Jinsi ya kuosha maiti hatua kwa hatua

Jinsi ya kuosha maiti hatua kwa hatua

mwaka flani nikiwa mkoa flani katika harakati za maisha jamaa niliyeenda nae aliugua ghafla akilalamika tumbo linamuuma ikafikia point akaanza kutapika vitu vya njano dizain kama nyongo vile, ikabidi nimpeleke hospital nilipofika nikamkabidhi kwa madaktari akawa amepewa kitanda, mimi nikatoka mara moja kwenda kuangalia shughuli iliyotupeleka huko mkoani, niliporudi hospital nikakuta kile kitanda cha mwana kimezungushiwa yale mashuka ya kijani nikamuuliza muhudumu wa ile ward vipi jamaa anaendeleaje? yule nurse akaniambia nenda pale ofisi ya wauguzi utapewa maelekezo nilipofika nikuliza hali ya mgonjwa wangu kuna mzee mmoja akaniuliza uhusiano wangu na mgonjwa nikamwambia ni mshkaji nafanya nae kazi, yule mzee akaniambia jamaa yako hutanae tena duniani, kiukweli nilishtuka sana sikuwaza kama jamaa anaweza kufa kiutani kiasi kile, ikabidi niende hadi pale walipozungusha mashuka nikaingia nikakuta wamemfunika nikamfununua jamaa alikua kama amelala nikamuita rama rama ila hakuitika, nilitoka pale wodini kama nimechanganyikiwa wale manesi wakaanza kuniita ila sikuwasikiliza nilienda breki ya kwanza guest tuliyofikia niliingia chumbani nikalia sana nikampigia simu bosi wetu nikampa taarifa, nikatoka nje ya pale guest nikawambia wale wahudumu yule jamaa yangu amefariki walishtuka pia, nikatoka na meneja wa guest hadi hospital kufika nikakuta ameshapelekwa mortually, nikaitwa ofisini nikapewa death certificate wakasema unaweza kuchukua maiti yako mkaendelee na taratibu za mazishi, kiukweli nilikua sijua naanzia wapi, hakuna siku nilivuta bangi nyingi kama usiku wa siku ile, nilikua napigiwa simu na watu wa ofisini na wa familia yao pia kujua nini kimetokea nyingi sukuzipokeA nilikua napokea ya bosi na kaka wa marehemu tu! kesho yake asbh yule mshkaji wa pale guest alinifanyia mpango tukatoa maiti tukapeleka kwenye msikiti fulani, mimi ndio mtu pekee niliyekua nafahamiana na marehemu ilibidi nishuhuduie kila kinachofanyika, kwa mara ya kwanza niliona waislam wanavyoosha maiti waliilaza juu ya kibaraza flani cha kuoshea maiti wakaifunika sana wakawa wanaosha kama jamaa alivyoeleza hapo juu wakamaliza wakaifunga vizuri nikamlipa yule ustaadhi elfu ishirini kama alivyohitaji, bosi akawa amewasiliana na watu wa mkoa ule tuikapewa gari kurudi dar nikiongozana na yule jamaa wa pale guest, ilikua ni experience ngumu sana kwenye maisha yangu hadi leo huwa naamini haya maisha ni fuckin tu yanaweza kukuacha muda wowote.
Asante mkuu kwa mchango
 
Hakuna Dini nyengine yeyote hpa Duniani inoendana kimaumbile kma Uislamu we ukikataa ni ww tu lkn Uislamu ndio dini Safi kabisaa ya kuifuata
Watu wengi wamekua wakiituhumu Uislamu kwa Ushirikina na Mambo mengine lkn ukweli kua izo ni Chuki zao tu juu ya Dini yetu Pendwa

Ukiwa hupendi kuitwa KAFIRI fanya Usilimu tuu
 
Uislamu ni Raha sana yni unatakiwa upelekwe kwa Mola wako ukiwa msafiiii na hata ukipelekwa kaburini unasindikizwa mpka pale ndani ya kaburi hebu angalia huruma na upendo wa Uislamu kwa mwanadamu sasa njoo upnde wa pili huku unashushwa na makamba kaburini ata hawataki ata kukusindikiza [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Najivunia kua Muislamu
Wakati huo wameshakukamua mavi,na mkeo yuko nyumbani
 
Wakati huo wameshakukamua mavi,na mkeo yuko nyumbani
Mbona hujaongelea suala la kusindikizwa kaburini ? kma mnapendana kweli mngekua mnafnya kma sisi
Ata Rais wetu alotangulia aliwahi kulisifia hili ilipotokea ajali kule ukerewe
 
