Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Nimekuwa nikifuatilia story tokea episode one. Kuna kipindi na doubt kama ni fiction ila sasa INSIDER anakupa zile details za ndani mpaka unasema mtu hawezi kutunga. Kama hii episode ya mwisho alivyo describe the horizon, kuanzia games zilizokuwepo. Picha kwenye kile kidaraja na cost za kwenda kwenye island. Kwa ambao mmefika pale ni accurate kabisaa na ile cocktail yao ya nanasi. Yaani akiwa anaelezea outing zake the accuracy of the details za sehemu ni very impressive kusema jamaa ana tunga.

Shida yangu tu ndio Maana nasubiria conclusion ni huyu IRYN. From the story she seems as a well off woman. Ana hela sana and pia ana vyanzo vingi vya mapato kutoka kwa mama yake. Why afanye kazi ya massage? Bado it’s a job ambayo sio respectable kwa mtu mwenye hela vile asinge jihusisha nayo. She makes more from her mother’s business than hio kufuata watu massage. Pia hapo uliposema mtu analipa 1500$ for a massage bila happy ending kidogo kuna fikirisha. The value of amount mentioned ni very unrealistic. Tena for a British guy hapo kidogo umeongeza salt, nadhani huwajui waingereza wewe when it comes to spending. Pia ukaongezea swala la French account, yaani a UK resident awe na account ina a french bank na ikatokea tu as coincidence na Irene nayo anayo. Unajua procedure za kufungua akaunti nje ya nchi especially European countries, Iry sio resident wa France. Kama alisoma inakuwa ni temporary account and it expires the moment your student visa has exhausted.
 
Hila na mimi nimeshtuka! Hii story ni ya kutunga haina uhalisia wowote! Kwa watafutaji tunajua hela ni mgumu kuipata! Sasa huyu jamaa kwanza wateja wake ni 'ke' na wote wanahela na wanampenda! Dah! Na wanashobokea kigari aina ya ist eti kwasababu ni kisafi!! Mh? Utajiri wa iryn hauendani na maisha halisi yakupanga apartment za kushare wapangaji kibao! Angalia matanuzi sehemu za starehe! Bili ya watu wawili eti laki tano! 😄 🤣 😂 😆 n.k.
 
Hila na mimi nimeshtuka! Hii story ni ya kutunga haina uhalisia wowote! Kwa watafutaji tunajua hela ni mgumu kuipata! Sasa huyu jamaa kwanza wateja wake ni 'ke' na wote wanahela na wanampenda! Dah! Na wanashobokea kigari aina ya ist eti kwasababu ni kisafi!! Mh? Utajiri wa iryn hauendani na maisha halisi yakupanga apartment za kushare wapangaji kibao! Angalia matanuzi sehemu za starehe! Bili ya watu wawili eti laki tano! [emoji1] [emoji1787] [emoji23] [emoji38] n.k.
Kitendo cha iryn kutokuwa na gari na kupanga appartment za kushare wapangaji watatu nilianza kuwa na mashaka na stori.

Insider kiukweli ni dereva wa uber Ila nimekuja kugundua ni mpenzi wa bata.

Ndo maana imekuwa rahisi kutengeneza hii fiction.

Utajiri wa iryn hauendani na uhalisia wa maisha yake.

Yaani ninavyojua foreigners walivyokuwa wagumu kutoa Hela mtu from no where Anatoa hela anavyojisikia.
 
Nimekuwa nikifuatilia story tokea episode one. Kuna kipindi na doubt kama ni fiction ila sasa INSIDER anakupa zile details za ndani mpaka unasema mtu hawezi kutunga. Kama hii episode ya mwisho alivyo describe the horizon, kuanzia games zilizokuwepo. Picha kwenye kile kidaraja na cost za kwenda kwenye island. Kwa ambao mmefika pale ni accurate kabisaa na ile cocktail yao ya nanasi. Yaani akiwa anaelezea outing zake the accuracy of the details za sehemu ni very impressive kusema jamaa ana tunga.

