Superficial
JF-Expert Member
- Nov 25, 2023
- 232
- 471
Hii script wakiipata nchi fulani basi kitu cha đ„
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamii forums wawauzie Dstv chini ya muongozaji Lamata. Then Insider awe na percent yake katika malipo.Hii script wakiipata nchi fulani basi kitu cha đ„
Lesson learnt:SEASON 02
EPISODE 25
âBY INSIDER MANâ
CONTINUE:
Kesho yake nilichelewa sana kuamka ni Junior ambaye alikuja kuniamsha chumbani kutokana na fujo zake na ile kuangalia muda ilikuwa ni saa 5 asubuhi.
Kwa upande mwingine mzee alikuwa kaningizia pesa ya Junior aliyokuwa ameahidi na alinitumia ujumbe niigawe na kwa mama yake. Sandra naye hakuwa mbali kunitumia message kuuuliza kama nimefika salama na palepale nilimjibu nimefika salama, nikaingia bafuni kuoga.
Kipindi najiandaa simu yangu ilianza kuita alikuwa ni baba mkwe, nilipokea ili nimsikilize, lakini nilijua lazima ni suala la plot. Baada ya maongezi ya muda mfupi tulikubaliana tukutane ili twende huko Mapinga mapema.
Muda mchache mbele niliondoka kuelekea ukweni, kumpitia baba mkwe na bila kuchelewa tulianza safari ya kwenda mapinga ilikuwa ni mbele kidogo ya Bunju. Mhusika mwenye plot muuzaji, alikuwa yupo tayari eneo la tukio akitusubiri, ambaye ni rafiki wa baba mkwe.
Plot ilikuwa nzuri sana, imepimwa tayari, ipo kwenye eneo zuri karibu na Barabara ya Bagamoyo na ina ukubwa wa sqm 1600. Nilipapenda na nikaomba kupewa bei elekezi, mhusika alisema naweza kulipa kwa awamu 4, lakini awamu ya kwanza lazima nilipie nusu ya gharama.
Tuliondoka kwenda kukaa moja ya bar pale Bunju mwisho kwaajili ya maongezi zaidi na tulikubaliana 23M nikafanya malipo nusu kabisa, sikuwa na wasiwasi wa kuita serikali za mtaa sababu biashara ni ya kindugu.
Kuhusu mkataba wa kuandikishana na kukabidhiana hati ya kiwanja, tulikubaliana kuwa mpaka nitakapomaliza kiasi kilichobaki, hati itakuwa chini ya uangalizi wa baba mkwe. Nilikuwa na imani kubwa na baba mkwe kwa kuwa ndiye msimamizi wa kila kitu, hivyo niliamini asingeweza kuniingiza chaka, na alinihakikishia uhakika wa 100%.
Kufikia saa 9 mchana tulikuwa tumemaliza kila kitu, hivyo tuliondoka kurudi home, kisha nikaanza kumshusha baba mkwe nyumbani kwake, lakini aliomba niingie ndani ili tufanye mazungumzo kidogo.
Kwa upande wake alinipongeza sana kwa hatua niliyoichukua na aliendelea kunishauri kwamba, kwenye ile plot nigawe nusu, kisha nijenge sehemu ya kuishi na nusu inayobaki nijenge nyumba za kupangisha. Nilitumia lisaa pale ukweni, kisha nikaanza safari ya kwenda Masaki kuonana na Hilda maana alikuwa ameshaanza kunipigia simu kwa fujo sana.
Niliwasiliana na Hilda tukutane Olive kwaajili ya maongezi na baada ya nusu saa alinipa taarifa kuwa amefika eneo la tukio tayari, hivyo ananisubiri mimi tu. Kwa upande wangu nilichelewa kama dakika 10 hivi kufika eneo la tukio, baada ya kuwasili tulisalimiana na tukaanza mazungumzo pale;
HILDA: âNambie Insider za huko Zambia, hope umeenjoy.â
MIMI: âNa enjoy wapi wakati umenitoa huko kwaajili yako.â
HILDA: âPole sana lakini mimi sielewi kabisa, nafikiri hata kuacha kazi, mmenisusia kampuni na sijui kinachoendelea, simu zenu wote hampatikani.â
MIMI: âPole sana mummy, ni kweli hatuko kwenye maelewano mazuri, lakini sioni sababu ya wewe kuacha kazi hasa kwenye kipindi hiki cha mpito.â
HILDA: âKampuni ikifeli si lawama zote zitakuja kwangu?, kuhusu suala lako la kwenda likizo si mama wala Iryn aliyenipigia simu na uliezea kuwa kampuni ipo kwenye mikono yangu.â
MIMI: âNajua unachopitia Hilda, nikutoe wasiwasi tuko pamoja na kila kitu kitakwenda sawa.â
HILDA: âKampuni haina cash nashindwa kufanya manunuzi madogo madogo, stock inaisha na hakuna taarifa yoyote kama mzigo umeagizwa au laah!, mama hapatikani kwa simu na nguvu ya kumpigia Iryn nakosa sababu hausiani na mimi ni wewe ndo wakuwasiliana nae.â
MIMI: âMama atakuwa field, nimeongea na Sumaiya na yeye ni muda mrefu hawajazungumza, si unajua kazi yake asilimia kubwa anashinda kwenye majanga?.â
HILDA: âHio ndo changamoto, sasa tunafanyaje?.â
MIMI: âStock imebaki kiasi gani? na account Receivable inasomaje?.â
HILDA: âStock iliyobaki asilimia kubwa ni zile product expensive ila kwa bei za kawaida sidhani kama itaweza kufika week 2 na itadepend na volume ya wateja.â
MIMI: âSawa sasa nisikilize, kuanzia leo ukifanya mauzo ya cash usiweke bank ili hizo pesa zisaidie kurun office, kingine wahimize customers walipe kwa cash ili iwe advantage kwetu.â
HILDA: âHow naweza kumwambia mteja asilipe bank na amezoea kutransfer moja kwa moja kwa account?â
MIMI: âNi simple tu, customers huwa wanapiga simu kufanya booking, kwahiyo palepale mwambie tuna accept na cash pia, inaweza kufanya kazi na kutusaidia.â
HILDA: âVipi na kuhusu stock?â
MIMI: âHuko tutafika bado sijamaliza, hujanijibu kuhusu madeni tunayodai kwasasa ni kiasi gani? Ambayo wewe umeyaandikia.â
HILDA: âNi kama million 3 na something hivi.â
MIMI: âKipindi nakukabidhi office receivables zilikuwa 67M nikijumlisha na hio ni 70M, Kampuni X na Y zimelipa tayari na mara ya mwisho kuangalia deni, limepungua mpaka 24M pamoja na deni lako. Sasa hawa waliobaki mimi nitaongea nao ili walipe kwa cash, hatuwezi kushindwa hili jambo.â
HILDA: âVipi kuhusu stock?, ikiisha hatutaweza kuendelea na kazi, na mishahara itakuwaje? Mwezi uliopita ilichelewa.â
MIMI: âKuhusu mishahara kama mambo bado hayaeleweki, nitaangalia means ya kufanya hata cash naweza kuwalipa. Kuhusu stock niachie hili nilifanyie kazi na nitakupa majibu soon, acha niwasiliane na dada agent huenda anamzigo.â
HILDA: âMmh sawa, lakini nikiangalia interval ya mzigo wa mwisho kuupokea na sasa, naona kama hakuna taarifa yoyote, angekuwa amekupigia simu.â
MIMI: âUpo sahihi, lakini tutajua tunafanyaje ndomana nimekwambia hili niachie mimi.â
HILDA: âSawa Insider nimefurahi kukuona.â
MIMI: âMimi pia, naomba tusaidiane hili jambo hii kampuni isifie kwenye mikono yetu.â
Hilda aliishia kufurahi pale sababu nilikuwa nina ratiba zingine ilibidi nimuage lengo niwahi kwa Lucy, tuliongozana mpaka parking tukaagana kwa kumbatiana, kisha nikaondoka kuelekea Mikocheni.
