Ambition plus
JF-Expert Member
- Feb 23, 2018
- 6,101
- 11,381
Ukifa umekufa,matendo yako ndio nauli yako.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi huweweseki usiku ukikumbuka maitiNimejikuta nakumbuka kazi yangu ya mochwari
Ni suala la imani mkuu , kwan na wale wanaomvalisha suti na Vito vya thamani hua inamaanisha nini au ndio anenda kuwaringishia wengine huko aendako kua yeye kapendeza ziadiMaiti inaooshwa ili iweje? Tayari haina uhai mbona inadharirishwa
Kwa maana hiyo kwa vile amekufa hata kuzikwa pia ni ujinga inafaa atupwe tu barabarani?mtu akifa amekufa huo ujinga wote wa nini
Tamaduni kabla ya uislamuSource ya comment yako??
Hii in kuwarahisishia walozi wala nyama za wafu wakimuibuia maiti kutoka malaloni akutwe akiwa msafi.Namna ya kumuosha maiti hatua kwa hatua
1.Kuoshwa (Kukoshwa).
Mazingatio kabla ya kuosha maiti.
(a)Maiti ya kiume ioshwe na wanaume na maiti ya kike ioshwe na wanawake pia.
- Maiti ya mtoto yaweza kuoshwa na yeyote.
- Ni Sunnah mke kumuosha mumewe na mume kumuosha mkewe pia
(b)Ni mtu mmoja tu ndiye anayeosha na mwingine ni kwa ajili ya kumpa msaada inapobidi.
(c)Ni muhimu muoshaji afahamu masharti ya kuosha maiti muislamu kama vile;
1. Muoshaji awe muislamu.
2. Mahali pakuoshea pawe faragha (pamesitirika).
3. Maiti aoshwe huku amefunikwa gubi-gubi na nguo nyepesi inayoruhusu maji kupenya kwa urahisi.
4. Ni vyema muoshaji asiishike maiti bali aoshe akiwa amevaa ‘gloves’.
5. Kuzingatia masharti ya mwenye kuoga josho la wajibu; kama vile kuwa na maji mengi na safi, pasiwe na kizuizi cha maji kupenya, n.k.
(d)Ni muhimu muoshaji afahamu nguzo na sunnah za kuosha maiti kama ifuatavyo;
- Nguzo za kuosha maiti ni mbili:
1. Nia
2. Kueneza maji mwili mzima wa maiti.
- Ni Sunnah kumuosha maiti mara tatu au zaidi kwa idadi ya witiri.
Namna ya Kuosha Maiti hatua kwa hatua.
i.Maiti awekwe juu ya kitanda chenye tobo katikati ili kupitisha uchafu unaotoka tumboni.
ii.Pawepo na shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda, kama hakuna uwekano chombo kiwepo cha kukingia uchafu unaotoka kwa maiti.
- Pia maiti inaweza kuoshewa bafuni au kwenye karo liliotengenezwa
kwa kazi hiyo.
iii.Maiti afunikwe na nguo moja kubwa yenye kupenyeza maji wakati wa kuosha.
iv.Maiti akalishwe juu ya kitanda usawa wa tobo na shimo (ufuo) na ainamishwe nyuma kidogo, kama ni mzito ni vizuri msaidizi wa muoshaji amuegemeze kwenye magoti yake.
v.Muoshaji apitishe mkono wa kushoto kwenye tumbo la maiti na kuliminyaminya taratibu ili kutoa uchafu ndani.
vi.Amlaze chali na kuminyaminya tumbo lake kama ilivyo mara ya kwanza.
vii.Aikalishe tena na apitishe mkono wa kushoto chini akiwa amevaa kitambaa au gloves na kusafisha tupu mbili kwa maji safi.
