Jinsi "wasaliti " wanavyoula CCM, huku wafia chama wakitoswa

Jinsi "wasaliti " wanavyoula CCM, huku wafia chama wakitoswa

baba anapo muoza chasaka, kwa kutumia mifugo ambayo watoto wake wanailisha kila siku,ndivyo wafia chama wanavyo jisikia.
 
Ni vizuri sana mana anawaandaa wafia vyama kisaikolojia ili waikubali katiba ya Warioba.

Naona kama Magufuli ana nafasi ya kuwa rais bora kabisa barani Afrika kwani naona jinsi anavyoweka mazingira mazuri ya kuileta ile katiba ya wananchi.

Wale majamaa ya kijani hayaikubali ile katiba kwa sababu ya kuwaza vyeo tu.
Sasa kimekija chuma na sasa anatema checheeeeeee!!

Hapa Kazi tu.

Tumuunge mkono Rais!
Anafanya vizuri sana kwenye teuzi zake.

Ili chakula kiwe safi ni lazima na sahani iwe safi.

Ni vema akawaweka pembeni baadhi ya watu walioshiriki sana kwenye madhaifu yaliyokuwepo hasa yale ya makusudi.

Tena ikiwezekana awachunguze sana mali zao kuanzia hao mabalozi, maDC, mawaziri ,Makatibu wakuu, MaRC, Wakurugenzi ili abaini kuwa wengi walikua wanahomora mafeze ya umma kwa manufaa yao ,wakae pembeni hata kama watahamia wote upinzani. Lakini tujenge Tanzania mpya na mawazo mapya. Uzalendo uwe wa kweli.
Nachukia mtu anayejiita mzalendo huku akijua wazi kuwa alifanya ubadhirifu wa mali za umma halafu bado anabaki kwenye serikali. Mkuu wa Taifa hili waweke pembeni wale waliokua wanshiriki huo uharibifu ili twende sawa na dhamira yako ya kweli.
Tusiwafunge gerezani lakini tusiwaache tena kwenye madaraka wale waliohujumu nchi .Wakae pembeni tupime uvumilivu wao. Nao waone machungu ya mabadiliko.
Hakuna kulinda cheo cha mtu.

Wapinzani wote wana sifa ya kupata nafasi kwani walipigania sana haki na uzalendo wa nchi hii wakati CCM bila aibu wakikua wanawazomea mchana kweupe.
Dr. Slaa akiwa mmoja wapo aliyepigania sana taifa letu.
Anastahili kupewa ubalozi.

Waache CCM URITHI wavimbe wapasuke. Mabadiliko ya kweli mbele kwa mbele.
 
Hata Dr. Slaa ilimuuma sana lowasa alivyopewa nafasi ya kugombea bure bure wakati waliosotea chama wapo.
Hivi ni akili gani imetumika hapa? CHADEMA kuna mnofu gani ukilinganisha na mnofu unaotajwa na mtoa ndani ya ccm? Halafu tunambiwa tanzania ya viwanda yaja! Hivyo viwanda viendeshwe na akili hii?
 
Kwa hiyo nyie CDM mnapojiunga na chama sio kuwa mnataka kuiendeleza Tanzania bali mnataka mkapewe kula?

Wana CCM halisi walimchagua Magufuli ili aiongoze Tanzania na kutuletea maendeleo. Sasa kama ameziona talanta ndani ya Kitila, Mgwira na Slaa ziungane na zile za viongozi maelfu wa CCM kutekeleza azma yake ubaya upo wapi?

Nyie hamna jema. Mkiwekwa pembeni mnasema Magufuli hataki ushauri wa wapinzani. Akiwachukua mumsaidie kufanya kazi zake manambeza eti mbona unawaacha wana CCM.

Kweli sikio la kufa halisikii dawa.
 
Ni matumaini hamjambo wote.
Tangu mfumo wa vyama vingi uanze rasmi mwaka 1992 kumetokea uhamaji hamaji sana wa wanachama wa vyama vya siasa kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.
Aidha hali hii imekuwa ikifanyika kwa hiyari ya mwanachama mwenyewe ama baada ya kuahidiwa vitu kadhaa ikiwa ni pamoja na vyeo au fedha taslimu.

Chama kikuu kinacholengwa zaidi huwa ni kile chenye mvuto mkubwa kwa wananchi.
Mfano Daniel Nsanzungwako kule Kigoma aliwasumbua sana ccm akiwa nccr mageuzi hali iliyotumika kutumia gharama yoyote aweze kuwa ccm hali iliyofanikiwa na yeye kuwa mbunge kisha akawa naibu waziri wa elimu. Hakika alivuna pesa na umaarufu kabla ya kupotezwa hadi sasa sijui aliko hadi sasa. Ila kisiasa keshapotezwa kabisa.

