Jinsi matapeli wa mjini wanavyotumia "harusi" kupiga pesa; inauma sana

Jinsi matapeli wa mjini wanavyotumia "harusi" kupiga pesa; inauma sana

Mbona hii mbinu ni ya kizamani sana
Jack Pemba mimi namjua tokea utotoni tunaishi nae Upanga, na hii ndio njia ilimpatia nauli ya kwenda UK.
Mkuu Makebo huu ndio utapeli mpya wa mujini. Watu wanakunja hela kiulaini bila jasho. Ni kadi yako tu na sio lazima umpelekee hard copy. Unamtumia tu kwa WhatsApp unalamba hela.
 
Mjini shule. Ndivyo unavyoweza kusema. Ukija mjini njoo na akili usije na jembe. Huku mjini ni mahali pa kutumia akili zaidi kuliko nguvu.

Kuna aina mpya ya utapeli imeibuka hapa mjini kupitia michango feki ya harusi. Mtu akijiona amepigika sana kimaisha hutafuta senti kidogo za kuchapisha kadi za harusi kisha huanza kuwapigia simu ndugu, jamaa, marafiki na classmates zake kuomba "michango" ili kuhalalisha utapeli wake.

View attachment 3653099

Watu hukamuliwa michango kama yote. Ndugu mmoja alituchangisha eti harusi ya Tshs 60m, tukanywe juice na sambusa eti akisema modern weddings hakuna mavyukula, next day akaja nimsaidie dealer ampe gari Vanguard! A week later he had a brand new model Subaru in town, shamelessly.

Na wakitaka kukupiga vizuri wanakuambia harusi hii itafanyikia huko kijijini Karagwe. Wanafanya hivi kwa makusudi ili kukupoteza maboya kwa kuwa wakisema harusi hiyo itafanyikia mjini, unaweza kuwashtukia haraka.

MAONI YANGU
Ndugu, jamaa au rafiki yeyote akikupigia simu, hasa wale ndugu na marafiki wa mbali ambao hamuwasiliani mara kwa mara, hebu jiridishe kwanza kama hiyo harusi ni genuine au ni ya mchongo. Usipokuwa makini utapigwa pesa mpaka utachakaa huku watu wakiendesha magari mazuri mjini na kula bata kila kona ya jiji kwa pesa zako.​
Kama alikuchangia kwanini ww usimchangie hata akienda kubetia ni haki yake
 
Eeh bwana hii harusi ya mjini ni uwanja wa kukimbizana ubavu kweli. Wale MC wanauliza "mchumba wa mwisho ni nani" hivi watu wanatolea pesa kama si hela zao, kumbe usiku wanalia kwenye kona. Niliona juzi mmoja akitoa laki tatu huku amevaa kiatu cha kupasuka, akili iliniuma. ngoma
 
Mkuu watu maskini wanapenda sifa sana. Haya mambo huwezi kuyakuta kwa matajiri.
 
Kinachofanya kuwe na gharama kwenye HARUSI ni nini mpaka muhusika achangiwe?. Sichangii HARUSI. Naamini muhusika alipaswa kujipanga namna sherehe yake itakavyokuwa kulingana na uwezo wake.
Sio uungwana unapiga hesabu zako za bajeti alafu unatafuta watu wakukufikisha kwenye lengo. Hata kama sio utapeli sio uungwana pia.

Sasa pesa ni kuchangie na muda wangu siku ya tukio niwepo ? Kivipi sasa.

View: https://x.com/PresenterNoah/status/2089393879460028585
 
Hakuna hela yeyote wanayopiga
Kunakuwa na kamati hiyo kamati inapanga kila kitu

inaundwa group, michango inawekwa wazi kamati inakuwa kazini

Ushauri wangu usitegemee utapata hela kupitia harusi sio kwa watu masikini.. utazidi kujipa umasikini

Pia mleta mada kama unaona 150 000 ni nyingi kumchangia mtu mweleze ukweli

Mimi sipendi masherehe ila anayependa kufanya kusherekea harusi na watu wake wa karibu kuna ubaya gani?

