Kuna watu wanasema hii stori ni chai kwa kutokuamini kwamba Mayor hawezi kumdate Khumbu. Jamani kwanza Mayor ni diwani tu (local concilor) kama alivyokuwa Baba Levo wa Wasafi. Baba levo alikuwa diwani wa Kigoma hivyo baraza la madiwani lingeweza kumchagua kuwa mayor. Kwa hiyo mayor ni mtu mdogo tu. Pili wanasiasa wa nchi za wenzetu hawana makuu kama wa kwetu huku. Huyo mayor, binafsi namfahamu. Alikuwa ananyoa kwenye saluni ya mshikaji wetu mburundi. Kinyozi wake ndio alikuwa pia kinyozi wangu. Kwenye hiyo saluni tulikuwa tunanyoa bure tu. Mnamkumbuka yule mburundi tuliyekuwa tunaishi naye kule Rossburg pamoja na baba Isa? Huyo mburundi alikuwa ni mmojawapo wa vinyozi wa hiyo saluni.