwa na pisi yake.
Baada ya kurudi kutoka Airport, nilimwambia Iryn ajiandae ili tukatembee na lengo langu nimpeleke Iyumbu akaione miti yake. Kwa upande wake alikuwa na shauku sana ya kujua wapi nina mpeleka, lakini nilimwambia ni surprise.
Saa sita mchana, tuliondoka kuelekea Iyumbu. Tulipofika eneo la tukio, alifurahi sana alipomuona miti yake ikiwa mirefu zaidi kuliko yangu.
IRYN: โDarling ona miti yangu ilivyokuwa mikubwa kuzidi yako.โ
MIMI: โJamaa alikuwa anaihudumia sana miti yako kuliko yangu, sababu ulimuahidi zawadi.โ
IRYN: โMhh! Kwahiyo, hapa una plan gani?โ
MIMI: โNikipata hela nitajua chakufanya.โ
IRYN: โUkijenga apartment nzuri za kisasa itakuwa investment nzuri?โ
MIMI: โOfcourse ni investment nzuri sana but itahitaji pesa ndefu.โ
IRYN: โKama return ipo, pesa sio tatizo tutaongea kuhusu hili.โ
Kwa upande wake, alifurahi sana kuona miti yake ikiwa imestawi na kurefuka, na aliniambia nimtafute jamaa ili ampe zawadi yake kama alivyokuwa ameahidi. Baada ya kutoka hapo, tulirudi hotelini kwa sababu ya jua kali, ambalo lilikuwa likimletea tabu Iryn, hivyo niliona bora nimrudishe hotelini ili apumzike.
Jioni, Mary alinipigia simu, na kwa wakati huu, Iryn alikuwa amelala. Hivyo, nilitoka nje kwenye gari ili tuweze kuongea vizuri, maana nilikuwa nimempa taarifa mapema kuhusu ujio wa Iryn.
MIMI: โHello baby.โ
MARY: โYes honey I miss you.โ
MIMI: โMiss you too. Bado upo Mwanza?โ
MARY: โYeah! Nitarudi next week, nishamaliza mambo yangu.โ
MIMI: โVizuri sana, nafikiri tutaonana hio next week, nami naweza kuwa Dar.โ
MARY: โTangu Iryn arudi naona kama umepunguza upendo kwangu, Do you still love me?"
MIMI: โYes, I still love you, na sijabadili maamuzi ya kunizalia mtoto.โ
MARY: โI thought umeghairi baada ya Iryn kurudi na mimba yako.โ
MIMI: โNo! nahitaji na wewe unizalie mtoto kama tulivyoongea before.โ
MARY: โLet me think about it.โ
MIMI: โSawa bae, see you then.โ
Baada ya kuongea na Mary bado mipango yangu ya kumzalisha ilibaki palepale. Niliona Mary anajitambua sana, hivyo anastahili kunizalia mtoto na nilijisemea โkwahili siwezi fanya makosaโ.
Usiku tulienda Chako ni chako maana alikuwa anataka kuku choma na ndizi, hivyo nilimpeleka pale ili atimize haja yake. Tulianza maongezi pale, nami nilitaka kujua anaondoka lini Dodoma maana hali ya hewa sio nzuri kwa upande wake;
IRYN: โBaby niko na wewe mpaka nitakapo karibia kujifungua.โ
MIMI: โWhat? Bhasi rudi Dar es Salaam, kufikia weekend, mimi nitakuwa nimerudi tayari, usiendelee kukaa huku, hali ya hewa sio nzuri.โ
IRYN: โHuku unaishi wapi?โ
MIMI: โNimepanga baby.โ
IRYN: โTutaenda kukaa wote na tutarudi wote Dar es Salaam.โ
MIMI: โWewe tangulia baby mimi nitakukuta, ninajali afya yako.โ
IRYN: โWhy unaforce niondoke kuna mwanamke unaishi nae?โ
MIMI: โHapana mummy.โ
IRYN: โNimefanya maamuzi, mtoto anakuhitaji kipindi hiki chote mpaka najifungua unatakiwa uwe karibu.โ
Sikuwa na chakusema kwakweli ikabidi niwe mpole tu maana alikuwa hanielewi kabisa.
