Jinsi ya kuandika Tangazo lako la biashara mtandaoni

Jinsi ya kuandika Tangazo lako la biashara mtandaoni

Njia zote hizo ni za kijinga a upuuzi mtupu .... motivation speaker tu mnajua kuandikaa
Wengi ni motivation speakers kama ulivyosema lakini wapo wanaotengeneza pesa sana tu ilamara nyingi hawaandiki about it.
 
Hatua kwa hatua Namna ya Kufanya Matangazo ya Kulipia Mtandaoni (Facebook sponsored Ads)

HATUA YA 1: SELECT A GOAL (KUCHAGUA LENGO LA TANGAZO LANGU)

More profile visits:

Hapa kupitia tangazo lako utakua unaelekeza watu wafike moja kwa moja kwenye ukurasa wako wa matangazo ili waweze kuona huduma/bidhaa ambazo unazitangaza,hapa utawapa uwezo wa wao kupitia huduma/bidhaa zako.

More website visitor:

Hapa ni kwa wale amabo tayari wana tovuti za biashara watakua wana waongoza wateja waweze kufika moja kwa moja kwenye tovuti zao na kuweza kuona huduma ambazo amewaandalia na hapo wateja wanaweza kufanya manunuzi ya bidhaa ambazo tayari wamependezewa nazo.

More messages:

Hapa utaweza kuwaongoza wateja waweze kufika moja kwa moja kwenye uwanja wako wa meseji wa FACEBOOK, INSTAGRAM au WHATSAPP kwa kupitia bidhaa hiyo ambayo umeifanyia tangazo.

HATUA YA 2: DEFINE YOUR AUDIENCE (KUCHAGUA AINA YA WATU AMBAO NATAKA TANGAZO LIWAFIKIE)

Automatic:

Ukitumia chaguo hili utaweza kuacha instagram/facebook kuweza kukuchagulia watazamaji wa kuliona tangazo lako wakiwemo wafuasi wa ukurasa wako.

Create your own:

Ukitumia chaguo hili utaweza kutengeneza aina ya watazamaji ambao unahitaji waweze kuliona tangazao lako kwa kuchagua jinsia zao, umri, na eneo la kijiografia unalotaka tangazo lako liweze kuonekana.

HATUA YA 3: BUDGETS & DURATION (BAJETI NA MUDA)

Hapa ndipo ambapo utachagua kiasi gani cha fedha unahitaji kukitumia kwenye tangazo lako na kwa mda gani mfano: dolla 5 kwa siku 10 inamaana kwamba unatakiwa uweze kua na kiasi cha dolla 50 sawa na shilingi 118,500/= kuweza kutangaza tangazo lako kwa siku 10.

HATUA YA 4: REVIEW YOUR AD (KUKAGUA TANGAZO)

Hapa utaweza kulikagua tangazo lako kua tayari limekidhi vigezo ambavyo unavihitaji, likiwa limeshakizi vigezo tayar unaweza kubofya kitufe cha BOOST POST.

Tangazo lako litapitia kwenye ukaguzi wa META kwa mda usiozidi masaa 24.

HATUA YA 5: KUFUATILIA MATOKEO YA TANGAZO.

Baada ya tangazo langu kuruhusiwa (approved), ni muda sahihi wa kuanza kuangalia na kufuatilia muenendo wa tangazo langu kwa ukaribu ili kama kuna mabadiliko yoyote niweze kuyafanya mapema kuepuka hasara.

Hizo ndizo hatua ninazo pitia hadi kutengeneza tangazo la kulipia Facebook na Instagram.

Kama unapata changamoto katika kutengeneza matangazo ya kulipia tunaweza kuwasiliana na kupata muongozo zaidi na kutengenezewa tangazo lako kwa ufanisi zaidi.

Tuma meseji whatsapp 0752026992.
Jinsi_ya_kutengeneza_Matangazo_ya_Biashara_ya_kulipia_Facebook_na_Instagram.jpg
 
Unaweza ongezea nyama hapo... Namna ya kufanya malipo ya haya matangazo (malipo yanafanyika Kwa namna ipi? Kati ya wewe/mimi na hao facebook/instagram?)
 
Kufanya ads fb na instagram kinachosumbua watu ni jinsi ya kufanya malipo basi,

Hayo ulioeleza ni mengineyo tu
 
Unaweza ongezea nyama hapo... Namna ya kufanya malipo ya haya matangazo (malipo yanafanyika Kwa namna ipi? Kati ya wewe/mimi na hao facebook/instagram?)
Unaweza lipia kupitia M-Pesa master card, airtel mastercard au ukatumia card yako ya benki ambayo ina uwezo wa kufanya malipo kimataifa.

Utaenda kwenye ads manager, sehemu ya BILLING, kisha utaona kipengele cha payment hapo utaweza kuongeza njia ya malipo kwa kujaza taarifa za kadi yako ya malipo.

Pia unaweza kwenda Instagram sehemu ya settings, halafu Ads kisha utaona sehemu ya payment.

Kama utapata changamoto tunaweza kuwasiliana 0752026992 kukusaidia.
 
Back
Top Bottom