Jinsi tunavyoishi wakristo hapa Zanzibar kipindi hiki cha mfungo

Hakuna kitu kibaya kwa mwanadamu kama unafiki, unafiki unaleta matatizo makubwa mno.
Ukiwasoma watu hapa unapata wakati mgumu kuamini kuwa hivi kweli tunayaandika haya kwa nia njema ya kuhabarisha au kuna agenda ya siri ambayo ni unafiki?
Kila mtu huru aliyepewa akili na Mungu afanye utafiti wake huru kuhusu hizi taarifa halafu achore mstari mwenyewe.
Nimeshuhudia kwenye taasis kubwa tu yenye wakristo wasiozid hata 5 wakipewa chakula dhidi ya waislam zaid ya 150 bila ubaguzi na story za kufunga sasa ukisikia hizo story unajiuliza ni Zanzibar ipi hiyo wanasema?
Kama unataka kuwafanyia watu dhihaka kwa kuwaringishia kula hadharani kwa kisingizio cha uhuru basi hata kwa asiyefunga au mkristo mwenzako atakubanjua makofi.
Pia kama unataka wamiliki wa migahawa wawe wanauza chakula kwa muda unaotaka wewe basi utakuwa na matatizo ya akili mbona unampangia mtu biashara.
Hizi unazoziona ni hadithi tu ila hayo mambo hayapo kabisa.
Sio waislamu wote wanafunga na uislam umeweka wazi hilo, sasa kichaa mmoja anataka kuwaaminisha watu kuwa ukipika tu utapigwa, jiulize kwa wale wagonjwa nao wanakula daku tu hawapikiwi chakula na ndugu zao au chakula wanapikia mahakamani? Hakuna muislam mwenye akili timamu anayejua uislam nini atakuvamia nyumbani au njian kisa unakula kwa kisingizio yeye umefunga, kijana kanyoa kiduku anakuletea fujo nyumbani kwako kisa unapika unamuacha tu hivi hivi? Mpige ngumi akashtaki kama utapata shida. Tatizo kubwa ni dhihaka, hebu jaribu kuwafanyia mzaha uone kama hata wakristo wenye adabu zao hawajajmkutia vitasa mchana kweupe.
 
Hizo sheria ndio zimewafanya muwe wajinga, hamtaki hata kutafuta maaarifa zaidi!

Kufunga ni zaidi ya kuacha kula. Dini yenu ni ya kuhuni sana hii
Sawa ila hiyo dini unayoita ya kihuni ninamuongozo wa watu waishi vipi kati ya waislamu kwa waislamu na waislamu na watu wa kitabu na waislamu na washirikina waabudu masanamu na mizimu. Sasa wewe dini yako isiyo ya kihuni haikufundishi hata utaishi vipi na mkeo na kwa muingiliano upi uishi vipi na watoto wako na jamii yako ila watu wachache ndio wanawaletea sheria muishi vipi na wakati wao wenyewe hawatambui waishi vipi, sheria ya kiislamu ilibaki vilevile toka Taurati ya musa Zaburi ya Daudi Injili ya issa ikiwa ni sheria ya kutoka kwa mungu na wala sio story za mtu alikuwa akifanya nini hadi hii Qur'an ya muhamadi sheria ni ileile ya Mungu Yule Yule ila ilikuwa inakolezwa kutokana na kaumu husika ila Qur'an imekuja kupambanua upotovu uliofanywa na watu kwa kuchafua misingi ya Mungu kwa kuweka maneno yao kwenye vitabu vyake ili wapate kuwatawala wenziwao
 
Hata huko zanzibar hotel zinatoa huduma za chakula ila migahawa yote imefungwa, kama una Pesa ya kula nenda kwenye mahoteli ukale
 
Huu uzi haunihusu mimi na kumbuka kuna wengi tu hawana kipato cha kula hotel za kitalii. Ni upuuzi wa hali ya juu kumpa mtu leseni ya biashara ya chakula na kumlazimisha kufunga biashara yake eti kwa Ramadhan. Si ajabu watu kama huyu mleta mada wapo wengi Zenj ama wanashindishwa na njaa au wanaenda kula sehemu hatarishi tena kwa kujificha utadhani wametenda uovu wowote ule hadi wanyanyaswe kiasi hicho.

Hata huko zanzibar hotel zinatoa huduma za chakula ila migahawa yote imefungwa, kama una Pesa ya kula nenda kwenye mahoteli ukale
 

Kukwepa ukweli wa mada iliyopo kwa kuleta hoja ya kiufundi kama yako hakuondoi mapungufu makubwa yanayotakiwa kuangaliwa katika nchi yetu. Kama kuna sheria au utamaduni wa kuzuia watu kula katika kipindi cha mfungo mtukufu, kwa nini sheria au kanuni hizo zitekelezwe kwa misingi ya ubaguzi wa rangi? Hivi madhumuni ya Mapinduzi ya Zanzibar hayakuwa ni pamoja na kuondoa uonevu na kero zilizozagaa kwa misingi ya ubaguzi wa rangi? Uongozi wetu, wa dini na Serikali Unguja ni bora wasilifumbie hili macho.
 
Japokuwa Mimi ni mtanganyika naipenda Zanzibar Daima.Watanganyika tuwape wazanzibar nchi yao.Mbona tunawanyanyasa wazanzibar?
 