Nilikuwa na ratiba ya kuonana na Lucy tangu asubuhi, ratiba ziliingiliana wakati niko njiani Lucy alipiga simu na kuuliza niliko na alihimiza nifanye haraka tukaongee kuna jambo.
Baada ya lisaa niliingia kwa kuchelewa sana pale ofisini sababu ya foleni na wakati nikishuka kwa gari, nilimuona Lucy anakuja usawa wangu na alikumbatia kwa nguvu sana, nilihisi akilia;
MIMI: âLucy mbona unalia kuna shida gani?.â
LUCY: âInsider nimeongea na Iryn sio muda mrefu sana, amefanya maamuzi ya kufanya abortion.â
MIMI: âNini? Sikuelewi amefanya au bado?â
LUCY: âBado sijui kama amefanya au laah! anasema ameshindwa kabisa kuhandle upinzani anaoupata kutoka kwa familia yake, na wewe pia hueleweki kama upo upande wake na hili ndo linampa wasiwasi, kitu kingine alikupa masharti ya mtoto, lakini umeshindwa kuyafuata na umetembea na Asmah.â
MIMI: âAmekutafuta kwa namba ipi?â
LUCY: âNimeongea sana na namba yake, nikijaribu kukuombea msamaha, lakini amenigomea. Anasema hawezi kurudisha tena imani yake kwako, hasa baada ya kutarajia kuwa mngekuwa pamoja katika kipindi hiki cha upinzani anachopitia. Lakini wewe umekuwa ukimpa majibu mepesi, ukionesha wazi huna mpango naye tena pamoja na mtoto, hata kama alifanya kwa reason zake. Insider, nimelia sana na nakuonea huruma mshikaji wangu. Sitaki kuamini kwa kipindi chote mlipokuwa na Iryn, mambo yanamalizika kwa njia mbaya hivi. Nimemwambia kuwa, kama atathubutu kufanya ujinga huu, nitaacha kazi."
MIMI: âJimmy alinambia Iryn anamaamuzi magumu sana na mpaka amesema hivo jua kweli kadhamiria, na huwa habadili mawazo yake, uzuri unamjua ni mtu wa aina gani, ooh shit.â
LUCY: âHapana embu mpigie before itâs too late, jaribu kuongea nae muda unaenda.â
Nilitoa simu ili nimpigie na nikakutana na ujumbe kutoka kwake ambao umetumwa dakika 5 zilizopita na ulisomeka;
âHello Insider, itâs been a while. I hope youâre doing well. I want to tell you that I donât hate you. Please know that youâre the most important man Iâve ever met in this world. I truly appreciate your contribution and everything you have done in my life.
Please understand that I am currently going through a very difficult time due to this pregnancy, especially when it comes to my siblings. All of them have been against me, and even worse, you, who I relied on to be close to me during this period, have distanced yourself from me.
I have chosen the side of my family because I donât see any future with you, and you have shown no intention of wanting this child. I donât like doing this, but I also want to avoid the problems that might arise later, especially for your family. I carried this pregnancy for my own reasons, and I am choosing to end it for my own reasons.
I am truly sorry for this and wish you all the best.â
Nilihisi kuishiwa nguvu na niliegemea kwenye gari hata sikujua nafanya nini muda huu na chozi lilianza kunitoka.
Wanasemaga mwanaume hatakiwi kutoa chozi, nikwambie unakuwa bado hujaingia kwenye 18, nilifungua mlango wa gari kwa haraka sana nikaingia ndani, kisha niliwasha gari kuondoka eneo hili.
Lucy alianza kuniita na kunigongea dirishani;
âInsider nini kinaendelea? Mbona umebadilika ghafla sana?â
Sikuwa hata nikimsikia Lucy, zaidi nilianza kuondosha gari na kumwacha kwenye mataa bila kujua afanye nini kwa wakati huu.
Haikukuchukua muda nilisikia simu ikiita, lakini sikuwa na habari nayo na niliendesha gari nikaja kuipark mbele kidogo ya shule ya Alpha, kama unaelekea Cocacola road, kuna maduka pale pamechangamka sana.
Nilipark gari maeneo haya nikatulia maana sikuwa najielewa huku nikihisi mwili kufa ganzi, machozi mazito yalikuwa yametanda kwenye mboni zangu. Nilikuwa kwenye dimbwi zito la mawazo, nilijiona ni mwanaume ambaye sina bahati, maisha yangu ni kama yamejaa na mikosi, ukizingatia nakwenda kumkosa mtoto kwa mara ya tatu.
Niliwaza mbali sana, nikajisemea âau Mungu ananiadhibu kwa kuchepuka?â Ni mtoto wa tatu sasa kwa jumla namkosa, before Prisca na Iryn, huko nyuma kuna tukio lingine lilitokea.
Nilichukua simu yangu nikaona calls kutoka kwa Lucy, ndo alikuwa akinipigia muda ule na nilitafuta namba ya Iryn, kisha nikafungua whatsapp ili nimpigie, lakini namba ilikuwa deactivated na normal call hapatikani.
Nilikuwa katika wakati ambao sijui nifanye nini maana nilikuwa dilemma, niliwaza nimpigie simu mama Janeth nimuombe anisaidie hili, nikakumbuka nae hapatikani.
Muda huu wazo lilinijia niende kwa sister yangu Arusha, nikamwambie kuhusu hili suala, kumpigia simu na kumwelekeza isingetosha, niliona sinabudi kwenda huko na nilimpigia simu palepale kumpa taarifa.
SISTER: âNambie kaka yangu unaendeleaje.â
MIMI: âDada niko njiani nakuja Arusha, nina maongezi na wewe muhimu.â
SISTER: âMdogo wangu si nilikwambia nikipata likizo ndo uje au umesahau?â
MIMI: âDada ni muhimu sana haya maongezi, tafadhali.â
SISTER: âKuna nini kinaendelea mdogo wangu? Umeshagombana na mama J?â
MIMI: âDada naomba nielewe, nikifika huko utaelewa ni nini nataka kukwambia.â
SISTER: âSawa karibu, utakuwa unaniambia safari ilipofikia, pole sana.â
Nilijifuta machozi yangu vizuri, kisha nikaondoka kurudi home kwaajili ya kuchukua vitu na kuanza safari ya kwenda Arusha. Nikiwa njiani nilimpigia simu dada Tyna kumuomba kama nitaweza kupata ticket ya kwenda Arusha, akanambia haiwezekani labda kwa kesho asubuhi.
Niliona kwa asubuhi ni mbali sana wacha niondoke hata kwa kuunga cha msingi nifike Arusha. Nilirudi home, kisha niliingia ndani kwa spidi sana, akina wife walikuwa pale seblen hata sikuwasalimia maana nilikuwa na spidi ya hatari.
Wife alikuja chumbani na alinikuta ninaweka nguo kwenye bag kwaajili ya kuondoka na alianza kuniuliza pale;
âBaba J, una safari ya wapi tena?â
âNakwenda Arusha mara moja kuonana na sister.â
âAre you okay? Mbona kama macho mekundu ulikuwa unalia? Kuna nini kimekupata?â
âNothing, mummy usiwe na wasiwasi na mimi.â
âJana tu! Umerudi kutoka Zambia kwanini usingesubiri hata kidogo ukaenda huko siku nyingine?â
âNi muhimu sana ndomana nakwenda sitakawia kurudi.â
âKuna jambo gani huko?.â
âNi masuala ya kifamilia, nikirudi nitakwambia.â
âMhhh! Sawa.â
Wife alikubali kwa shingo upande nami niliendelea kupanga vitu vyangu kwa haraka sana. Kwenye bag nilikuwa nina balance ya $1,800 ambazo zilibaki kutoka Zambia na nilitembea na cash Tsh 500,000.
Nilichukua bodaboda kwenda Tegeta-Kibo kutafuta gari za kwenda Arusha na ile nafika nabahatika kupata gari ya kwenda Moshi. Saa mbili usiku tulianza safari ya kwenda Moshi na njiani nilikuwa ni mtu mwenye mawazo sana, nilikuwa natamani hata gari ipae ili tu! nifike mapema.
