Jinsi polisi walivyonusuru maisha yangu last night

Ni shida sana mkuu. Ila hilo swala la kuwekeza nyumban ni zuri, maana kuna leo na kesho, mtu huwezi jua.

Ku risk maisha huku ni jambo la kawaida, maana hata mimi hii sio mara yangu ya kwanza. Imeshanitokea babkubwa zaidi ya hii mwaka 2008, ila nimeahidi hapo juu kwenye comment za juu kwamba siku nikipata muda nitakuja kuandika kilichonitokea.

By the way maisha ya mwanaume ni kuhangaika, na katika kuhangaika huko kuna risk nyingi unakutana nazo kama hivi.
 
Mmh pole sana mkuu hiyo nchi kila nikisoma matukio yake ya uhalifu kwenye social networks huwa na appreciate nchi yetu sana
 
Yah mwanume ninlazima kupambana , ila lazima uwe na exit plan , nimeona unasema hapo kuwa umeshaanzisha familia huku Sa , hapo sasa your hands are tied . katika vitu niliapa sitafanya ni kuanzisha familia kwa kaburu. Yani huko kutengeneza yatima ni dakika tu . Nimeingia sa mwaka 1999 na final goodbye ilikuwa mwaka 2008 . huwa naenda na kurudi . nimepata matukio mengi sana ya kupoteza pesa na kuibiwa na vibaka nikiwa kwa kaburu.
 
Dah aisee pole sana mkuu. Mimi nilianzisha familia huku baada ya kuona umri umeruhusu mimi kufanya hivyo.

Na obvious mara ya kwanza niliishi na mzawa tukapata mtoto mmoja, ila baadae tukashindwana kutokana na tabia na wivu wake usiokuwa na msingi, hivyo nikaruka mara 1 nyumban nikachukua jiko na kuja nalo huku ambapo nimezaa nae watoto wawili. Mmoja mwakani ataingia darasa la 3 na mungine ambae mdogo ataingia la kwanza.

Huyu niliezaa na mzawa alizaliwa mwaka 2013, kwa sasa ni darasa la 5 japo naamini kuwa hapa nimepoteza mbegu yangu, lkn inanibidi nimsapoti tu kwa ajili ya maisha yake ya baadae, kwani sio yeye aliepanga kujileta duniani, bali ni starehe zetu mimi na mama yake ndio zilizosababisha leo yeye kuwepo.

Hata hivyo huku elimu yao ni bora mara 100 ya elimu yetu, au ya nchi yoyote nyingine ya Afrika. Ndomaana nimeendelea kukaza tu ili watoto wapate elimu ya kuwasaidia hapo baadae hata tutapoamua kurudi nyumbani baada ya wao kumaliza shule.
 
Mimi nipo cape town hii ishu kama Yako ilinitokea mwezi wa 4 mwaka huu ilichonisaidia ni chuma niliipiga juu wakastop gari Yao ilikua saa Tano usiku mshukuru mungu sana ulikua unakufa
Asante mkuu, dah pole sana na wewe kwa kunusurika kifo cha aina hii.
 
Rabda kama sijaelewa. Lakini Nakushauri Rudi tu Nyumbani. Kwanini uteseke roho??
Mkuu japo ushauri wako mzuri, lkn tayari nina familia. Kurudi nyumban sasa hivi ni sawa na kuuwa ndoto za wanangu.

Labda nihame mji niende kuishi mji mungine πŸ‘‡
 
Ok mkuu, ngoja wateja wa tigo waje wasome na kukupa mrejesho.
 
OR Tambo Airport ni hatari sana kutoka nje kwa mida ya usiku. Ni hatari zaidi kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka (Peak Season). Majambazi wengi huwa wanakuwa hapo sehemu ya watu wanaowasili (arrivals) wakichora ramani ya wageni wanaowasili ambao Wana fedha nyingi ili wawafuatilie na kuwapora.
Aidha, majambazi hao pia Wana connection na wale watu wa "bureau de change" zilizopo hapo ndani airport.
 
Shukran sana kwa ushauri mzuri kaka yangu The Boss ila kabla ya kuhamia huko inabidi mtu ujipange. Mimi kwa sasa nina familia hapa SA, hivyo siwezi kuhamia huko kichwa kichwa bila connection au kujipanga sawa sawa.
Mkeo msouth?nimewahi sikia wanawake wa South Africa...mwanamume mgeni akipata hela wanachonga mchongo anauwawa ili wabebe mali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…