Hivi kushindwa kusamehe ni tabia ya introvert pia au ni litabia langu tu libaya?. Binafsi huwa sio mtu wa kukasirika kirahisi, mtu anaweza kunifanyia kitu kibaya sana na nikawa namchekea tu. Ila ikitokea siku nikakasirika, hiyo ndo nitolee....hata atembee kwa magoti kutoka kwake hadi nilipo siwezi hata kifikiri kumsamehe.
Huu ni mwezi sasa tangu rafiki yangu wa karibu sana (jinsia ke) anitamkie kauli ambayo sikuipenda (si kauli mbaya sana kiasi hicho na nadhani alisema katika hali ya kunitania), kuanzia siku hiyo nilamfungia vioo. Ametuma meseji kibao akiniomba lakini sijajibu hata meseji moja na sina mpango wa kujibu, amepiga simu sana lakini sipokei na sina mpango wa kupokea. Mpango nilionao ni kumwondoa mbali kabisa na maisha yangu.
Yeye ndiye alikuwa alikuwa rafiki yangu wa pekee wa kike. Tumepitia nyakati nzuri sana na yeye tukiwa kama marafiki wa karibu.
Sasa hivi nimebaki mwenyewe tena, nikiwa alone ni mwendo wa kubadili vifaa tu. Mara nishike simu, mara nishike peni na daftari, mara nitupe peni nichukue penseli, mara nishike pc, mara nishike kitabu.
Ila napenda jinsi nilivyo.