Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Tuendelee...

Mshikaji wangu Sandile alikuwa ni mpiga picha wa gazeti linaitwa Sunday tribute/tribune (nishaanza kusahau), kwa hiyo alikuwa anasoma huku anafanya kazi. Pontsho sasa hivi ni metro police lakini kipindi hicho alikuwa anafanya kazi bank. Hivyo wote wawili walikuwa na usafiri. Ilipokaribia saa 11 Khumbu akapiga simu kuniulizia nipo wapi? Nikamwambia bado nipo chuo ila anielekeze tu yuko wapi tuje tumchukue tusepe nyumbani. Akaniambia yupo stand. Hiyo taxi rank ilikuwa karibu na chuoni kwetu. Hivyo nikawashitua Sandile na Pontsho kuwa tuondokeni, kuna mtu inabidi tumpitie. Tukakubaliana tutumie gari ya Sandile, ya Pontsho tuiache tu huko parking maana italeta usumbufu usio wa lazima. Tukawaaga wana group wenzetu, tukaelelea parking kuchukua usafiri wa Sandile.

Picha linaanza,
Nikawaeleza kuhusu Khumbu kuwa inabidi tumpitie yupo stand, bila hiyana Sandile akawasha gari tukashuka kituoni tukamchukua Khumbu. Khumbu alipoingia kwenye gari nikafanya utambulisho na safari ya kwenda maskani ikaanza. Tukiwa njiani Sandile na Pontsho wakashauliana tupie KFC tununue chakula kabisa maana huko tuendako hakuna mpishi. Basi chakula kikanunuliwa na safari ikaendele. Pale nilipokuwa nakaa kulikuwa na nyumba nyingine inatumika kwa ajili ya mikutano na funguo zake mimi ndio nilikuwa nazo. Tulipofika nikampeleka Khumbu getoni kisha nikaenda kufungua ile nyumba ya mikutano kwa ajili ya kupiga kitabu. Chakula tukagigawa, tulichukuwa kinachotutosha sisi na kingine nikapelekea Khumbu.

Wadhamini wakaanza, Sandile na Pontsho wakawa wananidadisi kuhusu Khumbu. Of course waliona nakula chakula grade one ila nikiwaangalia kwa jicho la tatu nawaona kama wananiona nimepatikana. Khumbu alikuwa demu classic hivyo walikuwa na wasiwasi nimewezaji kummiliki. Nadhani walianza kuunganisha matukio ya mizinga niliyokuwa nawapiga, hivyo walipata jibu hiyo mizinga nilikuwa nagawana na Khumbu. Na kuna siku Sandile alinichana live kwa kuniambia "Konda msafi mie nakusupport financially ila siafiki mahusiano yako na Khumbu, sikupangii nani um-date ila siafiki mahusiano yako na Khumbu". Mie niliamua kumpotezea maana niliona kama ananichuria tu, naanzaje kuiacha ngozi tamu kama hiyo, kama kufa acha nife tu. Maisha menyewe mafupi.

Tulianza kujisomea lakini akili yangu ilikosa utulivu kabisa, maana nilikuwa nawaza kwenda kumtawanya miguu Khumbu. Naona jamaa waliona sina concentration kama wanavyonifahamu, wakaamua tuachane tu na discussion waniache niende nikacheze na makalio ya dada yao.

So discussion ikafa, wakaingia kwenye gari wakasepe, na mie nikachoma ndani.
 
Inaendelea...
Siku niliyotoka na boxer mpaka barabarani kama mtu aliyechanganyikiwa.

Baada ya Khumbu kuendelea kunibania, yaani mpaka nitumie nguvu sana kumfanya akubali kuja kuliwa, niliona napata stress zisizo na faida yoyote. Nikaamua nifanye mazoezi ya kumpotezea ikiwezekana niachane naye kabisa. Sikumbuki vizuri kama nilikuwa bado niko mwaka wa kwanza chuoni au nilikuwa nimeingia mwaka wapili. Khumbu alikuwa haji tena kunitembelea, ilipita karibia miezi miwili sijamuona. Kila nikipiga simu hata haeleweki kabisa.

Kuna siku jamaa zangu wa workshop walinipigia simu wakaniambia Khumbu kapita hapa akiwa na rafiki yake. Wananiambia huenda Khumbu kapata jamaa mwenye cash chafu maana amezidi kupendeza sana. Hayo maneno yaliniumiza sana. Dah! Kumbe Khumbu yupo tu hapa town ila nikimhitaji hataki kuja. Basi nikajikuta mpango wangu wa kutaka kumpotezea umefeli vibaya sana.

Nikaanza kumpigia simu mfululizo ili kumbembeleza japo aje tu nimuone maana nimemmiss ile mbaya plus machungu yakujua kabisa jamaa wenye hela zao wanamla na kushiba. Majibu yakawa yale yale, sometimes hapokei simu au akipokea anakuambia nitakupigia.

Kipindi hicho msela wangu muuza viatu alikuwa tayari keshaingia kwenye biashara ya sembe, na lile goli kamuachia mdogo wake. Sasa kuna siku nilikutana naye mitaa ya home akiwa kwenye rada zake. Anaendesha BMW kali, hata sikumbuki ilikuwa inaitwa jina gani maana hizi gari zina majina yake.

So, tulipokutana nikamkaribisha getoni maana alikuwa hajawahi kufika tokea nimehama kule Rossburg. Baada ya stori mbili tatu akaniachia mpunga wa kutosha. Dah! Nikajisemea moyoni, huu mpunga tunagawana na Khumbu. Swali likabaki Khumbu atajuaje kama nina mpunga? Nikimpigia simu lazima ataleta nyodo zile zile za siku zote. Nikaamua kesho acha niende kwao kabisa, nimfuate huko huko nije naye.

Itaendelea...
 
Lakini bwana konda hicho chumba si ulikihama ukapata nyumba nyingine baada ya kwenda shule?
 
Itupie tu mkuu hawa moderator nawafahamu vizuri.
Ukiomba ruhusa hawakupi ila ukituma hawana noma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…