MIMI: โKwahiyo utaenda jifungulia wapi?โ
IRYN: โNingeenda kwa mama mkwe wangu, lakini hujataka nimjue, nitaenda South Africa.โ
MIMI: โHata mimi nilitaka nikushauri hivo baby.โ
IRYN: โTukirudi Dar itabidi twende Arusha kwa wifi yangu nikamjue.โ
MIMI: โSawa haina shida, yeye ndo aliyetoa wazo la kuja South Africa.โ
IRYN: โKwanza hukunambia ilikuwaje mpaka mkapata hili wazo la kuja South.โ
MIMI: โTukirudi hotelini nitakusimulia mkasa mzima.โ
Baada ya kurudi hotelini nilianza kumsimulia mkasa mzima namna nilivyoenda Arusha kuonana na Sister mpaka tunafanya maamuzi ya kwenda South.
Baada ya kumaliza kumsimulia, Iryn alionesha tabasamu na alisema ametokea kumpenda dada yangu hata kabla ya kumuona. Aliomba nimpigie simu ili aweze kuzungumza naye moja kwa moja, lakini nilimkatalia nikamwambia tumfanyie surprise, itapendeza zaidi.
Muda huu, tulipokuwa kitandani, nilikuwa busy nikimchezea tumbo lake, bado nilikuwa siamini kama kweli ni mtoto wa kike. Nilikuwa na shauku kubwa ya kupata mtoto wa kike kwa kipindi hiki.
IRYN: โBaby unatakiwa kutengeneza njia ya mtoto ili apite salama.โ
MIMI: โNaogopa nisije nikakuumiza.โ
IRYN: โYou have to, but do it slowly.โ
Ukweli nilikuwa nina hamu nae sana, ni muda mrefu ulikuwa umepita bila kuionja, alikuwa yuko wet tayari, hivyo nikaanza kuiweka taratibu, lakini joto nililokuwa nalifeel muda huu lilikuwa ni balaa. Tuliendelea na shughuli kwa muda mrefu sana maana hata yeye alikuwa anahamu sana na akienjoy. Kuna muda nilikuwa nampa muda wa kupumzika tena shughuli inaendelea mpaka alivyoridhika ndiyo tukalala.
*****
Jumatatu asubuhi baada ya kuamka tulianza kujiandaa ili tuondoke hotelini na tulipanga tuanze kwanza kupitia dukani. Josephine alikuja kutusaidia vitu na Iryn alimtambulisha kuwa mimi ndiyo mme wake na dada alibaki anashangaa maana hakuamini.
Tuliondoka hotelini saa 4 asubuhi na breki ya kwanza ilikuwa pale dukani, nilifanya utambulisho pale kwa dada. Hatukukaa sana tukaanza safari ya kwenda workshop, baada ya kufika, nilimtambulisha dogo shem wake, kisha nikaingia ndani kumsalimia Sanchi.
Sanchi alikuwa ofisini akifanya kazi zake, lakini alipoona sisi alibaki ameduwaa, akimtazama Iryn kwa mshangao. Bila kuchelewa, nilifanya utambulisho pale;
MIMI: โBaby, huyu anaitwa Sanchi ndiyo mmiliki wa kituo hiki cha mafuta, na ndiye kanipangisha hapa.โ
IRYN: โWaow! Congratulations.โ
Muda huu Sanchi alikuwa akitabasam tu, hajui hata aseme nini.โ
MIMI: โSanchi, huyu unaye muona mbele yako ni mke wangu anaitwa Iryn.โ
SANCHI: โIryn, karibu sana wifi yangu, jisikie huru.โ
Sanchi alionekana kutoamini macho yake, akihisi kama namdanganya. Hata baada ya kutoka ofisini, alikimbia haraka ili kuzungumza na mimi.
