Marco Seth
JF-Expert Member
- Oct 21, 2022
- 5,373
- 6,904
YhKabisa... Waheshimiwa wasiojiheshimu hawastahiki heshima!
YhKabisa... Waheshimiwa wasiojiheshimu hawastahiki heshima!
Wapuuzwe na kudharauliwa.
Dah aisee nimecheka sana, unaishi zamani sana aisee.
Moja ya changamoto ya viongozi wetu ni kuishi nyuma ya muda ilihali waongozwaji wengi wako mbele ya muda.
Moja ya sifa ya kiongozi ni kuwa mbele ya muda kuliko watu unaowaongoza, ukishindwa kuwa mbele ya muda ya wale unaowaongoza lazima upanic kila muda na kuwaona wakorofi, wajeuri, hawana heshima nk.
Awe muadilifu na mchamungu,achukie maovu na kuyakemea.Azungumze na watu Kwa adabu na awashughulikie wakisoaji Kwa taratibu stahiki.Ni kitu gani kiongozi afanye ili aheshimiwe
Awe muadilifu na mchamungu,achukie maovu na kuyakemea.Azungumze na watu Kwa adabu na awashughulikie wakisoaji Kwa taratibu stahiki.
Wewe mtu ni ZEZETA POSITIVE. Alafu unatumia maandiko vibaya. DHAMBI haibembelezwi mjinga wewe. Umetaja hao Sasa nakwambia maneno aliyeongea Yesu alipoambiwa herode anataka kumuuwa. Ili Upumbavu ukutoke.Katika jamii ya leo ambapo uhuru wa kuongea umekuzwa sana, watu wengi badala ya kutoa maoni, wanajikuta wakitoa matusi kwa wakuu wa nchi au viongozi wa kisiasa. Matokeo yake maoni yao hayapewi kipaumbele kwa sababu ya ukosefu wa lugha ya staha. Hebu leo tujifunze jinsi tunavyoweza kusema ukweli na kukosoa, bila kuwavunjia heshima wakuu au wenye mamlaka katika nchi.
Umuhimu wa kuwaheshimu Wakuu
Mila na maadili ya jamii nyingi duniani yanasisitiza heshima kwa wakuu—iwe ni wazazi, walimu, viongozi wa dini, au watawala wa nchi. Hata Biblia inaeleza wazi kwamba kila anayestahili heshima, apewe heshima. Kuwaheshimu wakuu sio dalili ya woga, bali ni ishara ya hekima, nidhamu, na ukomavu wa mtu binafsi. Heshima hujenga daraja la mawasiliano na huonyesha kwamba tunajua mipaka yetu kama raia mbele ya mamlaka iliyopo. Ni rahisi kujua iwapo mtu ana heshima au la, kwa kusikiliza anayoyaongea.
Kuna methali ya kisasa inayosema hivi: “Mtu yeyote anayejua kuongea kwa heshima, ana nafasi ya kusikika hata kwa mfalme.”
Najiuliza: hivi somo la lugha ya staha na adabu katika mawasiliano halifundishwi mashuleni na vyuoni? Au wanaofundisha hawaeleweki? Kama linafundishwa na kuzingatiwa, kwanini watu wanatoa maoni yao mbele ya Wakuu wa nchi kwa ukali, kwa kubeza, au hata kukashifu wakuu wao?
Jinsi ya kutoa maoni kwa lugha ya staha
Zingatia mambo haya unapotoa maoni yako kwa wakuu:
Anza kwa heshima – Tumia maneno kama "Kwa heshima na taadhima, au Mheshimiwa, ningependa kueleza mtazamo wangu..." au "Kwa unyenyekevu mkubwa, naomba kutoa mchango wangu..."
Halafu elezea sifa njema na mchango wa mkuu huyo – Hata kama unapingana naye, tambua na kuelezea mema aliyowahi kufanya.
Epuka lugha ya mashambulizi – Badala ya kusema "Wewe hujui unachofanya," sema "Kuna baadhi ya maeneo ambayo naamini yanaweza kuboreshwa."
Toa mifano na hoja, bila jazba – na maoni yako yawe ya kujenga, sio ya kubomoa.
Malizia kwa upole na heshima – Mfano: "Kwa hayo machache, naomba nihesabiwe kama raia anayejali, si mpinzani." Au "kwa hayo machache naomba kuwasilisha hoja zangu."
Watu wanadharau kusoma Biblia, lakini Biblia ina mafundisho mazuri ya jinsi ya kuwaheshimu Wakuu.
Angalia mifano hii:
Yusufu alikuwa na ufunuo kutoka kwa Mungu, lakini alimwendea Farao kwa heshima (Mwanzo 41).
Danieli alitoa maoni yake ya kiroho kwa ujasiri mbele ya Mfalme Nebukadneza bila kumvunjia heshima (Danieli 4:19).
