Jinsi ya kuosha maiti hatua kwa hatua

Jinsi ya kuosha maiti hatua kwa hatua

Mambo mengine Ni Magumu kutafakari.
Amekufa,na atazikwa mavumbini,na ataoza muda si mrefu,alafu process hizi zote? WHY? Kama walipinduka na gari akazamishwa kwenye matope,au nyumba imeanguka akafukiwa na kifusi hapo inamake sense,
Anyway Mimi Ni kijana sijui mengi.
Umemaliza vizuri, kuwa hujui mengi, basi ulipaswa uwe mpole ujifunze toka kwa wanaojua. Hivyo ni vitu vya kawaida sana na ndivyo ambavyo hufanyika. Watu hufa wakiwa kwenye hali tofauti tofauti. Utu wa mtu huendelea hadi atakapolazwa kuzikwa.

Wengine humzika marehemu akiwa kavaa suti, tai, viatu, saa n.k sasa je huvishwa tu pasipo kuhudumiwa usafi? Unajua kule mochwari unapomuacha maiti hufanyiwaje?

Hatuna haja ya kuogopa wala kusema vibaya. Uislmau umeelekeza hatua kwa hatua nini afanyiwe marehemu kabla ya kwenda kuzikwa ikiwemo kuogeshwa kwa kuzingatia stara.
 
Ili maiti aweze kuoshwa vizuri hatua zifuatazo ziweze kupitiwa:
1. Maiti awekwe kwenye kitanda chenye tobo katikati kwa ajili ya kupitisha uchafu utokao tumboni kama upo.
2. Lichimbwe shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda ili kuhifadhi uchafu utokao kwa maiti.
3. Maiti afunikwe na shuka kubwa iliyonyepesi kiasi cha kuruhusu maji kupita.
4. Maiti ikalishwe kitako na makalio yake yaelekee kwenye tobo la kitanda.
5. Muoshaji apitishe mkono wake wa kushoto juu ya tumbo la maiti aliminyeminye kwa taratibu ili kutoa uchafu
6. Alazwe chali na aminyeminye tumbo lake kama hapo awali.
7. Aikalishe tena kisha apitishe mkono wa kushoto chini ukiwa umevalishwa kitambaa au gloves asafishe tupu mbili huku akijimiminia maji mkono wa kulia.
8. Ampigishe mswaki kwa kitambaa kilaini kilicho viringishwa kwenye kidole cha shahada cha mkono wa kushoto, akichove majini kisha amswakishe maiti vizuri meno ya juu na ya chini kisha akitupe ufuoni.
9. Azungushe kitambaa kingine kwenye kidole kidogo cha mkono wa kushoto, akichove majini, kisha amsafishe nacho tundu za pua kisha akitupe ufuoni.
10. Achukue kijiti laini achokonoe kucha zake, iwapo ni ndefu na chafu.
11. Akiwa pia kamkalisha maiti amtawadhishe maiti kwa kufuata utaratibu wa kawaida wa kutawadha.
12. Kumuosha kichwa kwa sabuni.
13. Kisha kumuosha kwa ubavu wa kulia kwa kumiminia maji mbele na nyuma.
14. Kisha hivyo hivyo na ubavu wa kushoto.
15. Baada ya makosho hayo mawili la maji na sabuni na kuondoa sabuni, pawe na kosho la tatu la maji yaliyowekwa karafuu maiti na marashi kidogo.
16. Baada ya makosho haya matatu, muoshaji anyooshe viungo vya maiti na kumlaza sawa sawa kama alivyolazwa mara ya kwanza baada ya kufa. Kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti tayari kwa kivishwa sanda.
Hili jitu la Simba na elimu kama hizi naweka mashaka makubwa!!???
 
Nani kakuambia najua wanazo? Nina uhakika hawana
Hivi kwenye huu uzi ulialikwa

Au ndio ukosefu wa akili

Maana kwa mwenye akili anajua tu kua huu uzi una wahusu waislamu na imani yao sasa sijui tueleze kama unaakili zinazo fanya kazi mpaka kuingia huku
 
Hivi kwenye huu uzi ulialikwa

Au ndio ukosefu wa akili

Maana kwa mwenye akili anajua tu kua huu uzi una wahusu waislamu na imani yao sasa sijui tueleze kama unaakili zinazo fanya kazi mpaka kuingia huku
Kuna sehemu imeandikwa huu uzi ni wa waislam?
Au ndo kukosa akili kwenyewe
 
Ndio katika imani ya kiislamu mwanamke humuosha mwanamke mwenzake na mwanaume vivyo hivyo.

Ila ni bora zaidi maiti ikaoshwa na mtu wa karibu yake kama mume kumuosha mke au mke kumuosha mume!

Ama ni vyema kuoshwa na mtu ndugu yako ili kuficha aibu itakayoonekana kwa maiti.Mfano harufu mbaya,vidonda visivyomithilika n.k.

Mungu ndie mjuzi zaidi.
Umenena vyema.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom