Jinsi ya kutoa maoni kwa Viongozi wakuu wa nchi bila kuwavunjia heshima

Katika jamii ya leo ambapo uhuru wa kuongea umekuzwa sana, watu wengi badala ya kutoa maoni, wanajikuta wakitoa matusi kwa wakuu wa nchi au viongozi wa kisiasa. Matokeo yake maoni yao hayapewi kipaumbele kwa sababu ya ukosefu wa lugha ya staha. Hebu leo tujifunze jinsi tunavyoweza kusema ukweli na kukosoa, bila kuwavunjia heshima wakuu au wenye mamlaka katika nchi.

Umuhimu wa kuwaheshimu Wakuu
Mila na maadili ya jamii nyingi duniani yanasisitiza heshima kwa wakuu—iwe ni wazazi, walimu, viongozi wa dini, au watawala wa nchi. Hata Biblia inaeleza wazi kwamba kila anayestahili heshima, apewe heshima. Kuwaheshimu wakuu sio dalili ya woga, bali ni ishara ya hekima, nidhamu, na ukomavu wa mtu binafsi. Heshima hujenga daraja la mawasiliano na huonyesha kwamba tunajua mipaka yetu kama raia mbele ya mamlaka iliyopo. Ni rahisi kujua iwapo mtu ana heshima au la, kwa kusikiliza anayoyaongea.

Kuna methali ya kisasa inayosema hivi: “Mtu yeyote anayejua kuongea kwa heshima, ana nafasi ya kusikika hata kwa mfalme.”

Najiuliza: hivi somo la lugha ya staha na adabu katika mawasiliano halifundishwi mashuleni na vyuoni? Au wanaofundisha hawaeleweki? Kama linafundishwa na kuzingatiwa, kwanini watu wanatoa maoni yao mbele ya Wakuu wa nchi kwa ukali, kwa kubeza, au hata kukashifu wakuu wao?

Jinsi ya kutoa maoni kwa lugha ya staha
Zingatia mambo haya unapotoa maoni yako kwa wakuu:
Anza kwa heshima – Tumia maneno kama "Kwa heshima na taadhima, au Mheshimiwa, ningependa kueleza mtazamo wangu..." au "Kwa unyenyekevu mkubwa, naomba kutoa mchango wangu..."

Halafu elezea sifa njema na mchango wa mkuu huyo – Hata kama unapingana naye, tambua na kuelezea mema aliyowahi kufanya.

Epuka lugha ya mashambulizi – Badala ya kusema "Wewe hujui unachofanya," sema "Kuna baadhi ya maeneo ambayo naamini yanaweza kuboreshwa."

Toa mifano na hoja, bila jazba – na maoni yako yawe ya kujenga, sio ya kubomoa.

Malizia kwa upole na heshima – Mfano: "Kwa hayo machache, naomba nihesabiwe kama raia anayejali, si mpinzani." Au "kwa hayo machache naomba kuwasilisha hoja zangu."

Watu wanadharau kusoma Biblia, lakini Biblia ina mafundisho mazuri ya jinsi ya kuwaheshimu Wakuu.

Angalia mifano hii:
Yusufu alikuwa na ufunuo kutoka kwa Mungu, lakini alimwendea Farao kwa heshima (Mwanzo 41).

Danieli alitoa maoni yake ya kiroho kwa ujasiri mbele ya Mfalme Nebukadneza bila kumvunjia heshima (Danieli 4:19).