Unachosahau mchango wako ji deni kama una mtoto au ndugu au wewe itarudishwa tu

Kuwa kama mwana FA ashasema hachangii harusi...halalamiki😀

Kama unaona ni dili la hela weka ya kwako watu wamimine hela...

Niandike Gily 300,000/- ahadi
Mtu unakosa aibu ya kutaka michango tena unaweka na kiasi huku ndoa ni yako na unaenda kufaidi ama kuumia peke yako?

Ndoa sio msiba useme kwamba ni ghafla. Ndoa ni maandalizi ya muda mrefu hivyo muoaji jiandae pele yako ualike tu watu ama ufanye kivyako vyako usisumbue watu na michango ya kipuuzi.

Binafsi nilijiamdaa mwenyewe vya kutosha kuanzia mahari hadi sherehe yenyewe watu wakaja kula na kunywa basi.

Kama hujajipanga acha kusumbua watu na utapeli wa michango.
 
Binafsi najisikia aibu kumuomba mtu mchango eti kisa naoa. Hii ni maajabu yaani starehe zangu binafsi nisumbue watu hadi kusababisha watu kukopa na kujiweka kwenye madeni? Big No.

Nipo na wake wawili na wote nilijifanyia maandalizi mwenyewe kuanzia mahari, ukumbi hadi sherehe nzima watu wakaalikwa kuja kula na kunywa na walijiuliza hili limewezekanaje maana walizoea kuona watu wanachangishana michango ya harusi.

Ni aibu na fedheha mwanaume kuwa na mke ndani huku ukijua kabisa bila michango ya watu usingefanikiwa kuwa naye.

Matokeo yake unagongewa mke maana ni mke wa wengi walifanikisha wewe kumuweka ndani. Pathetic.
 
Mjini shule. Ndivyo unavyoweza kusema. Ukija mjini njoo na akili usije na jembe. Huku mjini ni mahali pa kutumia akili zaidi kuliko nguvu.

Kuna aina mpya ya utapeli imeibuka hapa mjini kupitia michango feki ya harusi. Mtu akijiona amepigika sana kimaisha hutafuta senti kidogo za kuchapisha kadi za harusi kisha huanza kuwapigia simu ndugu, jamaa, marafiki na classmates zake kuomba "michango" ili kuhalalisha utapeli wake.

View attachment 3653099

Watu hukamuliwa michango kama yote. Ndugu mmoja alituchangisha eti harusi ya Tshs 60m, tukanywe juice na sambusa eti akisema modern weddings hakuna mavyukula, next day akaja nimsaidie dealer ampe gari Vanguard! A week later he had a brand new model Subaru in town, shamelessly.

Na wakitaka kukupiga vizuri wanakuambia harusi hii itafanyikia huko kijijini Karagwe. Wanafanya hivi kwa makusudi ili kukupoteza maboya kwa kuwa wakisema harusi hiyo itafanyikia mjini, unaweza kuwashtukia haraka.

MAONI YANGU
Ndugu, jamaa au rafiki yeyote akikupigia simu, hasa wale ndugu na marafiki wa mbali ambao hamuwasiliani mara kwa mara, hebu jiridishe kwanza kama hiyo harusi ni genuine au ni ya mchongo. Usipokuwa makini utapigwa pesa mpaka utachakaa huku watu wakiendesha magari mazuri mjini na kula bata kila kona ya jiji kwa pesa zako.​
Manina mimi sijawahi mchangia mtu namimi nilipooa hakuna michango ni simple like that,, Kila mtu aishi maisha yake, an unaoa kwa budget ambazo hazipo ndani ya uwezo wako ili uibuke kimaisha,, hakuna wa kunipata uzuri maisha yangu na sherehe ni paka na panya
 
Back
Top Bottom