Alikuwepo mwanasiasa maarufu wa cuf huko Mpanda aliyewasumbua ccm alijulikana kama Sambwe(sina hakika na kama jina linaandikwa hivyo). Kama kuingizwa choo cha kike basi ccm walifanikiwa sana hapa. Huyu jamaa kule Mpanda alikubalika na alikuwa mwiba sana kwa ccm. Kilichofanyika anakijua yeye ila hata sasa sijui aliko na kisiasa kwisha habari yake.

Mkoani Mbeya alikuwepo bwana shitambala huyu mwanasheria. Alikubalika vema na wananchi walimpa ushirikiano mzuri. Kila aliposhinda alionekana kutofuatilia hadi anatangazwa mwingine jambo lililopelekea kutuhumiwa kuwa anauza ushindi kutokana na ushahidi walioupata. Katu alikataa kata kata lakini miezi michache alihamia ccm kwa majigambo mengi. Ajabu aliporudi kushindana tena jimbo la Mbeya mjini alipigwa chini na sasa kateuliwa kuwa mkuu wa wilaya kama vyeo vya washindwa na kisiasa yuko mahututi.

Chadema walipomtuhumu naibu Mwenyekiti wao Said Arf kuwa anawahujumu kisiasa kupitia mizengo pinda alisimama akatupa kadi ya chama hadharani akidai si kweli.
Kabla hajawa mbunge kupitia chadema alikuwa na gari moja Land Rover aliyoitoa sadaka hospital ya Mpanda kubeba maiti kwa kuchangia mafuta wafiwa wote wakati huo pia akiwa shehe mkuu mkoa wa rukwa before mpanda kuwa mkoa. Alitangazwa mshindi baada ya mkurugenzi wa wakati huo isdory isakwisa bandisa kumtendea haki na chadema kupata mbunge kwa mara ya kwanza rukwa. Sifa pekee zimwendee Dr kaburu kwa kampeni zake akiwa katibu mkuu wa chadema.
Kilichotokea sasa Arf ni tajiri mkubwa mno ana kampuni ya kusafirisha mizigo na ukwasi wa kutosha. Sijajua kama bado ni shehe wa mkoa au laa ila najua ni mbunge wa ccm huko Mpanda kupitia sarakasi za wizi walizotumia huko last election.

Kabla ya Dr slaa alikuwepo katibu mkuu wa chadema wa viwango akitokea mkoani Kigoma aliyeibuliwa na mbowe wakati huo akiishi uingereza yeye na mkewe. Si mwingine ni Dr Amani Waridi Kaburu. Aliitendea haki chadema. Alizaa wabunge wengi. Kilichomkuta anakijua. Alipewa cheo kuwa mbunge Afrika mashariki baadaye kawa Mwenyekiti ccm mkoa wa Kigoma mpaka sasa kahujumiwa Kigoma mjini na ndg zake ccm na jimbo likaenda Act. Nasema alihujumiwa kwani wanaccm hawakumpigia kampeni wakampigia zito kiaina. Anakufa kisiasa kila sekunde. Keshakuwa mithili ya kondomu.

Ukisikia siasa za watu wasomi basi lazima umjadili mbowe aliyezunguka vyuo vikuu ndani na nje ya nchi kuwashawishi vijana wasomi kuwa wanachama wa upinzani hapo ndipo wakazaliwa akina zito unaowajua leo, mnyika, silinde, kafulila na wengine wengi.
Kafulila ametokea chadema akaenda nccr mageuzi, karudi chadema miezi michache huyo ccm. Sihitaji kusema mengi kwa ufupi kila mtu na tabia yake. Kafulila ana haraka sana ya Maisha aweza kupata ama kukosa au akaishi maisha kama ya Dr kaburu Kigoma yote yawezekana lakini namuona kama kijana anayezika uwezo wake kwa kaburi alilojichimbia mwenyewe. Ikiwa mtu kama Dr kaburu hana amani kama jina lake lilivyo licha ya uwezo wake wa kujenga hoja ulivyo Kafulila ataweza?. Tusubiri.

