Atakuambia anaenda kubariki ndoa kijijini kwao, hivyo anaomba michango kufanikisha hilo jambo. Rudia kusoma uzi mkuu.
Mbinu za manara hizo.Mjini shule. Ndivyo unavyoweza kusema. Ukija mjini njoo na akili usije na jembe. Huku mjini ni mahali pa kutumia akili zaidi kuliko nguvu.
Kuna aina mpya ya utapeli imeibuka hapa mjini kupitia michango feki ya harusi. Mtu akijiona amepigika sana kimaisha hutafuta senti kidogo za kuchapisha kadi za harusi kisha huanza kuwapigia simu ndugu, jamaa, marafiki na classmates zake kuomba "michango" ili kuhalalisha utapeli wake.
View attachment 3653099
Watu hukamuliwa michango kama yote. Ndugu mmoja alituchangisha eti harusi ya Tshs 60m, tukanywe juice na sambusa eti akisema modern weddings hakuna mavyukula, next day akaja nimsaidie dealer ampe gari Vanguard! A week later he had a brand new model Subaru in town, shamelessly.
Na wakitaka kukupiga vizuri wanakuambia harusi hii itafanyikia huko kijijini Karagwe. Wanafanya hivi kwa makusudi ili kukupoteza maboya kwa kuwa wakisema harusi hiyo itafanyikia mjini, unaweza kuwashtukia haraka.
MAONI YANGU
Ndugu, jamaa au rafiki yeyote akikupigia simu, hasa wale ndugu na marafiki wa mbali ambao hamuwasiliani mara kwa mara, hebu jiridishe kwanza kama hiyo harusi ni genuine au ni ya mchongo. Usipokuwa makini utapigwa pesa mpaka utachakaa huku watu wakiendesha magari mazuri mjini na kula bata kila kona ya jiji kwa pesa zako.
Na yalivyo manyumbu yanashindana kweli kutoa .🤣🤣🤣🤣🤣🤣mashabiki wa simba na yanga njooni apa tuone nani atatoa nyingi😃
Kwenye 60M ulitoa kiasi gani?Mkuu isije ikawa nawe ni mmoja wao umekuja kututuliza ili muendelee kutukamua. Tumechoka jamani, hebu mtupumzishe kidogo!
Nimekuambia juzi watu tumekamuliwa Tsh 60m, jamaa ameenda kununua prado. Unataka tuendelee kukamuliwa mpaka lini?
Mkuu hatujaelewana kitu kimoja. Sikatai kuchangia sherehe halali na za kweli. Ninachokataa ni kuchangia "sherehe hewa" na za kitapeli. Nikisema sherehe hewa unanielewa mkuu?Concern yangu ipo hapo kwamba lets assume una mama zako wadogo kwa wakubwa labda 8 wana watoto wao wa kike labda total 20 kwa hiyo idari hata average ya kuolewa ni tuseme wawili kila mwaka so je kumchangia ndugu yako laki kwa mwaka ni kitu kibaya sana?ngapi tunapoteza kila siku au nyie wenzangu vipato vyenu vipoje mimi kila mwezi sijisifii ila nazipend kwenye mambo tu ya starehe pesa nyingi sana sasa kutoa 50000 ya mchango si kitu cha kawaida sana hata kama harusi ziwe tatu kwa mwaka
Hata akina Wema na Zuku wa Daimond wanatumia mbinu hizo kuwapiga nyumbu hela. Juzi Wema katangaza sherehe ya 40 ya mwanaye ameweka kiingilio hadi 5M na mijitu inatoa kama kawaida. Mungu anajua kuibariki mijitu isiyojua matumizi sahihi ya pesa. Wazungu wana sema: "Fortune favours fools." Sijui hata inakuwaje.Mbinu za manara hizo.
Nilitoa laki 5 mkuu. Lakini kinachoniuma sio kiasi cha mchango nilichotoa bali ni utapeli tuliofabyiwa na huyu bwana. Haipendezi kuwachangisha watu fedha kwa sherehe feki na pia kuweka bajeti kubwa lakini unatumia pesa kidogo huku ukibaki na kiasi kikubwa cha fedha kwa manufaa yako binafsi. Huu ni utapeli kama utapeli mwingine. Naiomba serikali itusaidie katika hili.Kwenye 60M ulitoa kiasi gani?
Hiyo sherehe haikua na kamati?
Kwenye zawadi pia kwani mnalazimishwa kutoa ama ni hiari ?
Binafsi nilivyoona heading nikajua mmechangishwa kisha ndoa ikaota mbawa.