Saa 8 za usiku tuliwasili Kilimanjaro, nikabahatika kupata gari ya tour inayoenda Arusha, sikutaka kabisa kumsumbua sister maana ni mke wa mtu, hivyo niliplan kumpigia simu asubuhi.
Ulikuwa ni mwendo wa lisaa mpaka tunafika Arusha na jamaa alisema anaishia USA river, kutokana na mimi kuwa mgeni alinipeleka kwenye moja ya lodge ili nilale.
Kufika pale reception naambiwa room zipo ila sasa gharama zake ni za ajabu room ni elfu 90, nilishangaa sana, kwa lodge unalipia elfu 90? Ukizingatia nina masaa yasiyozidi 5 kulala. Muda ulikuwa umeenda sana, hata jeuri ya kutafuta lodge zingine sikuwa nayo afu ni mgeni na maeneo ya huku, kwanza niliogopa vibaka maana Arusha ina scandal nyingi sana.
Nilitoa pesa nikalipia na dada pale reception alianza kujichekesha chekesha, lakini mimi sikuwa hata na habari nae zaidi nilikuwa na mawazo kichwani. Nilioneshwa room yangu na kabla ya kulala nilimpa taarifa sister, kuwa nimefikia salama na nipo lodge ya Mzunguu, USA River.
Niliamka saa 2 asubuhi na kabla ya yote nilicheki simu kuangalia kama dada amenipigia maana simu ilikuwa silent. Baada ya kuangalia nilikuta kweli amenipigia mara 2 na alinitumia ujumbe kunambia nikiamka nimpigie. Kwa upande mwingine mama J nae alikuwa amenipigia simu za kutosha na kutuma message juu, kuuliza kama nimefika salama.
Nilianza kwa kumpigia simu sister, akasema yupo ofisini anaweka mambo sawa, atakuja saa 3 kunichukua lodge. Kisha nilimpigia simu wife, lakini hakupokea na nikamtumia ujumbe kumjulisha nimefika salama Arusha.
Niliingia bafuni kuoga kabisa ili sister akija anikute niko tayari, wakati nikijiandaa simu yangu ilianza kuita, ni Lucy alikuwa akipiga na nilipokea simu yake ili nimsikilize na tulianza maongezi pale;
LUCY: âInsider unaendeleaje?â
MIMI: âSalama Lucy, nashukuru Mungu.â
LUCY: âJana umeondoka ukaniacha niki hang na simu ukawa hupokei, nini kinaendelea?â
MIMI: âAcha tu, kuna ujumbe mbaya alinitumia kwamba anafanya abortion na mpaka sasa hapatikani hata whatsapp ameifunga.â
LUCY: âPole sana, wewe upo wapi sahivi?â
MIMI: âNaongea na wewe niko Arusha now.â
LUCY: âWhat? Umeenda muda gani? Na kuna nini?â
MIMI: âJana baada ya kuachana nilirudi home, kisha nikaanza safari na nimekuja huku kwaajili ya kuonana na dada yangu.â
LUCY: âJamani, mmeshaonana tayari?.â
MIMI: âBado Lucy, nimeingia late sana na soon tutaonana.â
LUCY: âNgoja niendelee kutafuta means ya kumtafuta Iryn kwa namba nyingine, lakini nataka kuacha kazi Insider.â
MIMI: âUache kazi kwasababu gani?â
LUCY: âNimemwambia jana naacha kazi kama atatoa mimba, nitakuwa nimekusaliti kama nitaendelea kufanya kazi chini yake.â
MIMI: âUsifanye maamuzi yoyote mabaya mpaka nitakavyo rudi sawa?â
LUCY: âSawa! see you then.â
Saa 3 ontime sister alikuwa amefika pale lodge na alinipigia simu kunipa taarifa kuwa yuko parking, nami nilitoka kwenda kuonana nae, alishuka kwenye gari na kunikumbatia pale. Ni miaka 2 ilikuwa imepita bila kuonana na sister na mara ya mwisho kuonana ilikiwa siku ya engagement ya mama J.
Nilirudi ndani kuchukua vitu pamoja na kusign out. Baada ya kurudi, sister alisema tunakwenda kwake, lakini mimi nilimgomea.
SISTER: âUnamaana gani hutaki kwenda kwangu?â
MIMI: âDada yangu naomba tutafute kwanza sehemu tukae, kisha tuzungumze.â
SISTER: âSawa! Twende Charity hotel tukazungumze pale tupate na breakfast.â
Tulikwenda Charity hotel ambayo ipo Sakina, palikuwa na kamwendo kutoka USA river mpaka hotelini, na baada ya kuwasili tulikaa nje, na kila mtu aliishia kuagiza anachotaka kula.
SISTER: âMama J kanipigia simu jana, wewe ulimuagaje home?â
MIMI: âNilimwambia nakuja kuonana na wewe kwaajili masuala ya kifamilia, ulimjibu nini?â
SISTER: âNilimwambia ukirudi utamwambia, sikujua hata cha kumjibu na sikutaka kumuacha kwenye question mark.â
MIMI: âUlifanya vema, sasa dada yangu mpaka nimekuja huku naomba utambue napitia kipindi kigumu sana, hili jambo naloenda kukwambia hakuna mtu yoyote kwenye familia anaejua. Kwa bahati mbaya ninakushirikisha leo, lakini mambo yameshaharibika tayari, wish ningekwambia mapema.â
SISTER: âKuna nini bro! embu niambie hii itabaki kuwa siri yangu na wewe.â
Alikaa mkao kuonesha kwamba yuko tayari kunisikiliza, nami nikaanza kumsimulia mkanda mzima kuhusu Iryn, jinsi tulivyokutana, tukaanza kujihusisha kimapenzi hadi kupelekea kupata mimba, na mambo yanayoendelea sasa, bila kusahau ukaribu wake na mke wangu.
Baada ya kumaliza kumsimulia mkanda mzima, sister alishusha pumzi ndefu sana na aliishia kusikitika pale;
SISTER: âDaah! Hizi habari kweli ni nzito, simpatii picha wifi yangu akija kujua hii siri, sijui kama utanusurika this time. Bro! unashida gani mpaka unashindwa kucontrol hisia zako?unaenda mbali na kumpa mimba, what are you doing?â
MIMI: âNimekosea ndio, lakini nimeshakueleza kuwa alibeba mimba kwa reason zake, mtoto anabaki kuwa damu yetu, hatuwezi mkataa.â
SISTER: âHata hivyo, mimi bado nina wasiwasi na zile dawa alizokupa Masai nahisi huenda kuna kitu alikuwekea, umekuwa mtu wa kupenda penda hovyo au sababu ya kuchelewa kuwajua wanawake?.â
Sister yangu kaplay part kubwa sana ya kunifanya kuwa mwanaume rijali, alinisaidia mambo mengi sana mpaka nikawa sawa, miaka 8 nyuma.
SISTER: âBro! ifike stage ujicontrol, haya yote unayofanya ipo siku yatakurudia wewe na utakuja kujuta kwenye maisha yako yote, mimi kama dada nimeumia sana juu ya mama J. Mtoto wa watu yuko loyal sana kwako, anakupenda, ametulia na hana mambo mengi ila wewe sasa, Mungu akusaidie.â
MIMI: âNi kweli nimezingua dada yangu hata mimi najisikia vibaya sana, lakini naomba tushauriane juu ya hili suala, haya mambo mengine tutaongea tuanze kwanza na hili, ndomana nimekuja kwako.â
SISTER: âUmefanya ujinga wako afu sahivi unaomba ushauri, mbona hukuomba ushauri kipindi unaanza?. Okay, ulikuwa Zambia kwa baba, why hujamwambia kuhusu hili?. Brother kwa hili sina cha kukushauri na kama anataka kufanya abortion, ni bora akafanya hivo maana huko mbeleni utakuwa kwenye wakati mgumu sana.â
MIMI: âSawa nashukuru kwa kunipa lawama zote, lakini tambua hakuna binadamu asiyekosea.â
SISTER: âInsider, unavyofanya ujinga kama huu naomba fanya kwa interest zako, lakini kaa ukijua kwamba mambo yakiharibika ni kwa faida yako, dont ever try to contact me again. Wewe tayari ni mtu mzima unajua ni nini unafanya, hufanyi kwa bahati mbaya, tusipotezeane muda. We done here, naenda washroom nikirudi tunaondoka kwenda home.â
MIMI: âMimi siwezi kwenda home nitarudi Dar maana sijaja huku kwa lengo la kukutembelea.â
Sister alinikataa na hiki kitendo kilizidi kunipa mawazo, ukweli sister na mama J ni marafiki sana na humwambii kitu kuhusu uhusiano wao. Dada yangu alikuwa sahihi kuchukia kwa hili jambo nililofanya, ukizingatia nilishakuwa nimetoa ahadi huko nyuma ya kutofanya tena, huu ujinga.
