Jinsi tunavyoishi wakristo hapa Zanzibar kipindi hiki cha mfungo

Wazungu wanavalishwa kanga sehemu zisizokuwa za Watalii, hapa Unguja,..

Kuhusu kula Wazungu wako tafauti wao moja kwa moja wanakuwa wanaheshimu itikadi, mila na tamaduni wa sehemu wanazokwenda kutalii..
Mkunazi 1 ni sehemu ya kitalii?

Mwanakwerekwe, Ikipida, Mitaa ya Malawi Road (kwenye mitambo ya ZECO) ni maeneo ya watalii?

Huku kote nimekutana na Watakii wakiwa wanagida soda zao na wamevaa kama wapo ufukweni.
 
Hata akila hadharani wewe ina kuathiri vipi?

Ndio maana tunawaambia hamfungi mnalazimisha kuacha kula mchana badala yake mnakula usiku
Alibughudhiwa na nani?Huyo alikutana na vibaka,ndio wakamtisha tisha,na kwa vile muoga akatishika.Kwa vile wewe pia uko muoga na lege lege,wamuunga mkono.Huyu alikutana na vibaka,na inawezekana pia wamemchomoa hela,badala ya kwenda kwenye vyombo vya sheria,kutoa malalamiko anakuja jf,mbona yaonyesha mawenge wenge ya kutishwa tishwa anayo.
 
Naona umeshavimbiwa cha saa 12 sasa unasubiri uvimbiwe cha alfajiri saa 11 ili mchana ujifanye umefunga
Ndugu yenu kakutana na vibaka,wamemtisha tisha,na yaonyesha na hela wamemkwapuwa,badala ya nyinyi kumuelekeza njia sahihi ya kwenda kwenye vyombo vya sheria,kutoa malalamiko yake,mwazidi kuuunga mkono.
 
Nyinyi mnakutana na wajanja wa mjini,badala ya kwenda kwenye vyombo husika kulalamika,mnakuja jf.Hebu jiongozeni,tumieni akili.
 
Huyu kakutana na wahuni wa mitaani,wamemtisha tisha,na yeye akatishika.Kama ingekuwa ni watu wa waliotumwa kisheria,lazima wangekuwa na sare maalumu,na wangempeleka kwenye vyombo husika.Ndugu yenu,badala ya kumfahamisha,amekutana na vibaka wa mtaani,mwazidi kumuunga mkono.
 
Wewe sasa unajielewa,hao wanaokamata watu,ni wajanja wajanja mitaani tu,ni vibaka,hakuna sheria katika uislamu inayomzuia mtu wa dini nyingine kula mchana wa Ramadhani, ndani ya uislamu na aliyemuislamu pia wapo
Wagonjwa,
Wazee wasiojiweza,
Watoto,
Waliojifunguwa,
Wanawake walio kwenye siku zao,
Wanawake wanaonyonyesha,
Wasafiri,
Wote hao hapo juu,wana ruhusa ya kutokufunga,na sharti mojawapo la kufunga katika uislamu ni kuwa muislam.
Nyinyi mnakutana na vibaka,wajanja wa mjini,huwenda pia ikawa ni wakristo wezenu walio wajanja wa mjini au wa sio na dini,wajanja wajanja,wanawatia mjini.Kama mngekuwa na akili,mngewafikisha kwenye vyombo vya sheria.
 
Mkunazi 1 ni sehemu ya kitalii?

Mwanakwerekwe, Ikipida, Mitaa ya Malawi Road (kwenye mitambo ya ZECO) ni maeneo ya watalii?

Huku kote nimekutana na Watakii wakiwa wanagida soda zao na wamevaa kama wapo ufukweni.
Mwanakwereke Watalii wamefuata nini?? Au wamefuata Tv na Mafrigi "Used" 😂🤣
 
Kiukweli sio Tabia nzuri kwa nchi ya aman kama Tanzania kuishi kama watumwa kwa kipindi kifupi kama hik ndio maan kuna dini mbili sio din moja itake dini nyingine ifuate wanachokifanya so tubadilike
 
huo mtazamo wako nenda Zenji kauze kitimoto chako mwanaharam mkubwa wewe hamtafaulu kunasibisha uislam na kitimoto ni wakristo tu ndio wanakula najisi hiyo ingawa bible inakataza
njoo kwa bibi janet hapa mbweni uone inavyolika mpaka na waislam tena maustaadh
 
Basi utakuwa wa ajabu sana. Mudy mwenyewe kawaambia mle mkiwa na njaa sasa sijui nani anakula wakati ameshiba!!!?
 