NB:sikatai kwenye mambo mengi kuna upigaji hata harusi uliyoitaja,kuna sehemu nilikwenda kufanya kazi wiki hii wenyeji wakawa wanamjadili binti mmoja anapokea michango ya sendoff ila wao wanadai hata mchumba hana!
Hata manabii feki hutumia mbinu ya kuuza mafuta ya upako na kuwapiga hela nyumbu wa mjini. Tazama Mwamposa anavyotajirika kwa kuuza mafuta ya korie kijiko kimoja tu 1000! Na wakati yeye akiuza mafuta anatajirika na kujenga hoteli za kitalii, anawadanganya waumini wake wasiwekeze bali wanunue tu mafuta watatajirika. Ngoja wapigwe hadi akili ziwakae sawa.😂 Mjini shule, Ukipata wajinga wajinga wa kuwanyoosha, ww wanyooshe tuu kmmk zao
Kwani kuchangia harusi ni lazimaa??Mjini shule. Ndivyo unavyoweza kusema. Ukija mjini njoo na akili usije na jembe. Huku mjini ni mahali pa kutumia akili zaidi kuliko nguvu.
Kuna aina mpya ya utapeli imeibuka hapa mjini kupitia michango feki ya harusi. Mtu akijiona amepigika sana kimaisha hutafuta senti kidogo za kuchapisha kadi za harusi kisha huanza kuwapigia simu ndugu, jamaa, marafiki na classmates zake kuomba "michango" ili kuhalalisha utapeli wake.
View attachment 3653099
Watu hukamuliwa michango kama yote. Ndugu mmoja alituchangisha eti harusi ya Tshs 60m, tukanywe juice na sambusa eti akisema modern weddings hakuna mavyukula, next day akaja nimsaidie dealer ampe gari Vanguard! A week later he had a brand new model Subaru in town, shamelessly.
Na wakitaka kukupiga vizuri wanakuambia harusi hii itafanyikia huko kijijini Karagwe. Wanafanya hivi kwa makusudi ili kukupoteza maboya kwa kuwa wakisema harusi hiyo itafanyikia mjini, unaweza kuwashtukia haraka.
MAONI YANGU
Ndugu, jamaa au rafiki yeyote akikupigia simu, hasa wale ndugu na marafiki wa mbali ambao hamuwasiliani mara kwa mara, hebu jiridishe kwanza kama hiyo harusi ni genuine au ni ya mchongo. Usipokuwa makini utapigwa pesa mpaka utachakaa huku watu wakiendesha magari mazuri mjini na kula bata kila kona ya jiji kwa pesa zako.
Kuna nabii nadhani kama sio mwamposa bc n kakobe, yeye binafsi hana akaunti ya benki ila pesa zake zote zipo kwenye akaunti ya benki ya kanisa lake, ili kuepuka kulipa kodi mana sadaka hazilipishwi kodi.Hata manabii feki hutumia mbinu ya kuuza mafuta ya upako na kuwapiga hela nyumbu wa mjini. Tazama Mwamposa anavyotajirika kwa kuuza mafuta ya korie kijiko kimoja tu 1000! Na wakati yeye akiuza mafuta anatajirika na kujenga hoteli za kitalii, anawadanganya waumini wake wasiwekeze bali wanunue tu mafuta watatajirika. Ngoja wapigwe hadi akili ziwakae sawa.
Kama kahusika moja kwa moja jamaa kafeli,ila yaweza kuwa shida ni wanakamati.Nilitoa laki 5 mkuu. Lakini kinachoniuma sio kiasi cha mchango nilichotoa bali ni utapeli tuliofabyiwa na huyu bwana. Haipendezi kuwachangisha watu fedha kwa sherehe feki na pia kuweka bajeti kubwa lakini unatumia pesa kidogo huku ukibaki na kiasi kikubwa cha fedha kwa manufaa yako binafsi. Huu ni utapeli kama utapeli mwingine. Naiomba serikali itusaidie katika hili.
Mkuu, katika kesi za utapeli kama hizi kunakuwa hakuna kamati. Tapeli anapita mwenyewe kugawa kadi na kukusanya michango au anaunda gurupu la whatsapp na kuanza kuwakamua watu bila huruma.Kama kahusika moja kwa moja jamaa kafeli,ila yaweza kuwa shida ni wanakamati.
Kuna watu ndio harakati zao hizi unaweza kuona wanajitoa kumbe wananufaika kwa namna fulani.
Binafsi hizi harusi napenda iandaliwe kinyumbani hasa upande wa vyakula yaani waalikwa wanashiriki maandalizi na si kamati pekee.