Jinsi Introverts wanavyopata tabu kuingiliana na watu wanaowazunguka

Unyenyekevu pia calm mind ya introvert ni ya kuzaliwa sio kuigiza
 
Hii hali inan kata sana yan niko too selective kwanzia mahusiano na mpaka washikaji yan nna circle ndogo sana ya watu
Ndivyo tulivyo we are too selective hata kwa habari ya kuchagua mwenza wa maisha.Huwa nawaza huenda kundi la introvert ndio linaloongoza kuchelewa kuyaingia maisha ya ndoa kwa sababu ya kutafakari sana kabla ya kufanya maamuzi.Najisikia amani nikiwa na circle ndogo ya watu
 
Hahah! Mm kazi zenyewe nafanyia kwenye pc home mwanzo mwisho ndani nikichoka nacheza game mwenyewe au move mda wa kutoka ni kwenda kula dakika kadhaa nmerud 😁😁
 
Acha tu yani circle yenyewe ya watu ndogo tutawapata wap,,mm mpaka nione ana interest na mm na amekidh vigezo vyangu lasivyo mda wa kum chatisha mtu sina
 
Ila jifunze kuepuka tu stress maana ni ngumu introvert kukosa stress maana wanatumia muda mwingi kuwaza
Kwenye stress nafikiri tatizo litakuja na mtu atakua anawaza vitu gani zaid ingawa stress haziepukiki
 
Mazingira nilikua napenda kwenda kuangalia mpira,michezo kama draft na marafiki nilio kua nao.. sema asili ni asili tu.. kwani sasa hivi naweza nikawa muongeaji kama siku hata mbili but week inayo kuja ntajifungia ndani na marafiki ntaanza kuwakwepa.
Hahhah! Nilitaka nishangae mkuu mimi nimejitahidi nimeshindwa kuchomoka
 
Duuh introvert by virtue of appearance and everything
 
Hahhah! Nilitaka nishangae mkuu mm nmejitaid nmeshindwa kuchomoka
Mbaya zaidi wale niliokuwa napiga nao story nachukia hata kukutana nao yaani nahisi kama wanafki fulani hivi... napenda kukaa gheto au kwenda sehemu ya peke yangu tu.
 
Nahisi mimi ni Introvert maana napataga shida sana kutongoza wanawake ila cha kushangaza wananitongoza wao wenyewe (wanawake), je hawa wanawake wanaweza kuwa extroverts maana pia wako too loud tunapokuwa faragha au na marafiki, yaani hawana aibu?
 
Dah aisee.

Mawazo, kuwaza Sana hii Hali inaniumiza sana. Nina marafiki wachache na sio mwepesi kushare kila kitu kwa watu.

Sio mwepesi kumzoea mtu, mara nyingi niko kimya, huwezi kunikuta vijieweni mara nyingi.

Kazini dereva wangu ni muongeaji Sana lakini kuna musa naona ananiboa Mana nakua kimya nikitafakari mambo mengi kichwani.

I hate this situation yani,I'm not happy wakati sitakiwi kuwa hivi.

Kipindi flani niko chuo nilienda hospital moja,daktari alivyoniona akaniita akaniuliza unawaza nini?akanipa ushauri na kunisihi nipunguze mawazo,haya maisha yapo tu.its almost 5 years lkn bado nakumbuka ushauri wake.


Sometimes nachukia kuwa introvert Mana nahisi najiua kimya kimya.
 
Hivi kushindwa kusamehe ni tabia ya introvert pia au ni litabia langu tu libaya?. Binafsi huwa sio mtu wa kukasirika kirahisi, mtu anaweza kunifanyia kitu kibaya sana na nikawa namchekea tu. Ila ikitokea siku nikakasirika, hiyo ndo nitolee....hata atembee kwa magoti kutoka kwake hadi nilipo siwezi hata kifikiri kumsamehe.


Huu ni mwezi sasa tangu rafiki yangu wa karibu sana (jinsia ke) anitamkie kauli ambayo sikuipenda (si kauli mbaya sana kiasi hicho na nadhani alisema katika hali ya kunitania), kuanzia siku hiyo nilamfungia vioo. Ametuma meseji kibao akiniomba lakini sijajibu hata meseji moja na sina mpango wa kujibu, amepiga simu sana lakini sipokei na sina mpango wa kupokea. Mpango nilionao ni kumwondoa mbali kabisa na maisha yangu.


Yeye ndiye alikuwa alikuwa rafiki yangu wa pekee wa kike. Tumepitia nyakati nzuri sana na yeye tukiwa kama marafiki wa karibu.


Sasa hivi nimebaki mwenyewe tena, nikiwa alone ni mwendo wa kubadili vifaa tu. Mara nishike simu, mara nishike peni na daftari, mara nitupe peni nichukue penseli, mara nishike pc, mara nishike kitabu.


Ila napenda jinsi nilivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…