1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,802
- 10,307
Katika jamii ya leo ambapo uhuru wa kuongea umekuzwa sana, watu wengi badala ya kutoa maoni, wanajikuta wakitoa matusi kwa wakuu wa nchi au viongozi wa kisiasa. Matokeo yake maoni yao hayapewi kipaumbele kwa sababu ya ukosefu wa lugha ya staha. Hebu leo tujifunze jinsi tunavyoweza kusema ukweli na kukosoa, bila kuwavunjia heshima wakuu au wenye mamlaka katika nchi.
Umuhimu wa kuwaheshimu Wakuu
Mila na maadili ya jamii nyingi duniani yanasisitiza heshima kwa wakuu—iwe ni wazazi, walimu, viongozi wa dini, au watawala wa nchi. Hata Biblia inaeleza wazi kwamba kila anayestahili heshima, apewe heshima. Kuwaheshimu wakuu sio dalili ya woga, bali ni ishara ya hekima, nidhamu, na ukomavu wa mtu binafsi. Heshima hujenga daraja la mawasiliano na huonyesha kwamba tunajua mipaka yetu kama raia mbele ya mamlaka iliyopo. Ni rahisi kujua iwapo mtu ana heshima au la, kwa kusikiliza anayoyaongea.
Kuna methali ya kisasa inayosema hivi: “Mtu yeyote anayejua kuongea kwa heshima, ana nafasi ya kusikika hata kwa mfalme.”
Najiuliza: hivi somo la lugha ya staha na adabu katika mawasiliano halifundishwi mashuleni na vyuoni? Au wanaofundisha hawaeleweki? Kama linafundishwa na kuzingatiwa, kwanini watu wanatoa maoni yao mbele ya Wakuu wa nchi kwa ukali, kwa kubeza, au hata kukashifu wakuu wao?
Jinsi ya kutoa maoni kwa lugha ya staha
Zingatia mambo haya unapotoa maoni yako kwa wakuu:
Anza kwa heshima – Tumia maneno kama "Kwa heshima na taadhima, au Mheshimiwa, ningependa kueleza mtazamo wangu..." au "Kwa unyenyekevu mkubwa, naomba kutoa mchango wangu..."
Halafu elezea sifa njema na mchango wa mkuu huyo – Hata kama unapingana naye, tambua na kuelezea mema aliyowahi kufanya.
Epuka lugha ya mashambulizi – Badala ya kusema "Wewe hujui unachofanya," sema "Kuna baadhi ya maeneo ambayo naamini yanaweza kuboreshwa."
Toa mifano na hoja, bila jazba – na maoni yako yawe ya kujenga, sio ya kubomoa.
Malizia kwa upole na heshima – Mfano: "Kwa hayo machache, naomba nihesabiwe kama raia anayejali, si mpinzani." Au "kwa hayo machache naomba kuwasilisha hoja zangu."
Watu wanadharau kusoma Biblia, lakini Biblia ina mafundisho mazuri ya jinsi ya kuwaheshimu Wakuu.
Angalia mifano hii:
Yusufu alikuwa na ufunuo kutoka kwa Mungu, lakini alimwendea Farao kwa heshima (Mwanzo 41).
Danieli alitoa maoni yake ya kiroho kwa ujasiri mbele ya Mfalme Nebukadneza bila kumvunjia heshima (Danieli 4:19).
Wakati kesi ya Paulo inasikilizwa mbele ya Mfalme Agripa – Paulo alianza kwa kusema: “Nina furaha, ee mfalme Agripa, kuwa leo nashtakiwa mbele yako...” (Matendo 26:2) – Ingawa Paulo alikuwa mtuhumiwa lakini alionyesha heshima kwa Mfalme kwa kusema: "Ee Mfalme"
Mfalme Sauli alikuwa anamuwinda Daudi ili amuue, lakini Daudi alimuita Mfalme Sauli kuwa ni Mpakwa mafuta. Kuna siku Daudi alipata nafasi ya kumuua Mfalme Sauli lakini akasema: “Siwezi kunyosha mkono wangu juu ya Mpakwa mafuta wa Bwana.” (1 Samweli 24:6). Watu wakiyazingatia haya hawawezi kamwe kumuita mkuu wa nchi (aliyepata mamlaka kihalali) "dikteta" au "kumbatiza" majina ya kubeza.
