SHIDA IPO KATIKA MUKTDHA AKILIFU WA FAHAMU/UFAHAMU; PIA SIFA NA HADHI YA DARAJA LA UTU NA KUJITAMBUA KWA JAMII NZIMA!
Kiuono na Ufikirifu Mifumo, ipo topografu ya muktadha akililifu ya Uono Fasaha ya Kwamba: Katika jamii yenye ‘Mioyo iliyovunjika’, katika Nchi nyingi za Duniani,
Pesa ndiyo ‘Mshipa Mkuu wa Fitina’; ambavyo kwa kadiri wanajamii hao wanakuwa si wenye ku-JUA ilivyobora na kukosa koherensia ya (ma)Shauri la Fedha na utumwa wake basi hawa wanaingia kwenye mzunguruko usiyokoma wa umaskini, mateso na kuhangaika patupu. Wengine wachache wakiogelea kwenye ubatili wa mali,
u-eliti na Ubeberu.
Kwa mintarafu ya hivi,
utajiri ama umaskini ni fanusi ya ‘UJINGA’ katika jamii; ambavyo si kweli khasa kudhani labda ‘matajiri’, watu wenye nacho, wanajua ilivyobora kuhusu hatma za maisha na kujichagulia, kwa kuwa
hata tamaa ya mali/madaraka/heshima za kijamii ni ‘Maradhi ya Kiroho’--maradhi kadiri vile vile ‘Umaskini nao ni Maradhi’.
Basi ndiyo yawa, kwa Taifa la Tanzania, Mwenge wa Uhuru, ni kielelezo cha
UTASHI BORA kimaisha na kujichagulia kwa Muktadha Akilifu wa UTU wa Dhahabu, Moyo Safi na Akili-Yenye-Mwangaza-Bora, kwa Wanajamii wote, ili kuleta TUMAINI, IMANI na UPENDO wa kweli ndani na nje ya Taifa na Nchi ya Watanzania; kama ikivyodhahiri kwenye robo ya juu ya ‘Ngao ya Ustawi : Mwenge na Mwangaza wa Dhahabu’.
Kiufundi, Mioyo Iliyovunjika na muktadha akilifu wa Usentienti, Konsayansi na Nuru ya Ufahamu kama asili ya ‘Uzima na Kujisikia’ iwe katika mtu mmoja mmoja ama jamii; ambavyo
mwili ni mfanyiko wa viungo vingi—kimojawapo kinapokuwa na maradhi basi mwili wote unaathirika na kutojisikia vema kwa kuwa Uzima wa Mwili ni Mfumo wa Mazazi na Utangamano.
Kwa mintarafu ya hivi, hata shauri la ‘Ngao ya Ustawi’ ni tunda la kheri kwa Mazazi na Utangamano wa ‘Taifa la Tanzania’; ambavyo
mmonyoko wa maadili ama/na ukiukwaji wa miiko, miongoni mwa wanajamii, daima unaleta namna fulani ya ‘Stresi’/’Maradhi ya Kiustawi’ kwa sura ya ‘Kero za Kijamii/Vilio vya Mateso/Malalamiko/Domoghasia n.k.
Basi ndiyo yawa,
Nchi-Dola ni Utaasisi—utaasisi unaotumia mrejesho wa viashirifu kama vile Kero za Jamii/Vilio vya Mateso/Malalamiko/Domoghasia n.k kama dalili/Ishara za (A) Uzima ama (B) Maradhi ya Taifa ili kutoa mwangaza wa utatuzi wa kimazingira na mazingara kwa mikwamo ya Taifa na Nchi-Dola.
Hili linawezekana kwa kutengeneza
mazingira ya ‘Upatanisho’ katika ya (1) Watawala, na (2) Wataliwa kwa kuzingatia ‘Kumbukumbu Uzoefu’ na ‘Katiba’ iliyopo; ambavyo daima ujamii wowote huandamwa na matatu (1) Roho ya Uharibifu yenye Kutenda ndani ama nje ya mazingira ya jamii/taifa, (2) Roho ya Majenzi yenye kutenda ndani ama nje ya Mazingira ya jamii/taifa, na (3) Roho ya Upatanishi yenye kutenda ndani ama nje ya mazingira ya jamii/taifa.