Mbona hujaongelea suala la kusindikizwa kaburini ? kma mnapendana kweli mngekua mnafnya kma sisi
Ata Rais wetu alotangulia aliwahi kulisifia hili ilipotokea ajali kule ukerewe
Rais yupi kama ni huyu john mzee wa fix achana nae
 
Rais yupi kama ni huyu john mzee wa fix achana nae
Ongelea basi suala la kusindikizwa kaburini
Yni nakuona ulivo mweupeee peee kua huna point bcz main point hujibu unajibu minor point
 
Ongelea basi suala la kusindikizwa kaburini
Yni nakuona ulivo mweupeee peee kua huna point bcz main point hujibu unajibu minor point
Kusindikiza kaburini kumefanyaje na kuna impact gani,mi nikifa nachomwa moto mambo ya kusindikizana sijui kukamuana kinyesi ujinga mtupu
 
Yani upande ule wenye mambo mengi kama unga wa ngano ndo hawamsafishi!!

Alafu upande huu usio na mambo mengi na ndio wanaomsafisha

And still you blame this beautiful side

Dear brothers & sisters why always u don't think about this fact

Acheni kukariri bhc
 
Kusindikiza kaburini kumefanyaje na kuna impact gani,mi nikifa nachomwa moto mambo ya kusindikizana sijui kukamuana kinyesi ujinga mtupu
[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Yani upande ule wenye mambo mengi kama unga wa ngano ndo hawamsafishi!!

Alafu upande huu usio na mambo mengi na ndio wanaomsafisha

And still you blame this beautiful side

Dear brothers & sisters why always u don't think about this fact

Acheni kukariri bhc
Tatizo watu wamefungwa akili zao na mapastor wao
 

Namna ya kumuosha maiti hatua kwa hatua​

1.Kuoshwa (Kukoshwa).
Mazingatio kabla ya kuosha maiti.

(a)Maiti ya kiume ioshwe na wanaume na maiti ya kike ioshwe na wanawake pia.
  • Maiti ya mtoto yaweza kuoshwa na yeyote.
  • Ni Sunnah mke kumuosha mumewe na mume kumuosha mkewe pia



(b)Ni mtu mmoja tu ndiye anayeosha na mwingine ni kwa ajili ya kumpa msaada inapobidi.


(c)Ni muhimu muoshaji afahamu masharti ya kuosha maiti muislamu kama vile;
1. Muoshaji awe muislamu.
2. Mahali pakuoshea pawe faragha (pamesitirika).
3. Maiti aoshwe huku amefunikwa gubi-gubi na nguo nyepesi inayoruhusu maji kupenya kwa urahisi.
4. Ni vyema muoshaji asiishike maiti bali aoshe akiwa amevaa ‘gloves’.
5. Kuzingatia masharti ya mwenye kuoga josho la wajibu; kama vile kuwa na maji mengi na safi, pasiwe na kizuizi cha maji kupenya, n.k.



(d)Ni muhimu muoshaji afahamu nguzo na sunnah za kuosha maiti kama ifuatavyo;
- Nguzo za kuosha maiti ni mbili:

1. Nia
2. Kueneza maji mwili mzima wa maiti.
- Ni Sunnah kumuosha maiti mara tatu au zaidi kwa idadi ya witiri.


Namna ya Kuosha Maiti hatua kwa hatua.
i.Maiti awekwe juu ya kitanda chenye tobo katikati ili kupitisha uchafu unaotoka tumboni.
ii.Pawepo na shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda, kama hakuna uwekano chombo kiwepo cha kukingia uchafu unaotoka kwa maiti.
- Pia maiti inaweza kuoshewa bafuni au kwenye karo liliotengenezwa
kwa kazi hiyo.



iii.Maiti afunikwe na nguo moja kubwa yenye kupenyeza maji wakati wa kuosha.



iv.Maiti akalishwe juu ya kitanda usawa wa tobo na shimo (ufuo) na ainamishwe nyuma kidogo, kama ni mzito ni vizuri msaidizi wa muoshaji amuegemeze kwenye magoti yake.



v.Muoshaji apitishe mkono wa kushoto kwenye tumbo la maiti na kuliminyaminya taratibu ili kutoa uchafu ndani.



vi.Amlaze chali na kuminyaminya tumbo lake kama ilivyo mara ya kwanza.



vii.Aikalishe tena na apitishe mkono wa kushoto chini akiwa amevaa kitambaa au gloves na kusafisha tupu mbili kwa maji safi.
- Kama hapaja takata, basi na avae gloves safi na ile chafu aitupe kwenye
ufuo na asafishe tena kama mara ya kwanza mpaka patakate.