Kwanza huo ukuu unapatikanaje ?
Tanzania ni nchi ya kidemokrasia . Hao watawala wenyewe hawana heshima kwa wananchi .
Wakati wa kugombea urais kama mwaka huu pakiwa na tume huru na Haki watu wote wangeheshimiana maana hakuna anayejua kuwa atashinda .
Kwa sasa Kuna wanaojua lazima washinde na wanawadharau wale wengine maana wanajua kuwa watatumia nguvu kushinda na atakayelalamika staitwa mchochezi na anayevunja amani .
Kuna wanaojua kuwa wao ni wa kuonewa na hawana pa kulalamikia . Sasa hawa kila wakijaribu kujieleza wanabezwa na kuitwa wachochezi na kupigwa . Hata Yesu hakutumia kauli ya kubembeleza kwa watawala waovu.
Enzi za utawala wakati wa mitume na manabii wa zamani hapakua na marais wala Bunge wala madiwani wa kuchaguliwa . Palikua na wafalme walioteuliwa na Mungu kwa kupitia manabii lakni pia palikua na wafalme walioingia madarakani kwa vita ,yaani watawala walikua ni watu mashujaa na wazalendo waliopambana kufa na kupona kuitetea nchi na kuondoa utawala mbovu.
Uimara wa Mfalme ulitokana na uwezo wake wa kupigana vita na kuwashinda wafalme wengine na kuwatoa madarakani .
Hawa mashujaa wa vita waliheshimika kwa sababu ya ushujaa wao uliowaweka madarakani .Hawa hapakua na namna yoyote ya kuwapinga bila kuuawa au uwapinge kwa vita uwatoe madarakani kwa vita sio kuwapinga kwa maneno tu . Hapakua na kura za kupata mfalme bila vita au kurithisha mtoto wa mfalme shujaa na mara nyingi mtoto anayerithishwa ni yule shujaa wa vita kuliko wenzake . Hapo ndipo Watu wanyonge na waliokua wanafuata sheria za nchi walihimizwa kutii Mamlaka hizo ili waweze kufanya kazi zao hasa za kuhubiri injili.Lakini pia Sifa za wafalme zilikua ni kusimamia sheria na kutii kiapo chao. Mfalme ilikua ni mwiko kuwa muongo au kuwa kigeugeu kama tunavyoona leo .Mara nataka maridhiano mara Mmeota mikia mara kifo ni kifo tu mara njooni tujenge nchi mara msinipangie.
Lakini kwa upande mwingine Watawala wa kiyahudi walikua ni tofauti na wale wa Nchi nyingine hasa warumi . Warimi walikua wasomi wa falsafa na sheria na walisimama katika kanuni za haki ikiwemo kuwashitaki na kuwasikiliza watuhumiwa na kutoa hukumu kwa haki.
Watawala wa kiyahudi walikua wanachanganya dini na siasa au dini na utawala . Kwa sababu Kwao Mungu ni Mfalme wa Wafalme wote .
Kwenye mfumo wa Demokrasia Watawala wanachaguliwa kwa kushindanishwa kwa kura . Usipotii chaguo la watu basi unakua ni Dikteta maana umeingia maarakani bila ridhaa ya wengi . Kwa karne hii dikteta sio tu hafai kuheshimiwa bali anastahili kupingwa kwa nguvu zote na hata kuchorwa kama katuni la Joka kubwa lenye vichwa saba yaani Dikteta ni Shetani katika umbo la binadamu .Muuaji ni jambazi anayepaswa kulaaniwa na kusomewa duwa zote mbaya mpaka awe kichaa kabisa aokote Makopo na kufukuzwa ikulu .
Hata wakoloni walikua watawala lakni wslipokosa utu walisababisha kuibuka kwa kundi la wapigania uhuru na baadae wakatolewa maarakani na nchi zikawachagua waafrika wenzao . Waliheshimika sana baada ya uhuru lakini wengi baadae walijawa na kiburi .Ndio wanaotusumbua mpaka sasa wanataka heshima wakati ni wahalifu wasiojali haki za waliowapa kura .
Kwenye mfumo wa kidemokrasia mabosi na wapiga kura maana ndio wanaotoa ridhaa ya nani akalie kiti .