DOKEZO Jinsi ziwa Tanganyika lilivyo na maji mengi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Uzi wa maana sana huu mkuu. Shukran nyingi kwa kuuanzisha.

Hata michango ya wadau inathibitisha kuwa Watanzania wengi ni watu wenye akili na uwezo mzuri wa kufikiri . Si kama watawala wanavyopenda kutuaminisha kwamba tutegemee mawazo ya mtu mmoja tu eti “mwenye maono na ambaye hutokea mara moja kwa karne”! Hii sio nchi ya kupata shida ya maji. Ni aibu na fedheha kubwa.
 
Kusema ni rahisi Sana ila sasa utekelezaji ndio tatizo
 
Ubarikiwe Sana kututoa ujinga.
 
Kijiografia ziwa Tanganyika linakiwango kidogo cha chumvi, kwa sababu limepakana na maeneo yenye madini chumvi.... Mvua ikinyesha uvinza moja kwa moja maji yake uelekea ziwa Tanganyika, sasa chumvi inakosaje??????
 
Kwa nini mradi wa maji Tabora - Nzega walichukua ziwa Victoria badala ya ziwa Tanganyika, wakati ziwa Tanganyika lipo karibu na Tabora kuliko ziwa Victoria?

Na ninasikia mpango ni kufikisha maji ya Ziwa Victoria Dodoma.
 
Kijiografia ziwa Tanganyika linakiwango kidogo cha chumvi, kwa sababu limepakana na maeneo yenye madini chumvi.... Mvua ikinyesha uvinza moja kwa moja maji yake uelekea ziwa Tanganyika, sasa chumvi inakosaje??????
Mkuu hivi unahisi ziwa tanganyika lipo kigoma tu?
 
Tatizo kubwa ninaloliona hapa ni ukosefu wa mipira ya kuvuta maji toka ziwa Tanganyika , kuleta mikoa mingine ili maji yatumike kwa kilimo cha umwagiliaji badala ya kutegemea mvua,, plastic za kutengenezea mabomba ni adimu sana
 
Hatujawahi kuwa na upungufu wa maji bali tuna upungufu wa akili! Hilo ndio tatizo letu la msingi.
Mkuu acha tununue ndege kwanza,, ujue ndege ni muhimu sana kuliko kitu chochote,, wapinzania mlitusema sana enzi za jk,, tunahitaji ndege nyingi[emoji847][emoji847]
 
Kuna vitu mkuu ukijiuliza na kutathmini umri wa taifa letu unabaki kuguna bhasi tu. Kwa miaka yote hii utoaji wa huduma muhimu za kijamii kama maji, elimu, umeme bado ni kizungumkuti. Labda tumelaaniwa bila kujijua!
Nikiwa Rais kipaumbele changu miundo mbinu, maji, barabara umeme hospital shule reli, meli.
Kisha kilimo lazima kiwe cha kumwagilia,, kuhusu umeme tuzalishe Dekawatt 1000.. sio mambo ya MW 3000
 
Tatizo kubwa ninaloliona hapa ni ukosefu wa mipira ya kuvuta maji toka ziwa Tanganyika , kuleta mikoa mingine ili maji yatumike kwa kilimo cha umwagiliaji badala ya kutegemea mvua,, plastic za kutengenezea mabomba ni adimu sana
Ni nia tu mkuu, na usafirishaji mkubwa hivyo hufanywa na mabomba makubwa ya chuma. Wanapump kwenye mabomba na sehemu nyingine yanashuka kwa gravity kwenye mifereji. Chuma cha kuunda hayo mabomba na pump zake tunacho. Watu wanapump mafuta toka Dar hadi huko Ndola, yanapita milimani juu kabisa. Ni nia tu.
 
Nikiwa Rais kipaumbele changu miundo mbinu, maji, barabara umeme hospital shule reli, meli.
Kisha kilimo lazima kiwe cha kumwagilia,, kuhusu umeme tuzalishe Gigawatt 1000.. sio mambo ya MW 3000

GWh au TWh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…