Shida yangu tu ndio Maana nasubiria conclusion ni huyu IRYN. From the story she seems as a well off woman. Ana hela sana and pia ana vyanzo vingi vya mapato kutoka kwa mama yake. Why afanye kazi ya massage? Bado it’s a job ambayo sio respectable kwa mtu mwenye hela vile asinge jihusisha nayo. She makes more from her mother’s business than hio kufuata watu massage. Pia hapo uliposema mtu analipa 1500$ for a massage bila happy ending kidogo kuna fikirisha. The value of amount mentioned ni very unrealistic. Tena for a British guy hapo kidogo umeongeza salt, nadhani huwajui waingereza wewe when it comes to spending. Pia ukaongezea swala la French account, yaani a UK resident awe na account ina a french bank na ikatokea tu as coincidence na Irene nayo anayo. Unajua procedure za kufungua akaunti nje ya nchi especially European countries, Iry sio resident wa France. Kama alisoma inakuwa ni temporary account and it expires the moment your student visa has exhausted.
Akijibu hapa nitag.
 
EPISODE 19
“A TRUE STORY BY INSIDER”

Saa 4 usiku ndo muda ambao nilimrudisha mama wa2 kwake na alikua kalewa haswa, baada ya hapo na mimi nikirudi kwangu kulala ili asubuhi niwai kuamka na niwai safari yangu.

Jumapili nilikua na safari ya kwenda Dodoma na niliamka asubuhi mapema sana na nikajiandaa kuondoka kuelekea JNIA. Hii siku nilifanya kurequest Uber kwenda Airport na ndo ilikua mara yangu ya kwanza kupanda ndege.

Na muda huo asubuhi dada Tyna alikua amenipigia simu na kunikumbusha niwe on-time kufika pale.

Saa 07:30 nilikua nimeshawasili pale na muda huo Tyna alikua akinisubiri. Sababu alisema anataka tuongee kidogo na mimi. Nilifika pale Terminal 2 na tukaonana na Tyna,

MIMI: “Dada yangu nakuona”

TYNA: “Nambie mdogo wangu za toka ile siku.”

MIMI: “Salama, vipi umekesha leo Airport?”

TYNA: “Niliingia shift ya usiku ndo nimemaliza asubuhi hii.”

MIMI: “Aisee siwezi kuoa mwanamke anayelala nje usiku.”

TYNA: “Na mke wako akiajiliwa huku?”

MIMI: “Si namkataza tu, atachagua moja kati ya mimi au kazi.”

TYNA: “Kwanza hongera kwa kuoa, nilipata taarifa kutoka kwa dada yako Violet (Hili ni Jina halisi la Dada yangu)

MIMI: “Ndo hivyo nilimtia mimba mtoto wa watu ikabidi nijilipue tu.”

TYNA: “Ulifanya jambo jema sana, mwezi huu ujao nitakuja kuwasalimia pamoja na mtoto.”

MIMI: “Uje kweli, vipi kuhusu wewe lini tutakula pilau?”

TYNA: “Insider mimi bado niko sokoni, bidhaa haijapata mteja bado.”

Na muda huu TYNA alikua akicheka…

MIMI: “Usije ukawa unachagua wateja.”

TYNA: “Mdogo wangu sikuhizi wanaume mmekua washenzi sana, ukishampa ndo imetoka hiyo. Waoaji ni wachache sana kwasasa.”

MIMI: “Dada ana watoto wa2 tayari, unatambua hilo.”

TYNA: “Violet anabahati yeye ndo alikua wa kwanza kuolewa kwa wanawake tuliokua pamoja pale mtaani.”

MIMI: “So unaishi wapi kwa sasa?”

TYNA: “Nimepanga tabata segerea.”

MIMI: “Nitakuja kukusalimia siku ila itabidi uanze wewe kuja kwetu.”

TYNA: “Insider nimefurahi tumeonana na tumeongea ni muda sana, muda umefika now unaweza kucheck-in uondoke, uwe na safari njema mdogo wangu.”