Niliinamia meza huku nikiendelea kuwaza next move, lakini sikuwa napata jibu, hivyo niliona wacha nirudi Dar nikaendelee na mambo yangu.
Baada ya dakika 15 Sister alirudi kutoka washaroom na alianza tena kuongea na mimi pale;
SISTER: âBro! nioneshe message aliyokutumia jana, niisome na mimi.â
Nilitoa simu nikamuonesha na alinyamaza kwa dakika 10 bila kusema kitu chochote, kisha akaendelea;
âKipindi niko washroom nilikuwa nafikiria hili suala, kwa maelezo yote uliyonipa nikweli dada anakupenda, na hii message aliyokutumia amecheza na mind yako, kuna ujumbe hapa amekuandikia ila umeshindwa kuutambua.â
Dada yangu anajua mambo ya saikolojia, maana anafanyia kazi moja ya NGO kubwa ya kimataifa kule Arusha, sasa baada ya kunipa hizi habari nilishindwa kumuelewa na nilichukua simu ili niusome ujumbe tena kwa makini, hata hivyo sikuelewa kitu.
MIMI: âMimi sioni chochote hapa dada, labda unambie umeona nini?.â
SISTER: âUjumbe wa hapo upo clear kabisa ni hivi, dada yuko kwenye kipindi kigumu hasa kwa upande wa familia yake, wewe ulishindwa kumshawishi toka mapema, kwa hapa ulifeli. Before unakumbuka nilikwambia kwamba wanawake tunapenda kudanganywa? Ni kosa kubwa sana kumwambia mwanamke ukweli, kwa ufupi hatupendi ukweli.â
MIMI: âKwahiyo unataka kusema nilikosea kumwambia ukweli? Ningemdanganya namuoa huoni kama ingekuja kuleta matatizo huko mbeleni?â
SISTER: âHili jambo lilitakiwa kuisha hata hayo mambo ya Ethiopia usingeenda, ndomana nakwambia ulishindwa kucheza na akili yake tu. Na kama ungenishirikisha mapema hili suala lingekuwa limeisha, sahivi tungekuwa tunajadili namna ya kudeal na mama J.â
MIMI: âNilitakiwa kufanya nini hapo.?â
SISTER: âNakupa mfano, kisha utanijibu. Una mtoto wako wa kike, anakuja kwako kukwambia ana mimba, na kapewa na mume wa mtu, utamuelewa?â
MIMI: âHapana siwezi asee, nitamlamba makofi ya kutosha.â
SISTER: âUli expect na yeye angekuwa na confidence ya kuongea hivo mbele ya familia yake?.â
Nilinyamaza kimya muda huu;
âBrother ulitakiwa kuisoma akili yake inataka nini kwa kipindi hiki, ulipaswa kumuonesha mpo pamoja no matter what, ulipaswa kumuonesha unampenda sana hata kwa kupretend na kitendo cha kumpiga hotelini, hapa pia ulikosea sana.â
MIMI: âAlinipanda sana kichwani ndomana nilimchapa vibao, nilimuomba msamaha lakini.â
SISTER: âUlishindwa kutambua ni mjamzito, na ile haikuwa sababu ya kumpiga, shida yako unahasira za haraka sana.â
MIMI: âNi kweli nilikosea ile siku, lakini bado sioni kama sababu ya kufanya abortion.â
SISTER: âMpaka sasa, dada anaonekana kuwa upande wetu, lakini bado anajifikiria kuhusu kufanya abortion. Inaonekana nguvu ya familia yake ni kubwa zaidi kuliko ya upande wetu, na mara nyingi, upande wenye nguvu zaidi hushinda. Dada ameona kuwa huna future kwa sababu umeshindwa kumjali katika kipindi hiki kigumu anachopitia. Huu ulikuwa wakati mzuri wa kumuonesha upendo, lakini badala ya kumsaidia, wewe umekuwa against naye wakati ulipaswa hata kwenda South Africa kumsalimia kama kweli ungetaka mtoto. Dada alikuamini, lakini sasa anaona unaweza kuharibu future yake na kumfanya apoteze ndugu zake kwa sababu yako, mtu ambaye si wa kutegemewa."
MIMI: âConclusion ni nini dada yangu? maana nahisi kuchanganyikiwa hapa kuhusu huyo mtoto bora hata angekuwa anapatikana kwenye simu.â
SISTER: âHuo ujumbe dada aliotuma kwako, ameandika kwa kumaanisha, ni kama amekupa last chance ya wewe kumtafuta, sasa tumia akili tunampataje?â
MIMI: âHapa ndo mtihani kujua aliko kati ya South, Ethiopia na Ufaransa, lakini anapendelea sana kwenda Ufaransa kwaajili ya mapumziko.â
SISTER: âDada bado yuko South Africa, kwenda Ethiopia kwa familia kwa kipindi hiki ni ngumu, atleast Ufaransa, kama alitumia namba ya South kukutafuta bhasi yupo huko. Tuna siku moja tu imebaki ambayo ni kesho, ya kwenda South Africa kumtafuta ili tuyaweke sawa haya masuala, tukichelewa tutamkosa mtoto.â
MIMI: âWhat? Twende South Africa?â
SISTER: âNdo maana yake, we are running out of time, letâs go, tuanze mchakato wa kufanya booking ya flight mapema.â
MIMI: âSister taratibu kwanza, tukienda huko tunampataje? Anaishi Capetown lakini sijui address zake.â
SISTER: âCome on, tutakwenda kuulizia chuo anachosoma na tutampata, lazima tutapata contacts za watu wake wa karibu.â
Sister alikuwa kaongea point tupu, ukweli mimi nilikuwa sijitambui kabisa muda huu maana akili yangu ilikuwa imevurugwa sana.
MIMI: âSawa na vipi kuhusu permits tutafanikisha kweli? Ukizingatia leo tuko weekend ofisi zimefungwa.â
SISTER: âSouth ni Passport yako tu na ticket ya kurudi ila lazima uwe na sababu maalumu ya kuingia kule, tunaweza kutumia barua ya ofisi yangu ikaonesha nakwenda south kikazi, tukatumia hii advantage.â
Na muda huu alikuwa akimpigia simu dada Tyna na aliweka loudspeaker.
âHello my loveâ
TYNA: âYes darling, I have missed you so much.â
SISTER: âOoh really?, niko na brother hapa tunajitaji ticket 2 za kwenda South Africa leo, ni muhimu sana.â
TYNA: âInsider jana amenicheki alikuwa anahitaji ticket ya kuja Arusha, sikujua kama anakuja kwako, vipi huko south kuna nini tena?â
SISTER: âDear kuna mambo tunaenda fatilia tutaongea, ila kwasasa tusaidie hili kipenzi, tukicheki bei za flight zipo juu sana.â
TYNA: âTicket inakuwa cheap ukikata mapema hizi za haraka nyingi ni za maagent, sasa nipe muda nifanye mpango wa kuwachekia, huko South mnabarua yoyote?â
SISTER: âNdo tunajadili hapa kipenzi, naweza tumia barua ya ofisi.â
TYNA: âNina rafiki yangu yuko South, anafanyia kazi Airport Johannesburg, ni rahisi kuwasaidia chap na uzuri yuko airport hamtapata tabu.â
Nilimpa Ishara sister akubali maana ilikuwa ni uhakika;
SISTER: âSawa dear, ongea nae afu tupe jibu.â
TYNA: âHuyuhuyu anaweza kutusaidia na ticket, ila niwashauri mje Dar kwa uhakika zaidi na ni rahisi kupata ndege za kuunga.â
SISTER: âBhasi tusaidie ticket za kutoka huku ili tuwahi kuja huko.â
TYNA: âSawa hili ni chap tu hakuna shida.â
Baada ya kumaliza kuongea na Tyna tulianza kupanga bajeti ya kwenda kule South Africa maana hatukujua tunaweza kutumia muda gani. Mimi nilikuwa nina $1,800 na 370k kama cash iliyobakia, kwa upande wa sister alikuwa ana balance ya 2M, bajeti ikawa inatutosha vizuri kabisa.