Orodha ni ndefu mno. Sijawataja akina Dr slaa, Prf mkumbo kitila, Mwigamba, wasira Steven, mpendazoe, shibuda magari na wengine wengi mno.
Hakuna ambaye aliingia ccm kwa style ya kushawishiwa kwa pesa na vyeo lukuki kisha akabaki salama na afya yake ileile. Wengi wamekufa kisiasa.
Ngoma anayoipiga rais leo kuua upinzani ilishakuwa zilipendwa tangu enzi na haijawahi kumuacha mcheza ngoma salama.
Anatumia msemo wa wazungu usemao "If they don't understand you, confuse them ".
Wasioelewa watakuwa confused too much. Lakini jiulize kila baada ya kufanya hivyo bado kura za ccm zimeendelea kushuka kila chaguzi.
Sasa naomba kuuliza kwako Dereva wa Lorry hivi mbinu na njia hii ya kurubuni wapinzani ina manufaa gani kwa ccm ikiwa hali na maisha ya watanzania bado ni tete?.

Hivi sasa badala ya kuboresha maslahi ya wakulima na watumishi wa umma mmekuja na mswada mpya ambao mkiupitisha tu basi wastaafu wengi baada ya April 2018 watajuta kuishi Tanzania kwa kiwango cha pesa mkupuo watakazopata. Ktk mazingira hayo mtaanza kushangaa msipoungwa mkono kwenye chaguzi.

Ikiwa wanaccm wote pamoja na Mwenyekiti wenu mtajua kuwa watanzania wana kiu na maendeleo na kukua kwa uchumi wao ktk uboreshaji wa huduma za afya, elimu bora, miundo mbinu bora, kodi stahiki za biashara, rushwa na uhakika wa amani ktk uhuru wa habari nina amini hamtatumia nguvu kuwaahidi vyeo na pesa wanasiasa wa upinzani.

Unapoumwa ukawa unatumia dawa lakini bado afya yako ikazidi kuzorota ni ishara tosha kuwa dawa unayotumia si stahili kwa ugonjwa wako ama siku zako za kufa zimetimia.
Kuondoka kwa wapinzani kadhaa kuingia ccm wakati huu ambao ccm imefanya mikataba ya hovyo huku aliyeingia mikataba hiyo na kuivunja kiholela, kununua mali za umma kinyume na sheria za manunuzi ya umma ppra akiwa ndiyo kiranja mkuu wa kandamiza upinzani nchini hakika naliona Giza tororo mbele ya nchi kisiasa, kiuchumi, kijamii na kidini pia.

Wale mashehe waliofungwa ni watanzania hukumu stahili ikitolewa juu yao italeta afya njema na umoja kwa taifa kuliko sasa.

Wanaoitwa wasiojulikana huku uovu wao wanaoufanya kwa kuua, kutesa, kunyanganya, kutishia ukijulikana wakijulikana ccm itanenepa bila chakula.

Ikiwa bunge litakuwa huru na wabunge watashindana kwa hoja ktk uwanja huru kura za ccm zitaongezeka mara dufu.

Ikiwa waliomtwanga Tundu lissu na wale wa kibiti watajulikana basi ccm itanawiri kama mti wa mzeituni.

Itakapofikia wakulima wakafurahia jasho lao kupitia mazao yako ktk soko huru basi hakutakuwa mtu atakayeipinga ccm daima.

Ni nani aliyewadanganya kuwa shetani akikuzidi nguvu njia rahisi ni kuungana naye kisha baadaye umtoroke. Nawaapia nyie viongozi wa ccm nchini mnayoyafanya sasa hata shetani kabaki kinywa wazi anawashangaa. Nendeni hata mlimani chuo kikuu mpate dondoo chache kwa wasomi mnaweza kupata ahueni.
Ngoma mnayoipiga na kuicheza ni zilipendwa haitaokoa chama bali kuongeza chuki zaidi.
Mungu ibariki familia yangu na wananchi wenzangu. Wabariki wenzangu wenye afya mgogoro wapate afya njema popote walipo. Usiwasahau vijana waliochanganyikiwa baada ya kukosa mkopo waguse baba.
Waliofungwa kwa sababu hawakubaliani na maamzi ya pilato wetu wakumbuke.
Tupe upendo usio wa kinafiki na wote waliopotezwa na wasiojulikana wape makao mema popote walipo haijalishi wamekufa au ni wazima.

Haki huinua taifa, ijueni kweli nayo ikae ndani yenu mpate kuwa huru kwelikweli. Asanteni.
 
bila juhudi za hao unaowakebehi kama wafia chama wahamiaji wasingeshawishika kujiunga na chama.

kwa vyovyote vile wahamiaji ni matunda ya jasho la wafia chama.

Kusema kuwa ccm inagawa vyeo ni kuitusi.