SANCHI: โInsider hivi ni kweli yule ni mke wako?โ
MIMI: โNdio huamini?โ
SANCHI: โUnajua siamini amini na Mary je?โ
MIMI: โNi mchepuko wangu, wewe si unaona hali yake unafikiri nyege zangu nazimalizia wapi?โ
SANCHI: โKhaaa! Wewe mwanaume ni kiboko una mwanamke mzuri sana. Nimetembea sana lakini huyu dada ni hatari, hata Mary yuko vizuri, lakini huyu ni funga kazi.โ
MIMI: โMtoto wa kihabeshi yule mixer uzungu chezea nini.โ
SANCHI: โYou have my respect, unakojolea pazuri sana. Mimi bado siamini ujue.โ
MIMI: โSawa, utamuona hapa ofisini wiki nzima mpaka tunaondoka kurudi Dar es Salaam na amekuja Dodoma kwaajili yangu.โ
Muda huu Iryn alitoka na akaanza kuangalia mazingira na akasogea mpaka usawa wetu akaanza kuongea na mimi;
IRYN: โBaby, this place is good, I love it.โ
MIMI: โTwende nikupeleke home ukampumzike mke wangu, hili jua la Dodoma halichelewi kuharibu uzuri wako.โ
Muda huu Sanchi alikuwa haamini na nilitoa mfukoni funguo za gari nikampa Iryn atangulie, nami nikaendelea kuongea na Sanchi. Kwa upande wake alinisifia sana kwa kuweza kumtia mimba mwanamke mzuri na nikamuaga.
Tulianza safari ya kwenda home na njiani nilipiga hesabu za haraka nikaona kuna haja ya kutafuta dada wa kazi ambaye atakuwa anamsaidia kazi, awe anakuja na kuondoka, lakini baada ya kumshirikisha alisema hakuna haja.
Baada ya kurudi home mazingira yalikuwa yametulia sana, hakukuwa na watu kabisa. Baada ya kuingia ndani, aliangalia mazingira yote kuanzia jikoni mpaka chumbani na akasema nikamnunulie ndizi, viazi, Magimbi, kuku na mahindi mabichi.
Niliondoka kwenda sokoni kununua hayo mahitaji bila kusahau zabibu maana alikuwa anazipenda sana. Stage aliyokuwa kafikia hakuwa na hamu ya kula vyakula vya kununua, hivyo alitamani awe anapika mwenyewe chakula anachopenda kula.
Tulipanga mipango ya kuondoka Dodoma na tukakubaliana Ijumaa turudi Dar es Salaam, halafu Arusha twende jumamosi. Pia, alisema anatamani sana twende kijijini Mondo, tulikoenda mwaka jana, ili akatoe misaada, hivyo tukapanga siku ya jumatano twende huko.
Kesho yake, saa saba mchana nikiwa ofisini, Iryn alinipigia simu. Aliniambia kwamba alikuwa amechoka kukaa nyumbani peke yake na alitaka kuja ofisini tushinde wote. Nilimtumia location, na ndani ya nusu saa, alikuwa tayari amefika. Nilimwongoza aende akae ofisini kwa Sanchi.
Iryn alitoka nje, na tukaanza kupiga story. Mada kubwa tuliyoijadili ilikuwa kuhusu mama Janeth. Nilimweleza kwamba tukirudi Dar, tunapaswa kufanya juhudi ili waonane na kumaliza tofauti zao. Nilimwambia hii ni fursa nzuri ya kumchimba mama na kujua ukweli kuhusu Smith. Kwa upande wake, Iryn alisema tayari anajua baadhi ya mambo kupitia baba yake, lakini alikubali kwamba ni muhimu kuhakikisha kila kitu kiko sawa.
Tulishinda pale ofisini na Iryn mpaka jioni, kwa upande mwingine alikuwa ni kivutio maana kila mtu alikuwa akimuangalia jinsi alivyobarikiwa kwa uzuri. Baada ya kurudi home tulianza kuandaa mipango ya safari ya kesho kwenda kijijini na alisema tutaanza kwanza kubadili fedha Bank, kisha tutaendelea na safari yetu.
Saa tatu asubuhi tuliondoka kuelekea Mondo, lakini tulianza kwanza kupitia bank. Baada ya kufanikiwa, tukaanza safari ya kwenda kijijini. Kwa upande mwingine, nilikuwa nimetoa taarifa kwa mtendaji asubuhi na mapema.
Baada ya kuwasili, tulikutana na mtendaji ambaye alifurahi sana kutuona. Alibaki akimshangaa Iryn, kwani hakutegemea kumuona akiwa mjamzito. Bila kupoteza muda, tuliomba kuonana na yule mzee mgonjwa ambaye alimsaidia mwaka jana.
Baada ya kufika pale kwake, tukaambiwa kwamba mzee ameenda mnadani kuuza kuku. Iryn alifurahi sana kusikia habari hiyo, kwani ilimhakikishia kwamba mzee ameshapona. Mtendaji aliagiza kijana akamwite mzee, na wakati tukisubiri, tuliendelea na maongezi. Iryn alionyesha nia kubwa ya kujua kama kuna watu wengine wenye shida ili aweze kuwasaidia.
