Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Baby In south Africa girls need money [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji119][emoji119][emoji119]

Dahh makavu live live
 
Inaendelea...
Nikawa narudi kuelekea kwenye gari maana aliyeniita tayari nimeshamjua. Alikuwa huyu jamaa yangu muuza sembe. Nikamfikia, akanionyesha kwa ishara nizunguke upande wa pili niingie kwenye gari. Akaniambia kuna pisi yake ameifata hapo kwenye lile ghorofa la hostel za chuo.

Nikajua tu mwamba anakula mwanachuo mwenzangu. Tulipokuwa ilikuwa ni mita chache tu kufika kwenye hiyo hostel hivyo akakanyaga mafuta na kujisogeza hapo. Kama sekunde chache nikamuona demu anatokea kwenye lile jengo anakuja sehemu tuliyokuwepo, inaonekana tayari alikuwa ameshapigiwa simu na anamsubiria tu jamaa. Jamaa akamfungulia mlango akakaa siti ya nyuma. Mimi nikaendelea kukaa siti ya mbele.

Tokea nimehamia hiyo sehemu jamaa alikuwa hajawahi kufika hivyo akasema acha apite mara moja apajue ninapokaa. Akageuza kipira tukaelekea getoni kwangu. Tukafika home, tukashuka tukamwacha demu kwenye gari. By the way ilikuwa pisi moja kali japo haiwezi kufikia kiwango cha Khumbu.

Tulipoingia ndani, jamaa akakiangalia chumba kisha akanitukana. "Halafu wewe mtoto mbona mshamba sana? Sasa ndio maisha gani haya? Tatizo lako kusoma hicho kichuo chako unajifanya maisha umeyapatiaaa, unatuona sisi ndugu zako tunaoshika haya madude hatufai. Wewe mtoto wa kiume utaogopaje jela? Mbona watu kibao tu wanasoma na wanafanya mishe zao? Hebu twende zetu nikakupe gheto ukae huko". Basi nikachukua baadhi ya nguo tukatoka, tukaingia garini tukasepa.

Jamaa akanipeleka kwenye suburb moja hivi nimeisahau jina lake. Tukafika kwenye complex moja hivi. Alikuwa na disc ya kufungulia geti. Akafungua geti tukachoma ndani. Akapaki gari, tukashuka ila demu akaendelea kubaki garini. Tukaingia mjengo mmoja hatari una kila kitu ndani.

Mjengo ulikuwa wa vyumba vitatu. Kila chumba ni master bedroom. Sebuleni kulikuwa na TV kubwa sana inatumia king'amuzi cha DSTv, ni vile ving'amuzi unavyoweza kurecord na kuona vipindi hadi vitatu vitakavyofuatia ukiponyeza kitufe cha info. Nyumba safi inanukia utuli. Halafu hakukuwa na mtu yoyote anaishi. Jamaa akanimbia utakaa hapa. Tukaagana, akaniachia remoti ya kufungulia geti na hela kidogo akasepa.

Itaendelea..
 
Sasa hapa kudadadeki mmeweza kumpata Sandile Ndlovu huenda hata mimi mtanipata. Sasa sijui niachane na hii stori maana kuna matukio watu wanaonijua wataanza kunishangaa. Au nitaachana na hayo matukio???
Hii imekuwa rahisi sana manake umegive away key details.
Na wabongo wanavyopemba umbea wamejaza traces zao Google.
Yaani ukiandila sandile tu inakuja search history sandile ndlovu photographer.
[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom