Kama mtu ataniomba nimwelezee Khumbu kwa maneno machache, haya ndio naweza kusema Khumbu alikuwa mwanamke wa aina gani: Khumbu alikuwa na roho nzuri sana, mcheshi. Alikuwa ni mtu mwenye huruma, unlike wasichana wengine alikuwa hapendi kuniona nadhalilishwa. Kuna siku tulikuwa kwenye daladala, kuna vijana walianza kuniongelea vibaya aliwapa vidonge vyao hadi abiria wote kwenye daladala wakamuunga mkono. Alikuwa hapendi kutumia hela yangu vibaya, mara nyingi sana alikuwa anakataa nisimnunulie chakula cha kwenye migahawa badala yake anasema twende supermarket tukanunue chakula tukapike wenyewe kupunguza gharama. Kule Rossburg pamoja na kwamba nilikuwa nalala kwenye kistore, godoro chini na kidirisha kimepasuliwa lakini hakujali. Akinizingua nilikuwa nanuna na kumchunia lakini nikimmiss na kuamua kumpigia alikuwa haendelezi ligi, alikuwa anaonyesha pia kunimiss maana alikuwa anakuja mara moja kama vile alikuwa anaombea nimpigie. Mara nyingi sana nilishamdhalilisha kwa maneno ya matusi, na alikuwa anachukia sana lakini hakuwahi kunitukana au kunidhalilisha kwa namna yoyote ile. Kila nikitafakari huwa naona alikuwa na mapungufu ya kawaida tu kama ilivyo kwa wanawake wengi. Swala la yeye kutokuja Bloemfontein na kuninyima k siku ile naondoka ni mapungufu ya wanawake wengi. Wanawake wanaojiona wazuri wana kawaida ya kujifanya wagumu kutoa mchezo hata kama anakupenda, Khumbu is not exceptional.