Kaka
INSIDER MAN
Kwa niaba ya wapenda/wafuatiliaji wa stori zako, nakuomba utuletee mwendelezo leo hii kama ulivyotuahidi. Kususa au kutokuileta stori kutawapa credit wapingaji wa hii stori.
Nakuomba sana ndugu yangu, historia inaonyesha hakuna kitu au mtu ambaye atakubalika na watu wote katika dunia hii, hata mitume ya Mungu ilipingwa hata Tanzania yetu sio raia wote wanaomkubali kuanzia Rais wa kwanza Mwl.Nyerere mpaka rais wa sasa Mh.Mama S.S.Hassan, hata nchi zilizoendelea pia ni hivyohivyo hakuna mtu atapendwa na jamii yote inayomzunguka wapo watakaomponda na kumpinga.
Hata Mungu mwenyewe aliyeumba binadamu na dunia wapo watu ambao wanapinga uwepo wake.
Kwahiyo ukiwa kama msomi wewe endelea na stori ili watu wajifunze kupitia stori yako.
Achana na wapingaji watatutoa kwenye reli.
Kwamfano huyu jamaa
2025DG analeta upinzani kwenye hii story halafu anasema "hajawahi kuwa na mashaka na story za
UMUGHAKA na
Analyse kwasababu stori zao zina uhalisia". Sipingani nae kwasababu ni mawazo yake hata mimi pia ni mmoja wa wapenzi na wafuatiliaji wa story za hao waandishi.
Lakini kiuhalisia hakuna storyteller yeyote humu Jf ambaye ameleta story yake halafu hajakutana na upinzani, hata hao aliowasema "hana mashaka nao" walitokea watu wakasema story zao ni chai na upinzani ulikuwa mkubwa lakini waliendelea na story mpaka mwisho na hii ndiyo sifa ya mwandishi kufikisha ujumbe aliokusudia kwa hadhira yake haijalishi itapokelewa vipi iwe chanya au hasi.
Kwahiyo hakuna story humu ambayo itaungwa mkono asilimia zote
Binafsi nawaheshimu storyteller wote ambao huacha muda wao na kazi zao kwaajili ya kutoa elimu,burudani,hamasa n.k kwa jamii hususani hapa JamiiForums.