Saa 6 mchana nilikua Dodoma tayari na nilifikia lodge moja ipo karibu na CBE. Nilimpa taarifa mzee Mollel kuwa nimefika tayari na kasema atakuja ndani ya nusu saa.

Wakati nimetulia mle lodge simu yangu ilianza kuita kucheki alikua ni Iryn. Nikaipokea simu yake,

IRYN: “Hi Insider”

MIMI: “Za wewe, now Unaendeleaje?”

IRYN: “Niko sawa now, vipi uko wapi? Nataka unipeleke kwa Mama Janeth.”

MIMI: “Sorry niko Dodoma nilipata emergence”

IRYN: “Toka lini?”

MIMI: “Sina hata saa toka niingie hapa.”

IRYN: “Mbona hukunambia kama unaondoka na umepatwa na matatizo?”

MIMI: “Nilipata taarifa jana na mzee wangu nije Dodoma kuna jambo la ku takecare hakuna matatizo.”

IRYN: “Sasa why hukunambia? Insider unaona mambo yako hunishirikishi inamaana bila kupiga simu usingenitafuta kabisa.

MIMI: “Jana nilikua busy na kazi nikasema nitakupigia lakini nilisahau naomba nisamehe Bossy wangu, nitakuletea zabibu kama zawadi.”

IRYN: “Ok no problem na unarudi lini?”

MIMI: “Kesho mchana nitakua huko, siwezi kukaa huku.”

IRYN: “Are you sure au upo kwenye mishe zako.?”

MIMI: “Trust me.”

IRYN: “Okay takecare, see you later.” Na akakata simu chap.

Mzee Mollel alinipigia simu na tukakutana pale CBE ambako alinipick na tukaelekea Makulu, tulisalimiana na pale ndo nikamkumbuka nilishwai kumwona kitambo sana akiwa na mzee. Pia kwenye gari alikua na vijana wa2 na akanitambulisha kama vijana wake.

Mzee Mollel alikua ni Engineer wa serikali kwenye moja ya Wizara hapa nchini.

Tulifika eneo la tukio na nikamwonesha kile kiwanja, na mzee Mollel alishangaa sana kuona namiliki kiwanya mitaa ile ya Oysterbay maana ni ngumu sana alisema.

Walipima na vijana wake na tulitumia kama 1hr kukagua eneo lile na kufanya vipimo vyao na tukaondoka pale. Mzee Mollel alinambia tunakwenda kwake nikapajue nile na lunch kabisa.

Tulifika kwake mapema tu na yeye anakaaa karibu na chuo cha Mipango ndo kajenga kule. Baada ya kufika pale nimsalimia mke wake na alinitambulisha kwa baadhi ya watoto wake ambao walikuwepo.

Tulipata lunch pale ya kibabe na tukakaa palepale dining kuendelea na maongezi ya ujenzi. Walipiga hesabu zao na tukapata gharama za kuanza ujenzi pamoja na ufundi, maana nilitaka wanipe kwanza gharama za kuanza msingi mpaka kupaua na kuweka grill na mageti.

Baada ya kumaliza na kupata figure halisi nilimwambia kesho ambayo jumatatu waanze ujenzi na mimi nikasema nitaacha kiasi cha pesa ili ujenzi uanze.

Sikuwa na wasiwasi kabisa na Mzee Mollel maana mzee wangu alinambia hana shida na anamuamini sana, wametoka mbali. Mzee mollel naye alinambia wale vijana wake watakua wanakwenda kusimamia kama yeye anakua busy hivyo kila kitu kitakwenda sawa kabisa.

Upande mwingine mzee Mollel alikataa kabisa malipo sababu alisema ananichukulia kama kijana wake na Mzee wangu wanasaidiana sana mambo yao. Ila mzee Mollel aliomba niwafikirie wale vijana wake ambao watakua wanakwenda kukagua na kuwasimamia mafundi.

Nilimkabidhi kiasi cha pesa ambacho kingesaidia katika kuanza ujenzi, maana nilibeba kiasi kikubwa cha pesa navyotoka home. Hata yeye hakuamini kama nimejipanga kuanza ujenzi kwa haraka vile na alinipongeza sana.