CCM inaangalia kwanza maslahi ya watanzania hivyo hata teuzi za Nafasi yoyote hufanywa kwa misingi hiyo.
 
bila juhudi za hao unaowakebehi kama wafia chama wahamiaji wasingeshawishika kujiunga na chama.

kwa vyovyote vile wahamiaji ni matunda ya jasho la wafia chama.

Kusema kuwa ccm inagawa vyeo ni kuitusi.

CCM inaangalia kwanza maslahi ya watanzania hivyo hata teuzi za Nafasi yoyote hufanywa kwa misingi hiyo.
stroke kama mfia chama namba moja humu jf, unafaidikaje? usifiche. Wafaidika hawashindi mitandaoni wanakuwa na shughuli nyingi. Utakufa kwa stroke soon.
 
Mgeni anapewa mnofu wenyeji wanaendelea kula vipapatio, makanyagio, utumbo na vichwa

Ningependa kusikia ya moyoni kutoka kwa wasotea chama waliokipigania chama kabla, wakati na baada ya uchaguzi ambao bado hawajateuliwa katika ngazi yoyote ile huku wapinzani ambao muda wao wote wamekuwa wakikiponda chama wanateuliwa na kupewa minofu mitamumitamu..

Hata kama wewe sio msotea chama ila umepata nafasi ya kuwasikiliza mkiwa either private au public nini mtazamo wao na wanajisikiaje

Ni kasumba ya mwanadamu ambaye analipigania jambo fulani baada ya kufanikiwa hupenda kuwa sehemu ya wanufaika hata kama amesahaulika... Anaweza akacheka na kuunga mkono maamuzi hadharani lakini ukimtazama sana kwa umakini unaweza kuona hisia zake, matendo yake, sura yake haviendani na kile anachokikubali hadharani..

Narudia tena ningependa kusikia ya moyoni kutoka kwenu either umemshuhudia au wewe mwenyewe ukiwa kama msotea chama uliyefungiwa milango nini maoni yakoView attachment 636840 View attachment 636839
Hii inatutia moyo sana wasotea chama tuliuloyo chadema maana tunajua ipo siku tutanunuliwa kwa dau kubwa kama la Dr. Makamanda mdichoke.
 
Africa ni bara pekee ambalo kulitawala unahitaji pesa tuu. Vijana wanalegea mbele ya pesa. Nyerere angekua ndio Kina Dr slaa, au Katambi bin kafulila, hata Leo tungekua bado tunatawaliwa.
 
Nyie hamna jipya lowasa,sumaye,kingunge na nyarandu wao ni wapya kwenu sio ? Acheni ushamba na majungu Tanzania ni nchi ya watanzania wote mtu kama ana sifa ya kuwa kiongozi mwacheni afanye kazi acheni majungu hata wewe mtoa post ungekuwa na sifa ungeteuliwa tu na cdhani kama ungekuwa na jeuri ya kukataa
 
Nyie hamna jipya lowasa,sumaye,kingunge na nyarandu wao ni wapya kwenu sio ? Acheni ushamba na majungu Tanzania ni nchi ya watanzania wote mtu kama ana sifa ya kuwa kiongozi mwacheni afanye kazi acheni majungu hata wewe mtoa post ungekuwa na sifa ungeteuliwa tu na cdhani kama ungekuwa na jeuri ya kukataa
aibu kutumia kodi za wananchi kuhonga.
 
Nyie hamna jipya lowasa,sumaye,kingunge na nyarandu wao ni wapya kwenu sio ? Acheni ushamba na majungu Tanzania ni nchi ya watanzania wote mtu kama ana sifa ya kuwa kiongozi mwacheni afanye kazi acheni majungu hata wewe mtoa post ungekuwa na sifa ungeteuliwa tu na cdhani kama ungekuwa na jeuri ya kukataa
Akili siyo sare kama nguo za ccm zilivyo. Unachotamani wewe usidhani wote tunatamani.
Entrance ya uliowataja kwenda upinzani ililenga mapinduzi na vyeo. Waliokosa walichofuata walirudi kutafuta tena wengine walitangaziwa hadharani kuwa warudi ccm vyeo bado vipo.
Akiwa shinyanga aliwaambia bado anazo nafasi nyingi za uteuzi wasihofu.
Huwezi kudumu upinzani kama hukujiandaa, uvumilie mabomu, kesi na kushinda mahabusu ni ngumu. Kupigwa risasi za moto huwezi.
Narudia tena ngoma hii ni zilipendwa na imeproove failures nenda kawaambie ndg zako hivyo.
 
Back
Top Bottom