Wakati kesi ya Paulo inasikilizwa mbele ya Mfalme Agripa – Paulo alianza kwa kusema: “Nina furaha, ee mfalme Agripa, kuwa leo nashtakiwa mbele yako...” (Matendo 26:2) – Ingawa Paulo alikuwa mtuhumiwa lakini alionyesha heshima kwa Mfalme kwa kusema: "Ee Mfalme"

Mfalme Sauli alikuwa anamuwinda Daudi ili amuue, lakini Daudi alimuita Mfalme Sauli kuwa ni Mpakwa mafuta. Kuna siku Daudi alipata nafasi ya kumuua Mfalme Sauli lakini akasema: “Siwezi kunyosha mkono wangu juu ya Mpakwa mafuta wa Bwana.” (1 Samweli 24:6). Watu wakiyazingatia haya hawawezi kamwe kumuita mkuu wa nchi (aliyepata mamlaka kihalali) "dikteta" au "kumbatiza" majina ya kubeza.
Heshima ni kitu cha bure, sasa tunaheshimu viongozi wasiotuheshumu sisi ili iweje? Mimi siheshimu kiongozi wowote, yaani nawaona ni wachawi tu kwangu., unateka na kumwaga damu za watu bila hata huruma?
 
Huyo alidai uhuru kwa heshima, sio kwa lugha za matusi ya nguoni. Vinginevyo asingekubalika kimataifa.

1000039931.jpg

1000039934.jpg
 
Rum 13:7
Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.
Ebr 13:17
Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea...
Wagalatia 2:14 Walakini, nilipoona ya kuwa njia yao haiendi sawasawa na ile kweli ya Injili, nalimwambia Kefa mbele ya wote, I
 
Kefa hakuwa kiongozi wa kisiasa
 
Kefa hakuwa kiongozi wa kisiasa
Marko 12:14 Hata walipofika walimwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu.

Luka 13:31 Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua

Luka 13:32 Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika.
 
Katika jamii ya leo ambapo uhuru wa kuongea umekuzwa sana, watu wengi badala ya kutoa maoni, wanajikuta wakitoa matusi kwa wakuu wa nchi au viongozi wa kisiasa. Matokeo yake maoni yao hayapewi kipaumbele kwa sababu ya ukosefu wa lugha ya staha. Hebu leo tujifunze jinsi tunavyoweza kusema ukweli na kukosoa, bila kuwavunjia heshima wakuu au wenye mamlaka katika nchi.

Umuhimu wa kuwaheshimu Wakuu
Mila na maadili ya jamii nyingi duniani yanasisitiza heshima kwa wakuu—iwe ni wazazi, walimu, viongozi wa dini, au watawala wa nchi. Hata Biblia inaeleza wazi kwamba kila anayestahili heshima, apewe heshima. Kuwaheshimu wakuu sio dalili ya woga, bali ni ishara ya hekima, nidhamu, na ukomavu wa mtu binafsi. Heshima hujenga daraja la mawasiliano na huonyesha kwamba tunajua mipaka yetu kama raia mbele ya mamlaka iliyopo. Ni rahisi kujua iwapo mtu ana heshima au la, kwa kusikiliza anayoyaongea.

Kuna methali ya kisasa inayosema hivi: “Mtu yeyote anayejua kuongea kwa heshima, ana nafasi ya kusikika hata kwa mfalme.”

Najiuliza: hivi somo la lugha ya staha na adabu katika mawasiliano halifundishwi mashuleni na vyuoni? Au wanaofundisha hawaeleweki? Kama linafundishwa na kuzingatiwa, kwanini watu wanatoa maoni yao mbele ya Wakuu wa nchi kwa ukali, kwa kubeza, au hata kukashifu wakuu wao?

Jinsi ya kutoa maoni kwa lugha ya staha
Zingatia mambo haya unapotoa maoni yako kwa wakuu:
Anza kwa heshima – Tumia maneno kama "Kwa heshima na taadhima, au Mheshimiwa, ningependa kueleza mtazamo wangu..." au "Kwa unyenyekevu mkubwa, naomba kutoa mchango wangu..."

Halafu elezea sifa njema na mchango wa mkuu huyo – Hata kama unapingana naye, tambua na kuelezea mema aliyowahi kufanya.