Baada ya nusu saa, yule mzee alifika, lakini hakuweza kumtambua Iryn kwa sababu wakati alipokuwa anaumwa, hakuwa na fahamu. Mtendaji alimweleza kwamba hawa ndio waliomsaidia na kumpeleka hospitalini kipindi alipokuwa mgonjwa. Hapo ndipo alipoanza kutoa shukrani zake kwa dhati.
Mzee alionekana kanawiri vizuri na afya yake ilikuwa imerudi vyema. Tuliendelea na maongezi, na Iryn alitaka kujua zaidi kuhusu maisha yao kwa ujumla. Mzee alieleza kwamba wao ni wafugaji, na siku za minadani ndizo wanazotumia kuuza mifugo yao ili kupata pesa kwa mahitaji yao.
Kwa upande mwingine, chakula kilikuwa tayari, na kililetwa mpaka chini ya mti tulipokuwa tumekaa. Walikuwa wametuandalia ugali na mchemsho wa kuku. Ilikuwa kama walijua kwamba kwa kipindi hiki, Iryn anapenda sana kula mchemsho wa kuku. Tulianza kula pale kwa utulivu, tukifurahia chakula na mazungumzo.
Baada ya kumaliza kula, tulipaswa kuendelea na mizunguko mingine. Iryn alitoa pesa za kutosha na kumkabidhi mzee ili zimsaidie. Mzee alishukuru sana kwa ukarimu huo na, kwa shukrani, alikamata jogoo wawili wakubwa na kutupa kama zawadi. Tulipokea zawadi hiyo kwa furaha, kisha tukaaga na kuondoka kwenda maeneo mengine.
Mtendaji alianza kutuongoza kwenye zile kaya maskini, na Iryn aliendelea kuwasaidia wale waliokuwa na mahitaji. Baadaye, Iryn aliuliza kama kuna kikundi cha akina mama ambacho angeweza kusaidia pia.
Mtendaji aliwasiliana na viongozi wa kijiji, na mara moja walifika pale ofisini kwao. Akina mama wa vijijini wana umoja wa ajabu, kwani ndani ya muda mfupi walikusanyika kwa wingi, tayari kupokea msaada.
Mtendaji aliwaeleza akina mama kwamba lengo la kuwaita ni kwa sababu mfadhili, Iryn, ameomba kuwaona ili aweze kuwasaidia. Kiongozi wao alielezea kwamba kikundi chao kinajihusisha na kuwekeza pesa, kukopeshana, na kusaidiana wakati wa shida, kuhakikisha wanainuana kiuchumi na kijamii.
Iryn alianza kwa kuwapa elimu kuhusu fedha, ikiwemo jinsi ya kutumia pesa vizuri ili kupata faida. Baada ya mafunzo, aliwachangia milioni 5 kwa ajili ya kukuza kikundi chao. Aliwaambia kwamba mwakani atarudi tena kwa ajili ya kupata mrejesho kuhusu matumizi ya pesa na maendeleo ya kikundi.
Iryn alitoa pesa kutoka kwenye handbag yake na kumkabidhi kiongozi wao mbele ya mtendaji na viongozi wengine wa kijijini. Wamama walifurahi sana, na baadhi yao walitoka na kuleta zawadi za kuku, mayai ya kuku, na kanga kama ishara ya shukrani.
Iryn aliomba kupiga picha za ukumbusho na akina mama kama kumbukumbu ya tukio. Baada ya kumaliza mazungumzo na akina mama, tuliendelea kuongea na mtendaji pale ofisini kwake.
Muda ulikuwa umeenda sana, ilikuwa saa 10 jioni, hivyo tuliona ni bora tuondoke mapema na kurudi nyumbani, kwani Iryn alikuwa mchovu sana. Kabla ya kuondoka, alitoa pesa kutoka kwenye begi lake na kumkabidhi mtendaji kama shukrani kwa msaada wake.
Mtendaji alitusaidia kupanga vizuri zawadi tulizopewa. Mayai ya kuku pamoja na kanga yalijaa sado ya lita 4, huku kuku majogoo walikuwa jumla sita.