Sister alimpigia simu shemeji na alimpa taarifa kuwa mimi nipo Arusha na alimuaga anaondoka kwenda South Africa, alimpa ABC kidogo ya kinachoendelea, na pindi akirudi atamsimulia vizuri.
Shem wangu hanaga noma kabisa, aliomba kuongea na mimi tukasalimiana pale na alinipa pole, tukaongea kidogo, pia alimind kwanini nakuja Arusha, halafu naondoka bila kuonana nae? ilibidi nimwambie tukitoka South tutaonana.
Baada ya dakika 2 shem alituma million 1 kwa sister na alimpigia simu kumwambia itatusaidia safarini, na akatutakia safari njema na mafanikio.
Sister alisema anaondoka kwenda home kubadilika haraka pamoja na kuchukua nguo za safari, na baada ya nusu saa atakuwa amerudi, hivyo aliondoka akaniacha hotelini nikimsubiri.
Mpaka sister anaondoka kwenda kubadilika tulikuwa tumetumia karibia masaa 3 pale hotelini, maana tulikuwa na maongezi mengi sana kuhusu hili suala, na hapa nimeandika baadhi tu yale muhimu.
Suala la Asmah sikutaka kabisa kumwambia maana lingeweza kusababisha mambo yawe magumu zaidi na kupoteza uaminifu kwa dada yangu.
Baada ya dakika 40 sister alirudi hotelini huku amependeza sana, alikuwa kavaa skin jeans ya blue, chini ana raba nyeupe, juu ana top nyeupe na sunglasses nyeusi, nywele zake ndefu ambazo hazijasukwa kaziachia kwa pembeni.
Kama nilivyowaambia awali kuhusu dada yangu, ana asili flani ya Kihindi, mweupe na mzuri by nature. Ukweli alikuwa kapendeza sana, na niliishia kujisifia kuwa nina dada mzuri na baada ya kufika usawa wangu nilimsifia tena kwa kupendeza.
Sister alifurahi sana kuona nikimpa sifa za kupendeza na tuliendelea na mazungumzo;
SISTER: âTyna kanipigia simu, anasema tusogee JRO.â
MIMI: âSawa haina shida, na kuhusu ticket za south?â
SISTER: âHili bado hajaongelea, nafikiri tuendelee kumpa muda.â
Ticket online zilikuwa zinapatikana, lakini sasa bei za ticket zilikuwa ziko juu sana, hizi safari za papo kwa hapo tuwaachie matajiri ndo wanaweza kulipia gharama yoyote ile, ila kwasisi masikini tuendelee kukata ticket mapema.
Sister alikuwa amekuja na dereva wa ofisini kwao kwaajili ya kutupeleka airport, sister alisema baada ya kutoa taarifa ya dharura kwa bossy wake, ndo kupewa na gari ya kumpeleka airport.
Hatukuwa na muda wa kupoteza hivyo, tulianza safari ya kwenda JRO na ndani ya lisaa tuliwasili na tuliendelea kumsubiri Tyna atupe direction.
Saa 11 jioni tulifanikiwa kutoka Kilimanjaro kwenda Dar, kwa upande wa Dar dada Tyna alikuwa around akitusubiri na ile kuwasili alikuja spidi akamkumbatia sister. Hawa ni marafiki wa longtime toka enzi za utotoni, wamekua pamoja, kusoma pamoja ni marafiki wa damu.
Tulikaa Cafe tukiendelea kupiga story, kwa upande wake alitaka kujua ni jambo gani linatupeleka South?, sister aliishia kumpa sababu ya uwongo, haya ni mambo ya kifamilia isingekuwa busara kumwambia.
Tyna alimpigia simu rafiki yake ambaye angetupokea kwa kule South Africa na alimpa simu sister akaongea naye. Jamaa wa kule South alitushauri tufikie Johannesburg na wakati wa kurudi tutaondokea Capetown.
Changamoto iliyojitokeza ni kwamba sisi tunakwenda Capetown na tukifikia Johannesburg, kwenda Capetown pana distance si chini ya 1,400km unaona umbali huo. Kwasababu ya ugeni na tulihitaji mwenyeji wa kutopokea kwa kule, hivyo hatukuwa na jinsi ilibidi tukubali.
Kwa upande mwingine jamaa wa South alipiga simu na kumpa taarifa Tyna kuwa amepata ticket 2 kutoka kampuni ya Ethiopian Airlines, hivyo alihitaji tumtumie taarifa zetu haraka, pamoja na muda tutakaotumia kule.
Tulimtumia Jamaa taarifa zetu kwa haraka na kuhusu gharama za tickets tulilipa $1,750 kwa wote wawili âGo and returnâ. Baada ya kukamilisha malipo na taratibu zote, alitutumia ticket zetu. Ndege ilikuwa inaondoka saa 9 usiku kwenda South, kwahiyo ingetubidi tusubiri mpaka muda ufike wa safari.
Muda ulikuwa ni saa 11 jioni tayari, tukaanza kushauriana na sister tunakwenda kulala wapi?. Tyna alisema tukalale kwake, hawezi kukubali kuona tunalala hotelini wakati anauwezo wa kutupeleka kwake, tulikwenda kulala kwa Tyna.
Plan yetu ilikuwa turudi Dar siku ya jumatano, hivyo tungekaa siku 2 kule. Kwa upande wa bajeti ilikuwa imekata kwa upande wa sister maana tulitumia pesa zake kulipia tickets na tuliacha dollar zitusaidie tunakoenda. Nilikuwa sijatembea na card, pia huduma za online sijajiunga, hivyo nilipiga hesabu za haraka nikaona nikope pesa kwa mtu, ili tuwe na akiba ya kutosha.
Kwa hesabu za haraka niliona nimuazime pesa Ghati na ile kumpigia simu na kuongea naye, kwa haraka sana alinitumia million 3 na nikazitoa kabisa kwa wakala.
Kesho yake, asubuhi na mapema, tuliwasili JNIA kuanza safari yetu ya kuelekea Afrika Kusini. Baada ya kucheck-in na kukamilisha taratibu zote, tuliingia kwenye ndege. Hata hivyo, tulikaa kwenye viti tofauti, dada yangu alikaa mbele yangu, wakati mimi nilikuwa kwenye kiti cha tatu nyuma kutoka pale alipokaa.
ITAENDELEA
I think wanaume wote tunafanana thinking ways zetu.Lesson learnt:
The way this "true" story is arranged and explained, makes you look like a person who has seen books, but the way you act, is like an idiot.
Hapana INSIDER MAN kazidi, kibaya zaidi he cannot make decision on his own, he depends on consultancy.I think wanaume wote tunafanana thinking ways zetu.
SifiriTuliza kishundu hicho
Wakati mwingine unajichanganya mpaka inafika sehemu unakua huna namna ya kufanya uamuzi. Sasa una mchepuko, ana mimba, unatembea na mfanyakazi wake.Hapana INSIDER MAN kazidi, kibaya zaidi he cannot make decision on his own, he depends on consultancy.
This one sound sarcasticThank you INSIDER MAN, unajua kuna Vijana wengi wanataMani kuwa kama Wewe lakini Map ya michakato yako umeiweka hapa naamini 99.9% hawaiwezi kabisa.
