Jinsi Natepe alivyomhenyesha Rais Ali Hassan Mwinyi

Story ya uongo na ya kutungwa
Mzee Mwinyi alijiuzulu 1976 sio 1983
Mkuu Pohamba , ni kweli huyu Konzo Ikweta ni muongo!. 1976 ni mwaka wa tukio lililosabisha Mwinyi kujiuzulu, ila alijiuzulu mwaka 1977. Aliyemtimua kwenye nyumba ni Jackson Makweta.

Watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe Mwanza, Masanja Makhulla Mazengenuka na Issac Mwana Mkoboko, walifariki kwa mateso katika mahojiano na polisi eneo la Kigoto.

Kufuatia vifo hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi alijiuzulu, IGP, Samuel Pundugu, Director wa Tiss, Emilio Mzena, na Mkuu wa Mwanza, Peter Kisumo wakastaafishwa kwa manufaa yang umma. Mzee wangu, RSO wa Mwanza, RPC wa Mwanza, DSO wa Mwanza na OCD wa Mwanza wakashitakiwa kwenye ile Kesi ya Mauaji Mwanza.

P
 
Mkuu Pohamba, 1976 ni mwaka wa tukio lililosabisha Mwinyi kujiuzulu.

Sawa Mkuu
 
Huyu Mzee ndiye Rais pekee mwenye sifa ya Uchamungu
Alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi mwaka 83 kama sijakosea nafasi yake aliteuliwa mzee mmoja kutoka zanzibar anaitwa mzee natepe kushika uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi.

Natepe alipoingia tu officen alimtaka waziri aliemtangulia kutoka katika nyumba ya waziri ili yeye aweze kukaa hapo kama waziri.

Ilikuwa shida kidogo maana waziri alieondoka bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka kutoka na Natepe.

Ikampasa mzee mwinyi kutoka kwa haraka na siku anatoka pale nyumbani alikuwa amenunua mabati 150 na mifuko ya saruji 100 ya kwake wala sio mali ya serekali.

Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya serekali kweli mzee mwinyi akaviacha akaondoka.

Baada ya miezi kadhaa tu mzee mwinyi akateuliwa kuwa Rais zanzibar Natepe wakati ana jifikiria jinsi ya kwenda kumpongeza na kumuomba radhi kwa aliyomfanyia kabla ya kufikiria njia mzee mwinyi akaletwa bara mwaka 1985 kama Rais wa JMT.

Hapa sasa Natepe akajua kazi hana na atatimuliwa haraka iwezekanavyo tena na kutengwa na nyadhifa za JMT kwakuwa kuna mabaya ya wazi na ya sirini aliyomtendea mzee mwinyi.

Mzee mwinyi baada tu ya kuapishwa kuwa Rais wa JMT wakati anateua baraza la mawaziri akamteua tena Natepe kuwa waziri pale pale mambo ya ndani.

Siku ya kumuapisha akamwambia Natepe sio kwamba nakupenda sana hapana ila napenda kazi yako unavyofanya endelea kufanya kazi.

Siku moja mzee mwinyi yupo ikulu kapumzika akaona malori yanaingia na akaambiwa mzigo wako huu mh Rais akashtuka mbona sijaagiza kitu mie??

Ndipo akaambiwa umetoka kwa natepe mzee mwinyi akacheka sana akawaambia wasaidizi wake shusheni mabati 150 na saruji 100 hizo ndio haki yangu zingine mrudishieni tu.
 
Ni hivi ukiingia tu kwenye chama lazima uache kazi ya jeshi utabaki tu unaitwa kwa title lakini kambini tena uendi kama mwanajeshi na majukumu ya kijeshi wanakuvua.

Mie Natepe watoto wake wa rika langu ndio vijana niliokuwa nao mtaani na nilikuwa naingia mpaka nyumbani kwake na najua kuna fursa kibao zilimpita kwa sababu akutaka kuacha jeshi mpaka umri wa kustaafu ulipofika na alipo staafu ndio alianza kufanya kazi za chama.

Isitoshe mie mwenyewe baba yangu alikuwa mwanajeshi.
Natepe kastaafu jeshini mwaka gani??
 
Natepe kastaafu jeshini mwaka gani??
Amestaafu jeshi rasmi kipindi cha Mwinyi sikumbuki mwaka.

Hila kweli alishakuwa waziri ya mambo ya ndani from 1980-83 (news to me) it makes sense kipindi hiki Nyerere alikuwa akijiami either way kushika nyazifa hizo inabidi uvue majukumu ya jeshi.
 
Basi ushakubaliana nami kuwa sio kweli zamani watu walikuwa hawashiki nafasi za kisiasa kabla ya kustaafu jeshini.

Luteni kanali Jakaya kikwete kawa waziri toka 1988 jeshini kastaafu 1992

Kanali abdulrahman kinana amekuwa waziri toka awamu ya kwanza ya mzee mwinyi na akastaafu jeshini awamu ya pili ya mwinyi 1992.

Meja jenerali abdallah natepe kawa waziri 1983 na akastaafu enzi ya mwinyi.
 
Basi ushakubaliana nami kuwa sio kweli zamani watu walikuwa hawashiki nafasi za kisiasa kabla ya kustaafu jeshini.

Luteni kanali Jakaya kikwete kawa waziri toka 1988 jeshini kastaafu 1992

Kanali abdulrahman kinana amekuwa waziri toka awamu ya kwanza ya mzee mwinyi na akastaafu jeshini awamu ya pili ya mwinyi 1992.

