Habari wadau.
Nilikuwa nawadharau sana vijana wanaoimba imba na kucheza cheza tik tok. Nawaona wapuuzi hawana kazi ya kufanya na wajinga.
Mtoto wa shangazi yangu ni mmojawapo wa hao wapuuzi wa tik tok. Ana followers laki 6 huko tik tok
Ni binti ana miaka 21 na Anasoma chuo kikuu kimojawapo nchini
Shangazi alikuwa analalamika anahisi mtoto wake amekuwa tapeli ama amepata madanga. Maana amekuwa na pesa huku hana ajira yeyote mara kanunua boda boda. Mara kanunua simu ya gharama, mara kanunua mavifaa ya saloon ya kike.
Baada ya dogo kuhojiwa sana akafunguka hela anavyozipata.
Yupo chuo mwaka wa pili now. Akasema hela anazipata kupitia tik tok.
Wasanii wa bongo fleva wanataka nyimbo zao zitrend tik tok.
Hivyo wakitoa nyimbo zao huwa wanawafata watu wenye followers wengi tik tok na kuwaambia waanzishe challenge za nyimbo zao ili ku wainfluence followers wao na wao waige na mwisho nyimbo inakuwa hit song. Hivyo wasanii huwa wanawalipa hao tik toker wa kuanzisha challenge kama yeye. Mfano yeye anachaji elfu 30 kwa challenge ya wimbo wa msanii
Wasanii wapo kibao na wengi ma underground na nyimbo mpya zinatoka kila siku. Hivyo kwa siku iliyokuja vizuri anaweza kuhudumia hata wasanii 10 na kuingiza laki 3 easy tu japo pia kuna siku huwa hapati mteja hata mmoja
Pia kuna wasanii wa kenya na nigeria nao wana mchezo huu.
Pia waimba nyimbo za injili na kwaya kina rose muhando, bukuku na wengineo nao wameiga mchezo huu
Hivyo ndio inampa hela anazonunua vitu.
Dogo katuonesha inbox yake tik tok na instagram tukaona wasanii kibao wamemfata dm na wanavyomtumia miamala kaonesha ili kutetea hela zake kwamba anazipata kihalali.
Binafsi nimeshangaa sana na kumpongeza dogo kwa jinsi alivyojiajiri