Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

MAPISHI YA CHAPATI ZA KITANZANIA

Mahitaji

  1. Unga wa ngano vikombe vitatu vya chai (all-purpose flour three cups)
  2. Chumvi 1/2 ya kijiko cha chai
  3. Sukari kijiko 1 cha chakula (Sugar 1table spoon)
  4. Maji ya uvuguvugu (warm water) kikombe kimoja
  5. Mafuta ya kupikia ya kumimina (vegetable oil) nusu kikombe
  6. Kibao cha kusukumia
  7. Kisukumio.
  8. Sahani
  9. Karatasi ya foili
Hatua

  1. Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia kisha tia chumvi na sukari.
  2. Changanya vizuri
  3. Pasha mafuta ya kupikia ya kumimina.
  4. Baada ya hapo tia mafuta ya moto ya kupikia ya kumimina vijiko viwili na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee.
  5. Mchanganyiko ukishachanganyika vizuri sasa unaweza kutia maji ya uvuguvugu kidogo, kidogo huku ukiwa unauchanganya ili kupata donge.
  6. Baada ya hapo anza kukanda hilo donge mpaka mabuje yote yapotee na unga uwe mlaini, ambapo itakuchukua kama dakika 10-15 hivi
  7. Chukua kibao cha kusukumia chapati.
  8. Weka unga kidogo ili chapati isinatie kwenye kibao.
  9. Sukuma donge moja la chapati mpaka liwe sawa (flat)
  10. Weka kijiko kimoja cha mafuta na usambaze.
  11. Ikunje (roll).
  12. Kata vipande vidogo vidogo kulingana na idadi ya chapati unazotaka.
  13. Tengeneza donge ya kila kipande.
  14. Baada ya hapo weka frampeni/kikaango (fry-pan) katika moto wa wastani.
  15. Kisha anza kusukuma donge moja kutengeneza umbo la chapati.
  16. Ukishamaliza hapo tia kwenye frampeni.
  17. Acha iive upande mmoja kwa sekunde chache halafu igeuze upande wa pili.
  18. Tia mafuta kama kijiko kimoja kikubwa cha chakula upande uliyoiva.
  19. Geuza chapati tena.
  20. Tia mafuta kama kijiko kimoja upande wa pili—utaona zinaanza kuumuka (bubbles will be coming out).
  21. Geuza upande wa pili kuhakikisha chapati ina madoa madoa ya kahawia pande zote.
  22. Kama ina madoa madoa ya kahawia na inaumuka, basi imeiva!
  23. Epua.
  24. Weka kwenye karatasi ya foili (kufanya zibaki kuwa moto wakati unaendelea kukanda zingine).
  25. Tia katika sahani chapati zilizofunikwa katika karatasi ya foili.

KUMBUKA (NOTE): Wakati chapati moja inaiva anza kusukuma nyingine! Usisubiri mpaka moja imalizike kuiva ili unapoipua chapati moja uwe na nyingine tayari kwa kuiweka jikoni.
 
Hapa yamekosekana maharage tu

chapati%2Bveg%2Broll.jpg
Aisee hii chapati haivutii kabisa sidhan kam imeivaa hii
 
usipokanda vizuri, unga wako sio mzuri na ubaridi ukizidi kwenye unga ukiwa unakanda. Ngano inaumuka kwenye joto bila kutiwa habira hii muhimu sana. unga upewe nafasi ya kuumuka
Khaaa [emoji15] [emoji15] [emoji15] chapati zatiwa hamira makubwa cc evelyn salt mamaa ya mapish njoo uone huku
 
Maelezo khs Chapati common instruction please?
Andaa unga wako kweny besen tia chumvi kidogo mafuta kidog ukitak unayapasha moto ukitaka hupash mim huwa sipash unaweka maji kidogo huku unakanda unga wako utakanda unga hadi ulainike kabisa
Unga ukishalainika unaukatakata matonge ya size yasiwe makubwa wala yasiwe madogo sana
c8da1111dd2e70ea50fff47c541cba35.jpg
size ya matonge kama hayo
Ukimaliza hapo unachukua kibao chako unakiweka unga kidog then unaweka hilo donge kweny kibao unalisukuma hadi lijae kweny kibao kwa ajil ya kukunja ukiwa unalisukuma unalipaka mafuta lazima utakunja kam hiv au vyovyoye unavyojua kama hivi
0f9d0c9b2a6ac05dfa3c946da75e6fa9.jpg
ukishafanya fanya hivyo utakunja vyovyoye unavyojua
d937fcd5e4d76e51a28660512b2847ec.jpg
kama hivyo
Ukishamaliza hatua zote unabandika pan yako jikon unaiwacha ipate moto ikishapat mot unasukuma donge lako kwenye kibao chako then unaweka kwenye kikaango chako usiiache chapat yako san jikon ikiiva tu kidogo unaigeuza upande wa pili unaiwacha kidogo then unatia mafuta unaicha inawiva huku unaigeuza ikiiva unaitoa inaita kwa sahani tayar imeiva karibu ten sijui utakuwa umeyaelewa
Maelezo khs Chapati common instruction please?
 
Khaaa [emoji15] [emoji15] [emoji15] chapati zatiwa hamira makubwa cc evelyn salt mamaa ya mapish njoo uone huku
wapo wanaotia hamira kwenye chapati
ngoja na mm nitajarbu kutia hamira nione zitakuwajee
 
Back
Top Bottom