Benbulugu usifanye Top up.
Riba ikiwa flat au inayopungua.
Haina athari yeyote coz utapata kiasi unachotaka. Ila kuna gharama utalipia.
AKILI BANDIA TUPITE MFANO WA 6M LOAN.
Kaselele amekopa 6M kwa 2yrs, monthly repayments (mr) ni almost 285k. Profit ya benki ni 846k. Loan fee tuseme ni 2.5% yaani 150K.
Akafanya marejesho ya 1yr. Ambayo ni almost 3.423M (kiasi cha mkopo kilicholipwa ni 3M faida ya benki ni 423k)
TAMAA ZA BANDIA.
Kaselele anapata ushawishi wa kijinga kutoka kwa watumishi wenzio anatamani top up, baada ya kupandishwa daraja kazini[emoji6]. Anakuja tufanye top up.
NDANI YA KUMI NA NANE
Benki yangu inamdai #Kaselele 3M haijarejeshwa. Kaselele anataka top up ya 6M.
NOTE: [Kazi ya Credit Officer ni kufanya biashara, masuala ya FL //Financial Literacy kalipie ada ukasome huko kwenye makongamano ya KIDINI. Hope TUGHE, CWT etc waichukue FL kama compulsory kwa wanachama wao].
TUENDELEE.
Mkopo mpya wa
Kaselele utakua ni 3M + 6M = 9M.
TUPIGE HESABU KIDOGO ya miaka 3.
Loan ni 9M kwa 3yrs
Mr itakua 303k
Profit ni almost 1.917M
Fees itakua ni 225k
*****TAFUTA UHALISIA
A) KWENYE MKOPO WA 12M kwa madirisha mawili ya miaka miwilimiwili bila top up, gharama zake zilikua ni (Fees 300k + Benki profit ya almost 1.68M= JUMLA NI 1.98M). Halafu rejesho lilikua 285k jepesi kidogo siyo.
B)KWENYE MKOPO WA 12M wa madirisha mawili yenye top up ndani yake wa miaka 4. Gharama zitakua ni fees (150k+225k= 375K) + Profit 423k + 1.917M = 2.35M JUMLA NI 2.725M. Halafu kuna rejesho la 303K zito kidogo kulinganisha na 285k.
Halafu 1.98M na 2.725M kuna tofauti ya almost 700k.
Niishie hapo kuhusu top up.
Kwa leo inatosha.