Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

Asante mama..... Yani nimejichokeaje?!
Nitajaribu badae sana..
 
Hizo chapati za leo me ninyimeni tu....niko radhii...yani me chapati za unga wa atta hazipandi kabisaaaa......
 
Sanaaaa nahisii kashamba namba mojaa heee heeee ntautafutaaa niuone

Google atta flour utaona ...

Kiufupi ni unga wa ngano whole wheat ambayo ni very healthy...

Kama ujuavyo kuna brown sugar na nyeupe basi ni kama hivo...
 
Kwa wale ambayo mnatumia whole grains hii inawahusu...

Mahitaji


Unga wa ngano weupe nusu kilo

Unga wa atta nusu kilo...

Chumvi kiasi

Maji ya uvuguvugu....

Samli vijiko 6 vya kulia vijaze...

Extra virgin olive oil vijiko vitatu (waweza tumia mafuta yoyote)...

Namna ya kutaarisha...

Changanya unga na samli na mafuta pamoja na chumvi...

Weka maji ya uvuguvugu na ukande kama chapati za kawaida...

Ukimaliza kukanda weka unga wako katika mfuko mweupe na safi (wraps)....wacha kwa nusu saa

Zungusha chapati zako na uziache kdg...

Sukuma na kaanga kama chapati za kawaida....

Tayar kwa kuliwa...

Mmmh! Hapo ulipo bado ni Tanzania?
 
Mashaallah,, Mm pia napenda kuutumia huo unga wa atta kuchanganya hata nikipika maandazi
 
Back
Top Bottom