Onesha aya Yesu anasema "Mimi Mungu".
Jesus spoke in parables, mafundisho yalikuwa ni ya mafumbo unabidi utafakari alichosema.
Ila makuhani/mafarisayo, wajuzi na wasomi wa vitabu na sheria za dini walikuwa wanamuelewa alichokuwa anaaminisha na ndo maana walisisitiza wamuue kwasababu machoni kwao yesu alitenda kosa kubwa kuliko yote la wakati huo, LA KUJIFANANISHA NA MUNGU"
YOHANA 10:29-33
29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.
30 Mimi na Baba tu umoja.
31 Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige.
32 Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe?
33 Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.
Pia Yohana 5:18
18 Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu.
Pia YOHANA 14:5-9
5 Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?
6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
7 Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.
8 Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.
9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
Kuna mistari mingine mingi ila hii niliyotoa inaonesha wajuzi wa dini/ma askofu wa wakati huo walikuwa kila wakimsikiliza yesu wa nasikia allkisema yeye ni Mungu ndo kitu kilichowakasirisha wakapanga kumua.