King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Kumbe Kumbhu ni pisi kali.Huyu w joberg sio[emoji1787][emoji1787][emoji1787]View attachment 1699866
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe Kumbhu ni pisi kali.Huyu w joberg sio[emoji1787][emoji1787][emoji1787]View attachment 1699866
Wanamuobea wivu khumbu.Mpaka sasa sijaona comment ya mdada humu ndani[emoji4]
Uzamwamwa huo tangulini dumu akamuita dume mwenzake kipenzi naona mmemsahau makonda nyie
Hali ya hewa na vyakula ndio inafanya wawe na ngozi tamu.
Usijali mkuu, tutafika tu hicho kipengele.Shusha masrory mkuu nakufuatilka mwanzo mwisho alooo usisahau 0712 uielezee ulishindwaje
We tulia tutakutag kwenye part ya mwisho nenda kazulule huko kwenye majukwaa mengine sisi tuache hapaFupisha story tunataka mkasa wa kuhatarisha uhai wa mwananchi wa jiwe
🤣🤣🤣🤣🤣🤣Kaka leta vitu
Huyu phumbu hadi aeleweke 🔊
Tangu mwanzo nilishaanza kuhisi Khumbu atakua tu ni Mama wa mtoto au watoto,
Tunafatilia kimya kimya na kwa ukaribu sana 😂 😂😂Mpaka sasa sijaona comment ya mdada humu ndani[emoji4]
Kabla hajasema,kichwani nilishaanza kuhisi na kweli nikakuta ipo hivyo.Umehisi wapi?
Mleta thread kaeleza hii mwanzo kabisa (post ya kwanza): halafu eti wewe umehisi toka mwanzo!
Sasa hapo kwenye hilo neno kula kimasihara mods wangetuekea linki ya ule uzi wetu pendwa kama refferenceInaendelea..
Mapenzi yetu yaliendea vizuri tu japo Khumbu alianza chenga chenga ninapomhitaji siku za weekends. Ilipoingia 2009 nilianza mchakato wa kuingia chuo. Kama mnakumbuka hapo awali nimeelezea kuwa nilipata ufadhili flani japo ulikuwa ni kwa amount ambayo haikidhi tuition fee kwa ujumla wake. Mie target yangu ilikuwa kwanza nipate admission. Vyuo vya South wanaruhusu kulipa kidogo kidogo. Kikubwa tu uwenze kulipa registration fee ili uweze kusajiliwa.
Ukishasajiliwa sasa unaanza kupambana kuhakikisha unamaliza deni lako kabla mwaka haujapinduka, maana usipomaliza deni lako huwezi kusajiliwa kuingia mwaka unaofuata. Siku ya usajili nilienda na Khumbu, dah! ilikuwa ni fahari sana kutinga viwanja vya chuo nikiwa na Khumbu pembeni. Khumbu alikuwa what is called "centre of attraction" Elimu yake ni high school tu lakini alivyo chuma na avyotembea utadhani ana Phd. Mambo ya kujisajili nikayakamilisha, nikaenda workshop kwa masela, na Khumbu akasepa kwao. Wiki kama mbili baada ya usajili masomo yakaanza rasmi. Ilibidi niachane na issue za kuuza viatu, na pia nikawa nimepewa sehemu ya kuishi na hao wafadhili wangu.
Kilikuwa ni kikuwa ni kijumba kidogo chenye chumba na sebule, jiko, bafu na choo. Kule wanaita cottage. Nikawa nimeanza maisha mapya ya kishule shule. Kule workshop nikawa naenda mara moja moja kuwatembelea masela. Masela wakanitungia na jina nikawa naitwa "wakusoma". By the way kule wabongo wote wana majina mapya. Ukienda kule unamtafuta mtu kwa jina unalomjua kutokea bongo huwezi kumpata. Watu wanaitwa wakina "Bozeni, Jakama, the game, etc.
Nilipoanza chuo hela za kuspend na Khumbu zikakata. Ikawa kumuona Khumbu lazima nitumie nguvu sana. Inaweza kukata hata wiki mbili sijamuona. Anyway nilianza kuizoea hiyo hali japo kwa kujilazimisha sana. Masela wangu wa workshop nikawa nawasiliana nao mara moja moja, japo nilipokuwa nafulia ile sana walikuwa wananiungia.
Chuoni nikaanza kupata marafiki wapya. Course niliyokuwa nachukua ilikuwa ya miaka 3. Darasani nilikuwa njema kinoma, kipindi cha tests na mitihani nilikuwa nazungukwa na warembo balaa, wote wanataka kusoma na mimi. Maana kila test tukifanya lazima niongoze, hivyo kila mtu akanijua. Mpaka nilishawahi kula kimashara demu mmoja aliyepata supp hivyo alihitaji nimfundishe hadi night kali.
Itaendelea..