Muda huo ilikua kama saa 10 jioni tayari na niliaga pale naondoka akasema kesho vifaa vitaanza kushushwa pale, mambo ya vibali nimuachie yeye atatakecare. Nilimshukuru sana na yeye akanipa lift mpaka pale CBE.

Nilirudi Lodge na nilikua nimetulia na laptop yangu nikiset mipango kuhusu ujenzi pia nilikua nawaza namna ya kupata hela ili ujenzi uende haraka.

Baada ya kumaliza mambo yangu nikampigia simu best yangu mmoja ambaye tulisoma naye chuo na tulisoma faculty moja. Maana yeye akija Dar huwa ananitafuta hivyo sikuona sababu ya kutomtafuta.

Nilimpiga simu Aggy ambaye ndo best yangu na nikamwambia niko Dodoma na akanambia soon atakua around. Aggy ni mshikaji wangu sana toka chuo na mpaka sasa, na alibahatika kupata kazi kwenye taasisi ya serikali ambayo makao makuu yake yapo pale Dodoma, pale ni kama Mchumi.

Ndani ya muda mfupi alikuwa around na tukaenda kwake alikopanga na tulipiga story sana baada ya hapo tulikwenda “chako ni chako” kupata dinna.

Lengo langu kubwa ilikua ni kuomba awe ananisaidia kufanya ukaguzi kule site, nilitaka na mimi niwe na mtu wangu. Hivyo nilimwambia kilichonileta Dodoma na yeye hakuwa na shida alikubali na akanipongeza kwa hatua niliyoamua kuchukua.

Nilimwomba Aggy kesho kama anaweza tuweze kwenda pamoja site na akasema hiyo haina shida atatoka ofisini na tutakwenda.

Tuliagana pale na yeye akanidrop pale CBE na muda huo ulikua usiku tayari, wakati naelekea lodge niliyofikia simu yangu ilianza kuita na ile kucheki alikua ni dada yangu Violet.

MIMI: “Nambie dada yangu kipenzi.”

VIOLET: “Safi tu za wewe.”

MIMI: “Safi kabisa, nipe habari.”

VIOLET: “Ulikua na Tyna na leo?”

MIMI: “Yeah, anasemaje?”

VIOLET: “Kanambia ulikuwa unakwenda Dodoma, vipi unamishe gani huko?”

Dada nilikua sijamshirikisha mipango yangu hivyo ilibidi nimwambie maana sikuwa na sababu ya kumficha na yeye kwa upande wake alizifurahia zile habari.

Suala lingine dada yangu aliongea ni kuhusu mimi na Mama Junior hivyo alinishauri na aliniomba niyamalize mapema, mtoto kukaa ukweni bila sababu za maana sio vizuri. Nilimuahidi Dada nikirudi Dar nakwenda kulimaliza hili jambo nayeye alifurahi kusikia hivo.

++++++++++

Jumatatu nilikua nasafari ya kurudi Dar na ndege ya saa7 mchana na siku hiyo asubuhi saa 3 tulionana na Aggy.

Aggy alikuja kunichukua pale lodge na tulikwenda pale site na tulikuta vifaa vishaanza kununuliwa na mafundi walikua wakifanya setting. Niliweza kuwakuta wale vijana wa Mzee wakisimamia muda ule na mimi niliwasalimia tukaendelea na mazungumzo.

Saa 4 mzee alifika na tulisalimina naye na nikamtambulisha Aggy kwake na nikamwambia atakua anapita pita pale site, Mzee hakuwa na shida, bhasi tuliaga pale na mimi nikarudi lodge kujiandaa ile niondoke kurudi Dar.

Nilijiandaa haraka sana na na saa 6 kasoro nilitoka pale na kwenda Airport, Aggy alinipa kampani mpaka Airport. Tuliagana pale na yeye akasema anarudi ofisini kuendelea na majukumu yake ya kiofisi.