Tukiwa njiani kurudi Dodoma, Iryn alisema kesho tunapaswa kwenda kituo chochote cha yatima kilichopo Dodoma ili akatoe msaada. Aliniachia jukumu la kutafuta kituo cha kwenda na kupanga ziara hiyo.
Kabla ya kurudi nyumbani, nilianza kupitia dukani na kumpa dada zawadi ya kuku. Kisha, nikaenda workshop na kumpa Sanchi zawadi ya kuku pia. Zilibakia kuku wanne, na nikapata wazo la kumpelekea Maggy kuku mmoja. Kuku mmoja tutambakisha na wengine nitawagawa kwa majirani.
Muda wote tukiwa barabarani, tulikuwa tukizungumza sana na Iryn, na njiani kote alionekana kuwa na furaha kubwa.
MIMI: โMama kijacho wangu, naona unafuraha sana embu niambie siri.โ
IRYN: โLeo nimeenjoy sana ule ungali na soup ya kuku, the food was so delicious.โ
MIMI: โUnaongea kiswahili gani hicho? ni ugali sio ungali.โ
Akanipiga na ngumi ya kichokozi pajani,
IRYN: โTunaenda wapi? Naona tunapitiliza.โ
MIMI: โTunaenda kwa Maggy unamkumbuka?โ
IRYN: โWaow! Hivi Aggy yuko wapi? Naona unatumia gari yake halafu simuoni.โ
MIMI: โYuko likizo kaenda kwao kusalimia na kupumzisha akili.โ
IRYN: โNimewaza kwanini tusiende moja kwa moja Arusha?, sioni sababu ya kurudi Dar.โ
MIMI: โNi wazo zuri mummy.โ
Ndani ya muda mfupi tulifika kwa Maggy, ambaye alitukaribisha ndani kwa furaha. Alishangaa sana kumuona Iryn akiwa mjamzito, na walianza kuzungumza pale. Kwa upande wangu, nilimuaga Maggy kwamba Ijumaa nitakwenda Dar es Salaam kusalimia familia na nitarejea hivi karibuni.
Nilimpa zawadi ya kuku na aliomba nimsaidie kumchinja kabisa maana wao hawawezi wanaogopa. Nilifanya kama alivyotaka, na baada ya kumsaidia, tuliagana kwa kumbatiana. Pia, alimtakia Iryn ajifungue salama.
Baada ya kurudi home majirani walikuwa pale nje na tuliishia kuwasilimia na waliendelea kutushangaa. Iryn, hakuwa na noma kabisa, kwani alikuwa anapiga nao story freshy kabisa.
Kesho yake, tulikuwa na ratiba ya kwenda kituo cha kulelea watoto yatima. Tulianza kwa kupita sokoni, ambapo tulinunua 500 kg za mchele, 500 kg za unga, 100 kg za maharage, sabuni za kufulia, sabuni za kuogea, ndala, na vitu vingine vingi.
Saa sita mchana, tuliwasili kituoni kwa gari kubwa imesheheni vitu vingi, na walitupokea kwa mapokezi ya moyo mkunjufu. Tulipokutana na mkuu wa kituo, alituambia kuhusu matatizo yanayowakabili. Alieleza kuwa wanakabiliwa na upungufu wa vitanda, vyumba vya kulala, na kwamba baadhi ya wanafunzi wanakosa mavazi rasmi ya shule.
Iryn alionyesha dhamira yake ya dhati kwa kusema kwamba atachangia milioni 10 ili kusaidia kutatua changamoto hizi. Aliomba apewe akaunti namba ya kituo ili aweze kufanikisha muamala huo kwa urahisi.
Kwa tabia yake ya kipekee, Iryn huwa anarekodi kila kituo anachokitembelea kwenye diary yake, akihakikisha kwamba mhusika mkuu anasaini msaada aliopokea. Hii ni sehemu ya kumbukumbu zake muhimu, ikionyesha kujitolea kwake kwa kina na umakini katika kusaidia wengine.
Kwa upande mwingine, aliagiza cake kubwa kwa ajili ya kula na watoto wa pale. Bila kuchelewa odda iliagizwa, na ndani ya muda mfupi, cake hiyo ilifika pamoja na vinywaji.
Baada ya kula chakula cha mchana pamoja na watoto, Iryn alianza kugawa zawadi kwa wale wanaofanya vizuri darasani. Kisha, alianza kuuliza maswali, ambapo kila aliyejibu ipasavyo alipewa pesa. Ilikuwa ni siku nzuri sana, ambapo furaha ilitawala, na picha za pamoja zilikuwa moja ya kumbukumbu nzuri sana katika maisha.