- Kama hapaja takata, basi na avae gloves safi na ile chafu aitupe kwenye
ufuo na asafishe tena kama mara ya kwanza mpaka patakate.
viii.Baada ya hapo, muoshaji afunge kitambaa safi kwenye kidole chake shahada na akichovye kwenye maji na kumswakisha maiti meno yote na kisha akitupe ufuoni.
ix.Muoshaji azungushe kitambaa kingine safi kidole chake kidogo mkono wa kushoto na kumsafisha nacho maiti tundu za pua kisha akitupe ufuoni.
x.Asafishe kucha za maiti kwa kijiti safi na laini iwapo ni ndefu na chafu.
xi.Kisha amkalishe maiti na amtawadhishe kwa kufuata taratibu za kawaida za kutia udhu (kutawadha).
xii.Maiti akiwa amekalishwa, ataanza kumuoshwa kichwa akiwa ameinamishwa mbele kidogo.
- Kama nywele au ndevu ni nyingi zichanwe na kuoshwa kwa sabuni na
maji mpaka zitakate.
- Mwanamke mwenye nywele nyingi zisukwe mikia, na zilizong’oka
ziambatanishwe na sanda.
xiii.Baada ya kuoshwa kichwa, maiti italazwa kwa ubavu wa kushoto na kuanza kuoshwa ubavu wa kulia, mbele na nyuma kwa pamoja kwa sabuni na maji safi mpaka itakate.
xiv.Kisha itaoshwa ubavu wa kushoto kama ilivyooshwa wa kulia.
xv.Baada ya makosho (maosho) haya mawili, la maji na sabuni na la kuondoa sabuni, kosho la tatu la maji liwekewe karafuu na marashi ili kulegeza viungo (maungo) vya maiti.
xvi.Baada ya makosho matatu haya, muoshaji anyooshe viungo vya maiti na kumlaza kama alikuwa mara tu baada ya kufa.
xvii.Kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti, na baada ya hapo maiti awekwe juu ya mkeka mkavu na kufunikwa kwa nguo kavu tayari kuvalishwa sanda (kukafiniwa).
Source: Bongoclass.com kupitia mafundisho matukufu ya Qur'an pamoja na sunnah za Mtume(s.a.w)
[emoji849][emoji849][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Nimejikuta nakumbuka kazi yangu ya mochwari
Sawa ni mengi lakini yanafanywa ndani ya muda mfupi tu....kazi inaishaAma kweli mbomba ngafu kufanya yote hayo maiti inaenda kuoza na kuliwa na funza kabrini
Ni usafi tu...Mtu akifa si azikwe tu biashara iishe! Mambo ya kukamua matumbo na kuchana ndevu yote inasaidia Nini?
OoohTamaduni kabla ya uislamu
Nyie zile suti munazowavisha ni zanini!Hii in kuwarahisishia walozi wala nyama za wafu wakimuibuia maiti kutoka malaloni akutwe akiwa msafi.
Haiwezekani kuangaika na usafi wote huo kisha mkamzamisha ardhini na kifusi kikubwa juu yake ili kuzuia harufu mbaya ya uozo itakayo kwenye mwili pamoja na bidii zote hizo za kuuosha mwili.
Uai ukikatika katika mwili wa binadamu, thamani yake uishia hapo hapo. Yanayofanyika baada ya hapo ni mbwembwe tu.
😂😂😂😂wee jamaa bhanaNyie zile suti munazowavisha ni zanini!
Au anaenda kugombea madaraka flani kaburini.
Sie akina nani!! Na wewe ni nani kwa mujibu wa maelezo yangu... Wapi nimetaja pande za sie na nyie? Ama umefufuka kutoka kuzimu kutetea walokufa. Nimezungumzia suala la kifo bila kubainisha upande unaohusika kuandaa mwili. Noa upeo wako kabla ya kujishtukia bladifakeni.Nyie zile suti munazowavisha ni zanini!
Au anaenda kugombea madaraka flani kaburini.
ushirikina unaletwa na hawa majamaa ndio utasikia maji ya maiti dili kwa wagangangaHayo Mavi wanayokamua ni ya muhimu sana maana Kazi mojawapo huwa yanatumika kumuita Jini makata