Hao maMC nao wanakuwa wamepewa semina behind the scene jinsi ya kuhamasisha ukamuaji. Event ikifika tamati huitwa chobingo kulamba mgao. Utapeli mtupu!2000s kurudi nyuma, watu walikuwa wanakuja na vitu vya kushikika kama zawadi kwenye harusi, mfano mkungu wa ndizi, pasi ya kunyooshea nguo
Leo eti unakuta MC anashindanisha watu nani atatoa pesa ndefu na kuwa kejeli wenye pesa ndogo.
Ni utapeli amid hali hii ngumu ya uchumuHao maMC nao wanakuwa wamepewa semina behind the scene jinsi ya kuhamasisha ukamuaji. Event ikifika tamati huitwa chobingo kulamba mgao. Utapeli mtupu!
mashabiki wa simba na yanga njooni apa tuone nani atatoa nyingi😃2000s kurudi nyuma, watu walikuwa wanakuja na vitu vya kushikika kama zawadi kwenye harusi, mfano mkungu wa ndizi, pasi ya kunyooshea nguo
Leo eti unakuta MC anashindanisha watu nani atatoa pesa ndefu na kuwa kejeli wenye pesa ndogo.
mungu anaingiaje tena hapo🤣We changia tu mungu atakulipa
Mkuu isije ikawa nawe ni mmoja wao umekuja kututuliza ili muendelee kutukamua. Tumechoka jamani, hebu mtupumzishe kidogo!Pia mleta mada kama unaona 150 000 ni nyingi kumchangia mtu mweleze ukweli
Mimi sipendi masherehe ila anayependa kufanya kusherekea harusi na watu wake wa karibu kuna ubaya gani?
Mjini shule. Ndivyo unavyoweza kusema. Ukija mjini njoo na akili usije na jembe. Huku mjini ni mahali pa kutumia akili zaidi kuliko nguvu.
Kuna aina mpya ya utapeli imeibuka hapa mjini kupitia michango feki ya harusi. Mtu akijiona amepigika sana kimaisha hutafuta senti kidogo za kuchapisha kadi za harusi kisha huanza kuwapigia simu ndugu, jamaa, marafiki na classmates zake kuomba "michango" ili kuhalalisha utapeli wake.
View attachment 3653099
Watu hukamuliwa michango kama yote. Ndugu mmoja alituchangisha eti harusi ya Tshs 60m, tukanywe juice na sambusa eti akisema modern weddings hakuna mavyukula, next day akaja nimsaidie dealer ampe gari Vanguard! A week later he had a brand new model Subaru in town, shamelessly.
Na wakitaka kukupiga vizuri wanakuambia harusi hii itafanyikia huko kijijini Karagwe. Wanafanya hivi kwa makusudi ili kukupoteza maboya kwa kuwa wakisema harusi hiyo itafanyikia mjini, unaweza kuwashtukia haraka.
MAONI YANGU
Ndugu, jamaa au rafiki yeyote akikupigia simu, hasa wale ndugu na marafiki wa mbali au ambao hamjawasiliana nao muda mrefu, hebu jiridishe kwanza kama hiyo harusi ni genuine au ni utapeli. Usipokuwa makini utapigwa mpaka utachakaa huku watu wakiendesha magari mazuri mjini na kula bata kila kona ya jiji kwa pesa zako.
The point ni hiyari kuchangiaMkuu isije ikawa nawe ni mmoja wao umekuja kututuliza ili muendelee kutukamua. Tumechoka jamani, hebu mtupumzishe kidogo!
Nimekuambia juzi watu tumekamuliwa Tsh 60m, jamaa ameenda kununua prado. Unataka tuendelee kukamuliwa mpaka lini?
Safari hii hatukubali kutapeliwa mkuu. Tutachanga lakini lazima tumtume spy aje kuchunguza kama kweli harusi imefanyika na atutumie video ili tujiridhishe. Harusi isipofanyika unarudisha fedha zetu.Nilikuwa nakuja kuwaletea kadi humu aiseeh😄😀😀
Double 100k
Single 70k
Alafu harusi Chome huko upareni Mililani. Nione mkija
Hapo sawa mkuu. Tunaogopa kutapeliwa. Kama mmeamua kuendesha harusi yenu kama Ronaldo ni sahihi kabisa.The point ni hiyari kuchangia
Juzi tumefanya shughuli ya ndugu yangu wa kuzaliwa tumetoa hela mfukoni hakuna hata mmoja aliyechangishwa
Ila sipingi kichangia, nachangia kwa hiari