Wakati kesi ya Paulo inasikilizwa mbele ya Mfalme Agripa – Paulo alianza kwa kusema: “Nina furaha, ee mfalme Agripa, kuwa leo nashtakiwa mbele yako...” (Matendo 26:2) – Ingawa Paulo alikuwa mtuhumiwa lakini alionyesha heshima kwa Mfalme kwa kusema: "Ee Mfalme"
Mfalme Sauli alikuwa anamuwinda Daudi ili amuue, lakini Daudi alimuita Mfalme Sauli kuwa ni Mpakwa mafuta. Kuna siku Daudi alipata nafasi ya kumuua Mfalme Sauli lakini akasema: “Siwezi kunyosha mkono wangu juu ya Mpakwa mafuta wa Bwana.” (1 Samweli 24:6). Watu wakiyazingatia haya hawawezi kamwe kumuita mkuu wa nchi (aliyepata mamlaka kihalali) "dikteta" au "kumbatiza" majina ya kubeza.
Mkuu unamuogopa mtoa mada?Ulitakiwa uanze hivi.
"Hongera sana mleta mada, kwa kweli umeleta hoja ya msingi sana ya kuimarisha kuheshimiana katika jamii pale tunapokuwa na mijadala namna ya kujadiliana kwa staha.
Ndugu mleta mada, kwa uzito ule ule na umuhimu huo huo wa hoja uliyoileta ningefurahi sana kama ungepata wasaa wa kushirikisha jamii yetu hoja yako hii kwa kuitisha Press Conference na kisha uonyeshe kwa vitendo kwa maana ya kuzungumza kisha uishauri serikali kwenye mambo kadha wa kadha yanayojitokeza nyakati hizi na utumie staili hii hii kuwaonyesha wote namna ya kuwasilisha ushauri kwa staha.
Natanguliza shukrani kwa kukubali wito wangu."
Kwa maelezo hayo hapo juu. Mleta mada nadhani angekuelewa. Lakini kwa namna ulivyoleta ushauri wako ni kama una mkebehi. Atakujibu lakini si kwa namna ambayo nadhani angependa akujibu.
TUJITEGEMEE amekujibu vizuri sana.Ingependeza kama ungefanya press utumie hizo mbinu tuone kama zitafanikiwa, tunakutegemea mama mchungaji utuambie tu utakuwa live muda gani!
Walianzia huko unakosema, walishafanya yote hayo bila mafanikio.Najiuliza: hivi somo la lugha ya staha na adabu katika mawasiliano halifundishwi mashuleni na vyuoni? Au wanaofundisha hawaeleweki? Kama linafundishwa na kuzingatiwa, kwanini watu wanatoa maoni yao mbele ya Wakuu wa nchi kwa ukali, kwa kubeza, au hata kukashifu wakuu wao?
Sawa, ila sarafu ina pande mbili,Mfalme Sauli alikuwa anamuwinda Daudi ili amuue, lakini Daudi alimuita Mfalme Sauli kuwa ni Mpakwa mafuta.
🤣🤣Wewe mtu ni ZEZETA POSITIVE. Alafu unatumia maandiko vibaya. DHAMBI haibembelezwi mjinga wewe. Umetaja hao Sasa nakwambia maneno aliyeongea Yesu alipoambiwa herode anataka kumuuwa. Ili Upumbavu ukutoke.
Luka 13:31-32
[31]Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua.
[32]Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika.
Hayo ni maneno Yesu anamwambia mfalme herode na kumwita mbweha Sasa wewe tutokee Upumbavu hapa watu hatulei maovu mjinga sana .
Mithali 26:1
[1]Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno;
Kadhalika heshima haimpasi mpumbavu.
Uwezi kuuwa tukakuheshimu sababu heshima AIMPASI mpumbavu. Wewe ni mmoja wa wapumbavu. Huu ushetani wako wa kutetea mauvu utakupa laana
Mkuu unamuheshimu vipi muuwaji?. Yesu mwenyewe alimjibu herode kwa kumuita mbweha walipoambiwa anataka kumuuwa YESUHekima ni jambo muhimu sana ata Mimi naliunga mkono kwa asilimia zote
Lakn tutambue biblia hyo hiyo inayotuhasa kuwa wanyenyekevu na wenye kutii imehitimisha kwa kutumia kuwa tuwe na upole kias na moyo wa kiasi
Sasa huyu mkuu ata ukimtazama si unamuona tu kuwa ni ZEZETA
Kwani kuheshimu mtu ni kumsujudu?Hakuna unafiki, yaan mtu anaboronga halafu unambembeleza kwani ye ni Mungu?!.
Mungu tuuu ndiye anayesujudiwa na kunyenyekewa, hao wapuuzi wwngine wanaojiita waheshimiwa unawachana makavu ili wasirudie kufanya ujinga!.
By the way hao viongozi wenyewe nao hawatuheshimu, mara watuite kenge, mara tunasali dini za mashetani (utadhani yeye alienda huko mbinguni Mungu akamwambia dini ya kweli ni ipi).
Upuuzi mtupu.
Mkuu huyu zezeta anataka kupindisha maandiko. Ili kutetea maovu. Hakuna kitu Mungu anachukia Kama maovu kuuwa watu mpaka anasema ATAITAKA DAMU ya mwanadamu kwenye kila mkono uliyoimwaga alafu mtu anakuja na maneno ya kufunika USHENZI