viii.Baada ya hapo, muoshaji afunge kitambaa safi kwenye kidole chake shahada na akichovye kwenye maji na kumswakisha maiti meno yote na kisha akitupe ufuoni.



ix.Muoshaji azungushe kitambaa kingine safi kidole chake kidogo mkono wa kushoto na kumsafisha nacho maiti tundu za pua kisha akitupe ufuoni.



x.Asafishe kucha za maiti kwa kijiti safi na laini iwapo ni ndefu na chafu.



xi.Kisha amkalishe maiti na amtawadhishe kwa kufuata taratibu za kawaida za kutia udhu (kutawadha).



xii.Maiti akiwa amekalishwa, ataanza kumuoshwa kichwa akiwa ameinamishwa mbele kidogo.
- Kama nywele au ndevu ni nyingi zichanwe na kuoshwa kwa sabuni na
maji mpaka zitakate.
- Mwanamke mwenye nywele nyingi zisukwe mikia, na zilizong’oka
ziambatanishwe na sanda.



xiii.Baada ya kuoshwa kichwa, maiti italazwa kwa ubavu wa kushoto na kuanza kuoshwa ubavu wa kulia, mbele na nyuma kwa pamoja kwa sabuni na maji safi mpaka itakate.



xiv.Kisha itaoshwa ubavu wa kushoto kama ilivyooshwa wa kulia.



xv.Baada ya makosho (maosho) haya mawili, la maji na sabuni na la kuondoa sabuni, kosho la tatu la maji liwekewe karafuu na marashi ili kulegeza viungo (maungo) vya maiti.



xvi.Baada ya makosho matatu haya, muoshaji anyooshe viungo vya maiti na kumlaza kama alikuwa mara tu baada ya kufa.



xvii.Kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti, na baada ya hapo maiti awekwe juu ya mkeka mkavu na kufunikwa kwa nguo kavu tayari kuvalishwa sanda (kukafiniwa).

Source: Bongoclass.com kupitia mafundisho matukufu ya Qur'an pamoja na sunnah za Mtume(s.a.w)
Washukrani jazillah
 
Usikute ata kumzika marehemu ni dhambi lakin hatujui tu.. utajua ujui
 
Hapa Mada sio kuoshwa.
Jamii zote zinaosha Marehemu wao, ha hata kuwavika nguo Safi kama sanda na suti.

Hapa Mada ni
Kumkamua Marehemu Masazo, ya ndani hadi tumbo liwe flati kabisa.
Wengine wanainamisha hadi kichwa kiguse miguu ilimradi Tu tumbo litoe kila kitu cha ndani.

Hapo ndipo tunaposema kama ni Amri za Kiislamu basi Aya zingezungumza.

La semeni tu ni utamaduni ulioigwa toka Uarabuni.

Na sio kusingizia ni maamrisho ya Dini.
Wewe unajuaje kuwa WAKRISTO HAWAKAMUIMAITI ZAO?
 
Ni dhahiri waislm wengi wanafuata utamaduni wa waarabu wa kale, utamaduni wameufanya ni sehemu ya imani, uarabuni sababu ya uhaba wa miti ya mbao walikuwa wanazika bila jeneza imeingia kwenye dini, kuzika maiti ubavu imeingizwa pia kwenye dini. MTU ULIYESTAHARABIKA HAIWEZEKANI KUKAMUA MAVI YA MAITI ILI IWEJE... MWARABU KAWAWEZA SANA
 
Ni dhahiri waislm wengi wanafuata utamaduni wa waarabu wa kale, utamaduni wameufanya ni sehemu ya imani, uarabuni sababu ya uhaba wa miti ya mbao walikuwa wanazika bila jeneza imeingia kwenye dini, kuzika maiti ubavu imeingizwa pia kwenye dini. MTU ULIYESTAHARABIKA HAIWEZEKANI KUKAMUA MAVI YA MAITI ILI IWEJE... MWARABU KAWAWEZA SANA
Binafsi ninapenda utamaduni wa Maiti kuchonwa Moto Tu
Ili kuhifadhi mazingira na ardhi kwa matumizi ya baadae.
 
UKRISTO ni kwa ajiri ya Watu walio HAI TU.
Maiti ni Maiti, ni za kuzikwa au kuchomwa Moto.
wewe sema una chuki zako binafsi na uislam.
Hata wakristo wanakamua maiti.
Kama wanaweza kumuosha Basi wakikutana maiti kaharibikiwa lazma watamkamua.ila hawawezi kukwambia
 
Back
Top Bottom