Epuka lugha ya mashambulizi – Badala ya kusema "Wewe hujui unachofanya," sema "Kuna baadhi ya maeneo ambayo naamini yanaweza kuboreshwa."

Toa mifano na hoja, bila jazba – na maoni yako yawe ya kujenga, sio ya kubomoa.

Malizia kwa upole na heshima – Mfano: "Kwa hayo machache, naomba nihesabiwe kama raia anayejali, si mpinzani." Au "kwa hayo machache naomba kuwasilisha hoja zangu."

Watu wanadharau kusoma Biblia, lakini Biblia ina mafundisho mazuri ya jinsi ya kuwaheshimu Wakuu.

Angalia mifano hii:
Yusufu alikuwa na ufunuo kutoka kwa Mungu, lakini alimwendea Farao kwa heshima (Mwanzo 41).

Danieli alitoa maoni yake ya kiroho kwa ujasiri mbele ya Mfalme Nebukadneza bila kumvunjia heshima (Danieli 4:19).

Wakati kesi ya Paulo inasikilizwa mbele ya Mfalme Agripa – Paulo alianza kwa kusema: “Nina furaha, ee mfalme Agripa, kuwa leo nashtakiwa mbele yako...” (Matendo 26:2) – Ingawa Paulo alikuwa mtuhumiwa lakini alionyesha heshima kwa Mfalme kwa kusema: "Ee Mfalme"

Mfalme Sauli alikuwa anamuwinda Daudi ili amuue, lakini Daudi alimuita Mfalme Sauli kuwa ni Mpakwa mafuta. Kuna siku Daudi alipata nafasi ya kumuua Mfalme Sauli lakini akasema: “Siwezi kunyosha mkono wangu juu ya Mpakwa mafuta wa Bwana.” (1 Samweli 24:6). Watu wakiyazingatia haya hawawezi kamwe kumuita mkuu wa nchi (aliyepata mamlaka kihalali) "dikteta" au "kumbatiza" majina ya kubeza.
Wenyewe wananuka damu za watu
 
Kefa hakuwa kiongozi wa kisiasa
Respect is earned by reputation.
Sio umri Wala ukuu wa cheo.
Na staha inategemea ulichoshauri mara ya kwanza alikifanyia Nini .kiongozi akishajenga bias kwamba ushauri nje ya mtazamo ni uadui dhidi ya maendeleo basi staha inakuwa kama kupulizia perfume kinyes
 
Marko 12:14 Hata walipofika walimwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu.

Luka 13:31 Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua

Luka 13:32 Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika.
Mbweha sio tusi hapo, ni lugha ya picha. Ntafafanua katika uzi mwingine. Hilo lingekuwa tusi Yesu asingesema watukanaji hawataingia mbinguni.
1 Wakorintho 6:9-10
"Au hamjui ya kwamba wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati, waabudu sanamu, wazinzi, walawiti, wafiraji, watukanaji, wanyang'anyi, hawataurithi ufalme wa Mungu.”
 
Katika jamii ya leo ambapo uhuru wa kuongea umekuzwa sana, watu wengi badala ya kutoa maoni, wanajikuta wakitoa matusi kwa wakuu wa nchi au viongozi wa kisiasa. Matokeo yake maoni yao hayapewi kipaumbele kwa sababu ya ukosefu wa lugha ya staha. Hebu leo tujifunze jinsi tunavyoweza kusema ukweli na kukosoa, bila kuwavunjia heshima wakuu au wenye mamlaka katika nchi.

Umuhimu wa kuwaheshimu Wakuu
Mila na maadili ya jamii nyingi duniani yanasisitiza heshima kwa wakuu—iwe ni wazazi, walimu, viongozi wa dini, au watawala wa nchi. Hata Biblia inaeleza wazi kwamba kila anayestahili heshima, apewe heshima. Kuwaheshimu wakuu sio dalili ya woga, bali ni ishara ya hekima, nidhamu, na ukomavu wa mtu binafsi. Heshima hujenga daraja la mawasiliano na huonyesha kwamba tunajua mipaka yetu kama raia mbele ya mamlaka iliyopo. Ni rahisi kujua iwapo mtu ana heshima au la, kwa kusikiliza anayoyaongea.