Sikwepi ukweli bali nawapa ukweli.
kimsingi mnashindwa kuelewa kwamba wazungu pale Zanzibar almost ni wageni/watalii. Kwa kawaida mgeni huwez kumlazimisha au kumtaka kufuata utamaduni wako. mgeni mpitaji ana hiyari. Weusi wanaolazimishwa kufuata Utamaduni wa WaZanzibar ni kwa sababu almost wengi wao si wapitaji bali wapo wapo sana Zanzibar kwa maana kwamba si wakuondoka leo wala kesho hivyo yafaa waamue na waijue Zanzibar na utamaduni wao na waufuate kwa hiyari ama la, .
 


Hiyo ni hofu yako tu, mie mbona Jumamosi hii iliyopita nilikuwa nakula mgahawani mida ya saa 9 alasiri, watu waliniangalia pia na wale vijana wajinga wapitao kukamata wenzao wasile walikuwepo na waliniona. uzuri walijuwa kuwa mie ni mtu wa bara ila nilijiandaa kuua mtu iwapo wangenivamia. Kula nakula mie kwanini mtu akasirike, nani aliyewakataza kula? Ujinga huu mie mwiko kwangu, wapigane wenyewe kwa wenyewe kwa ujinga wao, HAKUNA aliyekatazwa kula kila mmoja ana uhuru wa kula. Mi naua mtu aje kunivamia kisa nakula kwa raha na hela zangu mwenyewe.
 
Ogopa sana dini ya "kuosha kikombe wa nje"tu.
Mtoa mada ni mnafik
Kasema uongo
1.Kuna wasafir wanaruhusiwa kula
2.wagonjwa
3.watoto
4.akina mama walio katika siku zao
Hao wote wanapika majumban mwao.
Sema ukifika muda wa Ramadan
Waislamu wanaojitambua hufunga biashara zao.Zbar ni sawa na vatican
wanasimamia dini yao
Sasa nani afungue mgahawa
Huku wateja wako wamefunga?
Humu ndani ujinga umetawala
Mtu anabuni mada za uongo
na wenye chuki zao
Wanajitokeza .Ni Mara ngap kejel
Hutolewa dhidi ya wafungaj hata pasi
na sababu za msingi.
Hata ukienda vatikan hutaona msikit kiurahis na kanzu ndo kabisa
Bas tii sheria zao.
 
Ni kweli lakini mtoa mada amesema, ukipika hauruhusiwi kupikia nje ni unatakiwa upikie ndani.

Sasa mimi nikauliza mfano mimi nina jiko langu la kuni, bado nikapikie ndani?. Au hapo inakuwaje?
 

I really hate when people can't argue without insulting others. Shows just how small minded they are.
 
Ni kweli lakini mtoa mada amesema, ukipika hauruhusiwi kupikia nje ni unatakiwa upikie ndani.

Sasa mimi nikauliza mfano mimi nina jiko langu la kuni, bado nikapikie ndani?. Au hapo inakuwaje?
Sio kweli huyu mtoa mada wako kuna kitu anakitafuta, lakini kuhusu swala la kupika nje sio kweli na wala hukamatwi wala kufanywa lolote iwapo upo kwako umekaa au unapika kistaha, tatizo lipo kwa wale ambao wanazurura na kula ovyo hali ya kuwa inajulikana ni kipindi gani kinachoendelea. Yaani inamaanishwa wale wanaodharau tamaduni, mila, desturi, silka na ustaarabu wa wenzao.
Ngoja nikupe mfano:
Moshi wanakataza kutupa taka ovyo. Je wewe ukienda Moshi utatupa taka ovyo? Si utafuata utaratibu wa wenyeji wako hata kama hupendi, kwa maana unajua ukikamatwa utapigwa faini.
 
[emoji115][emoji115][emoji115][emoji115]
Ni kweli lakini mtoa mada amesema, ukipika hauruhusiwi kupikia nje ni unatakiwa upikie ndani.

Sasa mimi nikauliza mfano mimi nina jiko langu la kuni, bado nikapikie ndani?. Au hapo inakuwaje?
 
Sasa unajua haya mambo kila siku nayapiga vita humu ndani kwamba ni uchochezi.
Naanza kwa kumwambia Acha uchochezi wa kidini. Acha kutia fitna baina ya hizi dini mbili. Wewe nia yako ni nini. Unataka siku tuuane?

Hiyo sheria ambayo iko zanzibar sii elewi kiundani ila mimi nitasema kama muislamu. Uislam haumlazimishi mtu yoyote kufanya jambo lolote. Mambo yote yunayohimizwa na kuamrishwa kufanya ni kwa faida yetu. Tusipofuata hatumuongezei wala kumpunguzia mungu chochote. Hakuna sehemu yoyote duniani watu wanalazimishwa kufunga. Hakuna kitu kama hiko.

Na sasa wewe kama mkazi wa huko kama hizo sheria zinakubana kwa nini usipike chakula nyumbani, ukatia kwenye bakuli zuri tu ukaenda na lunch yako kazini?? Kwanza utasave pesa nyingi na pia hautopata shida na serikali. Labda kama utakuwa unaenda na hicho chakula katikati ya njia panda na kula.

Narudia tena. Kuwa na busara na maneno unayondika. Kuwa mwangalifu.

Mungu akubariki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…