Saa 9 mchana nilikua tayari JNIA na ilibidi nifanye kurequest Uber tena kurudi kwangu na tulitumia saa1 kufika home.

Nilifika Home na muda ule plan zangu zilikua nikwenda moja kwa moja kwa Mama Junior. Na muda huu nilikua nikijuuliza kama naweza mkuta au laah, sikutaka mpigia simu nilitaka iwe saprise.

Nikawasiliana na mdogo wake akanambia Mama Junior yupo home, bhasi nikajiandaa vizuri nikatoka kwenda kwao.

Nilifika pale kwao na nikafungua geti, pale kwao palikuwaga kama home tu, baada ya kushuka nilimwona dada akiwa na Junior na nikampokea, wanasema damu ni nzito kuliko maji, Junior baada ya kuniona alinifurahia sana.

“Mama J yuko wapi?”

“Yuko ndani anasoma”

“Kwanini mliondoka bila kutoa taarifa?”

“Dada ndo alisema tuondoke mimi sikuwa na jinsi.”

Ukweli niliona dada hahusiki na haya hivyo ikabidi niingie ndani, nilimkuta seblen mamdogo wao tukasalimiana. Hii siku nyumba yao ilikua na utulivu sana na sio kama nilivyozoea.

Mamdogo alinambia niende tu chumbani maana kile ni chumba chake anakaa na dada wa kazi hivyo hakuna shida. Nikagonga hodi kwa kugonga na akasema “come in”, ofcourse hakujua ni mimi ambaye nagonga mlango.

Nilifungua na aligeuka kuangalia ni nani baada ya kuniona ndo mimi alijifanya hana habari na mimi. Na muda huo nilikua nimemshika Junior na ile simu mkononi ilikua kwenye mfuko.

MIMI: “Nambie mke wangu, nimekumiss san.”

MAMA J: “Umekuja kufanya nini hapa?”

MIMI: “Si nimekuja kukuchukua mke wangu pamoja na mtoto.”

MAMA J: “Alokwambia mimi nataka kurudi ni nani?”

Na muda huu alikua anajifanya yuko busy sana na kusoma.

MIMI: “Niliona umenipigia nikajua umenimiss.”

MAMA J: “Mpaka nikupigie ila wewe huwezi kupiga ukanijulia hali na mwanao?”

MIMI: “I did lakini hukuwa unapokea simu zangu.”

MAMA J: “Baba J mimi naomba uondoke tu, kwanza unanipotezea muda mimi na kazi hapa.”

MIMI: “Mimi nimekuja kukuomba msamaha na tuyajenge, yule mwanamke sio malaya wangu kama unavyodai. Naomba uwe mwelewa wewe si ulikuwa unasoma chats uliona kuna sehemu yoyote nimemtongoza?, yeye ndo ananitaka ila nothing happened.”

Mama Junior alikua kama anajifanya hanielewi na hana habari na mimi bhasi nikaenda kulock
Mlango. Nikamsogelea nikasimama nyuma yake na yeye alikua amekaa kwenye kiti, sababu najua maeneo ambayo ni dhaifu kwake na yakumyegeza bhasi nikamshika maeneo yaleyale.

Mama J alikua anajifanya kama hataki ila nilikua naona ni mtu anayependa ila anafanya kunikazia tu na alikua amevaa kibukta cha adidas kinachoishia mapajani kwa juu, kilinifanya nipate mzuka sana.

Kutokana na yale maneo kuendelea kumpa khashikhashi aliendelea kulegea na mwisho wa siku nikampa mdomo kwa nyuma hata hakugoma akanipa ulimi.

Na muda huu Junior alikua busy sana na kuchezea droo za makabati alikua na miezi 9 ndo anajifunza kusimama na alikuwa akisamia vitu.

Na kadri muda ulivyozidi kwenda nilijua Mama J anataka zaidi nikamtoa kwenye kiti na tukakaa kitandani tukaendelea kubadilishana lita za maji ya baraka. Sikutaka kufanya makosa kabisa maana nilikua hii ndo tiketi yangu ya kumu-win na kuyajenga.