Unapambana na life, unawala mademu wa kali, unasoma chuo, una familia, unasimamia Kampuni. Hongera sana Kijana
Moja kati ya nyuzi zenye mafunzo sana hasa kwa waajiriwa na wanaotaka kuajiriwa.Habari wakuu!....
Tusubiriapo next ep., waweza pitia huu uzi...... full of lessons
View attachment 3067815
Link:
Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa
UTANGULIZI Wakuu habari. Naandika hii story yangu ikiwa ni mwaka sasa nipo mtaani nikiendelea na harakati za kusaka ajira mpya toka mkataba wangu wa ajira ulipoisha mnamo Desemba 2022. Nimeamua kushea uzoefu wangu kwa mtindo wa Masimulizi (katika episodes) kwa kuamini pengine inaweza kuwa na...www.jamiiforums.com
Unashoboka na wanaume wewe bwabwaSifiri
Imekuuma đ tuliza kishundu hicho bwabwa weweSifiri
Jifunze kuandika vizuriSifiri
LI UJUE HII NI STORY YA KUTUNGA INAISHIA PAZURI KABLA YA KUANZA EPSODE NYINGINE ILI KUMVUTIA ZAIDI MSOMAJI AENDELEE KUFUATILIAđEPISODE 8
A TRUE STORY BY INSIDER MANâ
Nilirudi nyumbani huku barabara nzima nikiwa nawaza mambo mawili kichwani. Jambo la kwanza nilikua nawaza Iryn atakua anafanya kazi gani?, nilikua bado najiuliza kazi gani hii ya usiku??, au anafanya illegal?, âŠmmh hapana yule dada ni mrembo, pia kaniambia ana saloon sidhani kama anafanya hizi dili.
ââŠ.Anyway mimi naangalia pesa mambo mengine mimi hayanihusu kabisa, atajua yeye na maisha yake bwana, as long I get paid no problemâ
Lakini pia nilikua nafuraha ya kufahamiana na mrembo kama yule niliamini pia ni bahati na nyota.
Upande mwingine nilikua nawaza jinsi ya kudeal na mama Junior maana sikutaka kumuweka wazi juu ya hili suala.
Nilikua bado najiuliza muda uleâŠ.
âHivi kama nitarudi usiku bila kuwa na reason maalum inayoeleweka ,sindo chanzo cha ugomvi na makelele?, au nimwambie tu kieleweke??â. Lakini bado nilikua nakosa maamuzi kwa upande wa Mama J.
Wakati muda ule nikiwa nawaza simu ilianza kuita kucheki naona DullahâŠ.Nikapokea.
âDullah vipi ndugu yangu hatuonaniâ
âTuonane wapi wakati ushaanza kuwa busy na watoto wazuri?â
Nikampa story Dullah jinsi ambavyo nimekutana na Iryn na mpaka kunipa kazi. Dullah akanambia ânaona ushaanza kupagawa mapema hivi ndugu yangu hio ni intro tuâ
Nikakatisha maongezi na Dullah baada ya kuona mama anapiga simu:
âMwanangu hujambo?, hivi mama Junior karudi nyumbani?â
âMama amerudi, haujaongea na mkamwana wako?â
âSijaongea naye na muda kweliâ
âMhh mama yakweli hayo, maana naona kama haiwezekaniâ
âKama amerudi nimefurahi msalimie Mjukuu wanguâ (Mama yangu na Junior wamefanana sana, humwambii kitu kuhusu mjuu wake)
Ipo hivi mama yangu na mama J ni marafiki sana, hata mama alivyokua ananiuliza kuhusu mama J kurudi home nilikua najua lazima anafahamu ila ananizunguka tu.
Sielewagi mama J alitumia mbinu gani kuwa close sana mama yangu yaani ni wanapatana balaa, sio kwa upande wa mama tu hata dada yangu pia. Yaani anaweza kuwa na kosa yeye ila mimi ndo nikaonekana mkorofi.
*******
Kesho yake niliwai kuamka ili niwai kumchukua Mama wawili na mwanae, baada ya kumdrop mwanae nikampitia Maggy hao Posta. Japo kuamka asubuhi sometimes ilikua inakera sana unakua kama mtumwa. Lakini ukicheki una mkataba wa kazi na watu huwezi kuleta ufedhuli inabidi uwe mpole tu.
Upande mwingine yule dada wa kule Masaki- Olive alikua kanicheki kwamba kama nitaenda masaki tuonane ili tukubaliane bei, jumatatu nianze kazi ya kuwachukua watoto.
Nikaenda Kariakoo kuchukua Rim za gari na tairi mpya ili kubadilisha muonekano wa gari yangu. Baada ya kutoka hapo nikaelekea â@thewheelâ Mikocheni, tukabadilisha tairi na Rim, aisee gari ikawa kali balaa, pale garage kila mtu akawa anaisifia IST yangu (nitawatumia picha chini).
Nikatoka hapo kuelekea Masaki kuonana na dada, nilikua pale saa 9 mchana, tukaongea pale, watoto walikua watatu (3) ambapo wakwanza nitakua namuacha pale Mikocheni karibu na Clouds media, hawa wawili walikua wanakaa Kunduchi- Bahari Beach ila maeneo tofauti.
Tukakubaliana kwa watoto wa Kunduchi atanipa 13,000 kwa kichwa na yule wa mikocheni atanipa 7,000. Japo baada ya week 2 aliongezeka mtoto 1 mwingine alikua anakaa kawe jumla nikawa na watoto 4, ila huyu mtoto wa kawe sikutaka kumtoza niliamua kutoa shukran kwa dada.
Hapo nilikua na uhakika wa kuingiza 165,000/= kwa week na tulikubaliana malipo yawe yanafanyika kwa week.
Baada ya deal kuwa done nikafurahi sana hapo tayari nilikua na uhakika wa kuingiza zaidi ya 2,000,000/= kwa mwezi.
Nilijiona na bahati sana kwa muda mfupi kupata wateja wa uhakika, hapo nilikua na uhakika hata nisipowasha App pesa itaingia tu.
******
Ijumaa ndo siku ambayo nilikua na miadi na Iryn kama tulivyokubaliana, niliamka asubuhi mapema sana 06:00. Kwa siku za weekend nilikua napenda sana kuvaa buti au sando, tshirt na cap kichwani, nikivaa buti/raba bhasi lazima nitembee na sando kwenye buti.
Nikapata trip ya kwenda Pwani âMarian boys schoolâ kuna mzee alikua anampeleka mtoto wake shule.
Nikampigia simu chap
MZEE: âKijana wangu hujambo nataka kumpeleka kijana wangu Marian schools pwaniâ
MIMI: âMzee unakwenda na kurudi?â
MZEE : âHapana kijana kuna kikao pia nitakuweka sanaâ
MIMI : âMzee mimi sina shida kama utanilipa muda wanguâ
MZEE : âsi nitatumia gharama kubwa sana, maana sijui kikao kitachukua muda ganiâ
MIMI: âSawa mzee wangu ila sasa kama unataka twende huko itabidi tusitumiee App, tukubaliane bei maana ukishaingia Pwani Uber haisomi, mpaka nirudi tena Dsm ndo nitaweza pata request. Na uhakika wa request mpaka nirudi Bunju atlist, kama upo tayari nikupelekeâ
MZEE: âSawa kijana wangu nimekuelewa unataka kiasi gani?â
MIMI: âMzee kwenye App ilikua inaonyesha kiasi gani?â
MZEE: â30,000/=â
MIMI: âBhasi utanipa 50,000â
MZEE: âNitakupa 45,000 kijana wangu, uje haraka tuondokeâ
MIMI: âSawa mzee nakujaâ
Mzee hakuwa mbali sana na mimi nakoishi yeye alikua anakaa nyuma ya Hospital ya Massana.
Unajua hawa watu ambao walikua wanaishi ushuani nilikua siwachekei kabisa, nilikua najua kabisa wanahela. Huwezi mpeleka mtoto Marian kama hauna hela.