Baadae, tulikata cake na kula pamoja na wahusika wote wa kituo. Tulifanya maombi kisha tukaondoka. Tukio hili lilimgusa kila mtu, si watoto pekee bali hadi wahusika wakuu, kwa sababu Iryn alifanya mambo makubwa sana. Iryn ana roho nzuri sana, hasa katika kusaidia watu, anajitoa kwa dhati na hana dharau kwa watu.
Baada ya kuondoka kituoni, nilimrudisha Iryn nyumbani ili apumzike. Kisha nikaenda dukani kumpa maelekezo dada kwa kuwa nilikuwa naondoka. Baada ya hapo, nikaenda kuonana na dogo pale workshop, nikampa maelekezo na kumuaga. Sikuwa na wasiwasi kuhusu vijana wangu, kwani walikuwa wanajituma kwa bidii na walikuwa vizuri sana.
Niliingia ofisini kwa Sanchi naye nilimuaga, pia nilimwomba awe ananisaidia kuangalia biashara yangu, kisha nikaondoka kurudi home kwaajili ya kupanga mipango ya safari ya kesho.
Baada ya kurudi nyumbani, niliwasiliana na sister kumtaarifu kwamba kesho nitakuwa Arusha. Baada ya hapo niliwasiliana na dada Tyna kumuulizia tickets, kwani nilikuwa nimempa taarifa mapema sana.
Kesho yake, Ijumaa asubuhi, tulianza safari yetu ya kuelekea Kilimanjaro. Saa sita mchana, tulifika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (JRO). Tulichukua private ya kutupeleka Arusha, ambapo tulifikia katika Hoteli ya Gran Melia.
Nilimpigia simu sister kumtaarifu niko Gran Melia hotel, hivyo nilimuomba aje hotelini;
SISTER: โBrother nilifikiri utakuja home umsalimie na shemeji yako maana ulimuahidi.โ
MIMI: โWewe njoo mara moja tuzungumze ndomana nimekuitia hapa.โ
SISTER: โKwanini umefikia hotel ya gharama sana, unapesa mingi kaka yangu.โ
MIMI: โPesa zinatafutwa dada yangu ukipata unazitumia, mimi nakusubiri hapa.โ
SISTER: โSawa haina shida nitakuja jioni hapo saa 12.โ
MIMI: โKaribu sana usiniangushe tu.โ
Mimi na mama kijacho wangu tulipumzika na muda huu tuliutumia vizuri katika kutengeneza njia ya mtoto. Iryn alikuwa makini sana kwenye hili suala kwani ilikuwa ni kazi ya kila siku.
Saa 12 jioni on time, sister aliwasili hotelini. Nilikuwa tayari nimeshuka kwenye lobi ya hoteli kumpokea, na kwa mbali nilimwona akiingia. Tulikumbatiana pale kisha tukaketi na kuanza maongezi.
SISTER: โNipe hayo madili unayopiga nami nikamate mahela.โ
MIMI: โHahahaa relax, ukitaka kulala hapa naweza kukulipia pia, tatizo ni shem hawezi kukuelewa.โ
SISTER: โNampigia simu namwambia leo tubadilishe sehemu ya kulala hahahaha.โ
MIMI: โWewe tu, mimi nimeshakupa offa tayari.โ
SISTER: โVipi biashara zako huko Dodoma natumaini zinakwenda vizuri kwasasa.โ
MIMI: โYeah! Namshukuru Mungu kwa hili, pesa yangu imeanza kurudi.โ
SISTER: โNambie umeniitia nini hapa, naamini kuna habari njema unataka kushare nami.โ
MIMI: โHabari njema ipo dada yangu wewe kuwa na subira mambo mazuri hayataki haraka.โ
Wakati tukiendelea na maongezi, nilimuona Iryn akija mahali tulipokuwa na alikuwa amependeza sana. Sister alimuona na alianza kumuangalia kwa makini, kwani alihisi kwamba ndiye Iryn. Iryn, baada ya kutufikia, alianza kumwangalia sister kwa umakini. Sister aliamua kusimama, na wakaanza kuangaliana kwa kimya, bila hata mmoja kuzungumza na mwingine.
TO BE CONTINUED