Kilikua ni kitendo kilichotokea haraka sana hata dakika 15 hazikuzidi ila tulikua tushafika sayari ya Jupita na kurudi duniani. Na baada ya kumwaga asali ya moto ndo nilipata akili kwamba niko ukweni.

Muda huo Junior alikua hana habari kabisa na sisi yeye alikua busy na mambo yake.

Na muda huo mimi na mama J ilikua tumemaliza tofauti zetu kwa njia hiyo na nikamkabidhi simu yake ile zawadi niliyopewa na Iryn. Mama J alifurahi sana kumpa ile zawadi na mimi nikachukua simu yake Iphone Xs Max.

Tuliongea pale na nikamwomba arudi home na alikubali akasema weekend atarudi home. Nilimwuliza kuhusu masomo yake na akasema anaendelea vizuri, nikampa na story za Dodoma akafurahi sana kusikia nimeanza ujenzi.

Nilikaa pale mpaka jioni saa 1 na mama mkwe alirudi akanikuta, tukasalimiana na nikaaga.

Baada ya kutoka pale kwa Mama J nilimpigia simu Prisca ili tuonane na akasema yupo kwao niende tu kwao, Mama yake hayupo ameenda kwa sherehe.

Nilifika pale kwao na nilikaribishwa nikaingia ndani, nilimkuta Mary seblen nimamsalimia lakini alikua ni mtu ambaye kama ana chuki na mimi hata Prisca alitambua hilo.

Nikamwambia Prisca mimi sikai sana hivyo twende kibarazani tuongee, lengo langu kwenda kwa Prisca ilikua ni kumchana ukweli kuhusu suala la mahusiano kati yangu na yeye. Baada ya kufika pale kibarazani tulianza mazungumzo;

PRISCA: “Insider nini kinaendelea kati yako na Mary?”

MIMI: “Jana kanipigia sana simu afu sikumpokelea, atakua kachukia hicho.”

PRISCA: “Nilishakuambiaga dada Mary ana tu feelings na wewe anyway, nitaongea naye nijue kama kuna lingine.”

MIMI: “Ooh sawa, but naomba nikwambie jambo moja before its too late.”

PRISCA: “Nini unataka kunambia Insider?.”

MIMI: “Prisca mimi nina Mke na mtoto ujue?, ndomana unaona mara nyingi nakuignore sababu hio hivyo sitaki kuendeleaa kukuficha.”

PRISCA: “Insider what are you talking about?”

MIMI: “Hata hivyo kuna option mbili you can choose, kama tuendelee kuwa na mahusino ila ufate sheria nitakazokupa au tuendelee kuwa washikaji wa kawaida.”

Muda huu Prisca alibalika sana na alikuwa kama mtu ambaye haamini maneno ambayo alikuwa akiyasikia kutoka kwangu.

PRISCA: “And if kama sina choice hapo?”

MIMI: “Ni maamuzi yako mimi sitakuwa na shida, think about that mimi naondoka inabidi nirudi home mapema.”

Nilimwacha Prisca katika situation ambayo hajui ajibu nini na mimi nikapotea eneo lile.
Hapa umefanya vyema kumweleza Prisca ukweli wako, maana itakufanya kuwa huru!
 
Nimekuwa nikifuatilia story tokea episode one. Kuna kipindi na doubt kama ni fiction ila sasa INSIDER anakupa zile details za ndani mpaka unasema mtu hawezi kutunga. Kama hii episode ya mwisho alivyo describe the horizon, kuanzia games zilizokuwepo. Picha kwenye kile kidaraja na cost za kwenda kwenye island. Kwa ambao mmefika pale ni accurate kabisaa na ile cocktail yao ya nanasi. Yaani akiwa anaelezea outing zake the accuracy of the details za sehemu ni very impressive kusema jamaa ana tunga.