Lakini sio mafundisho ya dini yanavyotaka, huu ni ukweli ysiopingika.

Ni wapi katika historia ya mtume S.w.a aliwabugudhi makafiri wa Makkah au Madina kisa kufunga?

Uislamu ni dini ya kisimamia maslahi ya kila mtu, ndiyo maana inaitwa dini ya haki. Uislamu unajali mpaka haki ya kuku anapotakiwa kuchinjwa.
 
Kumbuka pia mtume hakuwabughudhii watu wa Makka kwasababu kipindi alipokuwa alilingania Uislam kwa njia ya siri na hata baada ya kuwa Dhahiri ni miaka 10 tu ndio aliyokaa Makka, na sehemu kubwa ilibaki ya miaka 13 alikuwa Madina kwa maana alikuwa amejitenga na washirikina wa Makka. Kwa mantiki hiyo washirikina wa Makka hawakwenda kumbughudhi huko Madina alikokuwa, ijapokuwa Madina kulikuwa na watu ambao nao si waislam lakini waliiheshimu dini ya Kiislam na Waislam kwa ujumla wao. Ukiangalia Zanziba kiuhalisia imejitenga, ni kisiwani na ukiangalia kumejitenga na bahari sasa iweje wewe kutoka pande nyingine ukawabughudhi wazawa, wakati huo pia wapo Wakristo wazawa lakini hawawabughudhi Waislam? Hayo ni sawa na kusema leo hii mimi niende Mtwara then mila zao au ngoma zao usiku nitoke nje na kuwakataza kwavile kwangu mimi naona ni makelele.
NB
Ukiwa kwenye mji wa vipofu nawe jifanye Chongo.
 
Wewe ni msemaji wa waislamu ? Umetembelea grocery za Sinza, zinazouza kitimoto, ?/ waislam hawali nyama za porini? mfano nyati, viboko, tembo nk nani anachinja hiyo mifugo, uelewa wako ni mdogo kama ubongo wa mbu
 
Nchi yetu haina dini,kinachoendelea Zanzibar ni uvunjaji wa katiba na dola itawajibika
 
Mbona huku bara waislamu tuko nao maofisini, na muda wa lunch ukifika wanaendelea na mfungo wakati sisi tunakula, na wala sijaona hata mmoja aliyesema anakwazika sisi tunapokula? Tena mmoja rafiki yangu ananiambia anapofunga wakati wengine wanakula mbele yake anajisikia kweli amefunga kuliko ingekuwa kwamba wote hatuli ingekuwa ni kawaida tu.
Lakini kwa huko Zanzibar kwa kuwa ni sheria kabisa inasema hivyo hilo limeshakuwa jambo la kiutawala au kiserikali zaidi kuliko la kiimani, kwahiyo hata namna ya kulishughulikia ni ya kiserikali. Kupata au kutokupata thawabu hakuhusiani na sheria hiyo kwa sababu waumini wa kawaida wa kiislamu mnaoishi nao mitaani siyo wao walioweka hiyo sheria, kwenye suala la sheria ikishakuwa ya serikali basi sote inatuathiri tu hata kama hatukubaliani nayo. Inawezekana hata huko Zanzibar wapo waislamu ambao hawakubaliani na suala la kuwakataza wengine kula au la kuwawekea masharti, lakini sheria ndiyo hiyo iko hivyo na ni sheria rasmi ya nchi. Poleni wenzetu.
 
Ni kweli kabisa hamna wateja, wauza kitimoto nao wanalalamika biashara mbaya, wanatamani wafungue hata kesho ili biashara ya kitimoto irudi kwenye peak
Walaji wa kitimoto na wanywaji wa pombe ni walewale, kabla na baada ya Ramadhani. Kinachotokea wakati wa Ramadhani ni suala la kuheshimiana tu na ujirani, watu wanapunguza fujo ili wenzao wafanye ibada zao. Wanaepuka kuwakwaza wenzao. Ni hivyo tu. Mfungo ukiisha watu wanarudia bata zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…