tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,843
- 29,350
Mjini shule. Ndivyo unavyoweza kusema. Ukija mjini njoo na akili usije na jembe. Huku mjini ni mahali pa kutumia akili zaidi kuliko nguvu.
Kuna aina mpya ya utapeli imeibuka hapa mjini kupitia michango feki ya harusi. Mtu akijiona amepigika sana kimaisha hutafuta senti kidogo za kuchapisha kadi za harusi kisha huanza kuwapigia simu ndugu, jamaa, marafiki na classmates zake kuomba "michango" ili kuhalalisha utapeli wake.
Watu hukamuliwa michango kama yote. Ndugu mmoja alituchangisha eti harusi ya Tshs 60m, tukanywe juice na sambusa eti akisema modern weddings hakuna mavyukula, next day akaja nimsaidie dealer ampe gari Vanguard! A week later he had a brand new model Subaru in town, shamelessly.
Na wakitaka kukupiga vizuri wanakuambia harusi hii itafanyikia huko kijijini Karagwe. Wanafanya hivi kwa makusudi ili kukupoteza maboya kwa kuwa wakisema harusi hiyo itafanyikia mjini, unaweza kuwashtukia haraka.
MAONI YANGU
Ndugu, jamaa au rafiki yeyote akikupigia simu, hasa wale ndugu na marafiki wa mbali ambao hamuwasiliani mara kwa mara, hebu jiridishe kwanza kama hiyo harusi ni genuine au ni ya mchongo. Usipokuwa makini utapigwa pesa mpaka utachakaa huku watu wakiendesha magari mazuri mjini na kula bata kila kona ya jiji kwa pesa zako.