Maja jenerali abdallah natepe kawa waziri 1983 na akastaafu enzi ya mwinyi.
Good
 
Mkuu Pohamba, 1976 ni mwaka wa tukio lililosabisha Mwinyi kujiuzulu.
Watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe Mwanza, Masanja Makhulla Mazengenuka na Issac Mwana Mkoboko, walifariki kwa mateso katika mahojiano na polisi eneo la Kigoto.

Kufuatia vifo hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi alijiuzulu, IGP, Samuel Pundugu, Director wa Tiss, Emilio Mzena, na Mkuu wa Mwanza, Peter Kisumo wakastaafishwa kwa manufaa yang umma. Mzee wangu, RSO wa Mwanza, RPC wa Mwanza, DSO wa Mwanza na OCD wa Mwanza wakashitakiwa kwenye ile Kesi ya Mauaji Mwanza.

P
Mkuu Paskali,
Baada ya mzee Ruksa kujiuzulu na kutakiwa kupisha nyumba ili mrithi wa kiti chake achukue nyumba ya Osterbay, alikuwa ni nani?

F
 
Alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi mwaka 83 kama sijakosea nafasi yake aliteuliwa mzee mmoja kutoka zanzibar anaitwa mzee natepe kushika uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi.

Natepe alipoingia tu officen alimtaka waziri aliemtangulia kutoka katika nyumba ya waziri ili yeye aweze kukaa hapo kama waziri.

Ilikuwa shida kidogo maana waziri alieondoka bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka kutoka na Natepe.

Ikampasa mzee mwinyi kutoka kwa haraka na siku anatoka pale nyumbani alikuwa amenunua mabati 150 na mifuko ya saruji 100 ya kwake wala sio mali ya serekali.

Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya serekali kweli mzee mwinyi akaviacha akaondoka.

Baada ya miezi kadhaa tu mzee mwinyi akateuliwa kuwa Rais zanzibar Natepe wakati ana jifikiria jinsi ya kwenda kumpongeza na kumuomba radhi kwa aliyomfanyia kabla ya kufikiria njia mzee mwinyi akaletwa bara mwaka 1985 kama Rais wa JMT.

Hapa sasa Natepe akajua kazi hana na atatimuliwa haraka iwezekanavyo tena na kutengwa na nyadhifa za JMT kwakuwa kuna mabaya ya wazi na ya sirini aliyomtendea mzee mwinyi.

Mzee mwinyi baada tu ya kuapishwa kuwa Rais wa JMT wakati anateua baraza la mawaziri akamteua tena Natepe kuwa waziri pale pale mambo ya ndani.

Siku ya kumuapisha akamwambia Natepe sio kwamba nakupenda sana hapana ila napenda kazi yako unavyofanya endelea kufanya kazi.

Siku moja mzee mwinyi yupo ikulu kapumzika akaona malori yanaingia na akaambiwa mzigo wako huu mh Rais akashtuka mbona sijaagiza kitu mie??

Ndipo akaambiwa umetoka kwa natepe mzee mwinyi akacheka sana akawaambia wasaidizi wake shusheni mabati 150 na saruji 100 hizo ndio haki yangu zingine mrudishieni tu.
Dah mzee mpaka aliandika kwenye kitabu chake inaonekana alimmaindi sana Ila sababu ana roho ya utu alimwachia Mwenyezi Mungu tu.

Kweli malinza duniani si kitu cha muhimu uhai. Ona sasa mzee anakula maisha mpaka leo. Roho mbaya haijengi.

Na wenye roho mbaya mwisho wao mbaya sana . Kama jamaa yetu tu.
 
Jakaya na kinana wamestaafu jeshini mwaka 1992

Jakaya kawa waziri toka 1988.
Jakaya na Kinana walistaafu na kutoka jeshini baada ya kuanza kwa vyama vingi.

Kabla ya vyama vingi walikuwa wanashika nyazifa za kisiasa bila kuondoka jeshini
 
Uongo tu. Hakuna ukweli. Mwinyi alijiuzuru 1977 na aliyembadili ni Hassan Moyo.

Mwinyi alipelekwa kuwa Balozi. Sio kweli kwamba hakuwa na kazi.

Hassan Moyo Ali kuwa waziri mambo ya ndani muda mfupi.

Mwinyi alirudi kuwa waziri 1983

Stories za vijiweni
wewe ni stupid kabisz
 
Mkuu Pohamba, 1976 ni mwaka wa tukio lililosabisha Mwinyi kujiuzulu.
Watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe Mwanza, Masanja Makhulla Mazengenuka na Issac Mwana Mkoboko, walifariki kwa mateso katika mahojiano na polisi eneo la Kigoto.

Kufuatia vifo hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi alijiuzulu, IGP, Samuel Pundugu, Director wa Tiss, Emilio Mzena, na Mkuu wa Mwanza, Peter Kisumo wakastaafishwa kwa manufaa yang umma. Mzee wangu, RSO wa Mwanza, RPC wa Mwanza, DSO wa Mwanza na OCD wa Mwanza wakashitakiwa kwenye ile Kesi ya Mauaji Mwanza.

P
Sasa siku hizi mbona watu wananyiziwa vituo cha police hatusiki RSO , RPC, RC n.k wakijiuzuku
 
Hivi wewe uliyekuwa unapinga uzii kama leo bado yu hai unajisikiaje baada ya kusoma kitabu cha Mwinyi
 
Back
Top Bottom