Nikawapeleka mpaka Marian school, mzee akachukua namba yangu mimi nikageuka kurudi Dsm. Nilichoma wese, sasa wakati nakaribia âBunju mwishoâ nikapata request ya kwenda Airport.
Kufika pale nashangaa kumbe alikua ni kigogo wa serikalini.(Naibu waziri wa Wizara X)
âMzee shikamoo hata nyie huwa mna request kumbe?â
âKijana unashangaa tena, huu ni usafiri wangu sanaâ
âNilijua unapiga simu, dereva anakuja chap kukubebaâ
âDereva naye ni binadamu leo ni weekend pia na haraka acha apumzike najali pia maisha yao binafsiâ
âSawa mzee hata hivyo tunashukuru hata mimi hapa nimepata ridhikiâ
âNi kweli ndo kutegemeana huku, sasa tutapitia pale TFNC kumchukua mke wangu afu tutaelekea Airportâ
Tukatoka pale huku tukipiga story na yule Kigogo, akawa anauliza hali ya Maisha huku anamsifia Mama Samia na mimi namuunga mkono. Na mimi palepale sikutaka kuwa mzembe nikaanza kutengeneza connection maana nilisema hizi chance zinatokea mara chache sana.
Tulifika pale TFNC hizi ofisi zipo kule chini Ocean Road, bhasi tukafika pale tukasubiri kama dk 10 mke wake akawa amekuja hao tukaelekea Airport.
Kigogo alinisifia sana gari yangu kuwa safi, akanambia nimepanda Uber nyingi ila hii ni kiboko sana, akaniahidi atakua ananitumia. (Ila hakuwai nitafuta na alipigwa chini kwnye nafasi yake)
Niliwadrop pale Airpot Terminal 2, palepale kuna ndege ilikua inashuka nikapata request ya kwenda Mikocheni.
Baada ya kupiga kazi mpaka sa12 jioni nikasema acha nipumzike ofcoz ubao ulikua unasoma vizuri sana, kwenye ubao ulikua unasoma 95,000 ukijumlisha na ile 45,000 ya Asubuhi nakua na 150,000 tayari. Wakati nimemshusha yule kigogo pale Airport aliniongezea 10,000 ya ahsante nikasema hii nitaoshea gari badae.
âIpo hivi mimi pesa ya kuoshea gari huwa sitoi kwenye faida zangu bali huwa natoa kwenye zile ahsante ambazo mteja ananipa, kuna wateja wako poa sana akifurahia huduma utakuta anakuachia chenji, sasa hizi nilikuaga nazitunza kwenye drooâ
Nikapeleka gari carwash lipigwe usafi maana likikua lishachafuka tayari, nilitaka gari ingâae kabla ya kumiti na Iryn. Nilitaka akute gari ikiwa safi.
Muda huo ilikua sa12 na madakika tayari, Iryn akanipigia simu kunikumbusha niwe on-time, nikamwuuliza timetable ikoje tunakwenda wapi na wapi?.
âLeo tutakwenda Ledger Plaza na Serena Hotelâ, Iryn alijibu hivo.
Muda huo nilikua zangu pale Texas nimechili nimepumzika huku napiga story na wahuni. Texas nilipazoea sababu Uncle wangu alikua anapenda sana kuoshea gari pale.
********
Hatimae muda ulifika, ontime nilikua pale kumchukua dada kama kawaida alikua kawaka sana asee, niliishia kumtamani tu. Aliweka bag lake kwa nyuma ya siti âduffel bagâ akaingia kwenye gari akakaa siti ya mbele, tukasalimiana hao tukaanza safari ya kwenda Bahari Beach, Ledger plaza Hotel.
Wakati tuko njian IRYN alinambia atakua ananitambulisha mimi kama dereva wake kwa mabosi zake, nikamwambia sawa haina shida.
Tulifika pale Ledger Plaza nikapark gari mrembo akashuka akachukua bag lake akanambia kaka sitokaa zaidi ya masaa 2, nikamwambia usiwe na wasiwasi bossy wangu. Nikaishia kumtizama mpaka anavyopotea.
Mimi nikashusha kiti nikalala zangu nikiwa pale Parking, sikutaka kutoka ndani ya gari na muda huo ilikua saa 3 tayari.
Kwa muda wa usiku pale Ledger panakuaga pametulia sana, sikutaka kwenda upande wa kule chini maana hata ningeenda wahudumu wangenisumbua tu. Na sikuwa na mpango wa kutumia pesa yangu niliona bora nichill kwenye gari.
Nilikaa pale parking, nilipitiwa na usingizi nakuja kushtuka ilikua ni text ya wife âUnarudi sangapi?â
âWife leo ntachelewa kidogo samahani sikukupa taarifa nilikua nimebanwa, nimetembea na key zangu usiwe na wasiwasiâ
âOkay, takecareâ alijibu hivo.
Kuangalia muda ilikua ni saa 5 tayari lakini Iryn hakua na dalili za kurudi nikalala tena. Nilikuja kushtuka pale niliposikia mtu anagonga dirishani, nikashusha kioo fasta
âHuku aki tabasamu, Kaka sorry nimekuweka sanaâ
âHapana usiwe na wasiwasi Bossy wangu, upo tayari tuondoke?â
Nilimwona kabadili mavazi sio yale ambayo alikuja nayo, akaweka bag lake nyuma, hao tukaanza safari ya kwenda Serena hotel.
Baada ya kufika Serena hotel, huyo akaingia ndani mimi nikaenda kutafuta parking. Kwa mazingira ya hotel kama zile huwezi kutoka nje kushangaa lazima utakutana na upinzani wa Askari na mimi sikutaka kukaa reception, hivyo niliamua niwe nakaa ndani ya gari tu.
Alitumia masaa 2 pale akanipigia simu nisogee mpaka reception ili tuondoke, kufika pale nikaona kasimama na Mzungu. Akanambia Insider shuka msalimie bossy wangu, mimi nikashuka akanitambulisha pale.
âMr Robert, huyu anaitwa Insider ni dereva wanguâ (kwa kiingereza)
âNimefurahi kukufahamu Mr Insider naomba uwe makini sana na Irynâ
âDonât worry Mr Robert, Iryn ni Boss wanguâ
Palepale mzungu akatoa âŹ20 akanipa, nikamshukuru, hao tukaondoka nimrudishe kwake. Nikamdrop pale kwake na mimi nikarudi home.
Wakati niko njian nilikua nawaza Iryn anafanya mishe gani hizi? âHuyu dem anajiuza ila atakua ni International maana hata hotel anazoingia ni 5 starâ. Upande mwingine nilikua najiuliza mbona anaingia na kibag ndani au anauza sembe??
âIla mambo yake binafsi mimi hayanihusu, hiyo sio kazi tuliokubaliana lakini siku nitamwuliza.â
Niliingia home saa 9 kasoro mama J alikua kalala, na mimi sikutaka kumuamsha nikaoga nikapanda kulala.
*****
Kwa biashara ya Uber siku za kupiga hela ni weekend nazungumzia ijumaa, jumamosi na jumapili kwa siku za kawaida bhasi jumatatu na alhamis (mwisho wa hii story nitawaelezea)
Kama kawaida niliamka jumamosi nikaaendelea na majukumu yangu ya kutafuta hela, nakumbuka hii siku niliimalizia kisarawe huko. Nilipata customer alikua anakwenda huko akaomba nimsubiri amalize kikao afu nimrudishe Dar.
Mimi kama nalipwa pesa nilikua sijali kabisa cha msingi tukubaliane sina neno. Tulikaa sana pale kisarawe kulikua na kikao mambo ya chama, walimaliza kwenye saa 10 jioni.
Tulirudi mpaka Dar nikamdrop jamaa pale Lumumba, tulichelewa sana kuingia sababu ya foleni pale Mbagala, sababu barabara ilikua inatanuliwa.
Nilivyotoka hapo uelekeo ulikua ni Kijitonyama kuonana na Iryn, saa 2 kasoro ilinikutia getini. Nikampigia simu kuwa nimefika akasema anakuja.
