IKUNGURU IJIRU CHUKU
JF-Expert Member
- Feb 27, 2021
- 484
- 545
RAIS ALLY HASSAN MWINYI
Alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi mwaka 1983 kama sijakosea nafasi yake aliteuliwa mzee mmoja kutoka zanzibar anaitwa mzee Natepe kushika uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi.
Natepe alipoingia tu ofisini alimtaka Waziri aliyemtangulia kutoka katika nyumba ya Waziri ili yeye aweze kukaa hapo kama Waziri.
Ilikuwa shida kidogo maana waziri aliyeondoka bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka kutoka na Natepe.
Ikampasa Mzee Mwinyi kutoka kwa haraka na siku anatoka pale nyumbani alikuwa amenunua mabati 150 na mifuko ya saruji 100 ya kwake wala sio mali ya Serikali.
Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya Serikali. Kweli mzee Mwinyi akaviacha akaondoka.
Baada ya miaka kadhaa tu Mzee Mwinyi akateuliwa kuwa Rais wa Zanzibar.
Natepe wakati ana jifikiria jinsi ya kwenda kumpongeza na kumuomba radhi kwa aliyomfanyia kabla ya kufikiria njia Mzee Mwinyi akaletwa bara mwaka 1985 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hapa sasa Natepe akajua kazi hana na atatimuliwa haraka iwezekanavyo tena na kutengwa na nyadhifa za JMT kwa kuwa kuna mabaya ya wazi na ya sirini aliyomtendea Mzee mwinyi.
Mzee Mwinyi baada tu ya kuapishwa kuwa Rais wa JMT wakati anateua Baraza la Mawaziri akamteua tena Natepe kuwa Waziri pale pale mambo ya ndani.
Siku ya kumuapisha akamwambia Natepe siyo kwamba nakupenda sana hapana ila napenda kazi yako unavyofanya endelea kufanya kazi.
Siku moja Mzee Mwinyi yupo Ikulu kapumzika akaona malori yanaingia na akaambiwa mzigo wako huu. Mh Rais akashtuka mbona sijaagiza kitu mie??
Ndipo akaambiwa umetoka kwa Natepe Mzee Mwinyi akacheka sana akawaambia wasaidizi wake shusheni mabati 150 na saruji 100 hizo ndio haki yangu zingine mrudishieni tu.
Hapa kuna somo kubwa Sana. Ubaya hulipwa kwa Wema na Maisha hayana Mwalimu.
Kwa ujumbe huu nasi tujifunze mengi.
MUWE NA MWAKA WA BARAKA NYOTE!!
Tunapoanza mwaka mpya wa 2022 jitahidi kutolipa mabaya kwa mabaya
ASOMAYE na AFAHAMU.