Kiufundi, ‘Ngao ya Ustawi’ na ‘Pembe za Ndovu’ ni alama lugha-picha kwa ‘Roho ya Upatanishi’ inayokusudiwa kuwepo katika Uzima wa Jamii/Taifa; ambavyo
Upatanisho ni jambo lenye asili ya ‘Msalaba’: Wanajamii kupatana na hapo hapo Mambo ya Nchi na Mbingu kupatana.
Kwa mintarafu ya hivi, upatanishi ni
fanusi ya ‘NIA JAMII’ kwa Utashi wa ‘Maisha na Kujichagulia’ --Nia katika Shauri fulani Kuu lenye kuandama ‘Leo na Kesho’ ya Uzazi na Mazazi yake; ambavyo maisha ni vuta nikuvute ya pilika ama harakati za wanajamii katika kustahiki mambo kadhaa kimaisha ikiwemo (1) Uzima, (2) Liberiti, na (3) Udhamirifu wa Furaha.
Basi ndiyo yawa, Ngao ya Ustawi ni kwa ajili ya ‘Unasaba/Jinesi/Maumbile ya Kimwili na Uweza’ na Pembe za Ndovu ni kwa ajili ya ‘Maadili na Miiko inayokinga Mazazi na Uzazi wa Jamii/Taifa—
fanusi ya ‘Mali-Akili’.
Kiufundi, fitina ya Pesa juu ya Mazazi na Uzazi wa jamii/Taifa ni shauri linalotokana na ‘Vina vya Tafsiri’ kwa Uono Fasaha’ –
Uono juu ya ‘Uweza-Utayari-Umahiri’ wa wanajamii kulingana na ‘KUJITAMBUA’ kwao; ambavyo Wanajamii wenyewe kuwa ni Mali-Akili ndiyo ufunguo kwa ‘Usovereini/U-UMOJA’ wake wake wa Kweli katika kuyamudu mazingira; hata yale mazingira ya Utumikivu wa Fedha/Sarafu, kwa Maarifa na Maarifu juu ya Kazi na Ujenzi wa Kaya.
Kwa mintarafu ya hivi,
utendaji wa wanajamii unaweza kushambuliwa kiuchumi na nishati/tekinolojia hata kufikia kuzoroteshwa kwa UTU wale kimaamuzi ya Kijamii, Maendeleo na Ustawi; ambavyo, maisha daima ni vita/mapambano dhidi ya nguvu za Kiakili ama Kimwili kupitia Taasisi za Kibinadamu—‘kitaifa na kimataifa’/’Kidunia na U-intastela’.
Basi ndiyo yawa, mzunguruko usiyokoma wa vizazi kwenye lindi la
umaskini ni ishara/dalili ya wanajamii waliokwama kwenye daraja la UTU NA KUJITAMBUA kwa kule kukosa Uweza-Utayari-Umahiri wa kupanga/kupangua ‘Sura na Hadhi ya Utaasisi wake’ kama ‘Nchi-Dola/Taifa-Dola’; Kukosa kukamatia barabara ‘Ngao ya Ustawi’ na ‘Pembe zake za Ndovu’—Kuyamudu ya (1) Mazazi/Uzazi na (2) Nguvu za Kusimama katika ‘Mlima wa Utukufu’ : kwa Shauri la ‘UHURU NA UMOJA’; na basi kutojimudu kimavazi, malazi na wakati (Diplomasia na Biashara/Mabadilishano ya Mali ama/na Huduma) ilivyo ni
dhamira ya kutawala (1) Supasha (Pamba) na (2) Wakati (Karafuu na Marashi).
Hmmm
==
Shauri Kipande (Zana ya Kujitathmini Ufahamu) katika PDF ;
Kwa Shauri Kamili Tazama >
Hapa < ==