Alivyofika akanipa time table za usiku huo ilikua tunakwenda sehem 3, ratiba haikua ngumu sana kwani tulikua tunakwenda Hyatt, Golden tulip hotel ya Masaki na Palm village.
Yeye akasema tuanze na Golden tulip hotel, kama kawaida yake na kibag chake kakiweka nyuma tukaanza safari. Pale Golden alitumia masaa 2 tutatoka kuelekea Hyatt Posta, mimi kama kawaida yangu nikatafuta parking nikatulia.
Wakati niko parking mlinzi alikuja akanambia siruhusiwi kukaa parking, kama namsubiri mtu bhasi niende reception. Kama mnavyojua pale Hyatt ulinzi ni mkali sana.
Baada ya saa na nusu hivi Iryn akanipigia simu kwamba niende âlevel 8â ananisubiri, akaniambia niulizie nitaoneshwa iliko, ndo mara yangu ya kwanza naingia Hyatt. Kufika pale namkuta yuko na jamaa (kwa kumtizama alikua ni mtu wa S. Africa).
Level 8 ni restaurant ya pale Hyatt Hotel.
Akanitambulisha kwa jamaa kama dereva wake, Iryn akanambia niagize chakula tule then tuondoke. Mimi niliagiza seafood maana nilikua hata sioni cha kuagiza.
Jamaa akatusindikiza mpaka parking wakakumbatiana na Iryn, jamaa akaja upande wangu akanambia âTakecare of herâ, mimi nikatingisha kichwa kama kukubaliana naye.
Tukaondoka, uelekeo ulikua ni Palm village. Iryn akatoa $100 akanipa, akanambia jamaa alinipa hii pesa ya mafuta itakua so busara nikiiweka mfukoni so keep it.
Kwenye gari tulikua tunazungumza kwa nadra sana, wakati tuko pale mataa ya NMB HQ/Puma filling station, tulikua tunatokea Ohio street ili tuingie Alli hassan road, nikaamua kuvunja ukimya, nikamwuliza kwa utani âIryn wewe ni Mtanzania?â
IRYN: âHuku akicheka, kwani sionekani Mtanzania?â
MIMI: âKabisa hapa bongo kama umevamia hiviâ
IRYN : âMama yangu alikua Mmursi-Ethiopia ila baba yangu ni Msouth Africaâ.
MIMI: âSasa ilikuaje mpaka ukaja Tanzania?â
IRYN: âBaba ameishi Tanzania toka 1995 kuna kampuni zake alikua anazisimamia huku na mimi nimekulia Masaki na nimesoma pale FK international schoolâ
MIMI: âNdomana umebarikiwa kwa uzuri Bossy wangu maana watu wa Ethiopia ni hatariâ
Maongezi yetu yalipotea ghafla baada ya simu yake kuanza kuita, nilimind sana kimoyo moyo.
Tulifika pale Palm Village nikamdrop akanambia huku sitakaa sana, pale alitumia kama 1hr hivi akawa ametoka, muda huo ilikua saa7 tayari. Nikamrudisha kwake na mimi nikarudi home kulala.
Ile nimefika home namkuta wife hajalala yuko seblen anaangalia movie. Nikamsalimia nikakaa kwenye kiti.
WIFE: âBaba Junior umetoka wapi sahivi?â
MIMI: âNilikua nimemsindikiza Michael Airpot, anakwenda masomoni Scottlandâ niliamua kumdanganya tu.
Michael ni jamaa yangu sana mpaka sasa, wakati tumetoka kwenye ile Taasisi X yeye aliamua kwenda kusoma Mastaz huko Ulaya. Wife anamjua vizuri sana hyu jamaa yangu.
WIFE: âMbona kaondoka haraka hivyo hata kuniaga ameona shidaâ
MIMI: âMambo mengi wife si unajua sisi wanaume, umepika nini? Naskia njaa sanaâ ilibidi nipotezee mada.
Huku wife akiniandalia msosi,
WIFE: âMwanao anasumbua sana halali, kalala sio mudaâ
MIMI : âPole ndo maana ya kuwa mamaâ
Baada ya kumaliza msosi nikamwambia wife mimi naenda kulala baada ya kuona yuko busy na movie yake.
Nikachomeka simu kwenye chaji nikakutana na message ya Iryn akinitakia usiku mwema, nikareply âSame to you Bossy wanguâ.
*********
Jumapili sikwenda church kwanza nilichelewa kuamka, wife akaniamsha akaomba nikamsaidie kununua vitu sokoni.
Sababu dada alikua mgeni ikabidi niondoke naye hata akiwa peke yake awe anayajua mazingira.
Iryn akanipigia simu akanambia leo tutaenda sehemu 1 tu by 21:00 niwe around, tutakwenda Peninsula hotel. Hii Peninsula hotel ipo âHaile selasie roadâ karibu na Puma Filling station.
Nilitoka zangu home mapema nikaenda poteza muda pale survey, ilivyofika 3 kasoro nikaelekea Kijitonyama. Katika vitu ambavyo Iryn nilikua namsifu ni pamoja na kwenda na muda yaani akikwambia muda wa kufika utamkuta yuko tayari.
Nikamsifia pale, umependeza sana Bossy wangu,
akajibu âthank you, Gentlemanâ.
Siku ya leo hakua na kibag chake bali alikua na mkoba.
Kwenye upande wa kuvaa au kupendeza dada alikua yuko vizuri sana.
Ndani ya nusu saa tulikua tumeshawasili Peninsula hotel nikamdrop nikamwambia mimi nakwenda Samak samak kupoteza muda. Atakapokuwa tayari bhasi anipigie ili nikamchukue.
Nikachili pale Samaki samaki huku napiga zangu heineken mdogo mdogo. Wakati niko pale Samaki samaki kuna jamaa nilimkuta so nikaamua kumjoin story zikawa zinaendelea mdogo mdogo.
Iryn akanipigia simu nikamchukue yuko tayari nikamwaga jamaa huyo nikamchukua mrembo nikamrudisha kulala.
Wakati niko njiani nilijikuta ni mtu mwenye furaha sana. Nikawa najisemea huyu Iryn anaroho nzuri sana, kama anaweza kunipa $100 alopewa ya mafuta, je angekua mtu mwingine angenipa?? Na bado amenilipa 300,000 yangu.
Nikasema acha niendelee kuwa mpole tu, ni watu wachache sana wenye roho kama yake, mwingine asingenipa kabisa.
Nikawa nakumbuka jinsi anavyo nitambulisha kwa watu wake, nikasema huyu dada ananithamini na anaheshimu kazi yangu. Acha na mimi niheshimu kazi zake naamini ipo siku nitajua mishe zake.
Nilivyorudi home kama kawaida nilimkuta wife yuko seblen na movie yake, muda huo ilikua saa7 tayari. Nikamsalimia, hakujibu ila alikua akiniangalia, na mimi sikutaka kupoteza muda nikaingia chumbani then nikaenda kuoga.
Wakati naoga kumbe wife kachukua key na kwenda kukagua gari, ile natoka bafuni naona mtu kashika lipstick mkononi.
âNilijua tu lazima una mwanamke maana nilishaona dalili mapema, ukirudi tu breki ya kwanza kuoga. Toka ijumaa unarudi usiku afu unarudi umechoka kumbe kuna mwanamke anakuchosha huko. Hii lipstick ni yanani? Gari nzima inatoa harufu ya mwanamke, Baba Junior nataka maelezo yakueleweka mimi sio mtotoâ
Ghafla wife akaanza kubadilika
Tutaendelea:
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Hakika mkuu...Nami nikaona Ni vyema kushare coz twafundishwa kizuri Kula na nduguyo.Moja kati ya nyuzi zenye mafunzo sana hasa kwa waajiriwa na wanaotaka kuajiriwa.
Jamii Forum wauze kwani wao ndo wamiliki wa story?Jamii forums wawauzie Dstv chini ya muongozaji Lamata. Then Insider awe na percent yake katika malipo.
đđđ ila humu aiseeSifiri