Shida yangu tu ndio Maana nasubiria conclusion ni huyu IRYN. From the story she seems as a well off woman. Ana hela sana and pia ana vyanzo vingi vya mapato kutoka kwa mama yake. Why afanye kazi ya massage? Bado it’s a job ambayo sio respectable kwa mtu mwenye hela vile asinge jihusisha nayo. She makes more from her mother’s business than hio kufuata watu massage. Pia hapo uliposema mtu analipa 1500$ for a massage bila happy ending kidogo kuna fikirisha. The value of amount mentioned ni very unrealistic. Tena for a British guy hapo kidogo umeongeza salt, nadhani huwajui waingereza wewe when it comes to spending. Pia ukaongezea swala la French account, yaani a UK resident awe na account ina a french bank na ikatokea tu as coincidence na Irene nayo anayo. Unajua procedure za kufungua akaunti nje ya nchi especially European countries, Iry sio resident wa France. Kama alisoma inakuwa ni temporary account and it expires the moment your student visa has exhausted.
Demu alitaka kubakwa kirahisi rahisi akaamua kumsamehe jamaa kwa kulipwa hela ambayo ni dollar 7500 sawa na million 18.

Mzee maisha hayako kirahisi kiivyo
 
Hila na mimi nimeshtuka! Hii story ni ya kutunga haina uhalisia wowote! Kwa watafutaji tunajua hela ni mgumu kuipata! Sasa huyu jamaa kwanza wateja wake ni 'ke' na wote wanahela na wanampenda! Dah! Na wanashobokea kigari aina ya ist eti kwasababu ni kisafi!! Mh? Utajiri wa iryn hauendani na maisha halisi yakupanga apartment za kushare wapangaji kibao! Angalia matanuzi sehemu za starehe! Bili ya watu wawili eti laki tano! [emoji1] [emoji1787] [emoji23] [emoji38] n.k.
Mkuu acha ushamba ficha ujinga huo,, Kuna apartments kibao masaki Huku nazifahamu kodi 1500-3000usd na Bdo mnaishi watu wengi na mnaonana vzuri tu
 
Mkuu acha ushamba ficha ujinga huo,, Kuna apartments kibao masaki Huku nazifahamu kodi 1500-3000usd na Bdo mnaishi watu wengi na mnaonana vzuri tu
Acha ujinga na wewe ndo waanze kusalmiana kama tandale
 
Si kweli yeye sio Yesu apendwe na kila mtu na mfululizo wa matukio yanavyoungana easily plus kila mtu kumuamini yamekosa uhalisia kwenye fiction yake
Bila shaka wewe sio mpenzi wa kusoma hadithi.
Hapo jamaa haandiki mambo yote yaliyomtokea, anaandika yale yanaoendana na story aliyoilenga tu.

Ni sawa na wewe uamue kuleta story kuhusu elimu yako, utagusia marq chache mambo ya famili coz story inahusu sana elimu.

Mpaka hapa jamaa kajitahidi, kama ni chai basi ina mpangilio mzuri.
 
Hila na mimi nimeshtuka! Hii story ni ya kutunga haina uhalisia wowote! Kwa watafutaji tunajua hela ni mgumu kuipata! Sasa huyu jamaa kwanza wateja wake ni 'ke' na wote wanahela na wanampenda! Dah! Na wanashobokea kigari aina ya ist eti kwasababu ni kisafi!! Mh? Utajiri wa iryn hauendani na maisha halisi yakupanga apartment za kushare wapangaji kibao! Angalia matanuzi sehemu za starehe! Bili ya watu wawili eti laki tano! [emoji1] [emoji1787] [emoji23] [emoji38] n.k.
Mbona alishaweka wazi anamteja ambaye ni me, anampelekaga kwa mchepuko na huyu mzee anampa san maisha mwana, pia ana mteja ambaye ni either waziri au mbunge mstaafu, pia kuna msomali, na wengine wengi, na kana umekuwa mfuatiliaji hapo mwanzo alitueleza sana kuhusu huyu mzee
Nashauri tusome story tuielewe kwanza ndiyo tutoe comments zetu,
Pia kuna mzungu yule alikuwa ni me, na hakuna mahali insider amesema kuwa wateja wake ni wa jinsia ya ke tuu, na pia hakuna mahali amesema anakutana na madem wakali tuu
 
Kitendo cha iryn kutokuwa na gari na kupanga appartment za kushare wapangaji watatu nilianza kuwa na mashaka na stori.

