Antennah
JF-Expert Member
- Oct 14, 2015
- 7,035
- 9,279
mmmmhhhWe changia tu mungu atakulipa
mmmmhhhWe changia tu mungu atakulipa
Mkuu wewe ni mimi kabisa. Huwa sishiriki mashindano ya rejareja kama haya. Hata kanisani wachungaji hupenda kuyatumia wakati wa kuchangisha michango mbalimbali. Mimi nabaki kuwa mtazamaji tu!😂😅🤣mbinu ya kipumbavu kabisaa hiiii,,, mi naistukiaga mapema...naweka ushabiki wote pembeni najituliza tuliiiii
Unaweza usijiunge na kikundi chochote lakini, from no where, ukajikuta unaletewa kadi mkuu.Ili usiweze kuchanga mchango wa harus hakikisha hauwekwi wala kujiunga kwenye kikundi chochote cha kusaidiana kwenye shida na raha au toka utokewe,iwe kazini,mtaani,makanisani (uwe mwenyewe tu kwenye mambo zako)
Kinachofanya kuwe na gharama kwenye HARUSI ni nini mpaka muhusika achangiwe?. Sichangii HARUSI. Naamini muhusika alipaswa kujipanga namna sherehe yake itakavyokuwa kulingana na uwezo wake.Mjini shule. Ndivyo unavyoweza kusema. Ukija mjini njoo na akili usije na jembe. Huku mjini ni mahali pa kutumia akili zaidi kuliko nguvu.
Kuna aina mpya ya utapeli imeibuka hapa mjini kupitia michango feki ya harusi. Mtu akijiona amepigika sana kimaisha hutafuta senti kidogo za kuchapisha kadi za harusi kisha huanza kuwapigia simu ndugu, jamaa, marafiki na classmates zake kuomba "michango" ili kuhalalisha utapeli wake.
View attachment 3653099
Watu hukamuliwa michango kama yote. Ndugu mmoja alituchangisha eti harusi ya Tshs 60m, tukanywe juice na sambusa eti akisema modern weddings hakuna mavyukula, next day akaja nimsaidie dealer ampe gari Vanguard! A week later he had a brand new model Subaru in town, shamelessly.
Na wakitaka kukupiga vizuri wanakuambia harusi hii itafanyikia huko kijijini Karagwe. Wanafanya hivi kwa makusudi ili kukupoteza maboya kwa kuwa wakisema harusi hiyo itafanyikia mjini, unaweza kuwashtukia haraka.
MAONI YANGU
Ndugu, jamaa au rafiki yeyote akikupigia simu, hasa wale ndugu na marafiki wa mbali au ambao hamjawasiliana nao muda mrefu, hebu jiridishe kwanza kama hiyo harusi ni genuine au ni utapeli. Usipokuwa makini utapigwa mpaka utachakaa huku watu wakiendesha magari mazuri mjini na kula bata kila kona ya jiji kwa pesa zako.
Mtu anaweza akaunda hata sherehe 3 kwa mwaka na zote anakamua pesa kisawasawa. Mwezi wa kwanza unapata mwaliko wa harusi, mwezi wa 8 kipaimara, na mwezi wa 12 kubariki ndoa. Jamani tumechoka!amini kwamba mwmba. harusi siku hizi ni chanzo kizuri sana cha mapato kwa wajanja wa mjini
Ni ajabu mtu anaanda harusi ya 60M lakini anatumia only 20M huku 40M inayobaki anatanulia mjini. Hii sio sawa hata kidogo mkuu.Kinachofanya kuwe na gharama kwenye HARUSI ni nini mpaka muhusika achangiwe?. Sichangii HARUSI. Naamini muhusika alipaswa kujipanga namna sherehe yake itakavyokuwa kulingana na uwezo wake.
Sio uungwana unapiga hesabu zako za bajeti alafu unatafuta watu wakukufikisha kwenye lengo. Hata kama sio utapeli sio uungwana pia.
Sasa pesa ni kuchangie na muda wangu siku ya tukio niwepo ? Kivipi sasa.
Nilikuwa nakuja kuwaletea kadi humu aiseeh😄😀😀
Double 100k
Single 70k
Alafu harusi Chome huko upareni Mililani. Nione mkija
Mgodi wa GGM au Ulyankuru mkuu?
Yeye kwenye harusi ali plead kama milioni tano ili kuweka ulimbo wa kuwavuta watu wachangie. Kamati ikaweka bajeti kama milioni 45. Mwisho wa siku wachangiaji wakachanga chini ya kiwango na huku walishakodi maukumbi,MC na watu wa chakula. ilibidi akakope kausha damu kmmk.Hayo madeni yaliingiaje wakati yeye ndiye aliyekuwa anachangisha fedha mkuu?
Eneo gani hilo mkuu? Ni Morogoro au wapi? Anyway, tumuache Robert Heriel Mtibeli aje kutuelekeza🤣😅😂Aaah, ulikua wapi weye? Mtibeli eneo lake lilibahatika kugundulika madini
Mara wanaweka derby ya simba na yanga kwenye kukusanya pesa2000s kurudi nyuma, watu walikuwa wanakuja na vitu vya kushikika kama zawadi kwenye harusi, mfano mkungu wa ndizi, pasi ya kunyooshea nguo
Leo eti unakuta MC anashindanisha watu nani atatoa pesa ndefu na kuwa kejeli wenye pesa ndogo.
Du! Kiherehere hakijawahi kumuacha mtu salama aisee!😂😅🤣Yeye kwenye harusi ali plead kama milioni tano ili kuweka ulimbo wa kuwavuta watu wachangie. Kamati ikaweka bajeti kama milioni 45. Mwisho wa siku wachangiaji wakachanga chini ya kiwango na huku walishakodi maukumbi,MC na watu wa chakula. ilibidi akakope kausha damu kmmk.
Upo sahihi kabisa mkuu. Juzi Ronaldo alimaliza harusi yake mwenyewe bila kuwasumbua watu. Hata mama yake hakuhusishwa na wala hakushiriki.Siwezi kuchangia harusi na sijawahi, yaani uamue kuoa kwa sherehe kubwa kwa kutegemea hela za wengine huo ni wazimu. Nilioa sikuchangisha mtu na sichangii mtu. Kuna jamaa yangu hadi leo ana madeni makubwa kwa kutegemea michango ya harusi.