Kuna methali ya kisasa inayosema hivi: “Mtu yeyote anayejua kuongea kwa heshima, ana nafasi ya kusikika hata kwa mfalme.”

Najiuliza: hivi somo la lugha ya staha na adabu katika mawasiliano halifundishwi mashuleni na vyuoni? Au wanaofundisha hawaeleweki? Kama linafundishwa na kuzingatiwa, kwanini watu wanatoa maoni yao mbele ya Wakuu wa nchi kwa ukali, kwa kubeza, au hata kukashifu wakuu wao?

Jinsi ya kutoa maoni kwa lugha ya staha
Zingatia mambo haya unapotoa maoni yako kwa wakuu:
Anza kwa heshima – Tumia maneno kama "Kwa heshima na taadhima, au Mheshimiwa, ningependa kueleza mtazamo wangu..." au "Kwa unyenyekevu mkubwa, naomba kutoa mchango wangu..."

Halafu elezea sifa njema na mchango wa mkuu huyo – Hata kama unapingana naye, tambua na kuelezea mema aliyowahi kufanya.

Epuka lugha ya mashambulizi – Badala ya kusema "Wewe hujui unachofanya," sema "Kuna baadhi ya maeneo ambayo naamini yanaweza kuboreshwa."

Toa mifano na hoja, bila jazba – na maoni yako yawe ya kujenga, sio ya kubomoa.

Malizia kwa upole na heshima – Mfano: "Kwa hayo machache, naomba nihesabiwe kama raia anayejali, si mpinzani." Au "kwa hayo machache naomba kuwasilisha hoja zangu."

Watu wanadharau kusoma Biblia, lakini Biblia ina mafundisho mazuri ya jinsi ya kuwaheshimu Wakuu.

Angalia mifano hii:
Yusufu alikuwa na ufunuo kutoka kwa Mungu, lakini alimwendea Farao kwa heshima (Mwanzo 41).

Danieli alitoa maoni yake ya kiroho kwa ujasiri mbele ya Mfalme Nebukadneza bila kumvunjia heshima (Danieli 4:19).

Wakati kesi ya Paulo inasikilizwa mbele ya Mfalme Agripa – Paulo alianza kwa kusema: “Nina furaha, ee mfalme Agripa, kuwa leo nashtakiwa mbele yako...” (Matendo 26:2) – Ingawa Paulo alikuwa mtuhumiwa lakini alionyesha heshima kwa Mfalme kwa kusema: "Ee Mfalme"

Mfalme Sauli alikuwa anamuwinda Daudi ili amuue, lakini Daudi alimuita Mfalme Sauli kuwa ni Mpakwa mafuta. Kuna siku Daudi alipata nafasi ya kumuua Mfalme Sauli lakini akasema: “Siwezi kunyosha mkono wangu juu ya Mpakwa mafuta wa Bwana.” (1 Samweli 24:6). Watu wakiyazingatia haya hawawezi kamwe kumuita mkuu wa nchi (aliyepata mamlaka kihalali) "dikteta" au "kumbatiza" majina ya kubeza.
Upuuzi huu
 
Hongera, Umefanikiwa kunifikirisha kwanini umechagua kuwasemea zaidi watawala na sio wafuasi.

Hapo kidogo nadoubt Msingi wa Imani Yako japo najua you are too spiritual centered.
Hakuna spiritual yeyote anayesapoti UUWAJI huyu anasaporti UUWAJI kwa kutumia kutii wanaouwa sababu tu ni viongozi au watawala. Hana lolote. Uwezi kuwa spiritual alafu ukasapoti dhambi kwa namna yoyote ile
 
Back
Top Bottom