Insider kiukweli ni dereva wa uber Ila nimekuja kugundua ni mpenzi wa bata.

Ndo maana imekuwa rahisi kutengeneza hii fiction.

Utajiri wa iryn hauendani na uhalisia wa maisha yake.

Yaani ninavyojua foreigners walivyokuwa wagumu kutoa Hela mtu from no where Anatoa hela anavyojisikia.
Kwenye maisha kuna vipaumbele, ndg na siyo kila mtu kipaumbele chake ni gari, nahis Iryn hajataka kumiliki gari na pia anaipenda compNy ya insider maana anajua anapokiwa na insider anakuwa salama, hana hofu,
 
Nimekuwa nikifuatilia story tokea episode one. Kuna kipindi na doubt kama ni fiction ila sasa INSIDER anakupa zile details za ndani mpaka unasema mtu hawezi kutunga. Kama hii episode ya mwisho alivyo describe the horizon, kuanzia games zilizokuwepo. Picha kwenye kile kidaraja na cost za kwenda kwenye island. Kwa ambao mmefika pale ni accurate kabisaa na ile cocktail yao ya nanasi. Yaani akiwa anaelezea outing zake the accuracy of the details za sehemu ni very impressive kusema jamaa ana tunga.

Shida yangu tu ndio Maana nasubiria conclusion ni huyu IRYN. From the story she seems as a well off woman. Ana hela sana and pia ana vyanzo vingi vya mapato kutoka kwa mama yake. Why afanye kazi ya massage? Bado it’s a job ambayo sio respectable kwa mtu mwenye hela vile asinge jihusisha nayo. She makes more from her mother’s business than hio kufuata watu massage. Pia hapo uliposema mtu analipa 1500$ for a massage bila happy ending kidogo kuna fikirisha. The value of amount mentioned ni very unrealistic. Tena for a British guy hapo kidogo umeongeza salt, nadhani huwajui waingereza wewe when it comes to spending. Pia ukaongezea swala la French account, yaani a UK resident awe na account ina a french bank na ikatokea tu as coincidence na Irene nayo anayo. Unajua procedure za kufungua akaunti nje ya nchi especially European countries, Iry sio resident wa France. Kama alisoma inakuwa ni temporary account and it expires the moment your student visa has exhausted.
Ndio maana nasema kuna vingi vya kujifunza kwa watu smart kama wewe,hata kama una shaka,basi kwa point na maelezo mazuri kama haya.ngoja tusubiri ufafanuzi...

Katika maelezo yako kuna vitu vya msingi sana kuvijua.
 
Unaweza ukawa na billion na usiwe na Gari si.ndivyo
Alafu pia inatakiwa tujifunze kwa wenzetu waliofanikiwa na tusipende kuwa wakosoaji wa kila jambo kwa maana tuu maisha yetu ni duni au labda tumejaliwa kukutana na watu wanaomiliki kirikuu au boda au mtu ambaye anaingiza 200,000 kwa mwezi ukataka kumlinganisha na mtu anayeingiza 5,000,000 kwa mwezi, hapo lazima maisha na matumizi yatakuwa tifauti
 
Ndiyo kwani wapi imeanfikwa kuwa ukiwa na hela lazima umiliki gari au nyumba, hilo ni pendekezo la mtu binafsi na siyo lazima,
Bado ubongo wako.mzito.

Demu Ana appartmet ,saloon Kali,mirathi za maana,

Kutwa kuzunguka kwenye hoteli sijui kufanya massage.

Et analipwa dollar Elfu 10000.

Na hatoi uchi.

Anamlipainsider laki 3 kwa siku 3..

Hii story haina uhalisia hasa hapo kwa iryn sukari imekuwa nyingi.
 
Back
Top Bottom